Mshume Kiyate
JF-Expert Member
- Feb 27, 2011
- 6,764
- 896
sio siri yametengenezwa kwa ubora sana.Dah,dude lime crash afu hajafa mtu?
Hehe,ingekuwa ya nchi fulani hapo duh,majivi tu
Kwanini wamarekani wanakua wababe juu ya mataifa mengine? Je wanataka kumuua Gaddafi km walivyomnyonga sadam Hussein bila kupata walichoita silaha za maangamizi? AU nini maana ya uwepo wake km hawana maamuzi ktk hili?
sio siri yametengenezwa kwa ubora sana.
hata wangekufa isingeathiri operation hii ya kumwadabisha Gadaff kwa sababu operation yeyote ya kijeshi ni nadra kuepuka kifo.
Americans will die but pro-Gadaff will die too and suffer the most
Inaitwa operation odyssey down .ni kwamba huyo odyssey alikuwapo ni shujaa wa vita ugiriki,aliondoka kwa miaka 19 kwenda vitani,vita vya trojan amerudi akapokelewa na A THENA ,ambaye ni mwanamke ambaye sasa wanamuabudu kama mungu wa vita alizaliwa march,19 na birthplace yake ni libya.fanya research.
Hiyo ndege imepigwa waache longolongo.
Vita vinapingwana libya NO CEASEFIRE.history hii ni ya miaka ya 450 before jesus search
:lol::lol:.....wanaokufa Libya si pro Gadaffi tu....hata rebels na wale wasio na msimamo wanakufa.....makombora hayajui ku-identify pro Gadaffi,wakishaamua wana target sehemu fulani wao wanaenda....hivi wewe kule Iraq wanaokufa hadi leo ni Pro Saddam Hussein? si alishanyongwa siku nyingi....leo miaka kumi na usheee wanaokufa ni kina nani???wananchi wa kawaida.....Afghanistan je....? majengo yanayoharibika,miundombinu na watu kukosa huduma muhimu zinawakuta pro-gaddafi tu,ni Libya yote:washing:
Wamarekani kamwe hawawezi kukubali kuwa ndege yao imedondoshwa na anti-aircraft missiles za Libya unless kuwe na indisputable proof! Na hata kama kuna indisputable proof bado wata spin tu! Hivyo ndo vita zilivyo...full propaganda.
Kwanza nashangaa kwa nini mpaka sasa Ghaddafi hajajipa credit za kuitungua hiyo ndege.
Chelle...miaka kumi na ushee ya nini? Maana vita vya kumng'oa Saddam vilianza Machi 2003...au unazungumzia Operation desert storm?
Vita waga haianzii pale makombora yanaporushwa.....propaganda huwa zinatangazwa kuashiria vita.....inaanza vita ya propaganda,inapelekwa UN wanaongea weeee then vita ya makombora inaanza....na ndo maana yeye Gaddafi kasema ni vita ya muda mrefu, akijua hata pale mambo yatakapoonekana yametulia hali vita ya chini chini kama ya kulipua ndege mfano wa Lockerbie,kulipua bar na kuua watu wenye rangi fulani itaendelea.....:washing:
Nimekupata! Na ninakubaliana na wewe kuwa propaganda ni sehemu muhimu ya vita.
Na sasa hivi Marekani kuongoza mashambulizi dhidi ya Libya (licha ya kuwa sikubaliani na Ghaddafi) ndio kutazidi kuongeza maadui dhidi yake. Sitashangaa siku za hivi karibuni kusikia raia wa Marekani wamelengwa na shambulizi la kighaidi mahali fulani...
The thing is, the US has no clear objective(s) in this war. Now the million dollar question is, what if Ghaddafi survives this onslaught?
Hahaaaa let me get my popcorn ready...
Nilikua namsupport sana Obama,bila sababu ya msingi (huenda ni ngozi yake) lakini nagundua huyu bwana ni mwepesi as well...tokea awali niko tofauti sana na western kwa namna wanavyoichukulia Afrika,tena kwenye maeneo yenye manufaa kwao..ni wafitini,wazandiki na wanaopandikisha chuki kwa watu dhidi ya viongozi wao ili kuwajengea picha mbaya na mwishowe kuanzisha vurugu ambazo nao huingia lakini lengo lao ni kuhujumu tu....
Nasupport viongozi imara.......western nia yao ni kuweka watu dhaifu kwenye uongozi ktk nchi wenye maslah ili kuendelea kuvuna rasilimali ilihali wenye nchi wakiomba misaada kila kukicha! Ipo siku Mungu atawaadhibu as well! Mungu ibariki Afrika, ashame upon u American na vibaraka wengine!