Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,762
- 59,204
aje bongo tutampokea
Inasikitisha............ Yule awalishae wananchi wake bure, leo kawa mbaya simply because wazungu wameamua siyo?
hivi wale mabodigadi vimwana wa kike bado wapo nae....?
Where's OAU/AU?
Where's Arab League?
Where's China?
Where's EAC?
siku hizi mashine ya jamaa haichaji kwa sababu ya presha. mwanamke anataka 'dawa'. wamemkimbia.
Baada ya kumuondoa Gaddaffi nani atapata tenda ya reconstruction?
Kuna somo kutoka Iraq na Afghanistan.
Hizi nchi hazitaki demokrasia wa domokrasia. Wanafikiri hela tu na faida. how to make easy money!
Du....! ..... sasa kwa nini asiende kupata kikombe kwa babu...?
kuna gazeti la udaku (jina kapuni) limeandiika mtu kauwa kizazi baada ya kupiga kikombe cha babu
All in all Libya ni mali ya walibya wote na si Colonel na familia yake tu
siku hizi mashine ya jamaa haichaji kwa sababu ya presha. mwanamke anataka 'dawa'. wamemkimbia.
Mkuu.
Unapozuia upande mmoja usitumie silaha kali lakini unawapatia upande mwengine silaha na kutamka kuwa yule aliepo madarakani aondoke kuna walakini mkubwa.
Gaddaffi bila ya shaka ame-overstay katika madaraka yampasa aondoke lakini sio kwa aina hii ambayo Polisi wa dunia wanalazimisha.
Nchi za Ulaya na marekani hazina tabia ya kuunga mkono wazi wazi waasi..sasa hapa kuna nini?
Na jee sasa utakuwa ndio mtindo mpya kila wanapoona kiongozi hawataki tena awepo madarakani wataweka no fly zone na military strikes?
Kama waasi wana-control sehemu ndogo tu ya nchi ni wazi kuwa waasi walikosea strategy.. waliponyanyua silaha...sio kama ile iliyotumika Egypt na Tunisia ya maandamano au ile inayotumika Yemen na Bahrain. hakuna serikali itakayotizama tu waasi wwenye silaha ni lazima kama kufa itawashambulia.
Lakini wababe wameshaamua basi Gaddaffi ataondoka tu.
Mkuu mleta mada Unafiki si wa waarabu tu. Hizi nchi zinazoshadidia kumuondoa Gaddaffi wao ndio magwiji wa unafiki.
Hapa kwetu wanasema uchaguzi ulikuwa huru na haki. Nani hajui kilichofanyika?
wachangiaji wengine tutumie lugha za kiuandishi ,maandishi ambayo yanasomwa na wengi. Tuache matusi. Tutoe hoja.