Mkuu, kwani wewe hujui tofauti?
Umeshaona POLISI inakuja na Ndege za kivita kushambuliwa waandamanaji MJINI?
Polisi wanakuja na Vifaru? Polisi gani hao? Hivi haya maswali mengine huwa mnauliza, huko kwenye bongo zenu huwa hata mnafikiria mara mbili kabla ya kuandika au mnalipuka tu?
Kwani POLISI wana MARK usoni kuwa ni POLISI? Wanaweza kabisa kuwa wanajeshi wamevalishwa magwanda kama POLISI na pia wanaweza kuwa POLISI wamevalishwa magwanda kama Wanajeshi. Tofauti yao KUBWA siku zote si hayo magwanda. Yaani hili nalo hadi ufundishwe humu JF?
Polisi wamefunzwa kutuliza FUJO wakati wanajeshi wamefundishwa KUUWA. Ni matendo yao, uwezo wao, na mwisho SILAHA zao zinazowatofautisha. Magwanda kila mtu anaweza kuvaa.
Ndiyo maana POLISI wakiuwa Mwanajeshi, haiwi soo ila wakiuwa Komandoo, inakuwa SOO. Sasa tatizo liko wapi kama wote ni Wanajeshi? Ila hili utakuwa ndiyo haufahamu kabisa na kwako ni kama Complex number kwenye mahesabu.
Mlie saana au mcheke, ukweli ni kuwa sasa hivi F-16 sinashusha vitu na Tomahawk zinatua.
Kibaya zaidi, wengi wao wanaandika hapa, wamekaa hizohizo nchi za Wazungu, nchi za mashoga, nchi za Mafirauni na Makafiri, nchi za Mateja nk nk ila maisha yao jamaa, yako juu. Umeme, maji, usafiri, usafi ni wa hali ya juu. Ulinzi wa uhakika na siyo kuogopa vibaka watakubeba juu juu usiku, camera kibao mitaani................ Yes, Baniani, mbaya ila kiatu chake.....
Foleni za Viza USA na UK, Mitanzania inatukanwa na kunyanyaswa ila kila siku inajazana ila kuomba VIZA. Na hapo wapo wa DINI zote.
Mkuu hapo kwenye red napata shida sana kuelewa. Yaani unataka kusema kuua ni sawa iwapo tu ni polisi ndiyo wanaofanya hayo mauaji. Hivi kama ingekuwa ni hivyo, ingemshinda kitu gani Mzee Ghaddafi kuwavalisha magwanda ya polisi hao wanajeshi wake na kufanya mauaji.