afrika itatawaliwa na nchi za kimagharibi hadi mwisho wa kiama. Afrika haina umoja hata kidogo, afrika kilamtu yuko kibinafsi na kwa maslahi yake, laiti kama waafrika wangeungana na kuwa kitu kimoja haya manyanyaso ya nchi za kimagharibi kwetu afrika yasingekuwapo. Sijui ni linitutajifunza na sijui ni lini wafrika wataamka kwani kila kukicha kwa maslahi yao (magharibi) wantunyanyasa. Kama kweli wanapenda haki kwanini hawaendi somalia, sudani kwenda kutetea huko, ama kwa sababu ni nchi za kimaskini hakuna madini, mafuta na malighafi nyinginezo zitakazo wanufaisha wao.
Tunatawaliwa bila kujielewa kuwa tunanyonywa wanatufanya watakavyo, wanatulekesha wapendavyo afrika itabaki kuwa shimo la takataka kwa nchi za magharibi. Ukija upande wa libya kweli gadafi kama mwanadamu na mazuri na mabaya yake hata mimi yapo mazuri na mabaya yangu pia, kwanini tunaona mabaya tu mazuri hayaonekani. Libya watu wanasoma bure narudia tena bure kuanzia chekechea hadi vyuo vikuu wanatibiwa bure hakuna malipo, umeme na maji pia garama zake ni kidogo sawa na bure. Hivi vyote libya walipatiwa ni nchi gani ya afrika inapewa huduma hizi zote.
Upande wangu nchi za maghalibi zimepandikiza chuki na visasi kwa walibya na kamwe hii nchi ya libya haitokaa kwa amani kwani tayari wameshawekeana visasi, chuki na ukabila ndani yake. Na hii dhambi haitokaa ifutike vizazi na vizazi. Wataendelea kupigana sasa wenyewe kwa wenyewe kwani kila mtu atakakuwa kiongozi na kila atakae ingia madarakani ataonekana mmbaya. Nchi za magharibi zimepiga gadafi sababu ya mafuta sasa watachukua mafuta yao yakiisha wanaachia nchi yenu kama picha haina mwelekeo.
Gadafi mwanzoni alitaka nchi za kiarabu waungane wawe waoja na wenye sauti moja kwa maslahi ya nchi zao za kiarabu alijitahidi ikashindikana akageukia upande wa nchi zote za afrika akataka ziungane wawe wamoja wenye sauti moja wameshindwa kuungana. Daima nitamkumbuka kwa mema yote alioyafanya ameacha historia ingawa najua nchi za kimagharibi watajitahidi kuipotosha na kuanika maovu yake tu yale mazuri watayameza.
Afrika imebaki na kiongozi mmoja tu ambaye nae anawindwa sana na nchi za kimagharibi mzee mugabe peke yake ndie namwona kwangu ni jemedari hawaogopi hawa majitu anawaambia ukweli! Libya iko siku watakaa chini na kumkumbuka gadafi. Nimtazamo wangu binafsi.