The New York Times lasambaza uongo Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, ladai haukuwa huru na wa haki. Je, ni kweli tunyamaze, au uongo tukanushe?

Muandishi kama wewe unashindwa kuelewa simple English kama hio.

Wewe ndo unaepotosha actually hakuna sehemu kwenye article wamesema SMS zilifungwa.

Wameandika a " massive slowdown" sio kufungwa hio unaweza tafsiri kama kupunguzwa kasi au sijui tuiwekeje kwa kiswahili I make sense kwako but hauwezi toa tafsiri ya hovyo kama yako.
 

Yaani hawa journalists wa hii Banana Republic taabu sana. Hii ndiyo huyu Pascal anaisema, "a massive slowdown in internet and text-messaging services" tatizo lako ni kama la Bwana Yule, mastering your key language, English. Whatsapp, skype, Instagram, etc etc unaandika text message unatuma, zote hizo ni text messages; au unataka ziitweje?
 
Mzee baba Pasiko UNAPAMBANA sana pamoja na kupata kura "hakuna" pale Kawe

Haujakata tamaa unapambania uteuzi.

kila la heri Mkuu wa Wilaya au katibu wa PROPAGANDA ajaye pale Lumumba

Nyotaaa, nyota ndo tatizo lakeee!

Nyotaaa, wamemzidi wenzakeee!

”Kuapisha kunachosha, maDC na maRC chapeni kazi kweli kweli”.
 
Pasko, hongera kwa makala yako , unajitahidi Sana kuandika hongera kwa Hilo pia. Nina swali kwako .
JE NINI KITATOKEA KWENYE SIASA ZA NCHI YETU KWA HUU USHINDI WA CCM PEKE YAKE?
LENGO LA HUU USHINDI NI NINI NA ILI IWEJE?
Naomba ufafanizi wako, au naomba utusaidie kwa kuandika makala kuhusu Hilo Jambo.
 
Issue ya texting-messages kuwa controlled iko kwenye barua ya TRCA kwenda kwa service providers. Pili texting messages ukisoma is more than SMS-kuna SMS, EMS na MMS. Hivyo NYT sioni uongo wao, tena wao wanasema vitu vilivyokuwa reported na sio wao wenyewe kuwa source. Kiufupi naona Brother P kwa hili umetulisha matango pori.
 
Pas
Pascal asante kwa taarifa
kwa asili uongo unamuweka muathirika katika mazingira magumu- akiujibu anausambaza zaidi na inawezekana wengi wasIujali utetezi wake; kwa hiyo ni bora kunyamaza. Kwa upande mwingine ukinyamaza watu watauona kama ni ukweli kwa hiyo ni bora kuujibu kwa kutolea maelezo- sina uhakika kama melezo na majibu linamaana sawa.
Kwa vile tunaye msemaji mkuu wa serikali-- basi afanye anayopaswa kufanya- atoe maelezo uchanguzi wetu uliovyofanyika-ATOE AMAELEZO ASIJIBU
 
Paskal paskal paskal huaminiki mkuu. Watu hawasomi ulichoandika wanashambulia tu wazo lako
What went what? What went wrong?
Paskali!!Paskali!!!paskali!!! nilikuwa nikiona post zako na unavyo flow nilikimbilia kusoma!! Nahisi ile sindando ya Mayala=Njaa ikulu ilikuingia vizuri!!!
Hakika huaminiki!!! Kwa style hii nina hakika Utakumbukwa kama JM.
 
Mkuu, Paschal Mayalla,

Nakuunga mkono kabisa kwamba mamlaka husika zinapaswa kukabiliana na taarifa potoshi kwa wakati kwa kukanusha na kutoa taarifa zilizo sahihi kwa manufaa ya wananchi na mataifa ya nje ili kuondoa uchafuzi wa taswira njema ya nchi kwa nia ovu.

Mfano: Ethiopia kuna vurugu kubwa sana na mauaji yakiendelea lakini hakuna chombo chochote cha kimataifa kilichotoa tamko la kukemea au kutishia kuchukua hatua dhidi ya mamlaka iliyoko madarakani; Nigeria kuna vurugu na mifarakano kwa miaka kadhaa lakini hakuna taifa lolote lenye nguvu hata umoja wa mataifa kukemea au kutishia kuwachukulia hatua; Marekani imedhihirisha kwamba hakuna umoja, haki, na mtengamano kati ya wenye uwezo wa kiuchumi, ubaguzi wa rangi na ukiukwaji wa haki za binadamu, hakuna chombo chochote kilicho thubutu kuwachukulia hatua badala yake wamejitoa kwenye mahakama ya kimataifa na kuwakea vikwazo viongozi wa juu wa mahakama ya ICC.

Vyombo vya habari vingi vya kimataifa hata kama kuna wa WaTanzania wameajiriwa kufanya huko wanatii sera mbovu ya kuisema vibaya nchi na viongozi wake kwa maslahi ya nchi vyombo hivyo vya magharibi huu ni unafiki mkubwa.

Hakuna nchi duniani hapo inaweza ikatamba kwamba ina demokrasia isyo na doa na kunyooshea kidole nchi nyingine.

Kwa mantiki hiyo demokrasia ni pana kwa kulingana na jamii husika, utamaduni wake, maadili yake, hali ya kiuchumi, na ushirika wa kila mtu kwenye kuridhia uwepo wa uongozi.

Let's share below text on democracy such that everybody buy a leaf to enhance our integration as a nation and refrain from being machinized to practice something that does not support our core values.
Democracy does not involve a single set of institutions that are used worldwide. The specific nature of democracy is based on the political, social, and economic climate and is largely influenced by the country's history, ideology, and culture.

Many texts on democracy begin by identifying where the word came from and where the observance of democratic procedures was first copied and formalized. The text also provides definitions of democracy that have long been used. The following are some of the definitions, ranging from the simplest to the most complex. These definitions can be used to bring clarity to the definitions that scholars themselves have developed in the debates.

"Democracy is derived from the Greek word demos meaning 'people' and kratos meaning power or power." [1]

"… A government that is run on the basis of a voluntary permit." [2]

"… A system of government in which the central authority is in the hands of the people." [3]

"People's leadership in the country directly or through representation." [4]

"A system of government in which political leadership is exercised by the people, directly or through their elected representatives." [5]

"The word democracy itself means the leadership of the people. Democracy is a system in which people can change their leaders through peaceful means and the government is given the right to lead because people say it can. ”6

Quoted reference link: ACE
 
Huyu jamaa sio kama hajui ila anataka watu wafunguke
Hii ni point. Na katika kufunguka kwa watu, anapata uhalisia wa kilichotokea. Hili hata CCM katika kutathimini "ushindi wao wa kishindo" wanatakiwa kutumia njia kama hizi kuliko kubaki wakishangilia ushindi usio halisi.
 
Watu wana moyo sana kusoma thread zako...

Hongera kwa kuandika maoni yako kwa sababu unatetea tumbo lako..
 
Jifunzeni kukaza watoto wa kiume msiwe wanafiki yani ukweli unaujua lakini unajitoa ufahamu ili tu upate jambo fulani
kwa hali hii hata marinda yaweza kuwa sio ishu sana kwenu mradi tu mpate mnachotaka
Mtandao umezidiwa baada ya watu kununua sanaaa bando ili wafuatilie uchaguzi!!!!!!
Kweli?
 
Kati yako wewe Pascal Mayala na gazeti la The New York Times ni nani muhongo juu ya uchaguzi mkuu wa Tanzania uluofanyika tarehe 28 October, 2020? Au ndo tuseme kwamba ni kawaida yenu vijana wa ccm kujifanya hamnazo ili kumuwashia kwenye gia mwenyekiti wenu awateue?
 
Kati yako wewe Pascal Mayala na gazeti la The New York Times ni nani muhongo juu ya uchaguzi mkuu wa Tanzania uluofanyika tarehe 28 October, 2020? Au ndo tuseme kwamba ni kawaida yenu vijana wa ccm kujifanya hamnazo ili kumuwashia kwenye gia mwenyekiti wenu awateue.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…