The Only Thing We Have to Fear is Fear itself

The Only Thing We Have to Fear is Fear itself

Mwanakijiji,
Ni yapi ambayo hivi sasa unaona kuwa CCM inafanya kwa manufaa ya Watanzania? Ubinafsishaji? Kuwafukuza wakulima kutoka maeneo yao ili wachimba dhahabu wafaidike? Kuwaruhusu wachimba madini wa kigeni kuwapiga risasi wachimbaji wadogo wadogo ambao wameingilia maeneo yao? Waziri wa Kilimo kusema kuwa wakulima wadogo wadogo wapewe maeneo ya kilimo na wawekezaji? CCM inalinda maslahi ya nani?
 
mwanakijiji hatukatai kuwa ccm haijafanya kitu ,tunachosema ni kuwa HAKUNA CHA KUJIVUNIA !!!!!!!!!! pia hatutaki upinzani uoate dola kesho ila tunataka sustainable changes zianzie bungeni kwa wapinzani kupata viti vya kutosha bungeni.,ndio maana nataka niombe wote tuungane pamoja kuleta mabadiliko kuanzia chini...
wapinzani hatuwezi kuwapa nchi kwa majaribio,tuanze kuwapa kujiamini ,,uchaguzi wa 1995 mwalimu alimwambia mrema ,hata kama yeye mrema alikuwa safi ,lakini bado walomzunguka wasingeweza kuaminiwa kupewa dola ,akampa challange amtajie japo baraza la mawaziri kama alikuwa na watu makini,na tuliona kweli mwalimu hakukosea ,mnakumbuka kina lamwai,mbatia,ali sumaye,marando,nsazugwanko,makongoro..ndio mrema ..aliwategemea,.wangetufikisha wapi? mwalimu hapo ndio akamwambia mrema bora akagombee ubunge alete mageuzi kuanziA HUKO.
ili kuleta changamoto bungeni ingefaa kiongozi yoyote anayegombea urais na kupata kuanzia 2.5% apewe ubunge hii ingehuisha bunge ,...
 
Jasusi, uliyoyasema ni udhaifu mbalimbali uliopo katika CCM! Hakuna mahali hata pamoja ambapo nimesema kuwa CCM haina matatizo! Ila kuniuliza mimi ni kitu gani CCM "inafanya kwa manufaa ya Watanzania" ni zoezi ambalo sitaki kukufanyia! Watu wa kuwauliza ni wanakijiji wa Rufiji ambao miaka nenda nyuma walikuwa watumwa wa mto Rufiji lakini serikali ya CCM iliweza kujenga daraja la kisasa juu ya mto huo! Halafu mpinzani aende kuwaambia ati CCM haikufanya kitu chochote kwa manufaa yao!! Watakuonesha daraja la Mkapa!

Nenda kwa wananchi wa Boko ambao kutoka Wazo Hill kwenda Bagamoyo ilikuwa ni laana bin laana! Serikali ya CCM ikaitengeneza barabara hiyo na kuifanya ipitike vizuri! Halafu awaambie wananchi wa Boko kuwa CCM haikufanya kitu, watamuonesha barabara!

Huko nyuma tulikuwa tunahangaika watoto wetu wanagombania kwenda Chuo Kikuu cha Dar kilichokuwa na uwezo wa wanafunzi kama 3000 tu, leo chuo hicho kinachukua wanafunzi zaidi kidogo ya 10,000, kikishindana na vyuo vingine vikuu! Ukienda kuwaambia wazazi ambao wanachagua mtoto aende UDSM, Mzumbe, Tumaini, St. Augustine, Zanzibar n.k kuwa CCM haikufanya lolote kwenye elimu ya juu atakuonesha vyuo vikuu!!

Hakuna mahali ambapo palikuwa panaashiria kifo badala ya uzima kama hospitali ya Muhimbili. Ilikuwa imechakaa na inatisha. Leo imefanyiwa ukarabati ikiwa na vifaa vya kisasa, na ikijitahidi kutoa motisha kwa wafanyakazi wake. Ukiwaambia wagonjwa waliotibiwa hapo kuwa CCM haikufanya lolote, watakuonesha Muhimbili!!

Niendelee??????
 
Philemon, finally you are closer to my position kuliko wengine hapa ambao wanatutaka turukie treni la wapinzani alimradi ati sote tunaipinga na kuikosoa CCM!! Wapinzani hawataki kupata viti vingi bungeni, walikuwa na nafasi hiyo 2005 wakang'ang'ania Urais! Wangekuwa na nia, 2005 wangetilia mkazo kupata angalau viti 100 uwezo walikuwa nao, na 2010 wangejaribu Urais lengo likiwa kuupata Urais 2015! lakini wao hawataki hilo. Wanataka wawe Rais leo!! Hivi Mbowe anaweza kututajia baraza lake la mawaziri, wakuu wote wa mikoa, wilaya n.k watakaotoka Chadema?
 
Muhimbili ? Duh!!! My foot . Wanafunzi 10,000 ? Chuo kipi ? Mwaka huu wamefanikiwa wangapi kuingia Chuo Kikuu ? Tuache utani hapa . Kuna mambo ambayo Serikali imefanya na tunasema ni sawa na ni kazi ya CCM kufanya maana wakjo madarakani . Lakini uozo unazidi mazuri .
 
Lunyungu.. Muhimbili ndiyo- hutaki? nilidhani mlisema "CCM haikufanya lolote kwa manufaa ya wananchi"!? Angalieni mnavyojenga hoja! Msizungumze kwa jazba!! Sasa mnakubali kuwa imefanya mazuri kidogo japo mabaya yamezidi mazuri, mnataka tuanze kujenga hoja kuwa mazuri yamezidi mabaya!?
 
Nimeuliza Muhimbili maana ni juzi nimeona hata picha watu wana lala chini .Ndiyo maana nimekuuliza Muhimbili ? Ni magofu na wodi chache zinatoa huduma .Najiuliza JK alikuwa huko lakini sijaona alichopeleka hadi unasema wewe hapa wakati sisi tunaenda hapo ni aibu ni magofu unaongelea nini wewe ? Jazba ? Mimi sina jazba
 
Lunyungu, ni jambo moja kuwa na matatizo ni jambo jingine kutofanya lolote. Je Muhimbili ya leo ni mbaya zaidi kuliko ya miaka 10 iliyopita?
 
Mzee Mwanakijiji/Lunyungu

Chill-out guys a little bit.
 
Ama kweli kijiwe kimekolea haswaaaa!..

Shukran za dhati kwa Mzee Mwakijiji pamoja na kwamba kuna sehemu mbili tatu umezijenga mwenyewe...samahani nikiwa na maana kuwa upimaji wa mafanikio ya CCM hauwezi kupimwa kwa ongezeko la shule ktk miaka hii miwili hali CCM imetuongoza toka tupate Uhuru!...Chuo Kikuu na Muhimbili zote ni CCM ktk vipindi vyote kwa hiyo mabadiliko yake hayawezi kupimwa na kuyageuza kuwa mafanikio ya CCM....from who?.
Nilichokisoma hapa na muhimu kwa vyama vya Upinzani ni kuweka akili katika mageuzi ya Bunge letu kwanza...Hili mjomba nakupa zako zotee! kisha mengine yatafuata taratibu. Na kweli Ulivyosema kama Chadema wataweka akili zao ktk Wabunge kwanza nadhani kila hoja ya Kichwamaji jibu lake linatoka hapo!.Sisi wengine kura zetu ni ongezeko linalohitajiwa zaidi ya kuwa uanachama usioweza kupiga kura.

Tatizo kubwa ambalo nadhani litawakabiri Vyama vya upinzani ni FEDHA ama mbinu ambayo itaweza kushindana na Sisiemu binTakrima. Pili, Muundo wa serikali ambayo inaweza kuwapa wananchi tumaini na mwisho kuhakikisha kura za wabunge zitalindwa bila chombo cha dola FFU kuingilia kati kulinda baadhi ya wasoteuliwa....
Na mwisho, mmesahau kitu kimoja tu (mazingaombwe ya mtu mweusi) -CCM wana imani sana za kichawi.....mkiwa tishio lao kubwa mtaondoka wengiii?
 
Habari za Kitaifa Habari nyingine zaidi!

Mbowe adai CCM wanataka kumchukua
Mwandishi Wetu
HabariLeo; Saturday,January 06, 2007 @00:05
MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amedai kwamba amekataa ofa ya kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Mbowe alisema katika siku za karibuni kumekuwa na maombi kutoka CCM ya kumtaka yeye na viongozi wengine wa juu wa Chadema kujiunga na chama hicho kwa ahadi kadhaa lakini wamezikataa.

"CCM waliwahi kunifuata … Kila mtu makini aliyeko upinzani anafuatwa. Watu wanarudi CCM kwa ahadi za vyeo, fedha na biashara," alisema Mbowe na kudai kwamba CCM imepania kuusambaratisha upinzani kwa njia mbalimbali.

Alikataa kutaja wakati, waliomfuata na ahadi alizopewa. Viongozi wa CCM walipotafutwa jana hawakuwa tayari kuzungumzia madai hayo. Hata hivyo Mbowe, ambaye alisema utaratibu wa kuwashawishi viongozi wa upinzani ni sawa na rushwa ya kisiasa, alizungumzia uwezekano wa baadhi ya wanasiasa kutumia vibaya mwanya huo kwa kutapeli.

Kauli yake ya jana imekuja siku chache baada ya kumaliza ziara ya siku 10 mikoani kuwashukuru wananchi kwa kukipigia kura chama chake katika uchaguzi wa mwaka 2005, alipogombea urais wa Muungano kwa tiketi ya Chadema.

Kufuatia ziara hiyo, Katibu Mwenezi wa CCM Aggrey Mwanri aliitisha mkutano na waandishi wa habari juzi ambako aliponda baadhi ya madai yaliyotolewa na Mbowe kwenye ziara yake yakiwamo ya wizi wa kura na rushwa vinavyodaiwa kufanywa na CCM kwenye uchaguzi huo.

Mbowe pia alitetea matumizi ya helikopta katika ziara yake hiyo ya shukrani, kwa kusema wanaohoji "wana upeo finyu wa kufikiri." Katika mvua hii ningekuwa wapi katika siku 10, alisema na kuzungumzia jinsi ziara hiyo ilivyomfikisha wilaya kadhaa za mikoa ya Mara, Mwanza, Kagera, Kigoma, Shinyanga, Manyara, Arusha na Kilimanjaro.


Mwanafunzi Wa hull University imethibitishwa yupo DSM sio Hull kama wengine walivyodai ataanza labda Jumatatu 8/01/2007.
 
Dua,
Freeman anaondoka kesho kwenda London. Atakuwa Hull jumatatu 8/01. Kama unataka mtafute kule tuesday.
 
give me a break! Mbowe kama anawajua hao awataje!!!! Mimi mwenyewe mbona viongozi wa ngazi za juu wa Chadema wamenifuata na kutaka nijiunge nao kwa ahadi za vyeo?!!
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo asema CCM yataka kumnunua yeye pamoja na upinzani wote tanzania

Mbowe adai CCM wanataka kumchukua

Mwandishi Wetu,DUA Jambo Forums Senior Member

HabariLeo; Saturday,January 06, 2007 @00:05

MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amedai kwamba amekataa ofa ya kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Mbowe alisema katika siku za karibuni kumekuwa na maombi kutoka CCM ya kumtaka yeye na viongozi wengine wa juu wa Chadema kujiunga na chama hicho kwa ahadi kadhaa lakini wamezikataa.

"CCM waliwahi kunifuata … Kila mtu makini aliyeko upinzani anafuatwa. Watu wanarudi CCM kwa ahadi za vyeo, fedha na biashara," alisema Mbowe na kudai kwamba CCM imepania kuusambaratisha upinzani kwa njia mbalimbali.

Alikataa kutaja wakati, waliomfuata na ahadi alizopewa. Viongozi wa CCM walipotafutwa jana hawakuwa tayari kuzungumzia madai hayo. Hata hivyo Mbowe, ambaye alisema utaratibu wa kuwashawishi viongozi wa upinzani ni sawa na rushwa ya kisiasa, alizungumzia uwezekano wa baadhi ya wanasiasa kutumia vibaya mwanya huo kwa kutapeli.

Kauli yake ya jana imekuja siku chache baada ya kumaliza ziara ya siku 10 mikoani kuwashukuru wananchi kwa kukipigia kura chama chake katika uchaguzi wa mwaka 2005, alipogombea urais wa Muungano kwa tiketi ya Chadema.

Kufuatia ziara hiyo, Katibu Mwenezi wa CCM Aggrey Mwanri aliitisha mkutano na waandishi wa habari juzi ambako aliponda baadhi ya madai yaliyotolewa na Mbowe kwenye ziara yake yakiwamo ya wizi wa kura na rushwa vinavyodaiwa kufanywa na CCM kwenye uchaguzi huo.

Mbowe pia alitetea matumizi ya helikopta katika ziara yake hiyo ya shukrani, kwa kusema wanaohoji "wana upeo finyu wa kufikiri." Katika mvua hii ningekuwa wapi katika siku 10, alisema na kuzungumzia jinsi ziara hiyo ilivyomfikisha wilaya kadhaa za mikoa ya Mara, Mwanza, Kagera, Kigoma, Shinyanga, Manyara, Arusha na Kilimanjaro.

Mwanafunzi Wa hull University imethibitishwa yupo DSM sio Hull kama wengine walivyodai ataanza labda Jumatatu 8/01/2007.
__________________
Story by DUA JF Senior Member
Dua la kuku halimpati mwewe
 
Mwanakijiji, nimeona masononeko yako. Pole na amka

Kwa mazingira ya Tanzania, wapinzani ni wa kuungwa mkono badala ya kulaumiwa.

Wachawi wa kwanza ni jamii yenyewe kwa kuwa wepesi kijiweka kando na kuwa mabingwa wa kulaumu.

Mchawi wa pili ni CCM kwa kuzuga kuruhusu vyama vyingi. Hakuna sheria za kuruhusu vyama vingi hapa,hakuna tume ya uchaguzi, tuanatengeneza mazingira ya chuki na hasira kiala unapofanyika uchaguzi. CCM imejitengenezea mazingira haramu ya kuwa na rasilimali nyingi zaidi ya washindani wao.


Demokrasia hailetwi na vyama vyingi wala kimoja.Demokrasia ni zao la watu. Hata tungekuwa na vyama aina gani kwa jinsi tulivyozubaa,tulivyowaogoa,tulivyowepesi kusubiri wengine wafanye ili sisi tufaidike au tulaumu hatuwezi kuipata hiyo demokrasia na hata maendeleo.

Na demokrasia haitaletwa kwenye sinia! Nasema kwa jinsi mambo yanavyoenda,tunatengeneza baruti itakayolipuka vibaya sana.

Nasita kuvilaumu vyama vya upinzani kwa maana hatuna mazingira ya ushindani,ni vigumu mno kwa vyama vya upinzani kufurukata.Achana na matatizo ya kisheria twende kwenye uelewa na mtazamo wa watu.


Watu wana uelewa mdogo sana juu ya masuala ya uraia. Pili,kuna unyanyapaa mkubwa sana kwa viongozi wa upinzani.Hawa kwa kiasi kikubwa wamekanwa na jamii.


Ni lini umesikia kiongozi wa upinzani akaalikwa kwenye hafla za kidini?(mara chache sana) viongozi wa CCM wanaalikwa! Pia wakialikwa kwenye matukio ya upinzani hawaendi, CHADEMA kwa mfano iliwaalika kwenye uzindui wa tumaini jipya, hawakutokea kwenye mkutano mkuu huwa wanajazana, wanafiki wakubwa! kwenye mahafali mashuleni na hata michezoni umesikia viongozi wa upinzani wakwa wageni rasmi?si tumesikia wakina Tenga walimkimbia mbowe, pale CHADEMA walipokwenda kuchangia stars?

Jamii imevikana vyama shindani,imekataa kuwachukulia kama sehemu ya jamii,ni viumbe wapweke! Ni vigumu sana kushuhudia ushindani wa hoja kwenye mazingira kama haya!

Tatu pamoja na uelwa mdogo, wananchi wamejazwa hofu. Watu ni waoga mno,hata kwenye vyama vya siasa watu hawaminiani utasikia huyu usalama wa taifa n.k,hatujiamini.


NNe,siasa za Tanzania hazina sura ya sera. Kwa sabubu ya toafauti kubwa ya kirasilimali baina ya vyama,ushindani unakuwa tayari umeegemea upande mmoja!CCM inakuwa imepora ushindi kwa kujipendelea kiraslimali hivyo kuvutia wataalam na wanafiki upande wake na fedha pia inatumika kama silaha ya kuhadaa wananchi maskini.

Tuimarihe rasilimali kwa vyama ili hatimae ushindani uhamie kwenye sera na hoja badala ya rasilimali!


Nasema kwa mazingira yalivyo sasa, hata tukiwa na chama cha upinzani kinachoongozwa na malaika hakitafurukuta. kitafurukuta vipi? bila ya rasilimali na umekanwa na jamii utafanya nii?

Ili tufaidike na vyama vyingi, na ikiwa watu wataendelea kulaamu pasipo kufanya lolote kuviimarisha,tutalazimika kuwa na chama toka mbinguni na ili kishindane na chama kinacho ongozwa na "chaguo la mungu" itabidi muumba mwenyewe asimame kama mgombea uraisi wa chama hicho kisha manabii wake kama wakina Mussa,Ibrahimu,Isaya N,K wasambae majimboni kugombea ubunge kwa tiketi ya chama cha mbinguni,hapo sasa tunaweza kufaidi matunda ya vyama vingi katika mazingira tuliyo nayo na ikiwa tutakuwa na wasomi walio mabingwa wa kukosoa, kulalamika na kusubiri vyama vibadilike na ndio wajiunge!


Ndipo nasema,tumejifikisha hapa wenyewe kwa msaada mkubwa sana wa CCM! ni CCM na jamii ndio vinastahhili lawama na laana!


vyama vya upinzani ni vyama vya umma na si kampuni ya mtu. Ni kituko kulaumu mfumo ambao hajuwahi kujaribiwa.Ni uongo kwamba tuna mfumo wa vyama vingi nchini na ni uongo kwamba hali iliyopo sasa nchini inachangiwa na vyama vya upinzani.

Ili taasisi yoyote ikue,inahitaji;Rasilimali fedha,Rasilimali watu,dira na mtandao. Ni jukumu la nani kuvilea vyama vyama vya upinzan ili vipate mahitaji haya ya msingii? Jibu lake ni jamii ambayo ni mimi na wewe.

Vyama vya upinzani vimenyimwa vyote hivyo na jamii. Tulirudisha mfumo wa vyama vingi kwa mguu mbaya,katiba ikaendelea kuwa ile ile na CCM ikarisishwa mali zote ambazo wavuja jasho wa Tanzania walichangia.Vyama vya upinzani vilambiwa vijikuze vinavyoweza, katika mazingira magumu kama hayo nawapongeza kwa kuweza kuendelea kuwepo bila ya kukataa tamaa kama Mwanakijiji!


Vyama havina rasilimali kwa sababu hatuvichangii na havina rasilimali watu bora kwa sababu hatuendi. Vyama vimedai katiba na mgawanyo wa rasilimali,vimesukuma ajenda kwa jamii na bado jamii imekaa tu kuviangilia. Jamii imekana jukumu lake la ulezi.

Ikumbukwa kwamba,vyama vya upinzani vinapolalamika juu ya katiba,juu ya tume ya uchaguzi na na juu ya matumizi mabaya ya rasilimali za taifa kwa manufaa ya chama kimoja, vinafanya hivyo kuushataki utawala kwa jamii ili jamii ichukue nafasi yake.Sasa kama wana jamii ambao ndio kama mahakama wa kuamua mashitaka ya vyama vya upinzani nao wanakata tamaa hali itakuaje?

Sikubalini na sipendi tabia ya kusuburi mtu mwingime akufanyie kitu,Ukiwa mzalendo wa kweli na unaguswa na matatizo ya nchi huwezi kusubiri mtu mwingine akushawishi usikate tamaa. Hii ni hatua ya juu kabisa ya kutowajibika.


Na isotoshe tungependwa tufutwa wapi kushawishiwa? kwenye kaya zetu? Mbona wanaongea kila siku? Majuzi kulikuwa na mkutano wa jangwani,.jana ]Mvungi wa NCCR alikuwa anazungumza ITV,haipiti wiki vyama vya upinzani kuzungumza pamoja na upweke wao.


Na tunatumia mizani gain kusema vyama vya upinzani havifanyi kazi?
Baada ya uchaguzi mkuu kumalizika. Jukuma la kwanza la Vyama vyote ilikuwa ni kutathmini na kuangalia mambo yanaendaje na kujipanga upya.Vyama vya CUF,CHADEMA na NCCR wametoa matamko yao juu ya uchaguzi amabayo baadhi yalichapwa katika magazeti.

Pia wamejiwekea mikakati ya miaka mitano na kujipanga upya vingine vikienda mbali kujizindua upya(CHADEMA). Vimeendelea kufanya kazi yake ya asili ya kuibana serekali na kutoa mapendekezo yao ambayo hayapewi uzito sana na vyombo vya habari.

Vyama vya upinzani vimenedelea kutoa elimu ya uraia pamoja na changamoto za rasilimali,vimeandaa hadi vipindi maalum kwenye luninga. Na CHADEMA sasa wameanza kuzunguka nchi nzima kushukuru wanachi na kujiimarisha.

Mimi msimamo wangu unabaki kuwa,tatizo ni jamii ya laini tuliyonao na sio vyama. Hatujawa yayari kutetea mfumo wa vyama vyingi wala kuvilea na kuvitetea vyama vyama upinzani. Tumejaa unafiki na kuachia kikundi kidogo kiendeshe siasa za nchi.

Hivi karibuni umepitishwa muswada wa kumpa mamlaka waziri wa TAMISEMI kuteuwa madiwani kwa lengo la kupindua halmashauri zilizchukuliwa na wapinzani.Vyama vimekwisha shitaki kwa wananchi bado tumekaa kimya ili pengine tuje kuvialamu.

Ni katika mazingira hayo,najenga hoja kwamba watanzania wenyewe ndio tunapaswa kijulaumu na si vyama vya upinzani. Wanafanya kazi katika mazingira magumu sana na ya upweke mno.

Nilikuwa katika mkondo wa kuwalaumu pia,ushiriki wangu kamilifu katika uchaguzi mkuu wa 2005 ulikuwa ni ufunuo,kama raia ninaewajibika nimelitambua jukumu langu adhimu la kulea na kukuza vyama mbadala pamoja na mfumo wa vyama vyingi.

Demokrasia ni zao la watu na si mfumo. Jamii isjisute.


Na je jamii ambayo imejiweka kando na imekataa kuvilea vyama vya siasa inatambua hakuna mfumo muafaka wa vyama vingi na bado wana matarajio! Haya ndio matarajio imaginary,unapanda bangi unategemea mchicha! Haya endelea kusubiri,huwezi jua ipo siku bangi ita "mutate" kuwa mchicha na hatimae utajiunga na chama kimoja baada ya "mutatiom" ila kwa sasa endelea kupalilia bangi ukitarajia mchicha.

.Mimi naamini katika dhana ya Mahtma Gandhi kwamba napaswa kuwa sehemu ya mabadiliko. Ni kwa kutoa mchango wangu hatimae naweza kujenga chama ambacho kitaendana na mtazamo wangu. Unavyotarajia chama kiwe na fikra kama zako,zitatoka wapi? Zitawasilishwa na nani? Kwanini unasubiri mwingine afanye? Wajibika au kaa kimya.


Pamoja na hayo CHADEMA(Kwa mfano) tayari imezunguka nchi nzima kukusanya maoni ya marekebisho katiba,ikafanya mkutano mkuu kupitisha katiba mpya,imeendesha mafunzo katika wilaya ya kuiimirisha huoni kazi wanzao fanya?

Imetoa matamko mazito yanye mawazo mbadala,tukianzia tamko la siku mia la utawala wa awamu ya nne,tamko la uchaguzi na hotuba ya uzinduzi wa tumaini jipya amablo sasa linateremshwa kila wilaya!
Pia imeunga mkono shughuli za kijamii kwa kuitembelea na kuzichangia Taifa stars pamoja na Taifa Queens. Huu ni mwaka wa kwanza na mwaka baada ya uchaguzi


Kwa mfano huu unasemaje kazi ya vyama vya upinzani haionekani?

Na ikiwa mfumo wa vyama vya upinzani hakidhi matarajio na mahitaji ya wakati,hapa si ndio jukumu la wanachi kuingilia? jamii iko wapi? Ukraine walifanya uchaguzi wa kizushi,jamii haikuridhika,ikaingilia! Jamii yetu haingilii inasubiri mambo yajitengeneze yenyewe! Au pengine inakubaliana na hali ilivyo sasa kwa hiyo unaweza kuwa unaisingizia kwamba ina matarajio! Yenyewe iaonyesha kuridhika kabisa!
 
Sina cha kuongeza mwache aliye na Muhimbili na daraja la Rufiji akisema ndiyo Mambo makubwa ya CCM haya miaka 45
 
Si jambo geni na hata Zitto kafuatwa mno .CCM na JK hawana nia ya maendeleo ila kuendeleza utawala wa CCM na ndiyo maana wao na wabunge wao niu watiifu kwa CCM na si Tanzania .

Kazi kubwa sana na tutegemee mengi maana jamaa wanajipanga kuunujua upinzani ushahidi uko wazi .
 
Mwanakijiji amejitahidi sana kujibu hoja...akajaribu,, halafu akaishia njiani, jazba zikapanda, akakana uanaCCM wake; na akahitimisha kwa kuikumbatia CCM kama chaguo lake pamoja na mamilioni wengine.

Mwanakijiji ameridhika kwamba miaka 45 baada ya uhuru, nchi yetu inapaswa kuwa katika kundi la NCHI MASKINI SANA duniani - licha ya raslimali kibao ilizonazo. Hapo anaona jitihada za kutosha. Anaona mapinduzi makubwa katika elimu ya Watanzania wanaojengewa vyumba na kulazimishwa waviite shule, bila walimu wa kutosha, bila vitabu wala maabara - miaka 45 baada ya uhuru.

Anaridhika na matumizi holela ya raslimali zetu - na kodi - kununulia vitu visivyo priorities za nchi; rejea radar ambayo haikutumika,, na ndege ya rais ambayo sasa JK anaogopa kwenda nayo Ulaya! Usisahau Twin Towers za BoT pale Dar es Salaam! Haoni mabilioni hayo yangeweza kusaidiaje uimarishaji wa afya za wananchi. haoni mabilioni hayo yengejenga shule ngapi za kisasa!

Anaridhika na ushindi wa kishindo wa CCM - kishindo cha kumwaga noti na kununua shahada za wapiga kura, ongezeko la vituo bandia (au hili ni jipya kwake); mabavu ya FFU kufanya kazi isiyo yao (usisahau ya CUF na Mahita); Janjaweed na uchaguzi Z'bar (vijana waliopelekewa kutoka Dar, waliosombwa na kina Makanda na Tarimba bado wanalalamikia posho waliyopewa. Waliahidiwa laki 2 kwa kupiga kura Karume ashinde, wakaambulia sh 50,000 na msosi wa hotelini); mitutu ya majeshi ya ulinzi na usalama mbele ya vituo vya kura; amri za amiri jeshi mkuu (Mkapa) kwa baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya yenye upinzani mkuu kwamba majimbo yakichukuliwa na upinzani watakiona; matumizi mabaya ya walimu wetu katika kuiba kura za wapinzani; na hongo kwa wasimamizi wa kura dhaifu wa opposition ili wakubali yaishe - mbinu za ushindi wa kishindo wa CCM.

Kwamba chama kinachopendwa na Mwanakijiji na mamilioni wengine kinafanya hivi hakijui udhaifu wake, bali sifa anazotaja Mwanakijiji!

WABUNGE wengi: Ndiyo. Kila mwenye akili timamu atakubaliana na hoja hii. Na wapinzani wanataka kweli wabunge wengi. Mazingira ya kuwapata yanatawaliwa na wenye dola na pesa - CCM. Umaskini uliokithiri miongoni mwa wanakijiji anaowasema Mwanakijiji ndilo daraja linalotumiwa na CCM. Laiti CCM ingekuwa inajivunia kuwawezesha wananchi kiuchumi, isingewahonga Tshirt na kanga wakati wa uchaguzi. Laiti ingekuwa inajivunia elimu ya kutosha kwa wananchi wake, isingewahadaa kwa propaganda na ahadi hewa nao wakakubali. Wala isingewaambia kwamba ni CCM tu yenye uwezo wa kujenga barabara na madaraja; kwani hayo yanaweza kujengwa na chama chochote kwa kodi zetu... Tunachosema hapa ni kwamba kasi ya CCM kwa miaka 45 si ya kusifika. Na sana, ,kadiri umri wa taifa unvyoongezeka, maendeleo yaliyokluwapo nayo yanaendelea kuchakaa.

Wenye dola na pesa ndiyo walioshikilia mfumo wa uchaguzi, na kila wanapoguswa wanakimbilia bungeni kwenye wabunge wao wengi, hata tume za rais zilipojaribu kushauri zilipuuzwa. Na wapinzani wakisusa uchaguzi kwa sababu ya kutoridhika na mfumo, watakaoshiriki ndio watakaohesabiwa! Ya Zanzibar mwaka 2000 yawe funzo! Hata wakishinda, wenye uwezo wa dola wanaweza kubeba masanduku wakayaficha watakako, halafu wakatoa matokeo. Wananchi wakija juu, sana sana wataishia kurusha mawe dhidi ya mitutu...Hayo ni matumizi mazuri ya madaraka? Raslimali?

CHADEMA na urais: Kabla ya mwaka 2005, Chadema hakikuwahi kugombea urais. Mwaka 1995 kilimuunga mkono Mrema (NCCR-Mageuzi). Yaliyotokea bado mnayajua. Mwaka 2000 kilimuunga mkono Lipumba (CUF). Mnajua kilichotokea. Wakati huo huo kilikuwa na wabunge wa Kigoma, Moshi Mjini, Hai, na Karatu na mmoja wa viti maalumu (5) kama nakumbuka vema. Mwaka 2005 kikasema nasi sasa zamu yetu tuungwe mkono, vyama vingine nikasema hapana. Kikaweka mgombea wake (Mbowe). Hilo kosa!

Wapo wanaosema heri Mbowe angegombea ubunge kuliko urais ili atoe mchango bungeni. Sawa, lakini miaka mitano iliyopita alitoa mchango mkubwa bungeni - hasa hatika suala la ununuzi wa ndege ya rais ambayo haikuwa yay lazima kwa gharama hizo - serikali ilimpuuza! Hiyo si hoja sana. Lazima tuangalie mtandao na uhai wa chama chake. Kwa kugombea urais amekijenga zaidi chama nchi nzima; ameongeza idadi ya wabunge wa chama kutoka 5 hadi 11 na idadi ya madiwani imeongezeka...Ikumbukwe hakuanza tu kugombea, zilishafanyika jitihada za chini chini kuamsha chama nchi nzima. Kama angegombea ubunge, angekuwa amepuuza chama amejibeba mwenyewe. Hivi sasa ameanza tena kujenga chama kwa ziara zake na mikakati mingine aliyoitaja Mnyika hapa. Si kazi ya mara moja, lakini lazia ifanyike. Hili ni kosa analopaswa kuhukumiwa kwalo?


Umri wa uhuru wa taifa hauboreshi, bali unachakaza maendeleo yetu. Waulize waliosomea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam miaka ya 1967-78 hivi, kimeendelea leo kuliko kilivyokuwa wakati ule? Kumetokea nini? Mbona vyuo vizee zaidi duniani vimeendelea kuwa bora? Na leo mnajenga vingine kuongeza idadi...ubora je?

Nchi yenye miaka 45 ya uhuru bado inategemea umeme wa mabwawa ya maji ya mvua (nguvu za mungu)...teknolojia inatusaidiaje? Mungu keshatupatia raslimali zote hizo, mito, maziwa, mvua ya kutosha kila msimu (isipokuwa katika vipindi vichache), upepo, makaa ya mawe, na nishati nyingine...juu ya yote hayo wasomi...bado tunakwenda Thailand kuomba ndege za kutengeneza mvua ya kujaza mabwawa yetu!

We are not serious enough. CCM inazeeka vibaya. Haipati hekima, bali udahifu wa uzee. Itashabikiwa tu na wanaozeeka kama ilivyo! Mwanakijiji endelea na ushabiki, yawezekana itakuchukua muda mrefu kuelewa mabo haya madogo madogo. Hatulingani uwezo; Mungu alituumba tofauti. Lakini wenzio tumekueleza. Tafuta muda utafakari. Kama ni kuipenda CCM, wewe si wa kwanza. Wengine tulikutangulia. Lakini kama alivyosema Nyerere mwenyewe, CCM si mama yetu. Pale inapoonekana kuweka kpembeni malengo ya awali yaliyokusudiwa kuleta mapinduzi ya kimaendeleo katika maisha ya watanzania, pale inapoanza kutafuta hapa na pale kutaja mifano ya mafanikio (yasiyo mafanikio) yake...wenye akili wanatazamana na kutabasamu kwa dhihaka!

Aliyewahi kuwa Katibu wake Mkuu, Horace Kolimba, aliwahi kuwaeleza wana CCM kwamba hawana dira wala mwelekeo. Aliishia wapi? Mtu aliyekijua chama kweli kweli alisema hivyo. Hakutaja barabara, viwanda, wala madaraja...upeo wake ulikuwa juu ya hayo. Iweje sisi?
 
Umesema vyema sana na huyu kijana mwache aendelee kulia na Muhimbili akiwa US. Njoo TZ uende Muhimbili ukitoka njoo uandike hapa .
 
Nimesoma katika Mwananchi Makamba anakana kuwanunua wapinzani, Lakini waandishi wamesahau kumkumbusha kuwa alipomnunua Kabourou alihojiwa, akajitapa: "Nisipomnunua Kaburu, daktari, nimnunue nani?"

Si MBowe na Zito tu. Hata Chacha wa Tarime, amekuwa akifuatwa na akina Nsanzugwanko, wanamwambia aachane na CHADEMA aingie CCM mambo yatamnyokea kama wao! Zito aliambiwa kwamba anaonekana ana akili, na kwa kuwa Kigoma haina wasomi wengi, anaweza kuukwaa uwaziri. Akawajibu: "SItafuti uwaziri wa CCM..." Mnyika huyo ndiyo usiseme. Simu za Makamba zimekuwa zikiminimika kwake hata kabla hawajaenda kwa Kabourou! Nasikia hata Mama Komu wameshamwendea!

Ni hawa hawa wanaosema hawakiogopo CHADEMA. Sasa mbona wanawaandama kwa vijipesa! Wanaogopa nini? Mnakumbuka ile stori ya Tanzania Daima KUMBOMOA MBOWE? Nasikia kina JK na Lowassa wameshaanza kumwandama chini chini. Na hii ni mbinu mojawapo. Mbona hawakuiandama Chadema kabla ya profile ya Mbowe kupanda? Msisahau sakata la diwani wa Chadema Kigoma aliyetekwa na kutoroshewa Dar es Salaam na kina Nsazungwanko, wakawekewa mtego na kukamatwa naye uwanja wa ndege Dar es Salaam. Waache tu, ipo siku wataumbuka!
 
Back
Top Bottom