Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
We Kichuguu acha kutoa taarifa zisizothibitika kwa ma confidence kumbe uongo. Weka source yako kwamba mtoto wa Gaddafi kafa.Hapana, hakupigwa ni zile Tomahawk (yaani vishoka - katika lugha nyingi za wahindi wekundu) zilizoangushwa na majeshi ya kimarekani. Huyu kauwawa na mmoja wa mapailot wake mwenyewe ambaye hakutaka kutekeleza amri ya kwenda kuangusha mabomu kule Benghazi; akaamua kwa makusudi kuangusha ndege yake ya kivita mbele ya huyu kijana na kumjeruhi vibaya sana. Baadaye amefariki.
Mkuu.Hapo kwenye red baadhi ya hao wananchi wa Libya wanaomtaka aondoke madarakani wameomba msaada wa jumuiya ya kimataifa na wito wao umeitikiwa. mbona CUF ilivyokuwa inazunguka dunia nzima kuomba nchi wahisani ziinyime serikali ya Tanzania misaada watu walikaa kimya tu?
Sababu ya wao kupata kipondo leo ni nini?Mkuu.
Una mfano mwengine wowote ambapo waasi wa serikali wameomba msaada kwa mataifa haya na haya mataifa ya West na US kufanya haraka kupeleka azimio UN na msaada ukatolewa kwa waasi ili waiondoe serikali iliyopo madarakani?
Mkuu, kuna watu waliomba msaada wa kusaidiwa kama wapalestina duniani? response ya hawa West na US ikoje kwa waombaji hao msaada ambao wanapata kibano cha nguvu...hata leo hii wamechezea kipigo, watoto na wanawake ni katika waathirika.