mbwa wasio na meno
Gadafi asubiri kunyongwa(kama hajafa hadi sasa hivi) na Libya itagawanywa katika nchi tatu; 1)Cyrenia 2) Fezzan na 3)Tripoilitania. Libya haikuwa nchi kabla ya mwaka 1922 huo ulikuwa ni utashi wa wataliano tu na hivyo itagawanywa kama ilivyokuwa awali. Pia Saudia isubiri kugawanywa katika nchi zake za asili kabla ya uvamizi wa ibn Saudi.
Hapo kwenye bluu, labda kama umemjua Gadafi juzi.
Kwa taarifa yako nchi zote za waarabu zilizo Afrika, huwa wanajitambua zaidi kama waarabu na si waafrica (japo wapo barani africa). Mambo yakiwaharibikia na wanapotafuta support ya other Africans ndio wanaanza kujiita Africans. Soma historia ya huko nyuma jinsi alivyo jaribu ku-champion arab nationalism ndio utamjua vizuri. Siku zote alikuwa anataka waarabu waungane. Alipopigwa chini ndio akaja na kimbelembele cha kujifanya mwafrika na kubadilisha OAU kuwa AU huku akitoa misaada kibao kwa nchi zetu zilizochoka kiuchumi ili aungwe mkono.
Mimi sikatai kuwa si kiongozi mzuri kwa wananchi wake. Ni kiongozi imara kwa watu wake na amewafanyia mambo mengi mazuri. Lakini pia ana ubaya wake. Kuua ameisha ua sana and he has overstayed.
Watu wanashabikia hii vita na upofu fulani. Wengine ni kwa sababu hawapendi alivyokaa muda mrefu na kuua raia. Wengine wanamtetea kwa kwa sababu wanajiona ni kama "ndugu" yao mwarabu wako (watanzania wanaona ujiko kujihusisha na uarabu) na wengine hata wanamtetea kwa sababu wanafikiri ni muislam na yale mataifa ya magharibi ni "crusaders".
Nafikiri ni vizuri kuiangalia vita hii objectively
Kwa mtazamo wangu hii vita sio vita ya kimaslahi- maana kama mafuta, makampuni ya magharibi yalisharuhusiwa kuchimba na biashara ilikuwa inaendelea. Mimi nafikiri ni vita ya visasi (kwa kutumia mgongo wa kulinda raia). Wazungu huwa hawasamehi, wanapenda kusamehewa wao tu. Nafikiri Gadafi kachemsha kwa kuua raia na jamaa wamepata sababu ya kulipiza alivyowahi kuwashughulikia huko nyuma.
Utakumbuka Gadafi alipo mpindua King Idris alifukuza makampuni ya mafuta ya nchi za magharibi. Baadaye alileta chokochoko miaka ya 80 kutaka wasijipitishe pitishe mediteranian. Wakati huo alikuwa hata anawa-support akina Carlos the Jackal na magaidi wengine. Akatuma majasusi wake walipue club moja kule ujerumani ambayo ilikuwa inatembelewa sana na american marines, wamarekani walipokufa pale, Regan akamtwanga mwaka 1986 na kuweka vikwazo. Yeye akalipiza kisasi kwa kutungua ndege (Lockebie bombing) na wao wakaendelea na vikwazo mpaka alipoamua kum-surrender yule jasusi aliyehusika).
Kwa mataifa ya Magharibi, Gadafi si mtu wa kumwamini ukizangatia historia yake, kwa hiyo kuna kila justification (on their part) ya kumwondoa madarakani (huku kichini chini wakilipiza kisasi) kwa kisingizio halali cha kulinda raia wa Libya na kuleta demokrasia.
Mkuu revolution ikitokea Saudi Arabia ndio tutawajua wamarekani.
Yote tisa,kumi ukweli ni kwamba,mataifa ya ulaya pamoja na marekani yako kimaslahi zaidi! Sidhani kama kweli wana uchungu na raia wanaokufa bila hatia. Kama ni kweli wana uchungu, basi nadhani wangetuma ngege za kivita plus askari wa nchi kavu sehemu nyingi tu za dunia zenye machafuko na hasa kipindi kile cha mauaji ya halaiki ya Rwanda na Burundi.
Pamoja na hayo, nchi nyingi za kiarabu zimekua zikiangaliwa kwa karibu sana na nchi za magharibi! Hii ni kutokana na neema ya mafuta waliopewa. Mbaya zaidi raia wengi wa nchi hizi ni wenye imani ya kiislamu,ambayo haikubaliki na mataifa haya ya magharibi na imekua ikibigwa vita kwa visingizio vya kila aina(ugaidi,siasa kali n.k)
Takwimu zinaonyesha Gadafi ni moja kati ya viongozi wachache shupavu duniani na amefanikiwa sana kuingoza Libya na hatimae kuwa na uchumi Imara. Nguvu ya umma iliyomtoa Mubarak Misri haiwezi kufananishwa moja kwa moja na mvutano unaoendelea Libya.
Mkuu hapo kwenye red napata shida sana kuelewa. Yaani unataka kusema kuua ni sawa iwapo tu ni polisi ndiyo wanaofanya hayo mauaji. Hivi kama ingekuwa ni hivyo, ingemshinda kitu gani Mzee Ghaddafi kuwavalisha magwanda ya polisi hao wanajeshi wake na kufanya mauaji.Angalia kesi kama ya Yemen. Huko jeshi halijaanza kuuwa raia bali POLISI. Inakuwa ngumu sana kuvamia wakati ni POLISI wako kazini kama ilivyokuwa Arusha. Karibu nchi zote za Kiarabu kwa sasa ni kuwa wanapelekwa POLISI. Kama wangelipelekwa Jeshi kuanza kuuwa raia, nina imani keshi ingelibadilika kabisa.
Juzi nimesikia Mwaarabu mmoja wa Bahrain akijitetea kuwa wao hawajapeleka jeshi hata siku moja ila ni Polisi tu. Hata wao wanafahamu kuwa likienda Jeshi, watakuwa wamekaribisha kibano cha akina F-16 na Tomahawk.
Muafrika na muanzilishi wa AU anashambuliwa na raia zake wanauliwa na waAfrika wengine wanachekelea na kuona raha.
Wanadanganywa na "media" kabla ya mashambulizi kuwa Ghaddafi anaua raia zake, na mijuha mingi inakubali.
Wamesahau "crusade" aliyoitangaza Bush! Na wamesahau wamerekani walivyozuwa na kudanganya kuwa Iraq kuna silaha za maangamizi.
Waliosahau na wanaofurahia wanajulikana ni kwa nini wamesahau na ni kwanini wanfurahia haya yanayojiri.
Wakumbuke nguvu ya "crusade" haikushinda miaka na vikaka, itashinda sasa. Kumuuwa Saddam au Ghaddafi si ushindi ni ushindwa. Kwa mwenye kuelewa ataelewa na punguwani atabaki kuwa punguwani.
mbona CCM wanawanyima uhuru wa kujichagulia viongozi wenu na mnaufyata? ya qaddafi yanawauma sana eeh!!
Namashaka na barua hii inaweza kua na mlengo flanix2 either kwa ajili ya kuwaandaa kimaamuzi wananchi wao au kwasababu tu ya kumdhalilisha Gaddaf .Kwenye Blue jamaa anabembeleza kavukavu na kwenye Red anajaribu kupiga mkwara kimtindo.Anyway let us wait...we shal c...........Jamani hizi taarifa zimetoka kwa la princessa,msichana ana nifurahisha sana na mawazo yake...leo hii tunasikia Gaddafi kumbe aliandika barua kwa ufaransa Sarkozy, Ban Ki Moon, na Daudi Cameroun wa Uk.. Kweli nimecheka .. Mzee mzima maji shingoni imebidi tu amwambie Mtu Mzima Obama 'Nakupenda' no matter what
Letter to Obama:
To our son, the honourable Barack Hussein Obama,
As I have said before, even if, God forbid, there were a war between Libya and America, you would remain my son and I would still love you. I do not want to change the image I have of you. All of the Libyan people are with me, ready to die, even the women and children. We are fighting nothing other than al-Qaida in what they call the Islamic Maghreb. It's an armed group that is fighting from Libya toMauritania and through Algeria and Mali. ... If you had found them taking over American cities by the force of arms, tell me what you would do?"
___
And to Everybody else
Letter to French President Nicolas Sarkozy, British Prime Minister David Cameron and U.N. Secretary-General Ban ki-Moon:
Libya is not yours. Libya is for the Libyans. The Security Council resolution is invalid because it does not follow the charter regarding the internal affairs of any country. This is terrible oppression, crude aggression.
You never have the right to intervene in our internal affairs. Who gave you this right? You will regret it if you dare to intervene in our country. Our country is not your country. We cannot fire a single bullet at our people."
hapa La Princessa World: Letter to Obama From Gaddafi
Mkuu hapo kwenye red napata shida sana kuelewa. Yaani unataka kusema kuua ni sawa iwapo tu ni polisi ndiyo wanaofanya hayo mauaji. Hivi kama ingekuwa ni hivyo, ingemshinda kitu gani Mzee Ghaddafi kuwavalisha magwanda ya polisi hao wanajeshi wake na kufanya mauaji.
Sehemu zote anazo kwenda America jua kuna maslahi tu haendi hivihivi,nauliza Bahrain hakuna mauaji ya raia?hii lazima mtambue kuwa Libya kuna utajiri mkubwa wa mafuta,wakishambulia baadae wataikalia Libya mpaka wahakikishe wamefyonza mafuta ya kutosha kama walivyo fanya Iraq na kuacha nchi ikiwa hoi mpaka raia wanaanza kuuwana wenyewe kwa wenyewe,yaliyopo Iraq yanakuja Libya.
Mkuu, kwani wewe hujui tofauti?
Umeshaona POLISI inakuja na Ndege za kivita kushambuliwa waandamanaji MJINI?
Polisi wanakuja na Vifaru? Polisi gani hao? Hivi haya maswali mengine huwa mnauliza, huko kwenye bongo zenu huwa hata mnafikiria mara mbili kabla ya kuandika au mnalipuka tu?
Kwani POLISI wana MARK usoni kuwa ni POLISI? Wanaweza kabisa kuwa wanajeshi wamevalishwa magwanda kama POLISI na pia wanaweza kuwa POLISI wamevalishwa magwanda kama Wanajeshi. Tofauti yao KUBWA siku zote si hayo magwanda. Yaani hili nalo hadi ufundishwe humu JF?
Polisi wamefunzwa kutuliza FUJO wakati wanajeshi wamefundishwa KUUWA. Ni matendo yao, uwezo wao, na mwisho SILAHA zao zinazowatofautisha. Magwanda kila mtu anaweza kuvaa.
Ndiyo maana POLISI wakiuwa Mwanajeshi, haiwi soo ila wakiuwa Komandoo, inakuwa SOO. Sasa tatizo liko wapi kama wote ni Wanajeshi? Ila hili utakuwa ndiyo haufahamu kabisa na kwako ni kama Complex number kwenye mahesabu.
Mlie saana au mcheke, ukweli ni kuwa sasa hivi F-16 sinashusha vitu na Tomahawk zinatua.
Kibaya zaidi, wengi wao wanaandika hapa, wamekaa hizohizo nchi za Wazungu, nchi za mashoga, nchi za Mafirauni na Makafiri, nchi za Mateja nk nk ila maisha yao jamaa, yako juu. Umeme, maji, usafiri, usafi ni wa hali ya juu. Ulinzi wa uhakika na siyo kuogopa vibaka watakubeba juu juu usiku, camera kibao mitaani................ Yes, Baniani, mbaya ila kiatu chake.....
Foleni za Viza USA na UK, Mitanzania inatukanwa na kunyanyaswa ila kila siku inajazana ila kuomba VIZA. Na hapo wapo wa DINI zote.
Hizo collateral damage nadhani zimepikwa na Gaddafi. Itakuwaje maiti ziwe na majeraha ya risasi wakati wavamizi wa NATO wanatumia mabomu? Hii hainiingii akilini!Mkuu.
Observation yako ni kweli...lakini tayari West na US bombing tayari inazalisha collateral damage huko Libya. Umewasikia Arab league wanavyosema? Wao wanafaidika vipi na misaada ya Libya?
Bosnia kuna nini?
Afghanistan kunani?
Somalia kunani?
Grenada kunani?