The Only Thing We Have to Fear is Fear itself

The Only Thing We Have to Fear is Fear itself

Nashauri uiache hii thread maana haina makosa ikiwepo hapa . Wacha watu wawe wanaenda na kurudi nyuma tafadhali ili kuondoa mchanganyiko .
 
Nimekusoma Lunyungu... Pia nashukuru kwa kunielewa Jasusi; kamanda Mzee ES naamini umeshanielewa japo kiasi.

Hii sikupenda kuiondoa hivihivi kwani ilikuwa imechangiwa karibuni lakini nikahisi huenda hii ikawa inastahili kwenda kwenye Kabrasha ili isomekee kule chini bila kuendelea kuchangiwa. Nilitaka kama kuna mwenye hoja kwanini iendelee kubaki aseme ili kama vipi niiache.

Nisingependa kusababisha mkanganyo; ukiangalia thread nilizohamishia kwenye Kabrasha nyingi zilikuwa ni info au zililala kabisa bila kuwa replies. You can check and confirm this. Anyway, hii naiacha huenda Freeman kuna siku anaweza kuirejelea thread yake (kama ana kumbukumbu nayo).

Wasalaam
 
Nadhani makala hii hapa chini ni muafaka katika mada hii...


Wanaohama vyama vya upinzani kwenda CCM wananunuliwa?


Na Haji Mbaruku


Mwenyekiti wa chama cha upinzani nchini, CHADEMA, Bw.Freeman Mbowe amefanya ziara kadhaa mikoani za kuwashukuru wapiga kura kwa mchango wao mkubwa uliosababisha chama hicho kipate ushindi muhimu kwa upinzani hapa bara kuwa na wabunge wengi.

Bw.Mbowe ameonyesha uungwana wa kuwatembelea wananchi waliokipigia kura chama hicho na kuwashukuru kwa namna walivyoonyesha kukiunga mkono chama hicho tangu kurudishwa tena kwa mfumo wa vyama vya vingi vya siasa hapa nchini mwaka 1992.

CHADEMA hakikuwahi kumsimamisha mgombea urais kwenye uchaguzi wa mwaka 1995 na ule wa 2000 na badala yake kiliiunga mkono CUF.

Kwa mfano, kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2000, CHADEMA kiliisaidia sana CUF kuhakikisha kuwa kinaing'oa madarakani CCM bila mafanikio huku chenyewe kikijikita zaidi kwenye ushindani wa ubunge.

Chama hicho kikajipanga na kilitangaza kumsimamisha mgombea wake wa urais ambaye ni Bw.Freeman Mbowe kuwania urais pamoja na wagombea wenzake wanane toka kwenye vyama vya upinzani.

Katika kuhakikisha kuwa inawafikia wananchi wengi zaidi wakiwemo wa vijijini,mgombea wao alitumia helkopta iliyokodishwa toka nchi ya Kenya.

Usafiri huo, ulisaidia sana mgombea huyo kuwafikia wapiga kura wengi kwa muda mfupi sana.Yawezekana ikawa sababu ya Mwenyekiti huyo kuibuka mshindi wa tatu kwenye kinyang\'anyiro hicho akitanguliwa na Rais Jakaya Kikwete wa CCM na Prof Ibrahim Lipumba wa CUF.

Tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka jana, madai mbalimbali yamekuwa yakitolewa kuhusiana na ushindi wa CCM.

Chama cha CUF hadi leo hakitambui ushindi wa Rais Aman Karume wa Zanzibar kwa kile kinachosemwa kuwa uchaguzi uliohalalisha ushindi wake ulifanyika kwa mizengwe.

CUF inadai wapiga kura walitishwa endapo wangechagua upinzani wakati wa uchaguzi mkuu na baadhi ya watu walipiga kura mara mbili mbili wakiwemo watoto , wasiokuwa na sifa nao waliingizwa kwenye mkumbo wa kupiga kura, wapiga kura wengine waliambiwa kuwa endapo wangepigia kura upinzani majina yao yangeonekana kwenye kompyuta na hivyo wangepata usumbufu mkubwa maishani mwao.

CUF pia inadai kuwa kuna watu wasiokuwa na sifa walikodishwa kwenda kumpigia kura Rais Karume na ushahidi huo wanao.Wanadai pia watu waliandikishwa mara mbili kupiga kura na hivyo dhana nzima ya demokrasia kuingia dosari.

Mengi yanasemwa. Halidhalika UDP, NCCR-Mageuzi, NLD, SAU, CHAUSTA, DEMOKRASIA-Makini, PPT-Maendeleo, TLP na hata UPDP kila moja ana sababu zake.

Hata hivyo, sababu iliyotolewa hivi karibuni na Mbowe wakati akiwashukuru wapiga kura wake kwa mchango wao kwa chama chake zimeishtua sana CCM na kufikia hatua ya kumjibu mwenyekiti huyo.

Alikaririwa akisema kuwa CCM inawanunua wapinzani kwa kuwadanganya kuwapa vyeo endapo watakubali kurudi.

Madai yake kwa kweli sio ya kubeza hasa ukizingatia kuwa kila kukicha hivi sasa katika ulingo wa siasa, baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wanatangaza kurudi CCM. Ni juzi tu kundi lingine la wanachama 40 wa upinzani wametangaza kurudi tena CCM.

Lakini kikubwa zaidi ni pale tunaposhuhudia mikutano maalum ya hadhara inayofanywa na CCM katika kila kona halafu ghafla tunasikia kiongozi fulani wa chama cha upinzani ametangaza kurudi CCM.

Hata hivyo, yawezekana wapinzani wanaorudi CCM hawajashawishiwa wala kuhongwa wala kuahidiwa vyeo CCM kama tu wanafanya hivyo kwa hiari yao.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, John Samwel Malecela anasema kuwa CCM haigawi vyeo kama njugu na kwamba inagawa vyeo kulingana na taratibu na kanuni zilizopo na hawawezi kumrubuni kiongozi yeyote wa upinzani arudi CCM kwa cheo.

Alikuwa akitoa maoni yake siku Bw.Aman Walid Kaborou alipotangaza kurudi tena CCM akitokea CHADEMA ambako alifanikiwa kukijenga chama hicho na kukifanya kuwa imara sana.

Inasemekana kurudi kwa Kaborou kumeleta tafrani huko Kigoma ambako hivi sasa hali sio nzuri ndani ya chama hicho, ingawa CHADEMA wanasema hajaacha pengo lolote.

Kaborou hivi sasa ni mbunge wa Afrika Mashariki na kurudi kwake CCM na kisha akapigiwa debe la kuwania ubunge na kufanikiwa kushinda, kumezua maswali mengi kuliko majibu.

Ndio maana Mbowe anahisi kuwa ni lazima Dk.Kaborou atakuwa amefanyiwa mpango wa kuahidiwa cheo cha ubunge wa Afrika Mashariki, hasa ikizingatiwa kuwa aliangushwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana na kijana mdogo wa CCM katika jimbo la Kigoma Mjini, Peter Serukamba wa CCM.

Katibu Mwenezi wa CHADEMA, Erasto Tumbo ametoa taarifa akiinyooshea kidole CCM kuwa inachangia kudumaza upinzani kwa kuwanunua wapinzani.

Hata hivyo,Tumbo haelezi vizuri yeye na alianza siasa akiwa na UDP ya mzee Cheyo, lakini sasa mara baada ya kutoka masomoni nchini Uingereza amehamia CHADEMA kutokana na kuzozana na Cheyo.Ina maana na yeye alinunuliwa na CHADEMA?

Katibu wa Itikadi wa CCM, Bw.Matson Chizii anasema kuwa madai ya Bw.Mbowe hayana msingi hata kidogo na yanatia shaka na anashangaa kuona mwenyekiti wa chama hicho anaweza kusema maneno ya hovyo namna hiyo.

Bw.Chizii anasema kuwa uchaguzi nchini ulikuwa wa huru na wa haki na Mbowe ni mmoja wa wagombea waliokubali matokeo ya uchaguzi na kumpongeza Rais Kikwete.

Hata hivyo, Bw.Mbowe aliwahi kukaririwa akisema kuwa kumpongeza Rais Kikwete kwa ushindi wake wa kishindo hakumaanishi kuwa alikubaliana na mazingira yaliyohalalisha ushindi wake.

Alikuwa anasisitiza kuwa ni hila na mchezo mchafu ambao CCM iliutumia pamoja na dola katika kuhakikisha kuwa inashika hatamu.

Pamoja na madai hayo ya Bw.Mbowe ni vyema tukawaangalia baadhi ya wanasiasa walionogesha sana kambi ya upinzani na sasa wameasi na kurudi tena CCM.

Bw.Tambwe Hiza ambaye CUF ilikuwa inamuamini sana naye anajua ni kwa kiasi alivyokuwa na mvuto ndani ya chama chake.

Alianzia siasa akiwa NCCR-Mageuzi, akagombea mara kadhaa ubunge jimbo la Temeke lakini akaanguka mara zote.

Akaenda zake CUF ambako mara kadhaa nako alisimamishwa kugombea ubunge.Kibaso, Kusaga na Mtemvu wote walimpiga dafrao.Kiongozi huyo pia alikuwa na nyadhifa mbalimbali ndani ya uongozi wa chama hicho.Kwa mfano, aliwahi kuwa mkurugenzi wa Uenezi wa CUF.

Lakini Tambwe alikuja kukasirika mara baada ya uongozi wa chama hicho kufanya mabadiliko na kumuengua katika nafasi hiyo.Tambwe kama walivyo baadhi ya viongozi wa upinzani wanapoondolewa kwenye nyadhifa zao, alianza kulalamika kuwa hakutendewa haki na baadae akaibukia Mbagala akitangaza kurudi CCM.

Kwa hiyo, Tambwe aliondoka CUF baada ya kuondolewa kwenye uongozi na ni jambo la kawaida katika nafasi za uongozi.Hivyo, hakuna ushahidi wowote wa yeye kununuliwa.

Mwingine ni Frank Magoba. Aliingia kwa makeke kwenye siasa akianzia CUF na akafanikiwa kuiangusha CCM kwenye jimbo la Kigamboni.Alikuwa mgombea pekee wa upinzani katika majimbo ya mkoa wa Dar es salaam kushinda ubunge mwaka 1995.

Bw.Magoba hata hivyo alitangaza kurudi CCM baada ya kugaragazwa kwenye kura za maoni kule Mbagala, kitendo ambacho kilimuudhi sana kutokana na ukweli kuwa ni yeye ndiye aliyeifanya CUF iwe na nguvu Kigamboni.Yawezekana alirudi CCM bila kununuliwa.

Thomas Ngawaiya naye alitangaza kurudi CCM akitokea TLP. Alifanya hivyo baada ya kuona ugomvi wake na Mrema hauishi TLP tu kwani anadai alikabiliana na mambo mengi ya kuhatarisha maisha yake.

Naye Njelu Kasaka alifanya kioja kikubwa pale alipoihama CCM kwa kushindwa kwenye kura za maoni na kuhamia CUF.Huko nako alikosa nafasi baada ya kuwekewa pingamizi. Alidumu kwa muda mfupi na akaibukia Mbagala na kutangaza kurudi CCM.

Mazingira ya kurudi CCM yaliendelea kwa wanasiasa wengi tu kama vile Daniel Nsanzugwako ambaye sasa ni Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo Kazi, Dk.Lutter Nelson, DK.Masumbuko Lamwai, Leo Lwekamwa na akina Dk.Alec Chemponda.

Ushahidi unaonyesha kuwa wanasiasa hao wanarudi CCM mara baada ya azma na matakwa yao ndani ya upinzani yanapokwama.

Sasa wanasiasa wote waliokuwa kambi ya upinzani na kurudi CCM, yawezekana wako tayari kurudi tena upinzani, endapo watahakikishiwa maslahi bora.

Lakini kuondoka kwa wanasiasa hao, ambao Mrema amewahi kuwaita mamluki hakuwezi kuua upinzani nchini.

Vyama vya siasa vina kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa vinajipanga vizuri na vifanye shughuli zao kiutalaamu zaidi badala ya kung`ang`ania kuibuka wakati wa uchaguzi.

SOURCE: Nipashe Januari 22, 2007.
 
Haji Mbarouk amejitahidi sana katika makala yake. Bado hata mimi kichwa kinaniuma kuhusu wimbi la wanasiasa kurudi CCM. Kinachonisumbua zaidi, ni kwa nini ni wanasiasa wa bara tu? Si kawaida kusikia kiongozi wa CUF huko Zanzibar anarudi CCM, why bara tu? Is there something wrong with our politics in bara? Food for thought!
 
Mwanasiasa visiwani wanajau siasa na miiko ya Siasa ndiyo maana unaoa CCM ina hangaika hata kupeleka wapiga kura na kutumia majeshi yetu na usalama wa Taifa kuwapa ushindi . Kula Siasa iko bwana .Bara watu njaa wanaikatia BIMA wanadhalilika na kutumika baadaye wanaachwa hoi .
 
walionunuliwa walilipwa kiasi gani? na ni nani aliyewalipa? Endapo upinzani utapata kushika hatamu za uongozi wa nchi, wale waliokimbilia CCM wakitaka kurudi tena upinzani watapokelewa!! Ndugu zangu hawa huitwa Wanasiasa Vipepeo ambao huruka kwa kufuata ua lipi lina asali, hawahitaji kununuliwa wala kuimbiwa nyimbo!! Lenye harufu nzuri, hilo hulirukia!!
 
Lunyungu: hasa!

Mzee Mwanakijiji: Sidhani kama ni ua la waridi tu hapa, ni zaidi! Huu ni mjadala wa aina yake. Inabidi, kuanzia na jinsi wabara na wazanzibari wanavyoona maana na umuhimu wa siasa katika maisha yao. kwa haraka haraka, utaona kuwa kwa wabara wengi, siasa ni njia ya kupatia cheo cha kisiasa na hasa serikalini. Nasema huu ni mjadala hasa!
 
Mwanasiasa,
Nashawishika kufikiria kuwa huenda kwa Zanzibar kuna "mambo" zaidi ya siasa yanayofanya watu wawe na msimamo huo/ule. Mifano ya "dhana" yangu hii ni mingi. Mathalan, mtu yuko tayari amtaliki mkewe kwa vile mke kajiunga na chama cha siasa ambacho yeye bwana hakikubali. Mtoto anaweza kukataliwa na baba yake; majirani wanaweza kususiana misiba; watu wanasusia sherehe au miradi ya maendeeo, na hata mtu anaweza kukatwa mapanga na kuuawa kwa tofauti za "kisiasa". Nadhani hapo watu wanakuwa wamekwenda mbali zaidi ya siasa.
 
CCM iwe nambari wani pia katika uadilifu

VYOMBO mbalimbali vya habari, jana vilikuwa na habari juu ya malalamiko ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupinga kitendo cha Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwatumia wanafunzi katika sherehe zake za kutimiza miaka 30.

Chadema, katika barua yake ya malalamiko kwenda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, kimesema hatua hiyo ya CCM kuwatumia wanafunzi siyo tu imekiuka amri zilizowekwa na viongozi wa serikali hiyo ya CCM, bali pia imevunja sheria inayozuia taasisi za serikali kama shule na vyuo kutumika kwa masuala ya siasa.

Hofu ya Chadema na msingi wa kuwepo sheria hiyo ni kwamba, wanafunzi hawana utashi wa kuamua ni upande upi wanataka kuunga mkono na kujiunga nao kisiasa na pia kutumia taasisi hizo kunaweza kusababisha malumbano ya kisiasa kutokana na tofauti za kiitikadi na hivyo kukwamisha utendaji wa shughuli za serikali.

Tunadhani Chadema ina hoja kwani ni kutokana na sheria hiyo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mwaka jana, katika kikao na wakuu wa shule na walimu wakuu, aliwaonya wasithubutu kuruhusu viwanja vya shule kutumika kwa shughuli za siasa na wasiruhusu wanafunzi kwenda kuwavalisha skafu au kofia au maua viongozi wa siasa.

Pia, Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Utamaduni iliwahi kupiga marufuku wanafunzi kujipanga barabarani kusubiri mapokezi ya viongozi wa kisiasa ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanabaki darasani.

Japokuwa michezo si shughuli za kisiasa, Serikali ilisema inatambua umuhimu wake kwa wanafunzi na haikuwa na nia ya kuizuia, lakini ilizuia mashindano hayo kwa sababu yanawafanya washiriki wapoteze muda mwingi nje ya madarasa. Serikali iliruhusu michezo siku za mwisho wa wiki na sikukuu tu.

Chama cha Wananchi (CUF) kiliwahi kuwatumia wanafunzi katika shughuli zake mkoani Tanga, lakini kilipewa barua ya onyo na serikali.

Tunaamini kwamba amri na sheria hizo zilitungwa na viongozi wa Serikali ya CCM ili ziheshimiwe na vyama vyote ikiwamo CCM yenyewe, hivyo uamuzi wa kuwatumia wanafunzi ni dalili tosha za ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.

Kama serikali ilijisikia vibaya wanafunzi wakishiriki mapokezi au maandamano ya Chadema au TLP au CUF kwa nini ijisikie raha wakati CCM ikifanya kosa hilo hilo? Ikiwa Serikali inadai ni ukiukwaji wa sheria vyama kuwatumia wanafunzi kwenye shughuli zao, uhalali unatoka wapi CCM ikitumia wanafunzi kwenye mikutano yao?

Tunaamini Msajili atafanyia kazi malalamiko ya Chadema kwani madhara yake ni makubwa, nayo ni hofu ya kuwajaza watoto hao imani mbaya ya chuki dhidi ya vyama vingine ili waone ni dhambi kushiriki mikutano yao isipokuwa ya CCM. Ukiukwaji huu unaweza kusababisha vyama vingine kutaka haki ya kuwatumia wanafunzi katika mikutano yao jambo linaloweza kuzua tafrani kubwa.

Kwa kuwa kila siku CCM inajigamba kupitia nyimbo zake kuwa ni nambari wani, basi na kiwe nambari wani pia kuonyesha inajali misingi ya utawala bora na katika kuheshimu sheria na taratibu zilizowekwa

chanzo:-mwananchi
 
Kudesa mashuleni ni kosa lakini kwa manufaa ya nchi tunawaruhusu wote wenye mapenzi mema wadese kutoka JF.
Hii itupe motisha wa kutoa hoja za maana ili ziwape wapiga debe wa kisiasa pointi za kuongelea.
 
Nia kubwa ni ujumbe kuwafikia walio wengi ,kufanyiwa kazi na kuleta mapinduzi ya kiuchumi,maendeleo na utawala bora ambao kwa hivi sasa ni wimbo si kwa vitendo(Ada ya muugwana mja ni vitendo).
 
CHADEMA wapo sawa. CCM wamezoea kukiuka sheria. Wanatunga sheria na kanunI kudhibiti wengine huku wao wakitumia kwa maslahi yao.Wamedhibiti siasa vyuoni lakini itakumbukwa kwenye uchaguzi wa viti maalum wa CCM uliosimamiwa na UWTkulikuwa na wagombea toka vyuoni, siasa ilipigwa kama kawaida vyuoni kupata mgombea amabo Dr. Mighio alishinda katika kipegele hicho.

Pia sheria ya NGO ya saa inazizuia NGO kujihusiha na siasa!(Utata huu).Cha kushangaza wakati wa uteuzi wa viti maalum CCM kulikuwa na wagombea wa kundi maalum, toka mashirika ya kijamii, NGOs kazaa zilisimamisha wagombea kukiuka sheria walioanzisha wenyewe, katika kundi hili alishinda Magreth Sita toka chama cha walimu. Haya yangefanyika kwenye vyama vya upinzani hizi NGOs zingefutwa!!

Si sawa kuwa na sheria zinazopaswa kutekeleza na vyama vya upinzani pekee.

Huu ni mwanzao mzuri, natumai msajili wa vyama vya siasa hatajiuma uma kuwaonya CCM.
 
CHADEMA wana masikio, tunayoyaongea humu wanayasikia na kuyaona na kuyafikisha kwa wananchi moja kwa moja. Ndo raha kuwa na chama kinachojali.
 
Hongera Chadema kwa kutufungua masikio kuhusu hilo
Asanteni
 
Mwanasiasa kama maneno yako ni kweli mnayafikisha basi kula tano mzee wangu . Naomba kujiunga na Chadema ili niweze kusaidia kupeleka meseji inakotakiwa .
 
Down right AROGANCE on CCM part. They believe that they are above the law.And nobody should Dare point a finger at them ( treasonable offence )
 
haya ni MAONI YA MH FREEMAN MBOWE KWENYE GAZETI LAKE LA TANZANIA DAIMA, NAOMBA TUISOME KWA MAKINI NA TUTOE MAWAZO YETU, LAKINI NI FIKRA MBADALA KWA KUSHINDWA VIBAYA KWENYE UCHAGUZI ULIOPITA.NCHI YETU NI NCHI YA DEMOKRASIA BW MBOWE ANA UHURU WA KUZUNGUMZA KWA KILE ANACHOKIONA, LAKINI YANA UKWELI, YANA MALENGO NA MWELEKEO MZURI KWA WATANZANIA? AU NI MILINDIMO MIZURI YA MIZIKI INAYOWATAKA WATU WATOKE KWENYE VITI ILI WAANZE KUCHEZA?
mSOME MHESHIMIWA MAWAZO YAKE HAPO CHINI


Freeman Mbowe
KAMA ilivyo kawaida, ukiandika ukatoa hoja, tarajia maswali, pongezi na hata kejeli kutoka kwa wasomaji. Majibu yatategemea aliyeguswa kaguswa vipi.

Leo, nitajikita kwenye swali moja ambalo nimeulizwa.
Waungwana wamesema: “Mbowe tumekusikia na kukusoma hoja zako kuhusu mustakabali wa nchi yetu; sasa tufanye nini? Nashukuru kwa changamoto hii. Kama Mtanzania na zaidi kama kiongozi, nina wajibu wa kuweka fikra zangu wazi. Wenye hekima na busara wazitafakari. Wenye husuda wabeze!
Mawazo yangu si msaafu. Ni fikra mbadala ambazo zinakusudia kujenga hoja mjadala.

Ninaamini wako Watanzania wengi wenye uwezo mkubwa sana wa uongozi. Lakini mfumo wetu hauwapi fursa. Sasa si siri, nchi yetu imekwama. Ni dhahiri Rais Jakaya Kikwete amelemewa. Yeye hataki au pengine hana ujasiri wa kukiri kuwa chama anachokiongoza hakina jibu la umaskini wa Watanzania.

Taifa lolote lililokwama linahitaji mabadiliko. Mabadiliko hayo huweza kuja kwa njia mbili. Ama kwa mtindo wa kutumia nguvu, yaani mapinduzi (revolution), au kwa mtindo wa amani, yaani mageuzi (reforms).

Ni dhahiri kuwa Watanzania wanapendelea mabadiliko kwa njia ya amani, yaani ‘reforms’. Tangu tumepata uhuru, Tanzania imefanyiwa ‘majaribio’ mengi sana ya kisiasa, kijamii na hata ya kiuchumi, lakini ‘majaribio’ haya hayakutukwamua. Bado tumekwama. Yako maeneo machache tuliyopiga hatua kama taifa. Lakini mafanikio machache tuliyopata hayalingani na utajiri wa asili wa nchi yetu. Aidha, hayalingani kabisa na umri wa miaka 46 ya uhuru wetu.

Ni kweli subira huvuta heri, lakini subira inapoendelea kutumbukiza taifa kwenye lindi la umaskini, subira hii hukaribisha shari! Ni rahisi kufikiria kuwa kukwama kwetu leo ni tunda la ufisadi wa viongozi. Ni kweli hili linachangia. Tukumbushane historia kidogo. Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliongoza taifa hili kwa miaka 25. Alikuwa kiongozi aliyependwa sana na watu. Hakuwa fisadi na wala serikali ya awamu yake haikuwa ya kifisadi. Pamoja na uadilifu wa Mwalimu, bado nchi hii, ilikwama sana kiuchumi na hivyo kimaendeleo!

Kama taifa, tuna wajibu wa kutafakari tumekwama wapi? Ni dhahiri kuwa kutokomeza ufisadi pekee si suluhisho pekee la kuipeleka nchi yetu kwenye neema. Na wakati mwingine nimekuwa nikihoji: ‘Je, inawezekana amani yetu tunayojivunia ndiyo sababu ya kukwama kwetu?’ Sihitaji kujadili utajiri wa Tanzania. Wote tunaujua.

Katika kujadili kukwama kwetu na kupendekeza suluhisho, wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, nilizungumza kwa nguvu kubwa mambo kadhaa. Leo nitaanza kujadili machache ya msingi kama changamoto kwa Watanzania. Nilijenga hoja: Kwamba mfumo wetu wa utawala ndiyo chimbuko la umaskini na kukwama kwetu. Kwamba hata ukimleta ‘malaika’ ukamweka Ikulu awe Rais wa Tanzania, kwa mfumo wetu wa utawala uliopo, lazima atakwama! Kwamba utajiri wetu wa asili ndio utatumika kama chanzo cha kubomoa mshikamano wa taifa.

Kwamba, kwa matendo ya watawala wetu, ni wazi kwamba wamemsahau Mungu! Kwamba amani yetu ni tete! Sera iliyosikika sana wakati wa uchaguzi ni ile ijulikanayo kama sera ya majimbo. Sera hii ilikusudia (na inakusudia) kujibu hoja na hofu yetu kuwa mfumo wetu wa utawala ndio msingi wa kukwama kwetu.

Mada hii ni ndefu. Nakusudia kuijadili kwa kina na kwa mapana yake katika mfululizo wa makala kadhaa. Niliamini niliyozungumza wakati ule. Bado nayaamini. Hatimaye, nitayaandikia kitabu, ili dira yangu ibaki kama kumbukumbu kwa vizazi vijavyo. Kama ilivyotarajiwa kwenye ushindani wa kisiasa, wapinzani wangu wakiongozwa na mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete, walipotosha kisha wakabeza hoja zangu, tena kwa kejeli kubwa!

Kikwete aliponda asichokielewa. Alichokuwa anawaeleza wananchi si sera ya majimbo bali ni uzushi wa CCM. Natumaini naye sasa atasoma na aelewe. Kama ninavyosema siku zote, jamaa hawa kwa propaganda ni hatari!

Katika demokrasia ya mfumo wa vyama vingi, chama cha siasa kina wajibu wa kutoa dira ya nchi. Chama kinakuwa chimbuko la fikra. Fikra hizo zinatekelezwa na serikali. Chama kinaweka misingi ya kiitikadi, serikali inatengeneza sera na kuzitekeleza. Mageuzi yanayolikwamua taifa lolote huanzia kwenye mageuzi ya kifikra. Mageuzi ya kifikra hupatikana tu pale walio kwenye madaraka wanapotambua kwamba uongozi wa nchi ni dhamana na si miliki yao.

Ni pale tu wanapokubali ukweli kuwa rais na hata viongozi wengine wa juu peke yao hawawezi kuliletea taifa neema. Ni pale tu watakapoheshimu kuweka mifumo mizuri itakayotoa fursa kwa wote wenye uwezo wa uongozi kupata nafasi hizo kwa misingi ya chaguzi zilizo huru na za haki.

Kikwete na timu yake waliingia madarakani bila fikra wala dira. Ndiyo sababu alikiri kuwa wale wanaotegemea mabadiliko wasahau, kwani anataka kufuata yale ya waliomtangulia kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya! Waingereza wanasema ‘business as usual!’ Yaani, mambo yaleyale! Kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya, si dira! Si itikadi! Si sera! Ni kaulimbiu. Ni vibwagizo vya uchaguzi! Ni mbwembwe! Ni sanaa.

Watu waliopewa au kujinyakulia dhamana dhidi ya watu wao wanapokosa fikra na dira zao wanazoziamini, huwa watawala, na hivyo kusababisha utupu (vacuum) wa dira. Wanapokuwa na fikra zao wanazoziamini huwa na dira, nao huwa viongozi. Huongoza watu wao kuelekea kule wanakokuamini, hata kama ni kubaya.

Panapotokea utupu (vacuum) wa fikra za wenye dhamana, fikra za nje huziba utupu huo. Katika mazingira haya wanajitokeza wengi kujaza utupu huu kwa kuwa madalali wa watawala. Wanageuza Ikulu kuwa gulio. Hili ndilo linaloisibu nchi yetu. Tangu Baba wa Taifa aondoke madarakani, nchi imekosa fikra na dira. Viongozi wameacha kufikiri au hawana uwezo wa kufikiri? Utupu huu wa kukosa fikra mbadala za ndani, unawafanya viongozi wetu kila kukicha kutimkia nje ya nchi kusaka mawazo na fikra mpya. Ni dhahiri watu wa nje wakijaza utupu wetu, watajifaidisha kwanza wao!

Tahadhari! Katika historia ya dunia, hakuna taifa lililoendelezwa na fikra za taifa jingine. Kila taifa huvutia kwake kwa kuchuma kwa wengine. Fikra zitakazokomboa taifa hili lazima zitoke huku huku. Watu wapo! Vichwa vipo! Vimebanwa na mfumo. Nieleweke hapa! Sikatai wawekezaji. Ila sikubali kuwa ufumbuzi wa matatizo yetu ya umaskini utaletwa na wawekezaji na wafadhili wa nje. Sasa narejea kwenye hoja! Chimbuko la fikra ya hoja ya sera ya majimbo

Naam! Baada ya kutafiti kwa kina, kwa upande mmoja nilibaini kuwa ukubwa wa nchi yetu na utajiri wake wa asili vimelemaza taifa letu. Kwa upande wa pili, nilibaini na hivyo kuamini kuwa mfumo wetu wa utawala umeshindwa kutumia rasilimali watu na maliasili yetu kwa maendeleo ya taifa.

Kwanza, nilishangazwa na idadi ya Watanzania wasiojua ukubwa wa kijiografia wa nchi yao. Ni idadi ndogo sana ya Watanzania wanaojua kuwa nchi yetu yenye ukubwa wa kilometa za mraba laki tisa na arobaini na tano elfu (945,000 km2) ni zaidi ya ukubwa wa nchi za Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Lesotho na Swaziland zikichanganywa!

Tanzania kwa idadi ya watu (milioni 38) ni nchi ya 38 kati ya nchi 195 za dunia. Katika Afrika, Tanzania ni ya saba ikizidiwa na Nigeria (milioni 132), Misri (milioni 79), Ethiopia (milioni 75), Kongo (milioni 63), Afrika Kusini (milioni 44) na Sudan (milioni 41). Ni dhahiri basi kuwa Tanzania ni nchi kubwa ya kutisha, huku ikiwa yenye rasilimali za kupindukia. Ukubwa na utajiri huu kama hautawekewa mkakati, unaweza kuwa kikwazo kikubwa ambacho watawala wetu hawajaweza kukiona.

Aidha, kama hautadhibitiwa mapema, unaweza kuwa chanzo cha migongano ya ndani kwa ndani, kwani kuna utupu wa kutisha. Tanzania haiwezi kuendelea kutegemea kila kitu kutoka Dar es Salaam!

Chini ya utawala wa Mwalimu Nyerere, chini ya mfumo wa utawala wa kijamaa, nchi yetu ilitawaliwa kutoka kati, yaani kutoka makao makuu ya serikali. Serikali ilisimamia na kumiliki njia zote kuu za uchumi (command economy), ambazo ni pamoja na ardhi, maliasili zote, biashara, viwanda, mabenki, majengo n.k.Hata mfumo wetu wa kiutawala ulipata maagizo kutoka Dar es Salaam na hivyo kufanya makao makuu ya nchi na kiongozi mkuu kuwa na mzigo mkubwa sana wa kusimamia rasilimali za asili za taifa.

Ujamaa ulikwama. CCM, tangu enzi za Mzee Ali Hassan Mwinyi, ikautelekeza kisirisiri. Jambo la ajabu! Itikadi kuu ya nchi inatelekezwa kisirisiri bila wananchi kujua. Hii ndiyo fedheha ya watawala wasio viongozi. Kwa upande wa siasa, nchi nayo ikaingizwa kichwa kichwa kwenye mfumo wa vyama vingi. Balaa likaanzia hapa!

Tangu wakati huo, mserereko wa uchumi wetu umekuwa wa soko (market economy). Ujamaa umebakia kuwa usanii wa kuombea kura kwa wananchi.
Sera za ubinafsishaji sasa zikaanza na baadaye kushamiri chini ya utawala wa Awamu ya Tatu ya Rais Benjamin William Mkapa. Nchi yetu nayo haikusalimika na mabadiliko ya mifumo ya kiuchumi na kisiasa ya dunia. Hii ilitokana na kufa kwa vita baridi kati ya mataifa ya mashariki ya kijamaa na yale ya Magharibi ya kibepari.

Nchi yetu hapa iliingia kwenye mfumo wa uchumi wa soko kwa kushinikizwa bila maandalizi ya kutosha yaliyosababishwa na kukosekana kwa fikra za ndani. Rasilimali za taifa ghafla zikawa kama hazina mwenyewe. Viongozi wetu wakaanza kuzigawa kwa wageni bila kuweka mkakati wa ndani wa kuwezesha wazawa. Kupitia ubinafsishaji na sera za uwekezaji, viongozi wetu nao wakaanza ‘kujikatia’ mapande yao. Familia zao, wapambe wao nao hawakucheza mbali. Wawekezaji wa sampuli mbalimbali nao wakaingia ulingoni.

Kama nilivyokwisha kusema, nchi sasa ikageuzwa shamba la babu, ambapo kila mwenye kapu huvuna, na babu hana nguvu ya kuzuia. Uongozi wa nchi sasa ukawa biashara. Ufisadi wa kutisha ukazaliwa rasmi. Kazi ya kugawa rasilimali ya taifa ikaendelea kufanyikia Dar es Salaam. Bunge likageuzwa kituko. Likawa idara ya CCM, na likatumika kupitisha maagizo ya wakubwa, si matakwa ya wananchi.

Mali za nchi zikawa zinagawanywa na kikundi kidogo cha watu chini ya Rais, huku kikidhani kina akili kuliko Watanzania wote. Watanzania tukaendelea kupewa matumaini ya neema. Kila kukicha zinatolewa takwimu tamu tamu za kuonyesha uchumi unakua. Ni kweli, pato la taifa lilikua! Lakini cha kujiuliza, lilikua kwa faida ya nani ilhali wananchi waliendelea na wanaendelea kuwa maskini?

Sasa, hebu tuchambue bila woga ufisadi uliofanyika chini ya utawala wa Awamu ya Tatu, na ambao Rais Kikwete ameahidi kuuenzi na kuulinda! Mwanzo wa kuelemewa kwake.

Itaendelea wiki ijayo!
 
Jicho la Mbali,
Sasa u-alinacha uko wapi? Kipi alichokisema kinachokuwa ndoto?
 
Back
Top Bottom