ubepari ndio unaingia Libya sasa
yale mambo ya kulala na serikali kutoa huduma na kuwafanyia kila kitu imefika kikomo
ngoja nione waarabu hawa watakuwa wavumilivu kwa kiasi gani
Mkuu heshima mbele.
Ubepari hauingii leo Libya, ulukuwepo tangia enzi zileee. Watu wa Libya walikwishachoka na huyu jamaa ila walikuwa hawana jinzi ya kumuepuka.
Gaddafi amefanya mambo mengi ambayo ukipima utaona kwamba labda kulikuwa na haja ya kutokuwa nae akiwa kiongozi wa nchi hio. Kama zilivyo serikali nyingi kwenye nchi zinazoendelea suala la kukandamiza wakulima na wafugaji na wale watu wa kipato cha chini ni jambo la kawaida. Kunakuwa na mambo kama mfumuko wa bei kila mara huku huduma za jamii zikiwa hovyo kabisa.
Lakini ni huyu Gaddafi ndie alitaifisha shughuli zote za kiuchumi ambazo zilikuwa zikiwanufaisha wa-Libya wachache na wakoloni mabepari, ili watu wengi wafaidike. Wakti ule mfalme Idris alikuwa kibaraka wa nchi hizo na pia USA walikuwa na kituo kikubwa cha kijeshi nchi humo kilichoitwa Wheelus Air Base ambacho kilikuwa kikitoa msaada wakti wa vita kuu ya pili ya dunia na walikuwa wakibadlisha kwa bidhaa adimu kama mafuta.
Lakini Gaddafi alipoingia na serikali yake akawa na ajenda zake ambazo hazikufurahisha wengi. Kazi za Gaddafi za kuwasumbua nchi za Ulaya hazikuishia hapo, pia alikuwa akizishawishi (madai ya nchi za Ulaya) nchi za kiarabu kupitia OPEC kuamrisha au kuyumbisha bei ya mafuta duniani kama silaha ya kuweka hoja yoyote iliokuwa na dalili ya ukoloni. Kuna wakti bwana Henry Kissinger akiwa mshauri wa masuala ya usalama wa USA aliamua kutoa idhini ya kumuua Gaddafi na jaribio hilo la mwaka 1969 likashindwa.
Kinachochekesha ni kwamba eti NTC au baraza linaloendesha serikali ya mpito limeamua kutangaza siku ya kuikomboa Libya Jumapili kutoka kwa utawala dhalimu wa Gaddafi.
Lakini ukweli ni kwamba huu ni ushindi wa nchi zote za kibepari na washirika wao ambapo kwa sasa wameua sio tu Gaddafi, familia yake na wale walokuwa wakimzunguka bali hata watoto na akina mama. Ni kitendo cha kurudisha nyuma wakati kuwa uleule wa ukoloni mamboleo.
USA na nchi za Ulaya zikiongozwa na UK na France zilikwishapanga huu mpango ambao ni katika kutafuta usawa kwenye kuhodhi maeneo fulanifulani duniani au "geo-strategic and economic interests" ambapo nchi ya uchina na Russia zipo mbele kidogo kuzidi hizi nchi nilizotaja hapo mwanzo.
Bwana Putin anahoji kwamba kwanini NATO imemuua Gaddafi kwasababu anajua ni Russia na China pekee ndio wallikuwa wakifaidi matunda ya mikataba minono kwenye maeneo ya mafuta, uuzaji silaha na miundombinu ambayo waliandikishana na utawala wa Gaddafi.
Kitendo hiki cha nchi hizi za Russia na China kugombania nchi ya Libya yenye kutoa mafuta zaidi ya lita 450,000 kwa siku na ambayo ipo karibu na bara la Ulaya kutenganishwa na bahari ya Mediterranean, ndio kimesukuma vita hii iliotokea ambayo ina lengo la kuliweka eneo hilo la Libya ndani ya himaya ya nchi za Magharibi na USA.
Nchi za NATO zikapanga kumwondoa Gaddafi ili kudhibiti mafuta na mali asili yote iliomo nchi humo na kuruhusu kampuni zikiwemo BP, ConocoPhillips na Total za UK na EN ya Spain na zingine za France na Italy.
Sasa Gaddafi ameuawa na watu wake mwenyewe na kinachofuatia ni kuundwa serikali ambayo itajumuisha wale wote ambao walikuwa wakitaka wamrithi Gaddafi, na Benghazi na Tripoli kutakuwa makao ya serikali hiyo ya mpito.
Kutakuwa na kituo cha kijeshi chenye lengo la kudhibiti vurugu katika eneo hilo yakiwemo maeneo ya Tunisia, Egypt ambayo yalikumbwa na zagazaga la mapinduzi.
Gazeti la New York Times la USA toleo la Ijumaa lilikuwa linatoa ushauri kwa serikali ya raisi Obama kwamba, nanukuu-"More than money--thanks to oil, Libya is wealthy--Libya will need sustained technical advice and full-time engagement".
Kuzidi kuonesha kwamba Marekani wapo nyuma ya shughuli zote hizi siku ya Alhamisi raisi Obama akiongea kwenye hotuma yake juu ya kifo cha Gaddafi alisema nanukuu -"we are seeing the strength of American leadership in the world."
Kwa kweli kifo cha Gaddafi kimepokelewa kwa shangwe nchini Libya na katika ulimwengu wa nchi za Magharibi lakini ilibidi Gaddafi akamatwe na afikishwe mahakamani kujibu mashataka, kwani katika sheria za kimataifa kitendo likichofanyika ambacho ni mauaji ni kinyume cha sheria.