Mwanakijiji, nimeona masononeko yako. Pole na amka
Kwa mazingira ya Tanzania, wapinzani ni wa kuungwa mkono badala ya kulaumiwa.
Wachawi wa kwanza ni jamii yenyewe kwa kuwa wepesi kijiweka kando na kuwa mabingwa wa kulaumu.
Mchawi wa pili ni CCM kwa kuzuga kuruhusu vyama vyingi. Hakuna sheria za kuruhusu vyama vingi hapa,hakuna tume ya uchaguzi, tuanatengeneza mazingira ya chuki na hasira kiala unapofanyika uchaguzi. CCM imejitengenezea mazingira haramu ya kuwa na rasilimali nyingi zaidi ya washindani wao.
Demokrasia hailetwi na vyama vyingi wala kimoja.Demokrasia ni zao la watu. Hata tungekuwa na vyama aina gani kwa jinsi tulivyozubaa,tulivyowaogoa,tulivyowepesi kusubiri wengine wafanye ili sisi tufaidike au tulaumu hatuwezi kuipata hiyo demokrasia na hata maendeleo.
Na demokrasia haitaletwa kwenye sinia! Nasema kwa jinsi mambo yanavyoenda,tunatengeneza baruti itakayolipuka vibaya sana.
Nasita kuvilaumu vyama vya upinzani kwa maana hatuna mazingira ya ushindani,ni vigumu mno kwa vyama vya upinzani kufurukata.Achana na matatizo ya kisheria twende kwenye uelewa na mtazamo wa watu.
Watu wana uelewa mdogo sana juu ya masuala ya uraia. Pili,kuna unyanyapaa mkubwa sana kwa viongozi wa upinzani.Hawa kwa kiasi kikubwa wamekanwa na jamii.
Ni lini umesikia kiongozi wa upinzani akaalikwa kwenye hafla za kidini?(mara chache sana) viongozi wa CCM wanaalikwa! Pia wakialikwa kwenye matukio ya upinzani hawaendi, CHADEMA kwa mfano iliwaalika kwenye uzindui wa tumaini jipya, hawakutokea kwenye mkutano mkuu huwa wanajazana, wanafiki wakubwa! kwenye mahafali mashuleni na hata michezoni umesikia viongozi wa upinzani wakwa wageni rasmi?si tumesikia wakina Tenga walimkimbia mbowe, pale CHADEMA walipokwenda kuchangia stars?
Jamii imevikana vyama shindani,imekataa kuwachukulia kama sehemu ya jamii,ni viumbe wapweke! Ni vigumu sana kushuhudia ushindani wa hoja kwenye mazingira kama haya!
Tatu pamoja na uelwa mdogo, wananchi wamejazwa hofu. Watu ni waoga mno,hata kwenye vyama vya siasa watu hawaminiani utasikia huyu usalama wa taifa n.k,hatujiamini.
NNe,siasa za Tanzania hazina sura ya sera. Kwa sabubu ya toafauti kubwa ya kirasilimali baina ya vyama,ushindani unakuwa tayari umeegemea upande mmoja!CCM inakuwa imepora ushindi kwa kujipendelea kiraslimali hivyo kuvutia wataalam na wanafiki upande wake na fedha pia inatumika kama silaha ya kuhadaa wananchi maskini.
Tuimarihe rasilimali kwa vyama ili hatimae ushindani uhamie kwenye sera na hoja badala ya rasilimali!
Nasema kwa mazingira yalivyo sasa, hata tukiwa na chama cha upinzani kinachoongozwa na malaika hakitafurukuta. kitafurukuta vipi? bila ya rasilimali na umekanwa na jamii utafanya nii?
Ili tufaidike na vyama vyingi, na ikiwa watu wataendelea kulaamu pasipo kufanya lolote kuviimarisha,tutalazimika kuwa na chama toka mbinguni na ili kishindane na chama kinacho ongozwa na "chaguo la mungu" itabidi muumba mwenyewe asimame kama mgombea uraisi wa chama hicho kisha manabii wake kama wakina Mussa,Ibrahimu,Isaya N,K wasambae majimboni kugombea ubunge kwa tiketi ya chama cha mbinguni,hapo sasa tunaweza kufaidi matunda ya vyama vingi katika mazingira tuliyo nayo na ikiwa tutakuwa na wasomi walio mabingwa wa kukosoa, kulalamika na kusubiri vyama vibadilike na ndio wajiunge!
Ndipo nasema,tumejifikisha hapa wenyewe kwa msaada mkubwa sana wa CCM! ni CCM na jamii ndio vinastahhili lawama na laana!
vyama vya upinzani ni vyama vya umma na si kampuni ya mtu. Ni kituko kulaumu mfumo ambao hajuwahi kujaribiwa.Ni uongo kwamba tuna mfumo wa vyama vingi nchini na ni uongo kwamba hali iliyopo sasa nchini inachangiwa na vyama vya upinzani.
Ili taasisi yoyote ikue,inahitaji;Rasilimali fedha,Rasilimali watu,dira na mtandao. Ni jukumu la nani kuvilea vyama vyama vya upinzan ili vipate mahitaji haya ya msingii? Jibu lake ni jamii ambayo ni mimi na wewe.
Vyama vya upinzani vimenyimwa vyote hivyo na jamii. Tulirudisha mfumo wa vyama vingi kwa mguu mbaya,katiba ikaendelea kuwa ile ile na CCM ikarisishwa mali zote ambazo wavuja jasho wa Tanzania walichangia.Vyama vya upinzani vilambiwa vijikuze vinavyoweza, katika mazingira magumu kama hayo nawapongeza kwa kuweza kuendelea kuwepo bila ya kukataa tamaa kama Mwanakijiji!
Vyama havina rasilimali kwa sababu hatuvichangii na havina rasilimali watu bora kwa sababu hatuendi. Vyama vimedai katiba na mgawanyo wa rasilimali,vimesukuma ajenda kwa jamii na bado jamii imekaa tu kuviangilia. Jamii imekana jukumu lake la ulezi.
Ikumbukwa kwamba,vyama vya upinzani vinapolalamika juu ya katiba,juu ya tume ya uchaguzi na na juu ya matumizi mabaya ya rasilimali za taifa kwa manufaa ya chama kimoja, vinafanya hivyo kuushataki utawala kwa jamii ili jamii ichukue nafasi yake.Sasa kama wana jamii ambao ndio kama mahakama wa kuamua mashitaka ya vyama vya upinzani nao wanakata tamaa hali itakuaje?
Sikubalini na sipendi tabia ya kusuburi mtu mwingime akufanyie kitu,Ukiwa mzalendo wa kweli na unaguswa na matatizo ya nchi huwezi kusubiri mtu mwingine akushawishi usikate tamaa. Hii ni hatua ya juu kabisa ya kutowajibika.
Na isotoshe tungependwa tufutwa wapi kushawishiwa? kwenye kaya zetu? Mbona wanaongea kila siku? Majuzi kulikuwa na mkutano wa jangwani,.jana ]Mvungi wa NCCR alikuwa anazungumza ITV,haipiti wiki vyama vya upinzani kuzungumza pamoja na upweke wao.
Na tunatumia mizani gain kusema vyama vya upinzani havifanyi kazi?
Baada ya uchaguzi mkuu kumalizika. Jukuma la kwanza la Vyama vyote ilikuwa ni kutathmini na kuangalia mambo yanaendaje na kujipanga upya.Vyama vya CUF,CHADEMA na NCCR wametoa matamko yao juu ya uchaguzi amabayo baadhi yalichapwa katika magazeti.
Pia wamejiwekea mikakati ya miaka mitano na kujipanga upya vingine vikienda mbali kujizindua upya(CHADEMA). Vimeendelea kufanya kazi yake ya asili ya kuibana serekali na kutoa mapendekezo yao ambayo hayapewi uzito sana na vyombo vya habari.
Vyama vya upinzani vimenedelea kutoa elimu ya uraia pamoja na changamoto za rasilimali,vimeandaa hadi vipindi maalum kwenye luninga. Na CHADEMA sasa wameanza kuzunguka nchi nzima kushukuru wanachi na kujiimarisha.
Mimi msimamo wangu unabaki kuwa,tatizo ni jamii ya laini tuliyonao na sio vyama. Hatujawa yayari kutetea mfumo wa vyama vyingi wala kuvilea na kuvitetea vyama vyama upinzani. Tumejaa unafiki na kuachia kikundi kidogo kiendeshe siasa za nchi.
Hivi karibuni umepitishwa muswada wa kumpa mamlaka waziri wa TAMISEMI kuteuwa madiwani kwa lengo la kupindua halmashauri zilizchukuliwa na wapinzani.Vyama vimekwisha shitaki kwa wananchi bado tumekaa kimya ili pengine tuje kuvialamu.
Ni katika mazingira hayo,najenga hoja kwamba watanzania wenyewe ndio tunapaswa kijulaumu na si vyama vya upinzani. Wanafanya kazi katika mazingira magumu sana na ya upweke mno.
Nilikuwa katika mkondo wa kuwalaumu pia,ushiriki wangu kamilifu katika uchaguzi mkuu wa 2005 ulikuwa ni ufunuo,kama raia ninaewajibika nimelitambua jukumu langu adhimu la kulea na kukuza vyama mbadala pamoja na mfumo wa vyama vyingi.
Demokrasia ni zao la watu na si mfumo. Jamii isjisute.
Na je jamii ambayo imejiweka kando na imekataa kuvilea vyama vya siasa inatambua hakuna mfumo muafaka wa vyama vingi na bado wana matarajio! Haya ndio matarajio imaginary,unapanda bangi unategemea mchicha! Haya endelea kusubiri,huwezi jua ipo siku bangi ita "mutate" kuwa mchicha na hatimae utajiunga na chama kimoja baada ya "mutatiom" ila kwa sasa endelea kupalilia bangi ukitarajia mchicha.
.Mimi naamini katika dhana ya Mahtma Gandhi kwamba napaswa kuwa sehemu ya mabadiliko. Ni kwa kutoa mchango wangu hatimae naweza kujenga chama ambacho kitaendana na mtazamo wangu. Unavyotarajia chama kiwe na fikra kama zako,zitatoka wapi? Zitawasilishwa na nani? Kwanini unasubiri mwingine afanye? Wajibika au kaa kimya.
Pamoja na hayo CHADEMA(Kwa mfano) tayari imezunguka nchi nzima kukusanya maoni ya marekebisho katiba,ikafanya mkutano mkuu kupitisha katiba mpya,imeendesha mafunzo katika wilaya ya kuiimirisha huoni kazi wanzao fanya?
Imetoa matamko mazito yanye mawazo mbadala,tukianzia tamko la siku mia la utawala wa awamu ya nne,tamko la uchaguzi na hotuba ya uzinduzi wa tumaini jipya amablo sasa linateremshwa kila wilaya!
Pia imeunga mkono shughuli za kijamii kwa kuitembelea na kuzichangia Taifa stars pamoja na Taifa Queens. Huu ni mwaka wa kwanza na mwaka baada ya uchaguzi
Kwa mfano huu unasemaje kazi ya vyama vya upinzani haionekani?
Na ikiwa mfumo wa vyama vya upinzani hakidhi matarajio na mahitaji ya wakati,hapa si ndio jukumu la wanachi kuingilia? jamii iko wapi? Ukraine walifanya uchaguzi wa kizushi,jamii haikuridhika,ikaingilia! Jamii yetu haingilii inasubiri mambo yajitengeneze yenyewe! Au pengine inakubaliana na hali ilivyo sasa kwa hiyo unaweza kuwa unaisingizia kwamba ina matarajio! Yenyewe iaonyesha kuridhika kabisa!