The Only Thing We Have to Fear is Fear itself

The Only Thing We Have to Fear is Fear itself

Mwanasiasa,
Sitting on the fence is one way of saying I like things as they are. Hawa wanaolalamikia juu ya Chadema eti ni family business au eti upinzani ni weak ni dalili kwamba watu hatutaki kukunja mikono ya shati zetu (pull our sleeves) na kuingiza mikono yetu kwenye tope ili kujenga something from nothing. Wote tunasubiri vitu vipikwe viive ndio tuseme kuwa kumbe upinzani una nguvu. Nguvu zake ni sisi na kama tumeamua kukaa pembeni na kulalamika tu juu ya Mbowe na helikopta yake basi ni kwamba tumekubali kuachia CCM iendelee na maovu yake bila checks and balances.
 
Wacha,
Badala ya kusema kwa nini "wameshindwa" jiulize wewe "have I played my part" to change things? Mwalimu alisema it can be done, play your part.
 
Jasusi

Kama ukisoma vizuri hiyo artical utaelewa; vyama vya siasa tayari vinapata ruzuku kutoka serikalini ni jambo la kuhamasisha tu, I am not alone we are plenty plus waiting.

Unafikiri wale walioandamana juzi juzi wakati Israel walipoipiga mabomu nchi mja pale mashariki ya kati walipata ruzuku serikalini?
 
Mwanakijiji,
Ninatatizo na ushauri wako wa vyama vya upinzani kuungana ndipo watu waone kuwa wako serious. Kitu chochote chenye sura ya "social being" nimekosa maneno sahihi ya kiswahili, kina matatizo ya ndani na ya nje. Vivyo hivyo hilo lipo kwa vyama vya siasa. Ni ukweli usiopingika kuwa vyama vyote ikiwemo CCm vina matatizo yake ya ndani lakini pia yapo ya nje.
Kwa vyama vya upinzani mfumo wetu ndio kikwazo kikubwa, wizi wa kura, raslimali, matumizi ya dola n.k. Hiki chama unachoshauri kitawezaje kuruka viunzi vya mfano wa CUF kukataliwa kufanya mikutano ya kampeni kwa baadhi ya sehemu za majimbo? Au chama kimoja kitawezaje kuzuia uhuni wa wakuu wa tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo tofauti na matakwa ya wapiga kura? Chama kimoja kitawezaje kuzuia polisi kuchukua masanduku ya kura nakuyapeleka kusiko julikana nakisha kurudi na kutangaza ushindi kwa mgombea fulani?
Kafara ya viongozi; hivi ni nani baada ya Mrema kweli anaweza kutoka CCM huku anazijua mbinu chafu zinazotumika kwa yeyote anaotofautiana nao. Kuwasifu watu kwa kubakia kwao wakati wanachofanya ni kutetea unga wao ni kuwapa sifa wasizositahili. Na hili linatufikisha kwenye hoja yako nyingine kuwa Watanzania wanaona afadhali CCM kuliko vyama vya upinzani. Watanzania hawana uchambuzi wa aina hiyo. Mtu ambaye kanyang'wanya sehemu yake yakujipatia ridhiki, Mererani, Buhemba, Bulyanuhulu n.k kwa mazingira ya kitapelitapeli akiendelea kudai afadhali CCM kwa sababu tumeshaiona kuna kitu kina kasoro kubwa.
Kuwaona vyama vya upinzani wakiongoza itawezekana vipi wakati hujawapa nafasi ya kuongoza? Sikubaliani na kusema Watanzania wamekuwa human resources managers ati wanampima mtu kwa uwezo wake wa kuongoza maana vinginevyo wengi wawaliochaguliwa hawana sifa hizo. Wanachoangalia kutokana na mazoea, uoga wa mabadiliko na elimu duni ni njaa yao. Nani anaweza kutoa pilau, kanga, t shirt, pombe na pilau.
 
Tabasamu nakuunga mkono na naongezea kwamba kuna watu wanafuki hapa ambao wana maslahi na CCM watasimama nao kila siku no matter what na wao lazima kutafuta visingizio vichafu ili kukijenga Chama chao . Ila ukweli umesha usema . Kama mtu ni CCM damu halafu anawaza kuwa Cahdema kaona haifai sasa anataka kwenda CUF kuangalia huyu si mnafiki tu ? Akiingia huko anaweza kuondoka na kurudi CCM kwa madai kwamba amegundua ni bora zaidi ya Upinzani ? Bakini CCM jamani na wengine wakweli waende kwenye Vyama vingine .
 
Hivi vyama vya siasa Tanzania ni ulaji tu.

(1). Kwa nini wameshindwa kuandaa maandamano kumpinga Richmonduli kuwanyamazisha wabunge?

(2). kwa nini wameshindwa kuandaa maandamano kupinga mikataba feki?

(3). kwa nini wanashindwa kuandaa maandamano kupinga unyanyasaji wa watanzania na vishirika koko vilivyowekeza TZ kwa miradi bomu?

haya ni mambo ambayo vyama vya upinzani wanatakiwa wafanye sio kusubiri wakati wa uchaguzi ndio tuwasikie. [WORK UP YOU GUYS, THE COUNTRY IS JUST WAITING FOR YOU TO START]

Hapa napo napata taabu vilevile,
Maandamano, halafu wakisha kuandamana ndio iweje? Si tuliona maandamano ya CUF january 2001 sasa hayo yalisaidia nini? Mwaka jana CUF wamefanya maandamano makubwa Zanzibar na Dar es Salaam wakita uchaguzi urudiwe, kuna tetesi zozote kuhusu kurudiwa kwa uchaguzi ule? Ni kupoteza muda wa watu. Kinachotakiwa ni kuwaelimisha watu na hicho ndio Mbowe anafanya. Kuwaambia watu waandamane kwa ajili ya Umeme wakati zaidi ya asilimia 82 hawaathiriki moja kwa moja na kukosekana kwake ni kupoteza muda. Lazima waeleweshwe kuwa wanahitaji umeme katika dunia ya sasa ndipo watakapoweza kuudai.
Hata huko maandamano yalikofanikiwa ni kwa sababu watu wenyewe walikuwa wakijua wanataka nini viongozi kazi yao nikuwaunganisha tu. Huwezi kuachieve chochote kwa maandamano nchini. Na maandamano yanayoweza kueleweka ni yale yanayoweza kupambana na nguvu za dola Tanzania hatujafikia huko.
 
Tabasamu endelewa kuwapa shule hawa watumishi wa CCM hapa kwenye forum .Nakuunga mkono kwa uhakika
 
Mwanasiasa,

Ukisoma vizuri maelezo ya waungwana nadhani utapata somo zuri zaidi.
Binafsi navyoelewa hisia za wengi ni kwamba siasa za TZ bado ni ushabiki wa soccer! inachukua nguvu mpya kushawishi mtu aweze kuona mafanikio ndani ya Simba club ikiwa yeye kazaliwa mshabiki wa Yanga.
Na itachukua nguvu kubwa zaidi kumshawishi mtu yule ambaye ana upeo zaidi ya ushabiki.
Kwanza, ukijiunga na Simba kama mwanachama utasaidia nini ikiwa wachezaji wake uwanjani ni wabovu?..
Pili, kwa kadi gani itakayokupa nguvu ya kusema uongozi mbaya au kocha mbaya, mchezaji fulani hatakiwi na pengine formation ya uchezaji wetu ni mbaya.. Sauti ambayo haitachukuliwa tofauti na mpinzani ama itasikilizwa zaidi ya yule aliyesimama nje ya fence!
Swala la kura zetu sidhani kama lina uanachama -mtazipata IF.... isipokuwa hapa nadhani mtueleze nini nguvu ya mwanachama ndani ya Chadema! what changes naweza kuzileta nikiwa kama mwanachama zaidi ya michango ya fedha.
Navyoona mimi, Mwanakijiji na Wacha wameuliza maswali mazito na budi myafanyie kazi...nina hakika hakuna kati yenu mwenye uwezo wa kuyajibu hayo kwa sababu nyie ni wanachama tu. Na kijiwe hiki kilikuwa sehemu yenu muhimu sana ya hao viongozi wenu kusimama.
Pia nadhani utakumbuka niliwahi kuwaambia jiulizeni mtu kama Mtikila na Seif Sharrif walipata umaarufu wao kwa sababu gani..
Hawa jamaa walijitoa mhanga kwanza wao, walikuwa tayari kwenda Jela wakitetea wananchi pale walipoona maonevu na walifuata sheria zinazokubalika. Hata mzee Mtei mwenyewe aliweza kusimama mbele ya Nyerere na kumsema - he was wrong!..hakusubiri matokeo ya Ujamaa ktk swala la Uchumi..Lakini tofauti na Politicians wa leo, wengi wanakaa pembeni kusubiri matokeo hata RUSHWA linatembea machoni mwao.
Guys, ikiwa CCM ndio tatizo, unganeni pamoja na mfanye mkutano kubadilisha katiba ktk ngazi zote muhimu za uchaguzi na uongozi!
Hamkuyapata hayo kwa pamoja jitoeni ktk uchaguzi ujao!.. CCM hawatapenda kabisa hilo litokee kwani image yao nje ni muhimu kuliko wizi wao. Hii ni kijimila cha Mdanganyika yeyote hata mwizi au Jambazi hupenda kujikosha mbele za watu kama mtu mwema lakini inapotoka nje kuwa yeye ni jambazi basi huuhama mji.
 
Je vyama vya upinzani viko tayari kufanya mabadiliko ya ndani? Sheria zilizopo kama zinaweza kuijenga CCM bila ya shaka zinaweza kujenga upinzani. Hatuwezi wote kuingia upinzani na kuubadilisha wakati "Waasisi" hawako tayari vyama "vyao" vibadilike!

Lunyungu, CCM siyo Mama!!!! Sikufichi ningekuwa nyumbani sijui kama upinzani ungeweza kunihimili kwa mawazo yangu ya kuvibadilisha vyama hivyo kuvifanya kuwa relevant na vinavyohitajika! CCM ndo isingenipenda kabisa kwani utii wangu ni kwa nchi yangu na si kwa Chama! Ni kwa sababu hiyo, ningeipigia kura (kitaifa) na ningeangalia upinzani unafanya nini!

Najua wengi hapa mna maslahi kwenye upinzani (kama wengine wana maslahi kwenye chama tawala), lakini upinzani ulivyo Tanzania hautashika hatamu hata waendelee kutamani vipi! Wataendelea kubakia kuwa fisi akisindikiza mkono wa mwanadamu akitembea akidhania utanyofoka!! Najua mna nia nzuri na hamu ya kweli ya kuibadilisha Tanzania na kulifanya kuwa Taifa la kIsasa na la Kidemokrasia zaidi! Hata hivyo, kufikia huko ni lazima mfanye yale ambayo ni ya lazima!

Wote mlijua (hata mbishe vipi) hakuna kiongozi wa upinzani ambaye angemshinda Kikwete kwanini mlipoteza muda na fedha kunadi wagombea wenu badala ya kutilia mkazo wabunge? Hata hivi sasa badala ya kujenga vyama toka chini, bado mnaangalia juu!! 2010 itafika Mbowe, Mrema, Lipumba, Mbatia, Dr. Mvungi, watajaribu kusimama tena!!

Upinzani in Tanzania is irrelevant, wala msiwalaumu ambao hawajaiunga kwa kutokufanikiwa kwenu! Kama ninyi ambayo mko upinzani muda huu wote, wale wengine watakaoingia watabadilisha nini? Suala siyo wingi! je mawazo yao yatasikilizwa? Je kuna utaratibu wa kukubali kukosolewa na kubadilika? Nipeni mfano wa mwanachama wa kawaida aliyetoa mawazo ya mabadiliko akasikilizwa!!

Upinzani unajimaliza wenyewe!
 
Lunyungu,
Ndugu yangu sio vijimambo tu, nadhani hapa tunasaidia vya kutosha kwa hivyo vyama vya upinzani kuliko CCM...
Maswali ya Wacha muhimu sana na wengi wanajiuliza WHY?...sio Wacha peke yake.
Matokeo ya maandamano ni kuwa record inawekwa na hakuna chama duniani kinachopenda kuona maandamano ya wananchi kupinga utawala. Freeman au yeyote atakaye andaa maandamano kura zake huongezeka!..bsctime ilisifika nje kwa sababu upinzani wake kwa serikali ulikuwa na points nzito!... mengi yalifanyiwa mabadiliko.
Umaarufu wa Seif Hamad hakuupata kwa sababu ya sera za CUF wala Mtikila hakupendwa zaidi kwa sababu ya Upadri wake.. ila kile walichosimama kupinga na record itaonyesha kuwa hawa jamaa waliweza kuwavuta wananchi wengi uanachama kwa sababu waliweza kusimama KUONGOZA kundi la watu kupinga kunyanyaswa.
Na Mwanakijiji pia swali lake zito... nilichofanya mimi ni kujitoa ktk kundi moja na kutazama hoja hizi badala ya kuchukua upande na kutetea kutokana na mapenzi yangu ama ushabiki.
 
Opposition leaders accused of selfishness

2007-01-04 10:01:11
By Judica Tarimo

Top political opposition mandarins in the country have been accused of violating party constitutions, wrecking internal democracy and fostering disintegration of opposition parties.

?Most of these leaders are selfish, who are pushing hard to protect their individual gains rather than party or national interests,? said former Tanzania Labour Party (TLP) Secretary General, Hamad Tao yesterday.

In an exclusive interview with The Guardian, Tao said top opposition leaders violate party constitutions and laid down principles, rules and regulations to protect their personal interests.

Tao said top opposition leaders had been striving day and night to maintain their positions. In the process, he regretted, youthful leadership was blocked from taking the reigns of power.

Tao lamented that the leaders were denying youths from attaining positions of leadership in the country?s political realm.

Opposition leaders, according to Tao, do not respect rules, regulations, and procedures and even the constitutions, an important document, which guide operations of the party.

?True democracy is not practiced in these parties. Top leaders are the ones who destroy democracy and good governance. They are good at fighting for the national democracy, but internal party democratic institutions are worse,? he lamented.

The official took a swipe at the top opposition leaders for clamouring for respect for democratic tenets at the national level when they kill the same at party level.

?It?s senseless to strive for the country?s democracy and fail to protect democracy and good governance in your own parties. Charity must begin at home,? said Tao.

?These problems also accelerate off-and-on political squabbles within the opposition parties, and the country as a whole,? said Tao.

?We (opposition parties) cannot win in elections if we do not adopt concerted efforts to improve internal democracy, good governance and rule of law. This helps to build public trust and confidence,? he observed.

He called for opposition leaders to shun selfishness and protection of their personal gains and instead open doors for members to exercise their democratic rights at all levels.

SOURCE: Guardian
 
mwanasiasa, ukiwauliza watu utaona kuwa vyama vya upinzani bado havijawa chaguo la kwanza la wanaotaka kuingia kwenye siasa za nyumbani. Wengi wetu licha kasoro na kero zilizoko CCM bado tunavutiwa na CCM zaidi kuliko upinzani!! Siyo kwa sababu CCM ina sera nzuri kuliko vyama vingine, la hasha sababu kubwa tumeiona ikiongoza!! Viongozi wa upinzani hawajaonesha uongozi ulio mathubuti na wenye kujali Taifa!

Lazima tuwaone viongozi hawa wakiongoza ndipo tutavutiwa na vyama vyao!! Nilikuwa nakiheshimu Chadema sana, lakini baada ya kampeni za mwaka jana na hadi leo wamenikatisha tamaa!! Sasa naanza kukiangalia kwa karibu CUF huku moyo wangu bado uko CCM!!

Watu wanajiunga CCM kwa sababu ndicho chama kinachofanana na akili, hisia, na hulka zao. Ndimo yalimo maslahi yao. Nii chama cha watanguliza matumbo. CCM kwanza, Tanzania baadaye.

Lakini wapo pia wajinga wanaojiunga nacho kwa sababu za kihistoria tu, wakidhani CCM ya leo ndiyo ile uau Nyerere. Hawataki kutazama kina Patel wanafanya vitu gani vya kudhalilishah Unyerere ndani ya CCM. Na msomi aiyefuata sera, hasa kama ni kijana, nafaa kufungiwa jiwe la kusagia shingoni atoswe Bahari ya Hindi!

To sum it up, watu corrupt ndio wanajiunga CCM.
 
kichwamaji, unayoyasema kuhusu CCM yaweza kusema dhidi yavyama upinzani na yatakuwa kweli!! Hivi wapinzani hawatangulizi Matumbo yao?
 
Je vyama vya upinzani viko tayari kufanya mabadiliko ya ndani? Sheria zilizopo kama zinaweza kuijenga CCM bila ya shaka zinaweza kujenga upinzani. Hatuwezi wote kuingia upinzani na kuubadilisha wakati "Waasisi" hawako tayari vyama "vyao" vibadilike!

Lunyungu, CCM siyo Mama!!!! Sikufichi ningekuwa nyumbani sijui kama upinzani ungeweza kunihimili kwa mawazo yangu ya kuvibadilisha vyama hivyo kuvifanya kuwa relevant na vinavyohitajika! CCM ndo isingenipenda kabisa kwani utii wangu ni kwa nchi yangu na si kwa Chama! Ni kwa sababu hiyo, ningeipigia kura (kitaifa) na ningeangalia upinzani unafanya nini!

Najua wengi hapa mna maslahi kwenye upinzani (kama wengine wana maslahi kwenye chama tawala), lakini upinzani ulivyo Tanzania hautashika hatamu hata waendelee kutamani vipi! Wataendelea kubakia kuwa fisi akisindikiza mkono wa mwanadamu akitembea akidhania utanyofoka!! Najua mna nia nzuri na hamu ya kweli ya kuibadilisha Tanzania na kulifanya kuwa Taifa la kIsasa na la Kidemokrasia zaidi! Hata hivyo, kufikia huko ni lazima mfanye yale ambayo ni ya lazima!

Wote mlijua (hata mbishe vipi) hakuna kiongozi wa upinzani ambaye angemshinda Kikwete kwanini mlipoteza muda na fedha kunadi wagombea wenu badala ya kutilia mkazo wabunge? Hata hivi sasa badala ya kujenga vyama toka chini, bado mnaangalia juu!! 2010 itafika Mbowe, Mrema, Lipumba, Mbatia, Dr. Mvungi, watajaribu kusimama tena!!

Upinzani in Tanzania is irrelevant, wala msiwalaumu ambao hawajaiunga kwa kutokufanikiwa kwenu! Kama ninyi ambayo mko upinzani muda huu wote, wale wengine watakaoingia watabadilisha nini? Suala siyo wingi! je mawazo yao yatasikilizwa? Je kuna utaratibu wa kukubali kukosolewa na kubadilika? Nipeni mfano wa mwanachama wa kawaida aliyetoa mawazo ya mabadiliko akasikilizwa!!

Upinzani unajimaliza wenyewe!

Somahapo juu!!! Naona huyu jamaa hana mchango wowote wa kuleta kwa Watanzania. Bora aishi huko huko aliko, afie huko. Elimu yake haijamkomboa. Ana mawazo mafinyu mno! Sijui hata historia hakuisoma?
 
Maneno yako mazito sana Kichwamaji ninaya fuatilia kwa karibu yana ukweli mwingi . Huyu bado
 
Tabasamu / Lunyungu

Hivi mtu kama hukubaliani na Chadema basi anakuwa mwana CCM?

Naona mmewabatiza watu wengi tu humu ni CCM, mtu kama hakubaliani na mawazo yenu basi anarudisha maendeleo ya TZ ni mtu hatari.

Laiti kama mngekuwa na ufahamu wa kuielewa Chadema pengine mngebadilika. Kwa Taarifa tu wengine hapa hatuna vyama lakini TZ ni yetu wote. Kitu kinachonisikitisha ni kwamba hamjibu 'concrete questions'. Sasa kwa mwendo huu mkiingia madarakani mtaweza kutoa majibu sahihi?

Tuliambiwa mwaka jana kwenye hii forum Chadema ni chama cha kifamilia leo hii 2007 bado mnafanya kikao kutoa jibu, then mnakuja na kejeli na dharau ambazo hazina msingi. Hapa ni mahali pa kukata issues sio majungu jibu hoja kwa hoja sio uzushi.
 
Opposition leaders accused of selfishness

2007-01-04 10:01:11
By Judica Tarimo

Top political opposition mandarins in the country have been accused of violating party constitutions, wrecking internal democracy and fostering disintegration of opposition parties.

?Most of these leaders are selfish, who are pushing hard to protect their individual gains rather than party or national interests,? said former Tanzania Labour Party (TLP) Secretary General, Hamad Tao yesterday.

In an exclusive interview with The Guardian, Tao said top opposition leaders violate party constitutions and laid down principles, rules and regulations to protect their personal interests.

Tao said top opposition leaders had been striving day and night to maintain their positions. In the process, he regretted, youthful leadership was blocked from taking the reigns of power.

Tao lamented that the leaders were denying youths from attaining positions of leadership in the country?s political realm.

Opposition leaders, according to Tao, do not respect rules, regulations, and procedures and even the constitutions, an important document, which guide operations of the party.

?True democracy is not practiced in these parties. Top leaders are the ones who destroy democracy and good governance. They are good at fighting for the national democracy, but internal party democratic institutions are worse,? he lamented.

The official took a swipe at the top opposition leaders for clamouring for respect for democratic tenets at the national level when they kill the same at party level.

?It?s senseless to strive for the country?s democracy and fail to protect democracy and good governance in your own parties. Charity must begin at home,? said Tao.

?These problems also accelerate off-and-on political squabbles within the opposition parties, and the country as a whole,? said Tao.

?We (opposition parties) cannot win in elections if we do not adopt concerted efforts to improve internal democracy, good governance and rule of law. This helps to build public trust and confidence,? he observed.

He called for opposition leaders to shun selfishness and protection of their personal gains and instead open doors for members to exercise their democratic rights at all levels.

SOURCE: Guardian

Huyu mwandishi na huyo Tao wote wababaishaji. Utaitaje huu utumbo exclusive interview bila mifano hai? Hawezi kugeneralize mambo yalivyokuwa kwa Mrema na ikawa hivyo kwa vyama vingine. CUF na CHADEMA vina matatizo yake ikiwemo hilo la opportunisits ambao wanadandia kwa manufaa yao wakiona tumbo bado lina njaa wanakimbilia kusema hakuna demokrasia.
Nawahurumia Wadanganyika wanaoendelea kulishwa kasumba ati vyama vya upinzani havishindi kwa sababu ati havina demokrasia, hivi watu wa Ubungo kumchagua Mnyika dhidi ya Keenja kuna uhusiano gani na Mbowe kuwa dikteta? Je alikuwa anaenda kumwakilisha Mbowe au wana Ubungo. Kama suala ni kukosekana demokrasia ndani ya vyama, iweje CUF hii hii ambayo haina demokrasia ichukue viti vyote vya Pemba? Mbona watu wa Tarime na kwingineko walichagua wagombea wa CHADEMA kama suala ni kukosekana kwa demokrasia ndani ya vyama hivi?
Tutafute sababu nzuri za upinzani kushindwa lakini siyo hizi rahisi rahisi. Ati leo Tao au Hiza au Nsanzugwako wakisema hakuna demokrasia kwenye vyama tunaanza si mnaona.
Kichwamaji,
Well said. Mtu akisema leo anajiunga na CCM ni corrupt na anategemea mianya ya corruption to make the ends meet. Hao waliomo ni opportunists ambao hawezi kutoka kwa sababu njaa itawaua. Kama siyo corrrupt na opportunist huwezi kuacha kuhoji suala la Richmonduli na hilo la Buhemba watu kukausha dhahabu zetu halafu wananchi wanahamishwa tena eneo jingine kusudi jamaa wapewe tena vile wanajua Buhemba imejaa dhahabu.
 
mwanakijiji,
unaelewa maana ya mabadiliko? halafu mabadiliko yenyewe tunayopngelea hapa ni mabadiliko ya mfumo uliodumu kwa takribani miaka 45! lazima ujue kuwa sio kazi ndogo, ni kazi ngumu sana,
na ni watu wachache sana katika jamii zetu huwa wana courage ya kuleta mabadiliko katika jamii.
sasa wewe unanichekesha pale unapooneakana kulalamikia mfumo huo wa ccm kila siku halafu leo solution unayotoa ni ile ile ya kusema afadhali ccm..what a joke!!!
wewe kama ni mwanajeshi na unataka kuleta mabadiriko kuanzia kwenye vyama na hata taifa inatakiwa ujiunge na harakati hizo na kwanza kwa kufanya reforms ndani ya vyama na baadae taifa.
nilifurahishwa sana na zitto kabwe katika mahojiano yake na radio butihama pale aliposema yeye ana mission na kazi kubwa anayofanya kwa sasa ni kuhakikisha anafanya reforms kwanza ndani ya chadema yenyewe, huo ndio ujemedali unaotakiwa,
wewe huwezi tu ukawa critical of the current system and then you dont give any solutions and instead you are telling us we better continue with the same system, that is an insult!!
nenda kasome histroia za watu walioleta mabadiriko katika dunia hii huone njia waliyopitia, it is no aesy, mfano martin luther king ambaye aliwafanya weusi waonekane ni watu ended being assasinated,
abraham linkoln ambaye alianzisha sera za kupinga slavery akasababisha marekani igawanyike na kuingia kwenye civil war ended being assasinated,
so is nelson mandela ended 25 years in prison at al.
sasa hawa watu wote miaka mingi baadae wanaonekana ni watu wa maana.
kwasababu walikuwa sio waoga, watu wasiokata tamaa, na watu wenye mission.
na wakaleta mafanikio ambayo hata wewe leo hii unafaidika nayo.
wewe kama unaona hauwezi au umekata tamaa kaa pembeni ila usigeneralize kuwa ccm itatawala milele.
ngoja mimi nikuambie kitu kimoja, mabadiliko ni lazima, kila jamii lazima iendane na wakati either kwa kuchagua au kwa kulazimishwa.
kama ambavyo ulimwengu ulitulazimisha kuachana na siasa ya chama kimoja kwenda siasa ya vyama vingi, ndivyo itakavyotekea.
inawezekana isiwe 2010 au 2015 hata 2020,lakini ujue ccm wataendelea kuiba kula na siku watu watachoka na kwenda barabarani.
hii ni lazima kwasababu sio tu ni ccm kuchagua bali mfumo utatulazimisha tufanye hivyo. watu wameshachoka na hali ya umskini, vijana wengi wanvyozidi kukosa ajira bila kuwa na solution ya kudumu ya matatizo haya,
pia ujue kuwa pamoja na harakati za wana ccm kuumaliza upinzani hawataweza kuwaaccomodate watu wote wenye mawazo na imani tofauti katika jinsi ya kuleta mabadiriko, hii ni sababui kubwa inanifanya mimi niwe muumini mkubwa wa demokrasia ambayo ni njia sahii ya kuzuia dictatorship.
mabadiliko yanakuja ni bora kujiunga sasa ili tuwe sehemu ya historia.
may God bless Chama Cha Demokrasia na Maendeleo.
 
Wacha,
Swali hilo hilo unaweza kuulizwa wewe. Hivi kila asiyekubaliana na CCM ni mwanaCHADEMA? Kama wewe uanavyotetea CCM ilhali si mwanachama wake ndivyo na watu wengine tunavyoweza kutetea CHADEMA japo si wanachama.
Watu wanaotetea maslahi ya taifa hawawezi kusifia chama kinachofanya madudu kwa kasi ya kutisha. Huwezi kutetea mikataba ya ovyo ovyo kama inayoingiwa na serikali ya CCM halafu ukadai unajali maslahi ya taifa yapi hayo?
Hakuna maswali concrete humu zaidi ya tuhuma zisizokuwa na kichwa wala miguu. Nimeuliza kwenye post yangu ya mwisho, hivi kuchagua Wabunge wataolipa bunge letu meno kuna husiana nini na family business ya CHADEMA? Watu wa Kigamboni kuchagua mtu atakayepigania daraja lijengwe badala ya sasa ambapo serikali ya CCM haitaki kwa sababu wanapata 10 percent ya kukarabati vivuko vibovu kunahusiana nini na family business ya CHADEMA? List ni ndefu.
Soma tena post ya Kichwamaji ya 05/01/2007 saa 12:45 am. Huo ndio ukweli wenyewe hata kama watu hawaupendi.
 
Back
Top Bottom