The Only Thing We Have to Fear is Fear itself

The Only Thing We Have to Fear is Fear itself

Mkandara,
Nimeshakusikia mwanetu. Ntakaa kimya. Mwanakijiji, pongezi na uendelee kupanda juu.
 
Hahahahahaha....sasa Mkandara anamtaka huyo ES aanze balaa humu!!! Kuna mtu ambaye anaweza akavumilia mashuzi yake kweli?? Mhhhh....haya...mi yangu pua!!
 
Ngabu,

Sasa umenipa picha nzima kuwa hunifahamu toka Dar kwani neno hilo "SHUZI" limetumika enzi zetu kama ni kitu cha kusisimua!...
Lunyungu,
Wewe najua yamekupita mbali haya...
Hata muziki safi unaosisimua uliitwa shuzi...lugha ya mabaharia tena!
 
Mi mwenzio nilikuwa na respond hiyo comment ya Lunyungu. It doesn't mean I took your "mishuzi" comment literally!! Come on bro....loosen up. Don't be so uptight. Sometimes you got to joke a little bit. You are too intoxicated with politics. What else do you do in your spare time??
 
Super star Ebby Thriller, nitasema kwa heshima yako,

Ubunge ambao hata Amina Chifupa anao ni wa kujisifia tena ndio maana watu siku hizi hunyamaza kimyaaa!

Wenye elimu huwa hawasemi kuwa wanayo, ni madebe matupu ndiyo hayaishi kutika,

Ushamba ni maneno ndio hujisema, kati ya born town na watindiga na hasa majina!

Mzee Zanaki you got it right, hakuna mwenye ID ya mtu wala info, ila watu wanataka kutisha wengine waadike wanavyotaka wao, ndio maana tutaingilia siku zote tukiuona huo ujinga,

Mzeee MMJ maneno mazito, na Super Thriller heshima mbele, tuwasiliane!
 
I can't believe people in here really buy your mumbo-jumbo!!!!
You never make sense. You can't construct simple sentences let alone spell. You can't express yourself. You just ramble. And people listen to you??? That is beyond me.
 
please please tuvumiliane hata kama tunapishana kimawazo na mtazamo.thanx
 
Naona zoa zoa inaendelea, sijui itaishia wapi! Mwishowe kina Lyatonga nao watajisalimisha!

Kilio upinzani: JK leo kupokea vinara wengine

Na Mary Wejja, Jijini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, CCM, Bwana Jakaya Kikwete, leo anatarajiwa kupokea vinara waliotimka kutoka vyama mbalimbali vya upinzani.

Waliza wapinzani kwa kuwapokea rasmi vinara kadhaa wa kambi hiyo walioamua kutimkia CCM.

Hatua hiyo inatarajiwa kuibua kilio kingine kizito kwa kambi ya upinzani ambayo hivi karibuni, imeripotiwa ikitoa shutuma nzito kwa CCM, kwamba inawarubuni watu wake muhimu kwa nia ya kuisambaratisha kambi yao.

Malalamiko hayo mazito ya upinzani, na ambayo yamekuwa yakikanwa na CCM, yameibuka hivi karibuni baada ya vinara wao kadhaa kutimka upinzani na kwenda CCM, wakiwemo Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Tambwe Hiza na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Dk. Walid Amaan Kabourou.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe, amewahi kukaririwa katika moja ya mikutano yake, akimtaka Katibu Mkuu wa CCM, Luteni Mstaafu Yusuph Makamba kuacha kuwa `bize` katika kuwanunua wapinzani na badala yake, afanye kazi ya kumkumbusha Rais Kikwete juu ya ahadi walizotoa kwa wananchi wakati wa Uchaguzi Mkuu na kuzitekeleza.

Hatahivyo, CCM, kupitia kwa Katibu wake wa Uenezi na Itikadi, Bw. Aggrey Mwanri, wakatoa ufafanuzi wa madai hayo mazito, wakisema kuwa sera zao nzuri na mipango bora iliyonayo ndiyo ndoano yao katika kuwanasa wapinzani kila kukicha.

Akizungumza na Alasiri jana, Kada wa CCM ambaye pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Dk. Lenny Kasoga, amesema Rais Kikwete atapokea vinara 11 wa upinzani `waliojisalimisha` katika tawi lao la Chuo Kikuu na pia, atawapokea wananchi wengine kadhaa walioamua kutua CCM baada ya kuvutiwa na sera nzuri na zinazotekelezeka za chama chao tawala.

``Mbali na shughuli hiyo ya kuwapokea wanachama wapya wanaotoka upinzani, pia Mheshimiwa Rais atazindua Tawi la CCM la Chuo Kikuu huria,`` akasema Dk. Kasoga.

Bila ya kutaja majina ya vigogo wa upinzani watakaopokewa rasmi na Rais Kikwete leo, Dk. Kasoga amesema shughuli hiyo itafanyika katika viwanja vya CCM Mwinjuma na zimeandaliwa na Tawi la CCM Chuo Kikuu cha Dar es salaa, likishirikiana na wanachama wengine wa CCM wilayani Kinondoni.
 
Wapendwa,

Salaam,

Hivi karibuni tulijadili kidogo kwenye sekretariati ya chama tamko la CCM ambalo lilitoa shutuma kadhaa kwa CHADEMA ikiwemo uchaga nk. na kujibu hoja kadhaa alizotoa Freeman ziarani.

Naweka hapa tamko lililotolewa na Tumbo ambalo linajibu pia baadhi ya maswali yalikuwa yakiulizwa hapa hususani:

Je, CHADEMA ni chama cha wachaga?

Je, ziara ya Mbowe ilikuwa ni ya kushukuru tu na hivyo ilikuwa upotevu wa muda?

Je, CHADEMA ilikubaliana na matokeo ya uchaguzi mkuu 2005?

Je, CHADEMA haimpi ushirikiano kikwete katika vita dhidi ya rushwa kama CCM ilivyosema?

Je, Nani mwongo kati ya Mbowe na tahariri ya Mtanzania?

Sasa endelea,

Yale maswali ya family bussiness na conservative nitayajibu katika thread mwafaka katika wakati mwafaka:
TAARIFA KWA UMMA

SHUTUMA HIZI KWA CHADEMA NA FREEMAN MBOWE SI ZA KWELI

Utangulizi:

Mwishoni mwaka 2006 na mwanzoni mwaka huu shutuma kadhaa zimeelekezwa kwa CHADEMA na viongozi wake hususani Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe. Mwanzoni shutuma hizi zimekuwa zikitolewa na wanasiasa wanaojitoa kambi ya upinzani na kujiunga na CCM.

Shutuma hizi ni pamoja na:
1. Kuwa CHADEMA awali kilianzishwa wakati wa ukoloni kikijulikana kama Chagga Development Manifesto (CHADEMA) ambacho bado kinaendelea na mwelekeo huo(Rejea Majira: 24/12/2006.
2. CHADEMA ina mrundikano wa watu wa kabila la wachagga. Haipaswi kuwa ‘chama cha demokrasia na maendeleo’ badala yake inapaswa kuitwa “chagga development manifesto” Rejea Mwananchi: 24/12/2006.(Hoja hii ilirudiwa katika vyombo mbalimbali vya habari kwa wiki kadhaa mfululizo wakinukuliwa viongozi wachache waliojitoa kutoka upinzani).

Awali Chadema tulipuuza uzushi huu. Lakini kutokana na kauli hizi kurudiwa rudiwa mara kwa mara tunaamini kuwa uwongo na upotoshaji huu unaweza kugeuzwa na umma watanzania ukaaminishwa kuwa ndio ukweli.

Aidha, tunatoa taarifa hii kufuatia taarifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Aggrey Mwanri iliyochapwa katika vyombo mbalimbali vya habari 5 Januari 2007 ambapo CCM imetoa shutuma kadhaa kwa CHADEMA na Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe.

Pia taarifa hii imetolewa kujibu shutuma kadhaa zilizoelekezwa kwa Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe kupitia maoni ya Mhariri wa gazeti la Mtanzania la tarehe 5 Januari 2007 yaliyokuwa na kichwa cha habari “Wapinzani tafuteni njia bora za kukubalika”.

SI KWELI KUWA CHADEMA NI CHAMA CHA WACHAGA KILICHOANZISHWA TOKA WAKATI WA KUDAI UHURU

Mtanzania yeyote mwenye ufahamu wa kawaida kabisa wa historia ya nchi yetu, atakubaliana nasi kuwa katika orodha ya vyama vya siasa vilivyokuwepo kabla ya uhuru, hakuna chama kilichoitwa CHADEMA. Ukweli ni kuwa CHADEMA ni chama kilichoanzishwa na kusajiliwa mara baada ya Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi. Na jina la CHADEMA lilibuniwa na Simon Madete ambaye ni Msukuma. Hii inatufanya tubaki na maswali mengi kuhusu nia ya wanaosambaza uzushi huu.

SI KWELI KWAMBA CHADEMA IMEJAA WACHAGA

Kwa akili za kawaida, shutuma kwamba CHADEMA imejaa wachaga maana yake ni kwamba CHADEMA ina viongozi na wanachama wengi wachagga kuliko kabila lolote hapa Tanzania. Je ni kwa kiasi gani kauli hiyo ina ukweli?.

Katika safu ya juu ya uongozi wa kitaifa wa CHADEMA yenye viongozi sita: wenyeviti na makatibu mchaga ni mmoja tu-Mwenyekiti wa chama Taifa, Freeman Mbowe. Viongozi wengine wanatoka makabila mengine kama MuIraq, Myao, Mpemba na Mu-Unguja.

Aidha katika sekretariati ya chama taifa ambacho ndio chombo kinachosimamia utekelezaji wa kila siku wa shughuli za chama kikiwa na kurugenzi 9, kati ya wakurugenzi wake mchaga ni mmoja tu. Na wasukuma ni watatu. Kwa nini hawasemi kwamba CHADEMA ni chama cha wasukuma?

Kadhalika mpaka sasa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ameteua wajumbe wanne wa Kamati Kuu, kati yao hakuna mchaga hata mmoja na kati yao wawili ni wahaya, Profesa Mwesiga Baregu na Balozi Ngaiza. Kwa nini hawakusema kwamba CHADEMA ni chama cha wahaya?

Kwa upande mwingine kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi uliopita, jimbo ambalo CHADEMA iliongoza kwa uwingi mkubwa zaidi wa kura ni Tarime ikiwa asilimia zaidi ya 64. Kama CHADEMA ni chama cha wachaga kwa nini jimbo la kwanza lisingekuwa la mkoa wa Kilimanjaro?

Kati ya majimbo kumi ambayo CHADEMA ilifanya vizuri zaidi, jimbo la Kilimanjaro ni moja tu la Moshi mjini huku mikoa kama Kigoma, Rukwa ikiwa na majimbo mawili ambayo CHADEMA imefanya vizuri zaidi.

Kama CHADEMA ingekuwa chama cha wachaga si ingefanya vizuri zaidi katika majimbo ya Kilimanjaro?

Je, wanataka kutuambia kuwa Mara, Kigoma, Rukwa na mikoa mingine ambayo CHADEMA imefanya vizuri kote kumejaa wachaga?

Kwa mantiki hiyo basi, si kweli kwamba CHADEMA ni chama kilichojaa wachaga. CHADEMA ni chama cha kitaifa. Kinachojumuisha wanachama na wapenzi wa asili na hali mbalimbali.

Lakini swali la kujiuliza ni je wachaga hawana haki ya kuwa sehemu ya viongozi katika taifa na wanachama wa CHADEMA?

Zaidi ya hayo tunawashangaa wakitoa hoja kwamba CHADEMA imejaa wachaga. Lakini tunawashangaa zaidi kwa kuwa hatukuwasikia akisema chochote pale Rais Kikwete alipoteua wachaga na Watanzania wenye asili ya Kilimanjaro wengi zaidi katika baraza la mawaziri kuliko makabila mengine.

Je, kwa mantiki ya wazushi kama hao serikali ya Kikwete ni ya wachaga? Je, kwa kuwa wachaga ndio kabila lenye wabunge wengi zaidi kati ya wabunge wa viti maalumu wa CCM na CHADEMA, je kwa kigezo hiki tu tuseme kwamba CCM na CHADEMA ni vyama vya wachaga?

Je, kwa CCM kuwa na wabunge wa viti maalum wachaga hata katika mikoa mingine ya nchi yetu zaidi ya Kilimanjaro wanapotoka wachaga je, kwa uchambuzi wa wazushi kama hao wanaweza kusema kwamba CCM ni chama cha wachaga?

Hatukupenda kujadili viongozi kwa kutazama makabila yao. Lakini tumeamua kutoa uchambuzi huu kwa sababu suala la ukabila ni nyeti sana kwa mustakabali wa nchi yetu na kwamba kwa kutoa mifano hai tutathibitisha wazi uzushi wa watu hawa.

Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kuasa kwamba kufanya dhambi ya ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu, ukianza huwezi kuacha.

Sisi tunaamini kauli za wazushi kama hawa zinapandikiza mbegu ya ubaguzi miongoni mwa watanzania na kuwashawishi watu kutazamana kwa misingi ya makabila yao. Tukiwaruhusu watu kama hawa tutaweka mashakani mshikamano na amani yetu hapa nchini.

Tunatoa mwito kwa watanzania kupuuza na kukumea kauli za viongozi kama hawa. CCM inaendelea kukumbatia wazushi hawa na uzushi wao, watanzania watakuwa na kosa gani wakianza kuamini kwamba chama tawala kinapandikiza mbegu za ubaguzi? Na kwa upande mwingine, tunatoa rai kwa vyombo vya habari kuchambua kwa kina kauli za watu kama hawa kwani uwongo ukisemwa sana wananchi wanaweza kuaminishwa kwamba ni ukweli.

Katika taarifa yake CCM imeinukuu shutuma ya wanaotoka upinzani ya kulalamikia tabia za ubabe na udini ndani ya CHADEMA? Ni ubabe upi huo? Ni udini upi huo ulioko katika CHADEMA? Hivi katika vyama vikuu vya siasa hapa nchini kuna chama ambacho safu yake ya kitaifa ina uwiano wa kidini kama CHADEMA? Mwalimu Nyerere aliwahi kusema pia kwamba katika kutafuta uongozi kuna watu wanaweza kutumia vigezo vya kijinga kama udini na ukabila kujihalalisha ili kufikia malengo yao na ndivyo wanavyofanya watu jamii hii.

SI KWELI KWAMBA VYOMBO VYA HABARI VILINUKUU KWAMBA ZIARA YA MWENYEKITI NI KUSHUKURU WANANCHI PEKEE

Ukweli ni kwamba vyombo vya habari viliweka bayana kwamba malengo ya ziara za awamu ya kwanza ya CHADEMA iliyomalizika hivi karibuni yalikuwa:Kuwashukuru watanzania walioiunga mkono CHADEMA katika uchaguzi mkuu 2005; Kuwaandaa wananchi kujenga na kuimarisha CHADEMA kwa lengo la kuimarisha upinzani nchini na kuhamasisha uwajibikaji wa viongozi na wananchi baada ya mwaka mmoja wa serikali ya awamu ya nne. Ukweli ni kwamba Mwenyekiti alitumia kati ya dakika 45 na lisaa limoja unusu katika mikutano hii kuzungumzia masuala haya. Je, CCM ilitarajia Mwenyekiti wa CHADEMA afunge safari kwenda mikoani kusema asante pekee na kurejea?
 
KAULI YA MWENYEKITI KWAMBA CCM ‚INANUNUA WAPINZANI NI YA KWELI’.

Kauli aliyoitoa Mwenyekiti kwamba Katibu wa CCM, Ndugu Yusuph Makamba aihimize serikali ya CCM kuwaletea watanzania maisha bora badala ya kutumia muda mwingi ‚kuwanunua’ viongozi na wanachama maarufu kutoka upinzani ni ya kweli. Nani amesahau jinsi ambavyo CCM ilijaribu kumnunua diwani wa CHADEMA Kigoma Ujiji mwanzoni mwa mwaka jana na kumtoroshea Dar es salaam?

Huu ni mfano tu lakini yapo maeneo kadhaa ambapo hujuma kama hizi zimejitokeza. Ishara za ‚kuwanunua’ baadhi ya viongozi wa upinzani ziko wazi kwani hata Katibu Mkuu wa CCM, Makamba amenukuliwa na vyombo vya habari akisema hadharani kwamba wanaotoka upinzani wanakwenda CCM kuganga njaa.

Hata hivi karibuni wakati akiwapokea wanachama wa upinzani alitoa kauli iliyorushwa moja kwa moja (Live) na vyombo vya habari akimwambia Mwenyekiti kwamba ametimiza maagizo ya kuwapa ‚posho’ wanachama hao ili waweze kuwepo Dodoma. Lakini kwa upande mwingine sababu zinazotolewa na wanaotoka upinzani zinaacha maswali mengi; wengi husingizia ama ubaguzi au kwamba CCM imeweza kuleta maisha bora kwa watanzania.

Mwaka mmoja baada ya utawala wa awamu ya nne, serikali yenyewe imekiri kwamba bado inahatua ndefu katika kuleta maisha bora na kwamba kwanza Mwenyekiti wa CCM amekiri kwamba kasi ya kukua kwa uchumi imeshuka. Serikali imekiri pia kuwa mfumuko wa bei umeathiri maisha ya wananchi. Sasa CCM na hao wanatoka upinzani na kutoa kizingizio hiki kwa nini wasikubali kwamba kauli ya Mbowe ni ukweli?.

Kwa upande mwingine, viongozi wanaosimama kidete katika upinzani ni mashahidi wa jitihada za kuwaondoa kwa vitisho, ahadi za vyeo, biashara, fedha nk. Kama huu si mkakati wa kuwanunua’ ni nini?

NI UKWELI KWAMBA „CCM NI WEZI WA KURA“ NA KWAMBA ILITUMIA RUSHWA KUPATA USHINDI

Msimamo kwamba matokeo ya uchaguzi mkuu 2005 hayakuwakilisha na kuwasilisha matakwa halisi ya wapiga kura si wa Mbowe binafsi, ni wa CHADEMA kwa ujumla wake. Uamuzi huu wa kuazimia kwamba uchaguzi wa mwaka 2005 haukuwa huru wala wa haki ulifikiwa na Baraza kuu la CHADEMA Mei Mosi 2006 baada ya kufanya tathmini ya kina na tamko hili lilitolewa kwa vyombo vya habari mbalimbali ikiwemo kuchapwa kwa kina kama tangazo.

Katika tamko hilo tumeeleza hatua kwa hatua yaliyojiri katika uchaguzi mkuu 2005. Na mkutano mkuu wa CHADEMA uliofanyika mwezi Agosti 2006 nao uliazimia vivyo hivyo. Ni katika mazingira haya ndipo waliokuwa wagombea wote wanaoamini kwamba kuna nguvu inayozidi mipango ya binadamu ambayo wengi wanaiita MUNGU akiwemo Freeman Mbowe wanadiriki kusema kwamba watazikuta kura zao AHERA.

Swali la kujiuliza ni kuwa CCM haikukanusha wakati huo? Uamuzi wa CCM kukanusha baada ya ziara ya Mwenyekiti mikoani ni ishara ya kuweweseka kutokana na mafanikio ya ziara ya Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe katika mikoa mbalimbali. Ni ukweli kwamba CCM ilitoa rushwa katika uchaguzi na hili hata wakati wa kampeni CHADEMA tulilipinga.

Rushwa hii ilikuwa ni bidhaa mbalimbali mathalani khanga, sukari na maeneo mengine hata fedha taslimu. CCM ilijitetea wakati huo na kuiita hii kuwa ni takrima. Mara baada ya uchaguzi mahakama kuu imethibitisha kuwa takrima ni rushwa. Kwa mantiki hiyo CCM iliendesha wazi wazi vitendo vya rushwa wakati wa kampeni.

Nani asiyejua rushwa iliyokithiri pia katika mfumo wa kura za maoni ya ndani CCM na uchaguzi wa chama hicho? Viongozi wenyewe wa CCM wakiwemo Kikwete na Makamba wamekiri uwepo wa tatizo hili na kunukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari.

SI KWELI KWAMBA CHADEMA IMEMUACHA RAIS JAKAYA KIKWETE APAMBANE NA RUSHWA BILA KUMPA USHIRIKIANO

CHADEMA tunatambua kwamba kupambana na rushwa ni suala la jamii nzima kwa ujumla ikiwemo vyama mbalimbali vya siasa. Ndio maana suala la ufisadi limekuwa moja ya ajenda zetu za msingi za wakati wote. Na tumekuwa tukisisitiza haja ya kuwa na maadili ya taifa katika kupambana na rushwa na kubadili mfumo wa utawala.

Tumekuwa mstari wa mbele kuweka wazi masuala ambayo yana mazingira ya rushwa ikiwemo mikataba yenye utata hususani katika sekta ya nishati na madini. Tulimsaidia Rais kwa kuweka kama ajenda yetu ya msingi kuwa mikataba ipitiwe upya lakini kinachoendelea ni tofauti.

Hata Rais aliposema kwamba anawafamu wala rushwa na anawapa muda wa kujirekebisha tulimsadia kwa kumueleza wazi kwamba rushwa ni kosa la jinai hivyo kama wapo hawapaswi kwa namna yoyote kupewa muda wa kujirekebisha. Tumemweleza rais mambo kadhaa ikiwemo haja ya kuweka mikataba wazi na kuunda kamati ya kudumu ya bunge ya kukabiliana na rushwa ambayo itaongozwa na upinzani ili kusiwe na kulindana.

Pia katika bunge la Muungano michango ya wabunge wa CHADEMA katika vita dhidi ya rushwa inadhihirisha dhamira ya wanaCHADEMA kukabiliana na ufisadi. Vyombo vya habari navyo vimekuwa mstari wa mbele kuibua masuala ya rushwa kubwa kubwa. Viongozi wa dini nao wamekuwa wakikemea rushwa. Lakini tunachoona ni serikali ya CCM kukabiliana na rushwa kwa maneno kuliko vitendo na hivyo kushindwa kuendana na ushirikiano huu.

Tunaendelea kuitika mwito wa kushirikiana na chama tawala kukabiliana na rushwa na tunaitaka CCM na serikali yake ianzie kwa kuweka wazi kwa umma wamiliki wa RICHMOND, ni hasara kiasi gani tumepata kama taifa na iundwe tume ya kuchunguza suala zima. Waziri Mkuu Edward Lowasa ambaye ni mbunge wa CCM jimbo la Monduli amenukuliwa akisema kwamba wananchi wasipoteze muda kuzungumzia RICHMOND.

Kama sehemu ya kutoa kwetu ushirikiano wa kukabiliana na rushwa mikataba ya namna hii inapaswa kujadiliwa. RICHMOND ilikuwa ni kwa umeme wa dharura, hatujaupata mpaka mvua zimenyesha. Nani amewajibishwa? Uwajibikaji ni sehemu ya kupambana na rushwa. Watanzania hawapaswi kuaminishwa kwamba suala la RICHMOND ni kitu kidogo. Huu ni mkataba wa zaidi ya bilioni 260.

Leo serikali ya CCM imeahidi bilioni 1 kila mkoa kwa mwaka, mabilioni yanayodumbukia RICHMOND kwa mgao huu wa bilioni moja kwa mwaka ni pesa za miaka takribani 10 za kuwakopesha wananchi maskini! Kumbe pesa ambazo serikali imepanga kukopesha wafanyabiashara wadogo ni kidogo sana na zinaweza kuongezeka maradufu kama serikali ikidhibiti mianya ya rushwa. Rais amesema bado hatujaanza kuwalipa, lakini ukweli ni kuwa kama hatutaingia kwa kina na kuchunguza masuala ya rushwa katika mkataba huu mwishowe tutakuja kuwalipa pesa hizi kama tunavyowalipa IPTL. Huu ni mfano mmoja tu, kuna mingine. Je, ni ushirikiano wa aina gani ambao CCM itatutaka tuipe serikali?
 
TAHARIRI YA GAZETI LA MTANZANIA (5/1/2007) NI YA KISHABIKI NA YENYE KUPOTOSHA KAULI YA KWELI YA MBOWE KUHUSU MAKAMBA NA CCM

CHADEMA tunatambua uhuru na mchango wa vyombo vya habari kama mhimili muhimu wa kuleta demokrasia na maendeleo. Hata hivyo tumekuwa pia wakati wote tukisisitiza kwamba vyombo vya habari vitangulize mbele ukweli na maadili ya sekta ya habari. Tumeshangazwa na maoni ya mhariri ya gazeti la Mtanzania la Januari 5 mwaka 2007 hasa tukizingatia kwamba gazeti hili ni moja ya magazeti ambayo yamejijengea sifa huko nyuma.

Inasikitisha zaidi kwamba tahariri hiyo huitwa ‘Maoni Yetu ‘ ikiwakilisha maoni ya bodi ya wahariri, kwa yoyote ambaye amesoma tahariri hiyo atakuwa atakuwa amejiuliza kama kweli ni timu ya watu makini imekaa na kuandika maoni hayo ama ni mawazo ya mtu binafsi.

Mosi, maoni hayo yamejaa ushabiki wa kisiasa yakiwa na vionjo mbalimbali kwa ziara ya CHADEMA inalenga kuwashukuru wananchi waliokipa chama ‘kura chache’ na ‘kujipitisha’ kuonyesha kwamba chama kipo bado , Mbowe anaupotosha umma kwa kuzusha mambo ambayo si ya kweli na kwa kufanya hivyo kuwachonganisha wananchi dhidi ya chama tawala na serikali yake waliyoiamini ‘pasipo na shaka yoyote’(mhariri alipaswa kufahamu kuwa CCM haikushinda kwa asilimia mia na alipaswa kujua pia kwamba Rais Kikwete ametangaza kuwa hapendi kupewa sifa za uwongo na amekiri wazi kuwa kuna mapungufu kadhaa katika mwaka mmoja wa utawala wake), Mbowe hasemi ukweli na hii ni hatari sana kwa mustakabali wa ustawi wa siasa katika nchi hii nk.

Lakini pili, maoni hayo hayana ukweli wowote na ni dhahiri kwamba yalilenga kupotosha. Na ushahidi wa suala hili uko katika maoni yenyewe ya mhariri !. Tahariri imeanza kwa kujenga mazingira kwa msomaji ya kudhihaki ziara ya CHADEMA lakini pia kujenga picha kwa msomaji kwamba Mbowe anatishia mustakabali wa Taifa, lakini kichekesho ni kuwa tahariri inatolea mfano suala moja tu ambalo linamfanya Mbowe atishie mustakabali wa Taifa nalo ni kusema kuwa ‘Kwamba Makamba hajui siasa inavyokwenda na wala kwamba hajawahi kugombea nafasi yoyote ya kisiasa ya kupigiwa kura na wananchi’.

Hivi kauli hii hata kama ingekuwa si ya kweli inatishia maisha kiasi gani hata kuchambuliwa katika maoni ya mhariri ?. Wasomaji tumezoea kuwa maoni ya mhariri ni mahali kwa wahariri kujadili na kutoa maoni yako kuhusu masuala nyeti ya kitaifa. Ukurasa wa mbele wa gazeti la toleo ya siku hiyo ulibeba habari ya msiba wa Waziri Akukweti(Mungu amlaze mahali pema), IGP kucharukia wauza nguo zinazofanana na sare za Jeshi na Kawawa kuitaka SUA isipoteze maana ya kuanzishwa kwake.

Masuala haya na hii kauli ya Mbowe kuhusu Makamba kipi kilipaswa kutolewa maoni na wahariri kwa maslahi ya taifa ? Katika mazingira ya kawaida ilipaswa baada ya Mbowe kama mwanasiasa kutoa kauli Makamba naye ajibu kama mwanasiasa badala ya ukurasa wa mhariri wa ‘maoni yetu’ kutumika kama ofisi ya itikadi na uenezi ya CCM ama mhariri kuwa kama mwandishi wa habari wa Makamba!

Lakini kubwa kuliko yote ni kuwa kauli aliyoitoa Mbowe ni ya kweli, na tahariri yenyewe imetoa ushahidi wa ukweli huo. Katika sehemu ya kwanza ya kauli yake Mbowe alisema kwamba ‘Makamba hajui siasa inavyokwenda’, tahariri imesema kwamba muktadha wa Mbowe kusema hayo ni kauli ya Makamba kwamba vyama vya upinzani vitakufa.

Hivi kiongozi mwandamizi akisema vyama vya upinzani vitakufa anajua kweli siasa inavyokwenda ? Mhariri amekwenda mbali zaidi kutoa ushahidi wa uwezo wa Makamba kujua siasa ni kuwa alitunga na kuimba nyimbo nyingi wakati wa TANU! Ushahidi wa namna hii ulilenga kumsafisha au kumdhihaki mheshimiwa Makamba ? Kwa ushahidi kama huu mwanasiasa kama Mbowe anakuwa na kosa gani kusema kwamba Makamba hajui siasa inavyokwenda?

Sehemu ya pili kauli ya Mbowe amenukuliwa akisema kwamba ‘Makamba hajawahi kugombea nafasi yoyote ya kupigiwa kura na wananchi’. Mhariri anatoa ushahidi kwamba Mbowe hajasema kweli na kwamba Makamba amewahi kugombea ujumbe wa halmashauri kuu ya Taifa CCM akiwakilisha mkoa wa Tanga?

Hivi mjumbe wa NEC CCM anachaguliwa na wananchi ? Ni wazi anachaguliwa na wanachama wa CCM na si wananchi. Kwa mantiki hiyo, kati ya Mbowe na mhariri nani hajasema kweli ? Kwa hiyo ni ukweli kwamba Makamba hajawahi kuchaguliwa na wananchi hata nafasi ya mwenyekiti wa kijiji.

Kwa upande wake Mbowe alichaguliwa na wananchi kwa asilimia kubwa kuwa mbunge wa jimbo la Hai kuanzia 2000 mpaka 2005. Katika hali hiyo gazeti linapaswa ama kukiri mapungufu hayo ama wasomaji wa Mtanzania watapata hisia kwamba gazeti hili linatumika kubomoa CHADEMA na itakapobidi tutachukua hatua za kufaa na inapobidi kuwataka wanachama wetu kuacha kununua, kusoma ama kutangaza katika gazeti hili. Na rahisi kuwa na hisia hizi kwa kuwa taarifa mbalimbali zinaonyesha kwamba gazeti hili sasa linamilikiwa na mmoja wa viongozi waandamizi wa CCM na si mara ya kwanza kutoa taarifa potofu kuhusu CHADEMA. Na kama hivyo ndivyo basi gazeti lieleze upya sera yake kama bado ni katika kusimamia ukweli na haki ama ni mashine ya propaganda za kisiasa za CCM na serikali yake !



Mwisho :

Tunasikitika kwamba tumetumia muda wa wananchi kusoma taarifa hii ndefu. Kodi za wananchi zilizomo kwenye ruzuku ya chama na michango ya wanachama kutoa tamko hili. Tumetumia vile vile muda katika kuandaa taarifa hii ambao ungetumika kwa shughuli nyingine za kuleta demokrasia na maendeleo nchini.

Hii yote inatokana na watu waoamua kupotosha. Na tunasikitika zaidi CCM na taasisi nyingine zinapotumia fedha za umma na wanachama wao kusambaza uzushi. Tumeamua kujibu tukiamini kuwa ukweli ni uhuru! Tungependa kuwakumbusha watu wa jamii hii kwamba siasa sio uadui, CHADEMA kama chama mbadala ni chombo kinachopaswa kuheshimiwa na watanzania wote wapenda maendeleo.

CHADEMA kwa upande wake kitaendelea kutimiza wajibu wake. Tumemaliza ziara awamu ya kwanza. Tutaanza tena mchakato wa kwenda maeneo mbalimbali kujenga oganizesheni ya chama na kufanya uchaguzi ndani ya chama kupitia mpango wa CHADEMA ni Msingi. Tunajiandaa vilevile kwenda awamu ya pili ya ziara ambayo itahusisha mikoa iliyobaki. Aidha wakati wote tutaendelea kushirikiana na raia wote bila kujali itikadi kuhakikisha serikali iliyoko madarakani inatekeleza ahadi ilizozitoa kwa wananchi. Hakuna kulala, mpaka Kieleweke.

CHADEMA : Mabadiliko ya Kweli, Uhuru wa Kweli

Imetolewa 6/1/2007 :


Erasto Tumbo
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
0713 47 47 07
info@chadema.net
www.chadema.net
 
Mnapaswa kujua kuwa Mhariri wa Mtanzania anategemea kula yake kutoka kwa Bosi mpya wa Habari Corporation Bw RA. Kwa hiyo pengine ni sawa kuamini kuwa wataandika kile wanachoambiwa.
 
Nadhani hii thread haitokuwa na wachangiaji tena. Naifunga... Samahani kwa wale ambao wanaona baadhi ya sehemu sijajibu kitu nakaa kimya. Nshaongea na Brutus na kumpa real thing anaweza kutoa maelezo kwa niaba yangu kwani nami natoka muda si mrefu kuna issue muhimu nafatilia. Hakuna kufunga forum kama wadhaniavyo wengine. Kinachofanyika ni server upgrade ambapo nimekuwa nafanya BackUp tangia mida ya saa 2 za Tanzania mpaka muda huu.

Halafu sio kwa ajili ya hii Forum (updates zenyewe). Kama kuna mtu ameni-backdoor na kutoa wrong info naomba eleweni kuwa amekosea si sahihi. Kwa mwenye kujua masuala ya server upgrade anaweza kuwaelewesha. Kuna mtu anaweza kutoa habari ikaonekana ina ukweli ndani yake lkn ichunguzeni kwa mapana.

Am almost out and wanna wish you all nice discussions. Naomba ushirikiano wenu tu. Yote yanawezekana. Nakuwa busy kiasi nasahau mengi pia... Ndo maana nikafirikia suala la kuwa na msemaji wa forums... Mweka hazina nilisema kwani huenda kukawa na donors wakaamua kutusaidia kuhakikisha hosting yetu inakuwa safer than before na kuhakikisha costs nyingine zinapungua on our side.

Shukrani na kwaheri kwa sasa! Ngoja nipate lunch kwanza the am out as I've said before.

All the best
 
Mzee Invisible,

Heshima yako mkuu, hakuna aliyku-backdoor wote hapa ni watu wazima, na wengine tunajua kinachoendelea, na tulikuwa tunajua ila tulinyamaza kwa kuwa kulikuwa kmyaa, mpaka jana Mzee Alfa O, aliposema rasmi,

Sasa kama tatizo limekuwa-solved, dawa ni kusema ukweli sio kuzungukana na kuanza kutafutana uchawi, kama tatizo limemalizwa wewe ni kusema ukweli kuwa jamani eeh tatizo limekwisha, au mwambie mtu mwingine akuzungumzie, lakini hakuna backdoor maana ukweli tunaujua, na tumeheshimu kutousema hapa wazi, na ushahidi tunao, nia na madhumuni ilikuwa ni kulinda heshima ya forum, ambayo wewe ni mmiliki sisi ni wachangiaji tu! Sasa wewe ukiwa na attitude hiyo unayoionyesha hapo juu, je sisi cha kufia ni nini?

Na kama unayosema ni kweli, nashangaa kwamba mpaka sasa hujamjibu Mzee Alfa O, aliyekuwa wa kwanza kusema, please jiheshimu wewe kwanza na sisi pia tunaojali kwa kuwa mkweli, tunaeelewa kuna ambayo hayawezi kuwekwa hapa hadharani, lakini tumia lugha ya ki-forum inayoeleweka kuwaweka wananchi hapa sawa kwamba tatizo lipo au limekwisha, badala ya kuanza kutafutana uchawi!

Ninakushukuru kwa kunielewa bro na forum idumu!
 
Mimi sijaelewa labda kichwa changu kigumu lakini si kilaza . Invisible umesema unafunga nini ?
Maana mada hapa ni Mbowe sasa naona story kibao .

Chinga na Mbowe hawawezi kuiva maana Chinga ni mpenzi wa mafisadi Mbowe ni mtu wa kisasa ambaye akiwa na muda huja kujibu hoja na si CCM wanao tuma vijana kama Chinga kuleta vurugu hapa na kutukana . CCM yako ingalijua mambo haya unayo yasema wangalisema maana Mbowe anawabana sana .
 
Duuuh eee bwana wee Chinga!
Mimi nampigia deki Freeman ktk mada yake!...
Je, hiyo ya kwako nafanya nini?
 
Mimi sijaelewa labda kichwa changu kigumu lakini si kilaza . Invisible umesema unafunga nini ?

Heri wewe una kichwa kigumu... changu laini sana hadi nahisi ni kilaza maana kuelewesha kunanishinda kiasi! Namaanisha naihamishia hii thread kwenye KABRASHA pale chini as long as kuchangiwa kumeisha.

Nimeeleweka sio? Hope so... nikieleweka kwa wawili nakuwa nimeeleweka kwa wengi. Inshallah, huenda nikaeleweka kwa nilichoandika sasa.
 
Mimi sijaelewa, najaribu kuelewa suala la kuhamisha, lakini ninapatwa na swali why hiii thread tu ndiyo ilibidi itangazwe kwanza? Maana nafahamu thread zingine huhamishwa tu bila kutangazwa?

Mzeee Brutus, heshima yako mkuuu, sasa mzee anasema amekuelezea kwa undani na unaweza kusema on his behalf, hebu tuambie ili tuwekane sawa, maana maswali ni mengi?

Ahsante kwa kunielewa! na Nasubiri kwa hamu!
 
Back
Top Bottom