THE MODERN WAR: Simulizi ya kijasusi mapenzi na upelelezi

THE MODERN WAR: Simulizi ya kijasusi mapenzi na upelelezi

THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya..............45
Mtunzi: Saul David

ILIPOISHIA....
Ikiwa ni katika hatua za mwisho kabisa za kimahakama kabla ya kesi ya Osward kuamuliwa ghafula katikati hali isiyotegemewa Annah ambae ni shahidi pekee aliekuewa akisubiriwa anafika mahakamani hapo.
Upande wa pili Inspekta Aron aliyepigwa risasi ya mguu pamoja na Najma aliyepoteza fahamu wanafikishwa hospitali kwa ajili ya kupata huduma za matibabu.
Je, ni nini kitafuata?

SASA ENDELEA....
"Unamaanisha huyu mwanamke ndio Annah shahidi uliyeomba tumsubiri hapo awali?" Muendesha mashataka aliuliza swali
"Ndiyo, ndio yeye mheshimiwa"wakili Andrea alijibu
Hakimu pamoja na viongozi wengine wa mahakama walionekana kunong'onezana jambo na mwisho wakafikia makubaliano ya pamoja.

"Sawa tutamsikiliza shahidi wako, naomba Annah sogea mbele utaapa kama ilivyo taratibu kisha utahojiwa na mawakili wote wawili" Alisema hakimu.
Annah alipiga hatua kusogea mbele ya mahakama ile, alipokutana na wakili Andrea akasimama
"Pole sana Annah bila shaka umepitia wakati mgumu sana mpaka kufika hapa, lakini tushukuru mungu umefika salama. Hatukupata muda wa kuongea ila najua hauwezi kushindwa kujieleza, ongea kila kitu ulichokiona na kusikia siku hiyo wakati Osward anafanya yale mauaji" Wakili Andrea aliongea haraka haraka kwa sauti ya chini. Annah alitikisa kichwa chake ikiwa ni ishara kuwa amemuelewa wakili. Baadae taratibu zote za kumuapisha zilikamilika na baadae Annah akapandishwa kizimbani upande wa pili tofauti na ule aliopo mshitakiwa Osward, sasa akawa tayari kwa kuhojiwa. Wakili Andrea ndio alikuwa mtu wa kwanza kumuliza maswali shahidi.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Upande wa pili katika nyumba moja kubwa ya kifahari iliyokuwa imejegwa chini ya mlima mdogo pembeni kidogo ya mji, ilikuwa ni nyumba inayomilikiwa na mtoto wa kwanza wa Rais mstaafu Elizabeth Kulolwa ambaye kwa sasa yuko masomoni nchini Marekani. Nyumba hiyo ilijengwa kwa umiliki wake lakini ukweli ni kwamba ilikuwa ni nyumba ambayo inatumiwa sana na baba yake mzazi yaani Profesa Cosmas Kulolwa. Hapa ndipo alikuwa akipanga na kuendesha mipango yake mingi ya siri hata kipindi akiwa madarakani kama Rais.
Leo hii kwa mara nyingine katika nyumba hii yenye ghorofa sita kwenda juu, Profesa Cosmas anapokea ugeni mkubwa kutoka nchini Mexico ugeni ambao ulikuwa ni muhimu sana kwake.
Miongoni mwa wageni hao waliokuwepo wanaume watatu wa miraba minne waliojazia sana na wote walikuwa wamenyoa vipara mmoja kati yao alikuwa mzungu na wawili waafrika. Wageni wengine walikuwa ni wazungu watatu ambao wote walitoka nchini Mexico alikuwepo profesa Fernando Arturo mkurugenzi mtendaji wa maabara ya ZMLST inayomiliki kirusi cha V-COBOS, alikuwepo Dokta Codrado pamoja na mwanamke mmoja mwenye asili ya kihindi aliitwa Sharma Khumal.

Wote kwa pamoja wakiwa na wenyeji wao ambao ni Profesa Cosmas Kulolwa pamoja na Mkemia mkuu wa serikali Andiwelo katabi walikaa na kuizunguuka meza moja ya duara kisha wakawa wanafanya mazungumzo nyeti sana kwa lugha ya kingereza.

"Tumesubiri vya kutosha na katika kusubiri kwetu tumeona kuna mambo yameanza kuharibika na kama tutaendelea kusubiri zaidi basi tunaweza kujikuta tunapoteza kila kitu" Profesa Fernando alianzisha mazungumzo akatulia kwa muda kisha akaendelea.
"Mpango wetu ni ule ule kurudisha heshima ya maabara yetu ya ZMLST kama ilivyokuwa mwanzo na pili ni kutengeneza mabilioni ya pesa. Hivyo vyote vitaenda kwa pamoja na siraha yetu kubwa ni virusi vya V-COBOS. Ilikuwa tufanye hivyo miaka kadhaa iliyopita lakini virusi vya COVID-19 vilikuja na kutuvurugia ratiba hivyo tukasubiri. Korona imepungua kwa sasa ni wakati wetu wa kuitikisa Dunia tutapeleka mambo haraka haraka ikiwa ni pamoja na kuipata chupa ya kijivu ikiyopotea ndio maana tumekuja na kikosi kazi na hawa wanaume wa shoka hapa ni sehemu tu ya kikosi kazi chetu. Tukilazimika kuua tutaua tukilazimika kuchinja tutachinja ilimradi tu jambo letu lifanikiwe. Tunashukuru profesa Cosmas kwa kumuondoa Dunia Dokta Gondwe kwa sababu tayari alishakuwa kikwanzo kwetu tangu mda mrefu, huu ni mfano unaoonyesha ni jinsi gani hili suala halihitaji masihara hata kidogo. Kama akitokea mwingine akazingua ikiwa ni pamoja na kuleta usaliti basi sitosita kuondoa uhai wake mara moja. Kwa sasa naomba Profesa Cosmas utupe maelezo mafupi ni wapi vilipo vimelea vyetu na ni wapi ilipo chupa ya kijivu alafu baada ya hapo tutajua tuanze na nini" aliongea profesa Fernando hapo Rais mstaafu Profesa Cosmas alikohoa kidogo tayari kuzungumza lakini kabla ya kufanya hivyo mara simu yake katika mfuko wa shati iliita kwa kutoa mtikisiko. Profesa Cosmas aliichukua na kutazama namba ya mpigaji shika akainua macho na kuwatazama wenzake.

"Worry out if its important call just pick up"(usiogope kama ni simu ya muhimu pokea) aliongea Sharma Khumal kwa kingereza chenye rafuzi ya kihindi.
Baada ya kusema hivyo Profesa Cosmas alipokea simu ile kutoka kwa Asia mmoja kati ya kikosi hatari cha kunguru weusi.

"Nipe ripoti" aliongea Pro. Cosmas mara tu baada ya kupokea ile simu
"Mheshimiwa mambo yameharibika" Asia aliongea upande wa pili akiwa nje ya mahakama.
"Kivipi?"
"Yule binti, Annah amekuja hapa mahakamani, dakika za mwisho kabisa mkuu"
"Imekuwaje? Kivipi? Wenzio wako wapi?"
"Sijui, naomba uniambie nini cha kufanya la sivyo kila kitu kitaenda hovyo mheshimiwa, tuna dakika chache tu"
"Sawa subiri nákupigia"
Alisema profesa Cosmas kisha akakataka simu, sura yake ikiwa na wasiwasi kiasi na kila mmoja kwenye kikao kile aligundua hilo.

"Kuna nini?" Aliuliza Dokta Codrado
"Kuna kijana wangu mmoja yuko hatarini kufungwa, nilikuwa kwenye harakati za kumsaidia lakini kwa bahati mbaya mambo yameenda tofauti dakika za mwisho"
"Ni mmoja wetu?" aliuliza Profesa Fernando
"Ndio alikuwa chini ya Dokta Gondwe lakini nataka kumfanya awe chini yangu kwa sababu anajua siri yetu pia yuko vizuri kwa kazi"
"Okay, vipi unachochote cha kufanya kuzuia asifungwe kwa muda uliobaki au nikusaidie?"
Aliuliza Profesa Fernando Profesa Cosmas Kulolwa akawa kimya.
"Wewe ni Rais inakuaje suala dogo kama hili likushinde"
"Ni kweli lakini tatizo ni muda nahisi nimechelewa sana, dakika si nyingi hukumu ya huyu kijana itasomwa"
"Okay, nieleze kwa kina kisha tujue tunafanyaje eleza haraka haraka" Alisema Profesa Fernando.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Wakati huo kesi ilianza kusikilizwa mahakamani kwa mara nyingine Annah akiwa kizimbani kama shahidi...
"Annah, ni vipi unamfahamu mtuhumiwa" aliuliza swali hili wakili Andrea
"Nilimuona siku ya birthday yangu, kwenye mgahawa wa Affati"
"Kwa maana hiyo unataka kusema wewe ni mmoja kati ya watu waliokuwepo siku ambayo kulitokea mauaji pale katika mgahawa wa Affati? Tafadhali unaweza kutueleza japo kwa undani kila ulichokiona siku hiyo?"
Andrea aliuliza swali jingine na hapo Annah alieleza kila kitu kuanzia mwanzo mpaka mwisho hakuacha kitu.

"Mheshimiwa hakimu sina swali jingine" wakili Andrea alimaliza huku akiwa na imani kabisa kuwa kwa maelezo aliyoyatoa Annah yalitosha kabisa kumuweka Osward hatiani na nilazima angefungwa
Baada ya hapo hakimu alimruhusu wakili upande wa utetezi kumuuliza shahidi maswali. Kwa ufupi wakili huyu hakuwa amejipanga kumuuliza Annah maswali ya kumbana kitendo cha Annah kuingia ghafula mahakamani hapo kilivuruga kila kitu. Ilibidi tu atumie uzoefu wa kawaida alionao kwani maelezo ya Annah yalikuwa yameshiba.

"Annah unajua kwamba ikibainika unasema uongo mbele ya mahakama kifungo chake ni zaidi ya miaka 15 jela?"
"Najua, yote ninayoyasema ni kweli tupu"
Annah alijibu kwa kujiamini wakati huo kuna askari aliingia ghafula mahakamani hapo akapiga hatua hadi ilipo meza ya hakimu, askari huyu alikuwa na kipande cha karatasi akafika na kumkabidhi hakimu kisha akaondoka. Hii ilikuwa ni kinyume kabisa na utaratibu lakini hakuna aliyehoji. Hakimu alipofungua lile karatasi kulikuwa na picha ndogo kama passport kisha akasoma maelezo yaliyokuwa kwenye karatasi. Ni Andrea pekee ndio aliyeuona mshtuko alioupata hakimu mara baada ya kusoma maelezo yale moja kwa moja akajua kuna kitu hakipo sawa. Wakati huo wakili alizidi kumuuliza maswali Annah ambaye naye aliyajibu kwa ufasaha sana bila kupepesa.
[emoji294][emoji294][emoji294]

NUSU SAA BAADAE..
Gari moja ilifunga breki kali nje ya mahakama ya Ilonga, Inspekta Jada akiwa ndio dereva alishuka upesi na kuanza kupiga hatua kuelekea jengo kuu la mahakama hiyo. Alipotazama mazingira aliona kuna kila dalili kuwa amechewa sana, watu walikuwa ni wachache mno na wengine ndio walikuwa wakimalizaka kuondoka.
Akiwa ameukaribia mlango wa kuingia ndani ya jengo la mahakama Inspekta Jada anakutana na mwanasheria ambaye alikuwa ni wakili wa kesi ile bwana Andrea. Uso wa Andrea uliojaa huzuni ulitosha kabisa kumfanya Inspekta Jada aelewe kuwa mambo sio mazuri.

"Annah alifika?" Hili ndio lilikuwa swali la kwanza kutoka kwa Inspekta Jada.
"Alifika" Andrea alijibu kifupi huku akionekana mtu mwenye kukata tamaa
"Sasa imekuwaje, kwa nini tumeshindwa Andrea?"
"Ni nguvu Inspekta, hatukuwa na nguvu ila haki yetu ilikuwepo wazi" alijibu Andrea
"Una maana gani?"
"Namaanisha kuna nguvu ya ziada imetumika kupindua haki yetu, hakimu alitishiwa katika dakika za mwisho kabisa kabla ya kusoma hukumu kuna kila dalili kuwa watu wazito na wakubwa wameingilia hii kesi" alieleza Andrea japo ilikuwa ni hisia zake tu lakini alichokiongea kilikuwa sahihi kabisa.
Kimya kilitawala huku wote wakionekana kuwa na masikitiko makubwa sana.
" Vipi kuhusu Inspekta Aron" aliuliza Andrea
"Amekamatwa yupo hospitali anatolewa risasi aliyopigwa mguuni"
"Mmh! hali ni mbaya Inspekta Jada"
" Tena sana, Annah yuko wapi sasa?"
"Si..sijui alikuwepo hapa?"
"Hujuii?" Inspekta Jada aliuliza kwa mshangao ulioambatana na wasiwasi.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Annah alionekana maeneo ya mji akikatiza katikati ya barabara ya rami bila kujali magari mengi yaliyokuwa yakipita na kupishana kwenye barabara hiyo. Baadhi ya madereva walimpigia honi mfurulizo huku wengine wakimtukana matusi, nawengine kulazimika kusimama na kumuacha Annah apite kwanza.
"Muache kupenda mkiwa wadogo" Alisikika dereva mmoja wa roli akiongea huku anamchungulia Annah dirishani.
Annah alionekana ni kama mwendawazimu kwa namna alivyokuwa anatembea huku akionekana kuwa mtu mwenye mawazo sana. Annah alijikuta kwenye hali hiyo mara tu baada ya hukumu ya Osward kusomwa kuwa hana hatia, baada ya muda kidogo alipata pia taarifa za kukamatwa kwa mwanaume anaempenda kupita kawaida Inspekta Aron. Annah alijikuta anapatwa na wazimu wa ghafula akaanza kutembea hovyo asijue anakoelekea.
Haya ndio aliyokuwa akiyawaza Annah wakati akizidi kwenda mbele bila kujali kuwa alikuwa akipita katikati ya barabara kuu ya rami yenye gari nyingi.

"Kuna wakati binadamu huwafanya binadamu wenzao kuwa wabaya,nimeamini si kila anaefanya ubaya alipenda kuwa mbaya. Tunaishi katika ulimwengu ambao shida zako zinawapa watu wengine furaha na furaha yako inawapa watu wengine shida. Leo hii mbele ya macho yangu nimeona haki ikipindishwa kwa makusudi kabisa kwa ajili ya manufaa ya watu wachache watu wenye NGUVU watu wenye nyazifa kubwa. Sisi tusio na kitu tunaishia kunyanyasika na kuumizwa kila siku, wamemuua baba wakamuua mama, wanampeleka gerezani mwanaume wangu asiye na hatia. Hiki kilio chetu tukipeleke kwa nani, nani atatusikiliza? nani atasimama kutupigania sisi wanyonge?HAKUNA, NASEMA HAKUNA ni sisi wenyewe tunatakiwa kujipambania. Leo naondoka lakini nitarudi tena nikiwa Annah ambaye hawataamini kama ni Annah yule wanayemjua, nitawaadhibu wote waliohusika kuupindisha ukweli, wote waliohusika kuwaua wazazi wangu, na kamwe sito ruhusu Aron wangu aozee gerezani, ndio mimi Annah nimesema".

ITAENDELEA...
Naam huyo ni ANNAH, bila kusahau tayari timu ya ZMLST kutoka Mexico imeshaingia nchini, vipi kuhusu Inspekta Aron?
Sasa rasmi tunakwenda kuuwasha moto wa SEASON 4, karibu...
0756862047
 
Vipi kaka
Muunganishe Anna na yule INNOCENT THE KILLER . na mwambie wanajif tunapendekeza wakiwakamata wahusika wawachome moto Kwa kuwafunga miguu na mikono juu vichwa chini na chini kuwepo moto wa kawaidai yaani wabanikwe kama mbuzi.
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya..........46
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Osward anashinda kesi yake mahakamani licha ya kwamba shahidi wa pekee na aliyetegemewa Annah alifika na kutoa ushahidi wake lakini hii haikusaidia kitu kwani kuna nguvu ya ziada inaonekana kutumika na kumfanya Osward kuibuka mshindi na kuachiwa huru. Hali inazidi kuwa mbaya, Dokta Gondwe amekufa Inspekta Aron kakamatwa na Annah hajulikani alipo.

Je, nini kitafuata?

SASA ENDELEA...
[emoji294][emoji294][emoji294]
Tayari madaktari walifanikiwa kuiondoa risasi kutoka kwenye mguu wa kushoto wa Inspekta Aron, baada ya kumfunga kidonda walimuacha apumzike kabla taratibu nyingine za kisheria hazijaendelea. Ulinzi ulikuwa ni mkali sana hospitalini hapo hasa ukizingatia kesi aliyokuwa nayo kijana huyu Aron ilikuwa ni nzito na iliyoteka hisia za watu wengi sana. Kumuua waziri wa afya Dokta Isaack Gondwe halikuwa suala jepesi hata kidogo.
Akiwa amelala kitandani huku mkono wake ukiwa umeunganishwa kwa pingu na chuma cha kitanda. Inspekta Aron alikuwa akipiga hesabu afanye nini kujinusuru na kesi hiyo kubwa. Mchezo aliokuwa amechezewa na Osward kwa kushirikiana na malaika weusi ulikuwa si wa kitoto haikuwa rahisi kabisa Inspekta Aron kuchomoka kwenye kesi ile, wala hakujua ni wapi aanzie.
"Hivi inakuwaje Osward kamuua Dokta Gondwe mtu waliyekuwa wakifanya kazi kwa ukaribu? Alafu atakuwa ametoroka gerezani au ameua kisha karudi tena?" Inspekta Aron alikuwa akiumiza akili yake kufikiri na kuunganisha doti kama ilivyo kawaida ya askari wapelelezi, alitamani kujua ni mchezo gani anaucheza Osward

"Najma, Najma wangu" Ghafula Inspekta Aron alimkumbuka mwanamke muhimu sana ambaye tayari alishaanza kuchukua nafasi kwenye moyo wake, alikumbuka ni namna gani Najma aliumia hadi kupoteza fahamu mbele ya macho yake mara tu baada ya kufahamu na kuamini kuwa Inspekta Aron ndiye anaehusika na mauaji ya baba yake. Baadae waliletwa wote katika hospitali hiyo ya taifa Kirunguru kwa ajili ya matibabu.

"Hapana ni lazima Najma aujue ukweli, siwezi kuendelea kukaa hapa Najma anapaswa kujua ukweli. Mimi sijamuua baba yake, Osward ndio kamuua" Aliwaza Inspekta Aron huku akikikunja kidole gumba chake kwenye mkono aliofungwa pingu kwa namna ya ajabu sana. Mara mlio kama mfupa ulioteguka ulisikika na hapo ki ulaini sana Inspekta Aron aliuchomoa mkono wake kutoka kwenye ile pingu. Haraka akasimama na kupiga hatua kuelekea mlangoni.
Kupitia vitundu vidogo vya mlango Inspekta Aron aliweza kuwaona polisi zaidi ya wanne wakiwa nje ya chumba alichokuwa amepumzishwa.

"Hakuna njia!! Kama Dokta Gondwe ameuawa huu utakuwa ni mpango wa nani, Osward anafanya kazi chini ya nani sasa hivi?" Inspekta Aron alikuwa akiwaza huku akijaribu kupiga hesabu za haraka haraka afanye nini. Alisogea dirishani akafungua na kupanda juu. Alipochungulia kwa nje alibaini yupo juu ghorofa ya saba ya hospitali hiyo.
Inspekta Aron alianza kutembea kutoka dirisha la chumba alichokuwepo akihamia dirisha la chumba kingine kupitia ukuta mdogo uliomuwezesha kukanyaga na kutembea japo kwa tabu sana laiti kama asingelikuwa mtu wa mazoezi hakika angeanguka chini vibaya na kupasuka vipande vipande. Lakini haikuwa hivyo kwa Aron, alitembea kwa umahili mkubwa hadi alipofika dirisha la pili akalifungua na kirukia chumba cha pili. Kwa bahati nzuri mgonjwa wa chumba hicho alikuwa mwenyewe na amelala usingizi. Inspekta Aron alinyata hadi mlangoni akafungua taratibu na kutoka kwa mbali aliwaona wale polisi wakiwa makini kulinda chumba chake bila kujua tayari alikuwa ameshatoka.

"Haya mambo ndio huwa sipendi, ona walivyokaa kizembe" Aliwaza Aron akikumbuka namna alivyokuwa akiwakemea askari wenzake kufanya kazi kizembe namna ile.
Alianza kutembea huku akikatiza korido tofauti tofuauti za hospitali hiyo kubwa, alikuwa akisoma maelezo yaliyokuwa juu katika kila vyumba alivyopita, lengo lake ilikuwa ni kupata chumba alichopo Najma.

"Najma, Najma utakuwa wapi mama angu!!" Aliwaza Inspekta Aron
Akiwa anazidi kuhangaika na shughuli hiyo ambayo ilikuwa ni ngumu kutokana na ukubwa wa hospitali hiyo mara mbele yake aliwaona askari kama sita hivi wakija. Inspekta Aron aligeuka haraka na kuanza kurudi alikotoka akakata kona kulia na kuanza kufuata uelekeo wa korido nyingine ndefu, mara aliwaona tena askari wengine wawili wakija. Inspekta Aron alirudi nyuma haraka na kuzunguuka upande wa pili wa ukuta huo. Sasa akawa katikati kila upande wa pili ambao angeenda askari walikuwa wanakuja. Hakuwa na sehemu nyingine ya kwenda ni ama azunguuke kushoto au azunguuke kulia. Inspekta Aron alijikuta anawaza nini afanye kabla askari wale hawajafika na kumkuta pale lakini alikosa jibu. Sekunde zilizidi kusogea na hatimae vishindo vya askari wakija vilianza kusikika kutoka pande zote mbili.

"Oya Aron shika hapa"
Akiwa katika hali ya kukata tamaa mara alisikia sauti ikimsemesha, akageuka kulia na kushoto hakuona mtu.
"Huku juu" ile sauti ilisikika tena, Aron akainua usowake juu na hapo akaona mtu akiwa ametoa mkono kutoka kwenye uwazi mdogo uliokuwa juu ya dari la hospitali hiyo.
Licha ya kwamba alikuwa hajui mtu huyo ni nani Inspekta Aron aliruka na kuudaka ule mkono akanyanyuliwa juu upesi kisha akajitahidi na kupanda kuingia darini kupitia ule uwazi mdogo baada ya hapo haraka wakafunika mfuniko wa ule uwazi.
Ile wanamaliza tu kufunika mfuniko mara kulia na kushoto wakatokea askari ambao walifika na kusimama pale alipokuwa amesimama Inspekta Aron mwanzoni.

"Jambo afande"
"Jambo afandee"
Walisamiana na kupiga saluti
"Nini kinaendelea?"
"Tayari wamemtoa risasi mtuhumiwa, yupo wodini anapumzika"
"Sawa, hakuna muda wa kupumzika hali sio shwari huko nje wananchi wajaribu kuandamana, Rais kaaigiza mambo yaendele haraka haraka huku itolewe haraka "
Wale askari walizungumza kwa ufupi na mwisho kila mmoja akaelekea upande wake.
Mazungumzo hayo yalipenya moja kwa moja kwenye masikio ya Aron ambaye alikuwa juu yao darini wakati huo. Baada ya askari hao kuondoka ndipo Inspekta Aron aliimtazama yule mtu aliyempa msaada ambao hakuwa ameutalajia.

"Oho! Ni wewe tena? Yaani kila mahali upo?" Inspekta Aron aliuliza kwa mshangao baada ya kumuona yule mtu licha ya kwamba kulikuwa na mwanga hafifu kule juu ila alimtambua kwa namna alivyokuwa amevaa. Huyu alikuwa ni jasusi Shadow na kama kawaida yake alikuwa amevaa mavazi yale yale ya siku zote na kufunika sura yake kwa kitambaa cheusi

"Unataka kufanya nini Aron?" Aliuliza jasusi Shadow
"Kwani umeona nafanya nini?" Inspekta Aron naye akauliza swali badala ya kujibu swali.
"Kwa nini unataka kutoroka, unatoroka uende wapi?"
"Kwani mimi nimesema natoroka, alafu kwanza umekujaje hapa, bado unanifuatilia si ndio au wewe ndio kiongozi wa haya yote yanayonitoke?"
"Sikiliza Aron najua utafika muda utaniamini, nimeshakwambia mimi ni mtu niliyefanya kazi na marehemu baba yako jenerali Phillipo Kasebele, sikia Aron kwa sasa hautakiwi kufanya hivi unavyofanya, namaanisha usitoroke rudi chumbani kwako" Alieleza jasusi Shadow huku Inspekta Aron akimuangalia usoni asimuelewe kabisa.

"Hivi wewe unajikuta nani kwa nini unataka kunipangia kitu cha kufanya?"
"Uliambiwa mara tu utakaposikia au kuliona neno V-COBOS kila kitu kwenye maisha yako kitabadilika na rasmi utaingia kwenye kazi aliyokuwa akiifanya baba yako kwa ajili ya hii nchi sasa basi fuata maelekezo yangu, kila kitu kipo kwenye utaratibu usitoroke mikononi mwa polisi utaharibu mambo"
Inspekta Aron aliimtazama jasusi Shadow kuanzia juu mpaka chini huku akionyesha bado hamwamini.

"Huna haja ya kuficha sura yako tayari nakujua" alisema Aron
"Najua"
"Sasa kama unajua kwa nini umejifunika"
"Usijali sio mda na wewe utaanza kuishi kwa kufunika sura yako kama mimi"
"Alaa! Ni jinsi gani mnataka kunipangia maisha"
"Sio hivyo, alafu muda unazidi kwenda bado kidogo watagundua kuwa umetoroka"
"Mimi sitoroki"
"Ila?"
"Namtafuta Najma ni wapi amelazwa"
"Ni hilo tu?"
"Ndiyo hakuna lingine nataka kuongea naye"
"Haya nifuate"
Alisema jasusi Shadow akafunua ule mfuniko akatoa kichwa chake na kuchungulia chini hakukuwa mtu, akaruka hadi chini sakafuni, Inspekta Aron naye akafanya hivyo.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Najma alikuwa amerejesha fahamu zake alikuwa amelala kitandani huku drip ya maji iliyounganishwa kwenye mashipa wake mkono wa kushoto ikienda taratibu. Najma alionekana amelia sana, tayari alikuwa amempoteza baba yake mzazi aliyeuawa kikatili kwa kupigwa risasi mbele ya macho yake. Mbaya zaidi anaamini aliyemliga risasi ni Inspekta Aron mwanaume ambaye tayari alikuwa ameanza kumteka kihisia.
Akiwa bado kwenye dimbwi la mawazo mara mlango wa chumba chake ulifungua akaingia mwanaume ambaye hakuwa ametegema kumuona kwa wakati huo.
"Osward" Najma aliita
"Mpenzi wangu" Alijibu Osward huku akifunga mlango na kuanza kumfuata Najma pale kitandani. Kwa namna sura yake ilivyokuwa ikitia huruma usinge amini kama huyu ndiye haswa muuaji wa baba yake Najma yaani Dokta Gondwe tofauti na watu wengi walivyokuwa wakiamini kuwa Inspekta Aron ndiye muuaji.

ITAENDELEA...
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu..............47
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
"Osward" Najma aliita
"Mpenzi wangu" Alijibu Osward huku akifunga mlango na kuanza kumfuata Najma pale kitandani. Kwa namna sura yake ilivyokuwa ikitia huruma usingeamini kama huyu ndiye haswa muuaji wa baba yake Najma yaani Dokta Gondwe tofauti na watu wengi walivyokuwa wakiamini kuwa Inspekta Aron ndiye muuaji.

SASA ENDELEA...
"Pole sana Najma wangu, wamemuua mzee kikatili sana. Tangu siku ya kwanza nilipokuona ukiwa na yule Inspekta Aron karibu nilijua tu lazima kitu kibaya kitatokea, alianza kumuandama baba yako tangu mda mrefu sana" aliongea Osward huku akipiga hatua taratibu na kukaa pembeni ya kitanda alicholazwa Najma. Kauli ya Osward ilimfanya Najma kuongeza kasi ya kulia bila kutoa sauti huku safari hii machozi yakimtiririka kwa kasi kama maji.
Osward alimshika Najma mkono akijaribu kumfariji.
"Usilie mpenzi wangu, jikaze mimi nipo kwa ajili yako nitahakikisha namuadabisha Aron pamoja na watu wote waliopo nyuma yake, hukumu ya serikali mahakamani haitokuwa adhabu pekee kwake nitahakikisha nalipa kisasi kwa ajili yako, nitamuua kifo kibaya mno, atateseka sana kabla ya kufa. Kifo chake kitakuwa ni funzo kwa watu wengine waovu wenye tabia za kikatili kama zake" Osward alikuwa akiongea mfululizo pasipo kupumzika ili tu kumfanya Najma azidi kujenga imani na yeye. Ukweli Osward alikuwa akimpenda sana Najma na moja kati ya vitu alivyokuwa ameahidiwa na Mheshimiwa Rais mstaafu Profesa Cosmas Kulolwa ni kwamba atahakikisha anamuoa. Hii ilikuwa ni moja kati ya ahadi iliyomshawishi sana Osward kukubali kumuua Dokta Isaack Gondwe ambaye ni baba mzazi wa Najma.
"Osward" Najma aliita
"Nambie mpenzi wangu"
"Unadhani ni kwa nini Aron kamuua baba yangu? Kwa nini kafanya hivyo? Niambie ukweli je kifo cha baba kinahusiana na lile suala la virusi vya V-COBOS kutoka Mexico?" Najma aliuliza swali hali machozi yakiwa bado yanamtililika. Swali hili lilimshtua sana Osward lakini alijikaza kutoonyesha mshtuko wake.

"Hapana wala hayahusiani, Inspekta Aron kamuua baba yako kwa chuki zake binafsi alikuwa anamchukia sana baba yako tangu mda mrefu sana" Osward alizidi kudanganya kiasi cha kusababisha Najma kuanza kulia kwa kwikwi na mwisho akaanza kukohoa mfululizo.
"Pole pole mpenzi, ngoja nikupe maji...mmh! Hamna maji humu ndani..? Subiri nakuja" Alisema Osward baada ya kutafuta maji na kuyakosa aliinuka akapiga hatua na kutoka nje ya kile chumba.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Inspekta Aron alikuwa nyuma akimfuata jasusi Shadow ambaye alikuwa mbele akimuongoza kuelekea kilipo chumba alicholazwa Najma. Inspekta Aron alitamani sana kuonana na Najma angalau angepata amani ya moyo kama angezungumza naye hata kwa uchache kumueleza kuwa si yeye aliyemuua baba yake.
Wakiwa wamebakiza hatua chache kukifikia chumba alicholazwa Najma mara Jasusi shadow alirudi nyuma ghafula na kujibana ukutani. Inspekta Aron naye akafanya hivyo pia.

"Nini?" Aliuliza Aron
"Kuna mtu anakuja, anaelekea chumba cha Najma" alieleza Shadow, Inspekta Aron akasogeza kichwa chake kuchungulia
"Rudi huko unafanya nini wewe?"
"Kwa hiyo hutaki na mimi nione au?"
"Sasa utaonaje nimekwambia kuna mtu vipi kama ukionekana?"
"Basi rudi niache niende mwenyewe kwa Najma"
"Uende wapi bila mimi ungekijua chumba gani alipo?"
"Kwa hiyo unataka nikushukuru?"
"Punguza sauti jamaa anakaribia"
"Sawa, sogea basi na mimi nione"
"Haya pita taratibu, ona unanikanyaga mwanangu"
"Polee"
Yalikuwa ni maongezi kati ya Jasusi shadow na Inspekta Aron ambao taratibu walionekana kuanza kuzoeana na kuendana kitabia. Wote kwa pamoja walikuwa wakichungulia upande wa pili ndipo walipomuona Osward akiingia ndani ya chumba alicholazwa Najma.

"Ni Osward" alisema Inspekta Aron huku akionyesha mshangao
"Ndio ni yeye ameshinda kesi yake mahakamani"
"Kwa nini hukuniambia sasa?"
"Kwani uliniuliza?"
"Mbona vingine unaniambia hata kabla sijakuliza"
"Sawa, vipi ningekwambia ungeniamini?"
Inspekta Aron akawa kimya
" Sikiliza Aron inatakiwa urudi chumbani kwako ukatulie kabla hawajagundua kama umetoroka, kwanza mguu wako unajeraha la risasi pili usiku wa leo tuna kazi ya kufanya na wewe"
"Mnakazi ya kufanya wewe na nini? Wapi? Saa ngapi?"
" Kuwa na subira utanielewa"
"Unajua kwa nini sikuelewi, unaongea vitu nusu nusu mara baba yangu mara V-COBOS mara nisitoroke mara leo usiku kuna kazi sasa hata ungekuwa wewe ungeelewa hebu ku....." Aliongea Inspekta Aron lakini kabla hajamalizia sentesi yake Shadow akamziba mdomo

"Shiiii...nyamaza Osward anatoka"
"Safi, ngoja basi niende"
"Wapi? Vipi kama akirudi utaharibu mambo Aron"
"Hawezi kurudi"
"Wewe umejuaje"
"Bana najua hebu nipishe basi" Inspekta Aron aliongea kwa ukali kidogo safari hii kisha akaanza kupiga hatua kuelekea kilipo chumba alicholazwa Najma.
Jasusi shadow alibaki akimsindikiza kwa macho huku akiwa makini kuangalia pande zote kama kuna mtu yeyote anakuja. Aliamini kwa namna Osward alivyotoka anakimbia ilikuwa ni ishara kuwa angerudi si muda mrefu. Ni kweli Osward alikuwa ametoka kwenda kumtafutia Najma maji ya kunywa.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Inspekta Aron alifungua mlango taratibu na kuingia ndani kisha akaufunga, Najma akiwa kitandani aliinua uso wake taratibu akiamini Osward karudi lakini alishangaa kumuona mtu mwingine tofauti. Aliingia mtu ambaye hakuwa ametegema kumuona kwa wakati huo.

"Najma" Inspekta Aron aliita huku akisogea karibu na kukaa kwenye pembe moja ya kitanda miguu kwa Najma ambaye hadi dakika hii alikuwa kimya akimtazama Aron muuaji wa baba yake.
"Sikiliza Najma nimekuja ha..."
"Umekuja kuniua na mimi si ndio?"
"Hapana sio hivyo Najma mimi sio muuaji sijamuua baba yako, naapa kwa jina la mwenyezi Mungu sijamuua baba yako Najma"
"Aron inuka hapo na uondoke, niache niomboleze kifo cha baba yangu kwa amani, umeshafanikisha jambo ulilolitaka kwa nini unakuja tena kunisumbua mmm! Kwa nini Aron" Najma aliongea kwa uchungu machozi yakimtililika.
"Najma nimekuja kuongea na wewe najua nitafungwa pengine hata kuhukumiwa kunyongwa lakini nataka ujue sikumuua baba yako mimi sio muuaji unanijua vizuri Naj..."
"Nakujua? Nakujua vipi Aron? Tangu lini nikakujua wewe? Sikia Aron ninaye mjua ni yule aliyetengeneza urafiki na mimi kwa makusudi ili apate mwanya wa kumpeleleza baba yangu na mwisho ayaondoe maisha yake, Aron nilikushuhudia mwenyewe kwa macho yangu wala sijahadithiwa mimi mwenyewe nilikuona ukifyatua risasi na kumuua baba sasa unawezaje kusimama kwa ujasiri mbele yangu kisha unasema hujamuua baba? Unawezaje Aron? Humuogopi hata Mungu..." Najma aliongea akilia.
"Najma huu ni mchezo nimechezewa kisha nikapewa kesi hii ya mauaji ambayo sijayafanya, mimi sikuwa adui wa baba yako huu ni mchezo Najma. Je uliiona sura yangu wakati nampiga risasi baba yako?"
Najma akawa kimya
"Nakuliza uliiona sura yangu Najma?"
"Sikuiona lakini ni wewe uliyekimbizwa na mwisho ukakamatwa na polisi unataka kusema nini sasa eee!!" Najma alipayuka.
"Ni hilo tu? Hilo linatosha kuthibitisha kuwa ni mimi ndiye niliyefyatua risasi kumuua baba yako? Sikiliza Najma unamjua baba yako alikuwa mtu wa aina gani, unajua shughuli alizokuwa akizifanya nje na kuwa waziri wa afya, simsemi vibaya marehemu lakini na wewe usijaribu kukataa ukweli, baba yako alikuwa na maadui wakubwa na sio mimi Najma, siwezi na sijawahi kufikiria kuua, SIJAMUUA BABA YAKO" Aron aliongea kwa msisitizo
Najma alitulia kimya hali akishangazwa na namna Aron anavyoongea kwa ujasiri mkubwa kuukana ule alioamini ni ukweli.
"Anawezaje kukataa kitu ambacho alishuhudia kwa macho yangu anakifanya na mwisho akakamatwa, eeh! Mungu nipe ujasiri, nisaidi niomboleze msiba wa baba yangu kwa amani" Najma aliwaza akiwa ameinamisha uso wake chini huku machozi.

"Unataka kimjua mtu aliyemuua baba yako?"
Aliuliza Inspekta Aron huku akimtazama Najma kwa macho yaliyojaa huruma.

"Nakuuliza unataka kumju......" Aron alisita kumalizia kuongea mara baada ya kusikia mlango ukifunguliwa akageuka kutazama ni nani anayeingia. Uso kwa uso akagonganisha macho yake na macho ya Osward ambaye naye alibaki katika hali ya mshangao hakutegemea kumkuta Inspekta Aron mle ndani.
Wakati huo ving'ora na kengele zinazoashiria hatari zialianza kusikia katika kona zote za hospitali hiyo. Tayari polisi walishagundua kuwa Inspekta Aron katoroka.
ITAENDELEA....
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya..........48
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Inspekta Aron aligeuka nyuma uso kwa uso akagonganisha macho yake na macho ya Osward ambaye naye alibaki katika hali ya mshangao hakutegemea kumkuta Inspekta Aron mle ndani.
Wakati huo ving'ora na kengele zinazoashiria hatari zilianza kusikia katika kona zote za hospitali ya Mountenia. Tayari polisi walishagundua kuwa Inspekta Aron katoroka...

SASA ENDELEA...
"Ni wewe? Umefuata nini humu? Unataka kutoroka?" Osward aliuliza maswali mfululizo akimtazama Inspekta Aron kwa macho yenye hofu kiasi, Inspekta Aron akawa kimya hakujibu chochote. Osward akageuka upande wa pili na kumtazama Najma.
"Najma kakuambia nini huyu? Alichokisema ni uongo, mimi sijamuua baba yako wala usijaribu kumwamini" Osward alizidi kupayuka kauli iliyomfanya Najma amuangalie kwa mshtuko. Wala Inspekta Aron hakuwa ameeleza chochote juu ya Osward kuhusika na mauaji ya Dokta Gondwe baba yake Najma, Osward aliongea kwa papara akiamini huenda Inspekta Aron ameshamwambia Najma ukweli wote.

"Unasema nini Osward? Kivipi wewe tena ndio umuue baba yangu?" Najma aliuliza akimtazama Osward kwa macho ya kuuliza, Osward akawa kimya kwa muda kisha akaongea.

"Aa..ni..nilikuwa na maanisha huenda .. Aron akasema mi..mimi ndio.." Osward aliongea kwa kujiumauma lakini kabla hajamalizia sentesi yake Aron akadakia

"Sikiliza Najma mimi nimekwa..." Alisema Aron lakini Osward hakutaka kumpa mwanya azungumze, tayari alishagundua kuwa Najma hajaambiwa chochote.
"Kaa kimya wewe muuaji mkubwa nimesema kaa kimyaaaa...." Osward alifoka huku akipiga hatua kumfua Aron kwa kasi akiwa amekunja ngumi yake ya kulia. Alipofika karibu na Aron alirusha ngumi hiyo kwa kasi lakini tayari Aron alishajiandaa, akainama chini haraka ile ngumu ikapita juu yake kama upepo na hapo Aron akiwa bado ameinama alimsindilia Osward ngumi kali tumboni.

"Aaaighiiiiii...." Osward alipiga kelele za maumivu akashika tumbo lake akawa anainama chini taratibu lakini ghafula akasindiliwa ngumu nyingine iliyotua vizuri kwenye taya yake upande wa kushoto, ilikuwa ni ngumi kali sana ikiyompeleka moja kwa moja mpaka chini.

"Unaji...ji..fanya bondia...leo nitaku...kuonyesha" Aliongea Osward huku akijizoazoa pale chini kujaribu kusimama lakini hakuwa na nguvu za kutosha zile ngumi mbili alizopigwa zilikuwa zimetosha kabisa kumdhoofisha. Inspekta Aron alimsogelea na kuchuchumaa pembeni yake, akaongea kwa sauti ya chini ambayo Najma hakuweza kusikia.

"Sikia wewe mwanaharamu hata siku moja haki ya mnyonge huwa haipotei BALI INACHELEWESHWA TU, sio mda maovu yako yote yatafahamika wala mimi sijamweleza Najma chochote. Muda sahihi ukifika ataujua uchafu wako wote. Kunipa mimi kesi ya mauaji ya Dokta Gondwe sio kwamba umemaliza kila kitu ila huu ni mwanzo mpya wa kupambana na mimi nitarudi tena kwako na kamwe hautopata furaha maishani mwako kama mimi nitaendelea kuwa hai Osward" Inspekta Aron aliongea kwa kujiamini kisha akasimama na kupiga hatua kusogea karibu na Najma ambaye wakati wote alikuwa kimya akishuhudia vidume hao wawili wakifuana kiume mbele yake.

"Narudia tena sikumuua baba yako, muuaji wa baba yako huenda yupo karibu na wewe na hujui, kuwa makini Najma.." baada ya kusema hayo Inspekta Aron alifungua mlango na kuondoka
[emoji294][emoji294][emoji294]
Polisi walikuwa wamechachamaa huku wakiwa wametapakaa pande zote za hospitali ya Mountenia wakihangaika kumtafuta Inspekta Aron bila mafanikio. Zilikuwa zimepita dakika kama sita tangu walipogundua kuwa Inspekta Aron ametoroka hayupo chumba alichopumzishwa.

"Huu ni uzembe ni uzembe mkubwa umefanyika mlikuwa wapi? Tutaeleza nini kwa wananchi?" Polisi mmoja ambaye alionekana kuwa na cheo kikubwa kuliko wenzake alikuwa akiwafokea polisi wengine sita nje ya mlango wa chumba alichokuwa amepumzishwa Inspekta Aron.

"Yaani mtu anafungua pingu anainuka, anapanda dirishani anatoka nyie mpo tu mmesimama hapa mlangoni kama kama nguzo hivi ha..ha..hamu...!!" Alifoka yule polisi lakini mara alishindwa kumalizia sentesi yake baada ya kuona kitu cha ajabu mbele yake. Polisi wengine walishangaa kuona mkuu wao ameacha kufoka ghafula, wote wakageuka na kuelekeza macho yao upande ule alikogeukia.
Nao hawakuamini macho yao baada ya kumuona Inspekta Aron kwa mbali akija taratibu tena akitembea kwa kujiamini sana bila wasiwasi.
Ndiyo, Inspekta Aron hakuwa na mpango wa kutoroka kama alivyosema awali, baada ya kufanikisha kuongea na Najma angalau moyo wake ulitulia aliamua kurudi tena mikononi mwa polisi.
Wakati akipiga hatua kusogea Inspekta Aron aligeuka pembeni yake kwa mbali akamuona Jasusi shadow akiwa amesimama kwenye ngazi anamtazama. Baada ya kukutanisha macho yao Jasusi shadow aliweka mkono wa kulia kichwani akapiga saluti ya heshima Inspekta Aron aliinamisha kichwa kuipokea saluti ile. Mara Jajusi Shadow akapotea kama upepo, hakuna polisi aliyemuona wala kuelewa chochote.
Dakika moja baadae Inspekta Aron alifika akasimama mbele ya wale polisi ambao hadi dakika hiyo walikuwa bado hawaamini macho yao. Alinyoosha mikono yake mbele na kuiunganisha ikiwa ni ishara kuwa anataka kufungwa pingu. Wale polisi walitazamana kwa sekunde kadhaa na mwisho mkuu wao alitoa ishara kuwa wamfunge pingu, wakafanya hivyo.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Tino na Bosco waliokuwa ndani ya chumba kimoja katika kambi kuu ya siri iliyokuwa ikimilikiwa na marehemu Dokta Gondwe. Hiki kilikuwa ni chumba ambacho ilikuwa ni ofisi kuu ya Dokta Gondwe aliyokuwa akiitumia kufanya vikao na kutunza siri zake nyingi sana. Tino na Bosco walikuwa ndani ya chumba hicho kwa zaidi ya masaa mawili wakijaribu kupekua na kuangalia nyaraka mbalimbali za siri za marehemu.

"Ooops! Inatosha sasa kijana wangu, angalau tumepata sehemu ya kuanzia" alisema Tino huku akionekana kuchoka sana
"Ni kweli bosi, sasa ni kazi kazi lazima virusi vya V-COBOS tuvipate" alijibu Bosco
"Hakika, hawa watu wanaonekana wanatumia akili kubwa sana kwa namna walivyocheza huu mchezo ni wazi kuwa tunahitaji nguvu na akili ya ziada vilevile"
" Kwa hiyo tunaanzia wapi bosi?"
"Tutaanza na Osward ili tujue anafanya kazi na nani kati ya Rais mstaafu Profesa Cosmas Kulolwa au Mkemia mkuu wa serikali Andiwelo katabi maana hawa watu wanaishi kwa kugeukana aliyemuagiza Osward amuue Dokta Gondwe ndio atakuwa target yetu ya kwanza maana yeye alitambua kuwa Dokta Gondwe anakaribia kuvileta virusi vya V-COBOS kwetu ndio maana akamuagiza Osward amuue kwa faida ya kumtoa gerezani na kisha kumkamata mdogo wangu Aron. Kuna akili kubwa sana imetumika hapa" Tino alieleza kila kitu kwa uhalisia wake kama ilivyokuwa, masaa mawili waliyokaa kwenye ofisi ya marehemu Dokta Gondwe yalitosha kuwafanya wazijue siri nyingi sana.
"Kwa hiyo kumuua Dokta Gondwe na kumpa kesi ya mauaji Aron malipo yake ni kusaidiwa kutoka gerezani?"
"Yes, bila shaka iko hivyo.. kwa sasa Osward atakuwa ni chawa wa Cosmas Kulolwa au Andiwelo katabi"
Wakiwa kwenye mazungumzo hayo mara mlango uligongwa na kisha kufunguliwa akaingia kijana mmoja akiwa na bunduki mkononi mwake.

"Mkuu watu wote wameshakusanyika kama ulivyoagiza" alisema yule kijana
"Sawa nakuja" Tino alijibu kifupi.
Baada ya hapo alisimama akavaa koti lake na kuweka tai yake sawa kisha akatoka huku Bosco akimfuata nyuma taratibu.
Tino alikuwa amesimama kwenye varanda moja juu ghorofa ya kwanza huku watu zaidi ya 30 walionekana kuwa vikosi tofauti tofuauti wenye siraha mkononi wakiwa wamesimama chini na kupanga mistari miwili. Moja ya kikosi kilichokuwepo miongoni mwa vikosi hivyo ni Kunguru weusi kikosi hatari kuliko vyote kinachotumia siraha kali ikiwa ni pamoja na bunduki aina ya SAR 109T zinazotoa miale yenye rangi nyekundu.
Tino alitazama chini kuwakagua vijana hawa ambao awali walikuwa wakifanya kazi chini ya marehemu Dokta Gondwe na yeye akiwa kama kiongozi wao, akaongea....

"Najua mmeumizwa sana na kifo cha mkuu wetu Dokta Gondwe, ni kifo ambacho hatukikitegemea kabisa lakini ndio hivyo mzee wetu ametutoka. Nimewaita hapa ili kuwaelezeni hatima yenu. Ndugu zangu hakuna kitu kilicho haribika, kuanzia leo mimi Tino nilikuwa kamanda wenu nitaendelea kuwa Kamanda wenu lakini pia nitakuwa mkuu wenu, nafasi ya Dokta Gondwe kuanzia sasa nitaishikilia mimi, mimi ndio mkuu wenu kwanzia sasa" Tino aliongea kwa sauti kubwa iliyojaa mamlaka.

"NDIO MKUUU" Vijana wote waliitika wakapiga goti moja chini na kuinamisha vichwa vyao, hii ikiwa ni ishara tosha kuwa wamekubali kwa moyo mweupe kile alichokisema Tino, walimkubali sana.
"Moto wetu utakuwa ni uleule, lengo letu ni lile lile tutafanya kila kitu tutakachoamua kufanya, hakuna mtu atatuzuia, tutasafisha kila uchafu utakao jitokeza mbele yetu. Tukiamua tunaweza hata kuingia hata Ikulu tukaipindua nchi na kuitawala, mimi Tino nitafanya kazi kwa ukaribu sana na ninyi kama nilivyofanya na Kikosi cha Kunguru weusi kama nilivyofanya kwa Sniper G na wenzake nitaendelea kuwa hivyo siku zote. Kwanzia leo mishahara yenu itakuwa mara mbili ya ile mliyokuwa mkilipwa mwanzo.
Tino alimaliza kuongea vijana wote wakalipuka kwa kelele za shangwee...

NUSU SAA BAADAE...
Tino na Bosco waliendelea na mazungumzo ndani ya ile ofisi waliyokuwepo mwanzo.
"Umeongea vizuri sana bosi" alisema Bosco
"Yes! inabidi niwateke mioyo yao ili wafanye kazi kwa uaminifu na kujituma, sasa niwakati wangu wa kuanza mapambano nguvu yote nitaelekeza kwenye zoezi la kuhakikisha navipata vimelea vya V-COBOS, najua itakuwa ni vita kali tena ngumu sana kwa sababu napambana na watu wakubwa nchini na wengine kutoka nchi za nje lakini najiamini mimi na vikosi vyangu lazima TUTASHINDA HII VITA" Aliongea Tino
"Vipi kuhusu mimi, vijana wamesemaje unakumbuka mara ya kwanza wao waliniteka wakanileta hapa?"
"Yes kila kitu kipo sawa uliondoka hapa kwa heshima tena ulisindikizwa na dereva wao, nimewambia tayari ulikuwa kitu kimoja na marehemu" Alieleza Tino
[emoji294][emoji294][emoji294]

Upande wa pili katika hospitali ya kimataifa ya Mountenia Madam Sultana mama wa Inspekta Aron na Tino alikuwa amesimama dirishani ndani ya chumba chake ambacho sikuzote huwa amelazwa akijifanya mgonjwa mahututi. Alikuwa akitazama nje kupitia kioo cha dirisha huku akionekana kuzama kwenye dimbwi la mawazo.

"Hii vita ni kali sana, inabidi niongeze nguvu. Sidhani kama Jasusi shadow atafanikiwa huenda akaanza kunizunguuka baada ya kutambua mipango yangu ni tofauti na mipango ya marehemu mume wangu. Siwezi kuendelea kukaa na kubweteka eti kwa sababu mimi ndio najua chupa yenye kinga na dawa ya vimelea vya V-COBOS ilipo hapana inabidi nifanye kitu, kifo cha Dokta Gondwe ni ishara tosha kuwa vita sio ya kitoto huko nje, sijui mwanangu asiye na akili Tino anawaza kufanya nini? Sijui wale watu waliokuwa wanashirikiana na Dokta Gondwe watafanya nini? Amka Sultana amka upambane" Aliwaza Madam Sultana

je nini kitafuata?
Nini hatima ya Inspekta Aron mikononi wa polisi?
Vipi kuhusu Najma na Osward?
Timu ya ZMLST itafanya nini?
Annah yuko wapi?

ITAENDELEA...


0756862047
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya.........49
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA....
Baada ya Inspekta Aron kufanikiwa kuonana na Najma kisha kumwambia ukweli kuwa hausiki na mauaji ya baba yake Dokta Gondwe anarudi tena na kujikamatisha mikononi mwa polisi. Upande wa pili Tino kaka yake Inspekta Aron anajipa uongozi na kuchukua utawala kwa vikosi vyote vilivyokuwa vikimilikiwa na marehemu Dokta Gondwe. Kazi yake ya kwanza inakuwa ni kuviwinda virusi vya V-COBOS. Wakati huo Sultana naye anaanza kujenga mipango mipya baada ya kuhisi Jajusi Shadow anamzunguuka.


SASA ENDELEA...
Ilikuwa ni majira ya saa tatu na robo usiku, Inspekta Aron alikuwa amejikunyata kwenye kona ndani ya chumba kimoja kidogo sana(rumande), humo ndimo alimokuwa amefungiwa mara baada ya kutolewa hospitali. Kwa kuwa muda ulikuwa umekwenda na mtuhumiwa alikuwa ni mgonjwa polisi walishauriana kuendelea na taratibu nyingine siku inayofuata ikiwa ni pamoja na kumuhoji kiundani Inspekta Aron kujua ni nini hasa sababu iliyomfanya aamue kumuua mtu mkubwa serikalini yaani waziri wa afya Dokta Isaack Gondwe kwa kumpiga risasi. Macho na masikio ya watu wengi yalikuwa yakifuatilia kiundani taarifa hii ambayo iliteka vichwa vya habari katika vyombo vyote vya matangazo.
Inspekta Aron alikuwa akiwaza ni namna gani ataweza kujiokoa dhidi ya tuhuma hizo ambazo hazikuwa na ukweli ndani yake. Alitegemea pengine Inspekta Jada angejitokeza angalau kumpa maneno ya faraja kuwa angeweza kufanya chochote kumsaida lakini haikuwa hivyo Jada hakuwa ameonekana hadi dakika hiyo. Kesi iliyokuwa mbele yake ilikuwa ni ngumu tena ngumu mno na hukumu yake ilikuwa ni ama kunyongwa au kifungo cha maisha na si vinginevyo. Kila alipowaza hivyo Inspekta Aron alikosa amani kabisa akajikuta anamkumbuka Jasusi Shadow licha ya kwamba alikuwa hamuamini lakini taratibu alijikuta anaanza kuutamani msaada wake.
........Sikiliza Aron inatakiwa urudi chumbani kwako ukatulie kabla hawajagundua kama umetoroka, kwanza mguu wako unajeraha la risasi pili usiku wa leo tuna kazi ya kufanya na wewe.........
Inspekta Aron aliyakumbuka maneno haya aliyoambiwa na Jasusi Shadow wakati ule wakiwa hospitali.

"Kwani usiku ni kuanzia saa ngapi, mbona huyu jamaa hatokei" Inspekta Aron alijikuta akijisemea mwenyewe.
Haukupita muda Aron alisikia vishindo vya mtu akija, sekunde chache baadae aliona sahani ya chakula ikisukumwa kutokea nje kupitia kijinafasi kidogo kilichokuwa chini ya mlango wa chuma wa chumba hicho. Inspekta Aron alikitazama kile chakula ilikuwa ni mkate na chai isiyoungwa. Alitamani kuachana nacho lakini kwa njaa kali aliyokuwa nayo Inspekta Aron aliisogeza ile sahani karibu kisha akachukua kipande cha mkate na kukimega akaanza kula.
Katika hali ambayo hakuitegemea Inspekta Aron aliona karatasi likidondoka kutoka kwenye ule mkate mara tu baada ya kuumega. Aron aliduwaa kwa sekunde kadhaa kisha akaweka mkate pembeni akaokota lile karatasi akalikunjua. Kulikuwa na maandishi lakini pia chini ya maandishi hayo kulikuwa na nembo moja yenye alama ya Nyoka kajiviringisha kwenye mshale. Alama hii haikuwa ngeni machoni kwa Inspekta Aron, aliijua ni alama aliyopenda kuitumia marehemu baba yake. Hata ile nyumba ya siri msituni ilikuwa na sanamu kubwa lenye nembo kama hiyo. Kwa ufupi ilikuwa ni alama inayotumika katika harakati mbalimbali za siri alizokuwa akizifanya marehemu baba yake jenerali Phillipo Kasebele. Ingawa Inspekta Aron alikuwa hatambui harakati hizo ki undani lakini alikuwa akiifahamu vyema alama hiyo. Haraka alianza kusoma kile kilichokuwa kimeandikwa kwenye karatasi kwa makini.

,,,,Tunajua kwamba haujamuua waziri wa afya, tulitamani kukusaidia lakini ni ngumu kuthibitisha ukweli huu. Kitu pekee tunachoweza kufanya kukuokoa dhidi ya hukumu mbaya iliyopo mbele yako ni kukufanya uzaliwe upya na kuwa mmoja wetu. Kwenye huu mkate kuna vidonge wivili utavimeza na baada ya dakika nne mapigo yako ya moyo yatasimama kwa masaa matatu mfululizo baada ya watu kuamini kuwa umekufa sisi tutakuja na kukuchukua kisha tutakupa dawa nyingine ambayo itakurejesha katika hali ya kawaida. Utaanza maisha mapya pamoja na sisi huku Dunia nzima ikiamini kwamba umekufa. Njoo uikamilishe kazi ambayo aliianzisha marehemu baba yako, usiogope kila kitu kitakwenda sawa tuko nyuma yako kwa kila hatua, meza hivyo vidonge ifikapo asubuhi ya saa kumi na mbili unusu, itakuwa nusu saa kabla hawajaja kukuchukua watakuta tayari hujitambui hata wakifanya vipimo wataamini umekufa. Masaa mawili na nusu yatakayobaki yatakuwa ya sisi kufanya kazi yetu,,,,,
Inspekta Aron alimaliza kuusoma ujumbe huo kisha haraka akachukua tena mkate na kuukatakata hapo akaona mfuko mdogo sana wa nailoni ukiwa na vidonge viwili ndani yake vyenye rangi ya manjano.
Inspekta Aron aliduwaa kwa muda kisha akarudia tena kuyasoma yale maelezo.
"Hii inawezekanaje, hawa ni akina nani? Mbona kuna alama aliyokuwa akiitumia baba yangu hapa chini?" Inspekta Aron alikuwa akijiuliza maswali yasiyo na majibu huku akivitazama vile vidonge.

MASAA MAWILI YALIYOPITA-IKULU
Turudi nyuma masaa mawili yaliyopita. Hapa ni Ikulu, ndiyo ilikuwa ni ikulu nyumba anayoishi Mheshimiwa Rais Dkt Alfredo Zabron Zumo huyu ndiye aliyempokea madaraka ya Urais Mheshimiwa Profesa Cosmas Kulolwa baada ya kumaliza utawala wake wa miaka 10.
Dkt Alfredo Zumo Rais kijana kuwahi kutokea katika historia aliingia madarakani akiwa na umri wa miaka 36 pekee kwa kumbwaga mpizani wake akimzidi kula nyingi sana.
Watu wapatao watatu walionekana wakiwa kwenye moja kati ya vyumba vya siri sana ndani ya Ikulu hiyo chumba ambacho kilikuwa chini ya ardhi liliposimama jengo la ikulu. Watu hao walikuwa wamefunika nyuso zao kwa vitambaa maalumu na kuacha sehemu ya macho pekee huku wakiwa wamevaa mavazi meusi ikiwa ni pamoja na vazi maalumu la kuzuia Risasi(bullet proof). Chini walivaa buti kubwa nyesusi zilizokalibia kufika kwenye magoti yao huku miili yao ikionekana kujengeka vizuri kutokana na mazoezi makali wanayoyafanya.
Mlango wa chumba hicho ulifunguliwa akaingia Rais Dkt Alfredo Zumo akatembea na kwenda kukaa kwenye kiti cha mbele akiifanya idadi ya watu waliokuwa ndani ya chumba hicho kuongezeka na kuwa wanne. Wale watu walisimama kwa heshima kubwa mara baada ya Rais kuingia kisha wakakaa kwenye sehemu zao mara baada ya Rais kukaa.

"Mmefikia wapi?" Aliuliza Dkt Alfredo Zumo
"Mheshimiwa bado hatujafikia muafaka kila mtu anahofu, njia uliyopendekeza inaweza kuyaweka maisha ya Inspekta Aron hatarini badala ya kumsaidia tukampoteza" alijibu mmoja wa wale watu waliofunika nyuso zao.
"Nafikiri tangu mwanzo mlinielewa niliposema hakuna njia nyingine ya kumsaidia Inspekta Aron tofauti na hii, ili awe mmoja wetu ni lazima Dunia iamini kuwa amekufa, lazima afe kwanza ndio awe na sisi" alisisitiza Rais.
"Ni kweli mheshimiwa lakini hata Daktari ameshauri kuwa kama kuna njia nyingine tofauti basi itumike, ila hii njia ya kumeza vidonge vitakavyosimamisha mapigo yake ya moyo ni 50 kwa 50 huenda Inspekta Aron akafa au akapona" Alieleza mwanamke mmoja kati ya wale watu watatu.
"Tuliapa kufa kwa ajili ya wengine, kifo cha mtu wetu mmoja kinaokoa maisha wengine elfu moja naomba niwakumbushe hilo. Tutafanya kama tulivyopanga naomba kuufunga mjadala huu na sasa kila mtu arudi kwenye majukumu yake" Aliongea Rais kwa sauti kubwa iliyojaa mamlaka.

Wale watu watatu waliinamisha vichwa vyao kwa heshima kubwa kisha wakasimama na kuanza kuondoka.

"Shadow utabaki mara moja nina mazungumzo na wewe" Alisema Mheshimiwa Rais.
Mmoja kati ya wale watu alisimama huku wengine wakiingia kwenye lifti maalumu ambayo iliruhusu mtu mmoja tu kuingia kila mmoja akaingai kwenye lifti yake, baada ya muda kila mmoja alionekana akitokea kwenye chumba tofauti tofuauti ndani ya Ikulu.
Ukuta ulikuwa ukifunguka akishuka unajifunga tena, haikuwa rahisi kwa mtu asiyejua kutambua kuwa mahali hapo palikuwa na ukuta unaofunguka na kujifunga, sasa kila mmoja alikuwa katika ofisi yake ndani ya jengo la Ikulu.

Yule mmoja aliyebaki na Rais ndani ya kile chumba cha siri alivua kitambaa kinachoficha sura yake, amini usiamini alikuwa ni Jasusi Shadow yule jasusi mashuhuri anayefanya kazi chini ya Sultana.

"Mheshimiwa ni kweli umedhamilia kufanya hivyo?"aliuliza Jasusi Shadow huku akimuangalia Rais usoni.
"Huwezi kuamini shadow hata mimi naogopa sana nimejikaza tu ninahofu tunaweza kumpoteza kijana wetu mtoto wa rafiki yangu kipenzi. Kama Aron atakufa basi sitokuwa na amani maisha yangu yote. Nilimuahidi vitu vingi sana baba yake jenerali Phillipo Kasebele kabla ya kifo chake ikiwa ni pamoja na kuhakikisha namlinda mwanae" Alisema Mheshimiwa Rais.
"Sasa tunafanyaje Mheshimiwa, kwa nini tusihailishe mpango huu wewe ukafanya jitahada nyingine za kumnusuru Inspekta Aron"
"Ni ngumu sana Shadow, mimi ni Rais sawa lakini nipo kama sipo nimekaa kwenye kiti ambacho napangiwa kitu cha kufanya. Kama nikijaribu kuingilia kesi ya Inspekta Aron nitaulizwa maswali mengi yasiyo na majibu. Ndio maana nawatumia ninyi kurekebisha mambo ambayo naona hayaendi kwenye hii nchi. Ona polisi ninao wanasheji ninao lakini siwezi kuwatumia badala yake nawatumia ninyi kuendesha hii serikali na bila ninyi hii nchi ingekuwa ishauzwa kitambo sana, tunapandana kuzuia mipango yao mingi bila wako kujua. Hata kuhusu hii vita ya vimelea vya V-COBOS iliyoanzishwa na baba yake Aron nitawazuia kwa kuwatumia ninyi bila wao kujua kuwa mimi nahusika" Alisema Mheshimiwa Rais.

"Lakini inakuwaje Rais mstaafu anakuwa na nguvu kuliko wewe uliepo madarakani Mheshimiwa?"
"Kijana wangu hii nchi inasiasa ngumu sana, kama katiba ingekuwa inaruhusu Profesa Cosmas Kulolwa angeendelea kuwa Rais milele, aliachia madaraka kwa sababu alibanwa na Katiba tu lakini hivi sasa bado anaendesha kila kitu mimi nipo kama Rais kimvuli. Isingekuwa kulazimishwa na baba yake Aron namaanisha jenerali Phillipo Kasebele nisingekubali katu kugombea kiti hiki cha Urais ila mzee alinitaka nifanye hivyo"
"Nalijua hilo mkuu, labda nishauri kitu Inspekta Aron si lazima sana akawa mmoja wetu kama maisha yake yako hatarini ni bora ahukumiwe kifungo cha maisha kuliko kuyaweka rehani maisha yake"
"Hapana Shadow, Inspekta Aron ni lazima awe mmoja wetu ni lazima aje kuimalizia kazi iliyoanzishwa na baba yake enzi hizo. Ni kijana safi jasiri mwelevu na shupavu mkiungana atatufaa sana. Yeye pekee ndiye ataweza kukabiliana na Mama yake Sultana pamoja na kaka yake Tino kuhakikisha anawazuia wakati huo sisi tunapambana na Profesa Cosmas Kulolwa pamoja na watu wake kutoka Mexico"
Baada ya maelezo hayo Jasusi shadow alitulia kimya huku akionekana kutafakari jambo.
"Shadow vipi kuhusu Sultana nakumbuka uliniambia leo amekuagiza ukavamie maabara kuu ya serikali uchukue vimelea vya V-COBOS" Aliuliza Rais.
"Ndiyo, huyu mama anarahisisha sana yeye na mtoto wake Tino wala hawajali kuhusu matatizo yaliyomkuta ndugu yao Aron. Nitajua cha kumjibu ngoja tumalize kwanza zoezi la kumuokoa Aron"
"Sawa lakini kuwa makini usije kupoteza ushirika na Sultana hakuna anaejua ilipo chupa ya kijivu zaidi yake"
"Sawa Mheshimiwa"
"Basi fanyeni kila mnaloliweza vile vidonge na ile karatasi ya maelezo imfikie Inspekta Aron leo usiku"
"Sawa Mheshimiwa"
[emoji294][emoji294][emoji294]

SASA TUENDELE...
Hadi inatimia saa 12 kamili asubuhi Inspekta Aron hakuwa amepata hata repe la usingizi, aliendelea kutafakari kwa kina ujumbe aliotumiwa huku akiwa hana majibu ya nini cha kufanya.
Baada ya kufikiri kwa muda mrefu Inspekta Aron alirudia kwa mara nyingine kusoma maelezo yaliyokuwa kwenye lile karatasi, akavuta pumzi ndefu na kuitoa taratibu.
"Hivi inawezekanaje mapigo ya moyo yakasimama alafu baadae nikaendelea kuwa hai" Aliwaza Inspekta Aron jambo hili likionekana kutokumuingia akilini kabisa lakini kila alipoitazama nembo ya marehemu baba yake kwenye ile karatasi alijikuta anapata msukumo wa kufanya kama alivyoambiwa.
"Anyway la kuwa na liwe" Aliwaza Inspekta Aron kisha akafungua ile nailoni akachukua vile vidonge na kuvibugia mdomoni akavimeza.
Haraka akaichukua ile karatasi na lailoni iliyokuwa na vidonge akaingia chooni akavitupa katika tundu la choo na kuviflash na maji. Akiwa anatoka chooni Inspekta Aron alianza kuhisi mabadiliko kwenye mwili wake haukupita muda akajikuta anakakosa nguvu, akaanguka chini na kutulia kimya.
ITAENDELEA....
 
Back
Top Bottom