The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

Ila wamemtenda vibaya mno sina uhakika kama hata hitra alitendwa hivi!
 

Qaddaffi alijua atakufa na amekufa, na aliapa kuifia nchini mwake hakutaka kutoroka. Wale waliomuua walikuwa wakiteleza maagizo ya Marekani kumbuka siku moja kabla ya kukamatwa na kuuawa kikatili, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani aliitembelea Libya na kuamuru atafutwe auwawe. Ndio maana jumia ya kimataifa iliposema kifo cha Qaddaffi kichunguzwe NTC ilikataa kwanza ikiogopa kuwaudhi marekani.
Utashangaa mtu kama Charles Toyler wa Liberia ambae aliua maelfu ya watu na kupora mali, kama viongozi walioendesha mauaji ya watu zaidi ya laki nane Rwanda, au mtu kama Ratco Mladic ambae alisimamia mauaji ya zaidi ya watu elfu tano huko yugoslavia na wengine wengi wamefikishwa katika mahakama ya kimataifa ambayo haina hukumu ya kifo kwa nini Qaddaffi ambae amewahudumia watu wake kwa kiwango cha kushangaza barani Africa ameuawa kikatili.
 

Kwa mara ya kwanza nilipowaita hawa wa WAHUNI WA BENGHARZ baadhi ya watu hawakuniamini na waliniona mi ni punguani maana nitawaitaje wahuni wakati wana support ya WEST empires! Mmeona wenyewe.
 

ni kweli uko comfused kutokana na upupu umemwaga hapo juu.
 
majirani hawakumpenda kwasababu ya wema wake wa kuzisaidia nchi masikini.
 
hivi kipigo cha gadaffi kinatofauti na kipigo cha Yesu ! Hata yeye walimdhihaki na kumtemea mate ! Au?

Tofauti kila kitu, mmoja Mtakatifu mwingine mwovu, mmoja Yesu kafia ulimwengu Ghadafi kafa aking'ang'nia madaraka, acha kumfananisha Yesu na Ghadafi wewe! Ghadafi wawezamfananisha na mojawapo ya wezi waliosulubiwa karibu na Yesu.
 
Wamedai waliomuua gadafi wa kristo hii sharia wanaipata wapi wakristo
wanavuna walichopanda mkuu usiwaonee huruma hao
shule nalo nijanga lingiine la kitaifa walibya walisoma wengi wakonje

Sijakuelewa!
 
1. Hamna bili ya umeme Libya,umeme ni BURE kwa wananchi wote
2. Hamna riba katika mikopo itolewayo na mabenki Libya,benki zote zinamilikwa na serikali na zinatoa mikopo kwa riba ya aslimia
3. Nyumba ni haki ya msingi ya kila mwananchi wa Libya,Gaddafi aliapa kuwa wazazi wake hawatopata nyumba hadi ahakikishe kila mtu Libya ana mahali pazuri pa kuishi.Baba yake Gaddafi alikufa wakati mke wake Gaddafi,mama yake na mke wake wakiwa bado wanaishi kwenye hema.
4. Wanandoa wapya wote Libya wanapokea dola elfu hamsini($50,000) kwa ajili wa kuanzia maisha kutoka kwa serikali.
5. Elimu na huduma za afya ni BURE Libya,Kabla ya Gaddafi asilimia 25% tu ndo walikuwa wanaelimu Libya,lakini sasa zaidi ya aslimia 83% wana elimu.
6.Mwananchi yoyote wa libya akitaka kujiingiza kwenye kilino atapewa nyumba,vifaa vyote,pembejeo na mifugo BUREE
7. Kama Mwananchi wa Libya yoyote akishindwa kupata kiwango cha elimu ccha kumtosheleza Libya atapewa ufadhili wa kwenda kusoma chuo chochote nje ya nchi na huko atalipiwa malazi,usafiri,chakula na atapewa dola elfu mbili na miatano kila mwezi(2500) mpaka anamaliza kusoma.
8. In Libyan, if a Libyan buys a *car*, the government subsidized 50% of the price.9. BEI YA MAFUTA LIBYA NI $0.14 KWA LITA
10. Libya haina madeni ya nje na imejiwekea akiba ya zaidi ya dola milioni mia moja hamsini ($150 million).
11. Mwananchi yoyote wa Libya akisoma akamaliza na akashindwa kupata kazi atalipwa na serikali kiwango cha mshahara kilekile kama vile ameajiriwa tayari hadi pale atakapopata kazi.
12. Kiasi fulani cha mauzo ya mafuta nchini Libya kinaongezwa moja kwa moja kwenye akaunti ya benki ya kila mwana Libya
13. Mama anayejifungua mtoto Libya anapokea dola elfu tano ($5000)
14. Slesi 40 vya mkate Libya zinauzwa dola $ 0.15
15. 25% ya wananchi wote wa Libya wana digrii
16. Gadaffi alianzisha project kubwa kuliko zote duniani ya umwagiliaji inayoitwa Great Man-Made River project ambayo ingeondoa kabisa tatizo la maji katika nchi hii ya jangwani

NI DIKTETA GANI MWINGINE ALIYEWAFANYIA WANANCHI WAKE MAMBO KAMA HAYA
RAI:KAMA GADDAFI NI DIKTETA,BASI HATA TANZANIA TUNAHITAJI DIKTETA KAMA YEYE
 
WANASEMA TENDA WEMA UENDE ZAKO- huu msemo alinambia Mohamed Dewji pale alipopata kura ambazzo hakuzitarajia aki compare na big investments in singida
 
Naona kwa sasa inatosha maana kama sifa amekwishaipata na kufa kafa,tufanye kazi sasa ili nasi tuwe kama wao maana yote hayo hayakuja bure kuna watu waliumia na kufanya kazi kwa bidii.
 

Naunga mkono hoja.
 

Mungu aliumba vitu viwiliviwili, Kuna walefu na wafupi,Wanene na wembamba, Wakubwa na wadogo, Juu na chini,Mbele na nyuma, Kulia na kushoto, MAZURI na MABAYA
Umetueleza mazuri hebu sasa eleza mabaya yake. Ili tutoe Maksi na kusema huyu hakuwa Dikteta. Ila ktk yote nampongeza kwa Nchi kutodaiwa maana TZ deni karibu litatuua.
 
17. Aliwaua kama alivyojisikia.
18.Mwishowe na wao wamemuua.
 
@ lwamayanga, Hivi utajisikiaje mwanaume mwingine akawa anakulisha wewe na mkeo na watoto wako? Ni aibu gani kurudi kwa mkeo na vijihela ulivyopewa na mwanaume mwingine? Na ni wapi au lini watu wa Libya walisema wanataka kumuondoa Ghadafi kwa sababu hawalipwi allowance za nyumba, mishashara au posho zingine? Huwezi kununua UTU? Na wananchi wa Libya wamekuwa wanasema hili; wanataka freedom & dignity. basi.

Kwa miaka 42 watu wa Libya hawajahi kufanya uchaguzi, kama haitoshi vile, Ghadafi alikuwa anamwandaa mwanawe achukue nafasi yake! That man aliifanya nchi ya Libya kama 'duka' lake. Ilifikia kipindi watu wanaanza kujisikia kama 'nusu binadamu' mbele ya watoto wa Ghadafi. unakuwa kama mbwa mlamba makombo.

For better for worse, wananchi wa Libya waache wafanye maamuzi hata kama ni mabaya waachwe wafanye hayo maamuzi lakini sio mtu mmoja na familia yake (tena kwa nguvu) wanaamua kutawala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…