The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

US will continue to help Libyans with humanitarians and economic assiatance-US
 
Baada ya kumuondoa Gaddaffi nani atapata tenda ya reconstruction?
Kuna somo kutoka Iraq na Afghanistan.
Hizi nchi hazitaki demokrasia wa domokrasia. Wanafikiri hela tu na faida. how to make easy money!

 
Last edited by a moderator:
Where's OAU/AU?
Where's Arab League?
Where's China?
Where's EAC?
 
hivi wale mabodigadi vimwana wa kike bado wapo nae....?
 
Inasikitisha............ Yule awalishae wananchi wake bure, leo kawa mbaya simply because wazungu wameamua siyo?

Ndugu MTM; sidhani kwamba kitu pekee anachohitaji mwanadamu/mwananchi ni kulishwa, kavalishwa, au hata kupata malazi ya bure. Hata kama ungetoa vyote hivi bure na kugawa mamilioni ya dola kwa kila mwananchi; kama hujampa UHURU kamili wa mawazo na kutoa hisia zake bado ni sifuri. Alichokosea Gaddafi (na wengine wa aina yake) ni kutoruhusu demokrasia kamili kwa wananchi wake.

UHURU wa mawazo ni kitu ambacho kwa asili Mwenyezi Mungu amemjaalia kila mwanadamu na hauwezi (UHURU) kuwa "replaced" na kitu kingine chochote; iwe kizuri au kibaya. Watu wasio huru wata-react tu japo unaweza kuzima kwa kipindi fulani lakini "time will tell".

Kati ya mambo ya hovyo kabisa mtawala (au kundi lake; vyama cha siasa, serikali, bunge, n.k) anaweza kufanya ni kudhani kwamba anaweza kufikiri kwa niaba ya watu wake - na hiki, kwa maoni yangu, ndicho kinachomsumbua Gaddafi na tawala za aina yake.
 
Baada ya kumuondoa Gaddaffi nani atapata tenda ya reconstruction?
Kuna somo kutoka Iraq na Afghanistan.
Hizi nchi hazitaki demokrasia wa domokrasia. Wanafikiri hela tu na faida. how to make easy money!



All in all Libya ni mali ya walibya wote na si Colonel na familia yake tu
 
Last edited by a moderator:
kuna gazeti la udaku (jina kapuni) limeandiika mtu kauwa kizazi baada ya kupiga kikombe cha babu

zamani waliita mfadhaiko ..... jamaa kwenye daladala walikua wanachakachua mapenzi ...... itarudi tena kwa sababu ya kikombe
 
This shows that it is more than libyans who want Ghadafi out of power
 
Mkuu.
Unapozuia upande mmoja usitumie silaha kali lakini unawapatia upande mwengine silaha na kutamka kuwa yule aliepo madarakani aondoke kuna walakini mkubwa.

Gaddaffi bila ya shaka ame-overstay katika madaraka yampasa aondoke lakini sio kwa aina hii ambayo Polisi wa dunia wanalazimisha.

Nchi za Ulaya na marekani hazina tabia ya kuunga mkono wazi wazi waasi..sasa hapa kuna nini?

Na jee sasa utakuwa ndio mtindo mpya kila wanapoona kiongozi hawataki tena awepo madarakani wataweka no fly zone na military strikes?

Kama waasi wana-control sehemu ndogo tu ya nchi ni wazi kuwa waasi walikosea strategy.. waliponyanyua silaha...sio kama ile iliyotumika Egypt na Tunisia ya maandamano au ile inayotumika Yemen na Bahrain. hakuna serikali itakayotizama tu waasi wwenye silaha ni lazima kama kufa itawashambulia.

Lakini wababe wameshaamua basi Gaddaffi ataondoka tu.
Mkuu mleta mada Unafiki si wa waarabu tu. Hizi nchi zinazoshadidia kumuondoa Gaddaffi wao ndio magwiji wa unafiki.
Hapa kwetu wanasema uchaguzi ulikuwa huru na haki. Nani hajui kilichofanyika?

wachangiaji wengine tutumie lugha za kiuandishi ,maandishi ambayo yanasomwa na wengi. Tuache matusi. Tutoe hoja.

Mkuu USA sidhani kama ilikuwa inataka Gadhafi aachie ngazi. Gadhaffi amejiingiza mwenyewe kwenye crossheir baada ya kukosa washauri. Alitakiwa awaache walibya waandamane hata miezi kumi na kuruhusu vyombo vya habari vya magharibi kupiga picha watakavyo. Na angekuwa akiwapatia maji, juice na mikate mpaka watakapochoka. Kitendo cha kuanza crackdown wakijua kuwa watu wataogopa ni kosa kubwa alilolifanya, maana kwa mauaji yale huwezi kuwa salama hasa kama watu walikuwa wanakutafutia sababu baada ya kuanguka kwa ndege yao. Hii hatua iliyopo sasa ni sawa na mmakonde kakukuta unapanda kwenye mnazi wake upo katikati anakwambia UCHIPANDE UCHICHUKE, UKIPANDA NCHALE UKICHUKA NCHALE,UKIKAA HAPOHAPO NCHALE
Yaani kwa sasa ni kwamba the hague inamuita labla auwawe au ajiue, maana hataendelea kuiongoza Libya. Busara ikitumika akajiuzulu bado hatakuwa salama.
 
Back
Top Bottom