Hivi vyama vya siasa Tanzania ni ulaji tu.
(1). Kwa nini wameshindwa kuandaa maandamano kumpinga Richmonduli kuwanyamazisha wabunge?
(2). kwa nini wameshindwa kuandaa maandamano kupinga mikataba feki?
(3). kwa nini wanashindwa kuandaa maandamano kupinga unyanyasaji wa watanzania na vishirika koko vilivyowekeza TZ kwa miradi bomu?
haya ni mambo ambayo vyama vya upinzani wanatakiwa wafanye sio kusubiri wakati wa uchaguzi ndio tuwasikie. [WORK UP YOU GUYS, THE COUNTRY IS JUST WAITING FOR YOU TO START]
mwanasiasa, ukiwauliza watu utaona kuwa vyama vya upinzani bado havijawa chaguo la kwanza la wanaotaka kuingia kwenye siasa za nyumbani. Wengi wetu licha kasoro na kero zilizoko CCM bado tunavutiwa na CCM zaidi kuliko upinzani!! Siyo kwa sababu CCM ina sera nzuri kuliko vyama vingine, la hasha sababu kubwa tumeiona ikiongoza!! Viongozi wa upinzani hawajaonesha uongozi ulio mathubuti na wenye kujali Taifa!
Lazima tuwaone viongozi hawa wakiongoza ndipo tutavutiwa na vyama vyao!! Nilikuwa nakiheshimu Chadema sana, lakini baada ya kampeni za mwaka jana na hadi leo wamenikatisha tamaa!! Sasa naanza kukiangalia kwa karibu CUF huku moyo wangu bado uko CCM!!
Je vyama vya upinzani viko tayari kufanya mabadiliko ya ndani? Sheria zilizopo kama zinaweza kuijenga CCM bila ya shaka zinaweza kujenga upinzani. Hatuwezi wote kuingia upinzani na kuubadilisha wakati "Waasisi" hawako tayari vyama "vyao" vibadilike!
Lunyungu, CCM siyo Mama!!!! Sikufichi ningekuwa nyumbani sijui kama upinzani ungeweza kunihimili kwa mawazo yangu ya kuvibadilisha vyama hivyo kuvifanya kuwa relevant na vinavyohitajika! CCM ndo isingenipenda kabisa kwani utii wangu ni kwa nchi yangu na si kwa Chama! Ni kwa sababu hiyo, ningeipigia kura (kitaifa) na ningeangalia upinzani unafanya nini!
Najua wengi hapa mna maslahi kwenye upinzani (kama wengine wana maslahi kwenye chama tawala), lakini upinzani ulivyo Tanzania hautashika hatamu hata waendelee kutamani vipi! Wataendelea kubakia kuwa fisi akisindikiza mkono wa mwanadamu akitembea akidhania utanyofoka!! Najua mna nia nzuri na hamu ya kweli ya kuibadilisha Tanzania na kulifanya kuwa Taifa la kIsasa na la Kidemokrasia zaidi! Hata hivyo, kufikia huko ni lazima mfanye yale ambayo ni ya lazima!
Wote mlijua (hata mbishe vipi) hakuna kiongozi wa upinzani ambaye angemshinda Kikwete kwanini mlipoteza muda na fedha kunadi wagombea wenu badala ya kutilia mkazo wabunge? Hata hivi sasa badala ya kujenga vyama toka chini, bado mnaangalia juu!! 2010 itafika Mbowe, Mrema, Lipumba, Mbatia, Dr. Mvungi, watajaribu kusimama tena!!
Upinzani in Tanzania is irrelevant, wala msiwalaumu ambao hawajaiunga kwa kutokufanikiwa kwenu! Kama ninyi ambayo mko upinzani muda huu wote, wale wengine watakaoingia watabadilisha nini? Suala siyo wingi! je mawazo yao yatasikilizwa? Je kuna utaratibu wa kukubali kukosolewa na kubadilika? Nipeni mfano wa mwanachama wa kawaida aliyetoa mawazo ya mabadiliko akasikilizwa!!
Upinzani unajimaliza wenyewe!
Opposition leaders accused of selfishness
2007-01-04 10:01:11
By Judica Tarimo
Top political opposition mandarins in the country have been accused of violating party constitutions, wrecking internal democracy and fostering disintegration of opposition parties.
?Most of these leaders are selfish, who are pushing hard to protect their individual gains rather than party or national interests,? said former Tanzania Labour Party (TLP) Secretary General, Hamad Tao yesterday.
In an exclusive interview with The Guardian, Tao said top opposition leaders violate party constitutions and laid down principles, rules and regulations to protect their personal interests.
Tao said top opposition leaders had been striving day and night to maintain their positions. In the process, he regretted, youthful leadership was blocked from taking the reigns of power.
Tao lamented that the leaders were denying youths from attaining positions of leadership in the country?s political realm.
Opposition leaders, according to Tao, do not respect rules, regulations, and procedures and even the constitutions, an important document, which guide operations of the party.
?True democracy is not practiced in these parties. Top leaders are the ones who destroy democracy and good governance. They are good at fighting for the national democracy, but internal party democratic institutions are worse,? he lamented.
The official took a swipe at the top opposition leaders for clamouring for respect for democratic tenets at the national level when they kill the same at party level.
?It?s senseless to strive for the country?s democracy and fail to protect democracy and good governance in your own parties. Charity must begin at home,? said Tao.
?These problems also accelerate off-and-on political squabbles within the opposition parties, and the country as a whole,? said Tao.
?We (opposition parties) cannot win in elections if we do not adopt concerted efforts to improve internal democracy, good governance and rule of law. This helps to build public trust and confidence,? he observed.
He called for opposition leaders to shun selfishness and protection of their personal gains and instead open doors for members to exercise their democratic rights at all levels.
SOURCE: Guardian