[h=6]Ilikuwa ni nchi ambayo Raia ndiyo wenye sauti na mamlaka ya mwisho ya kuamua hatma ya maisha yao na mgawanyo wa rasilimali za Taifa, kupitia kamati mbali mbali za umma (Representativeness)
"Green book" ni kijitabu ambacho Gaddafi alivumbua, kama mfumo wake wa katiba na kanuni za kuongoza Taifa lenye utawala usiolazimika kuiga "style" za tawala za Kibeberu wala za ...ki-nyenyepa.
Ndani ya kitabu hicho, Gadafi kwa ushauri wa kamati mbalimbali za umma (representative commetees), iliwekwa miiko, miongozo na kanuni za Haki na wajibu wa Raia pamoja na Serikali. Kipaumbele cha wajibu za Raia ilikuwa ni Uzalengo na kuipenda nchi na viongozi wake. Kuombea nchi, kusimamia nchi na kulinda Nchi, rasilimali na viongozi wa nchi kwa Gharama ya maisha.
Serikali ilikuwa na wajibu wa kusimaia falsafa zake za kupigania utu, heshima na ustawi wa watu wa Libya na Africa kwa ujumla. Kuwa na Jeuri ya wazi, ikiwezekana, dhidi ya uonevu, ukoloni mamboleo na u-magharibi. Zaidi sana, Serikali ya Libya,chini ya ghaddafi, pamoja na mambo mengine, iliapa katika "Green Book, kusimamia Haki kadhaa, hizi hapa ni miongozi tu mwa Haki za wananchi wa Libya ya Ghadafi
1. Elimu ni haki ya kila raia.Na inatolewa bure kuanzia awali mpaka ukomo wa Akili yako
2. Huduma bora za afya ni Haki ya kila raia, na inatolewa bure kwa ngazi na magonjwa yote
3. Umeme bure
4. Maji bure
5. Ruzuku kwa wasiokuwa na ajira na kazi za kuwaingizia kipato
6. Ruzuku kwa wazee (kwa mujibu wa sheria na maelekezo ya kamati za umma)
7. Ruzuku maalumu kwa walemavu/wasiojiweza
8. Mikopo isiyo na riba (0% Interest) kwa Wajasiriamali wadogo na wa-kati
9. Mikopo isiyo na riba (0% Interest) kwa Fresh Graduates
10. Nyumba/ Makazi bora ni Haki ya kila Raia
Yasemekana aliwahi kujiapiza, kuwa hatamjengea nyumba hata mama yake mzazi iwapo kuna Raia (mtu mzima) wa Libya hana nyumba/makazi bora ya kuishi.
'UDIKTETA' HASA NI KITU GANI, NA DEMOCRASIA NI NINI?[/h]