The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

Yule bwana alokua akijifanya chizi kwa kuua watu wake kila kukicha, amepata akili baada ya kuchezea kichapo kutoka France, US na UK. BBC wameonyesha live viongozi wa jeshi wakitoa amri kwa vikosi vyote kusitisha mashambulizi ya aina zote kwa hao waliokua wanawaita 'rebels' wametoa amri kwamba badala ya kushambulia watu wahakikishe watu wote wako salama, hakuna ruhusa kushambulia mtu yeyote...Hongera Obama and the co, kumbe huyu bwana akili anayo ule uchizi ulikua wa kujifanyisha

Hayo mataifa Wameyafanya ya Iraki yamewashinda, wameyafanya ya Afganstan yamewashinda sasa ni Libya!

Sioni sababu ya wao kuingilia na kujifanya wanatetea wananchi, Wana lao jambo wale hamna kitu, Hawawezi kwenda Somalia wala Ivory Coast.
 
Mimi simmpendi Gaddafi kwa yale yote anayofanya kwa kuwanyima demokrasia na baadae kuuwa watu wake, lakini ningependa kujua maoni yako kuhusu Sudan na Somalia ambako raia wengi sana wameuawa na serikali zao au vikundi vya kigaidi lakini hatujaona effort yoyote ya kijeshi kutoka Western powers, unafikiri ni kwanini?
Ongea wewew maana watu wanaangaliaga tu upande mmoja
 
Lets be realistic on this. Inawezekana kabisa ile uprising ilikuwa legitimate. Lakini ule uhalali unaondolewa na uvamizi wa aina hii. Walibya hawatakuwa proud kwa kuondoka kwa Col Gaddafi maana hawajamuondoa wao bali atakuwa ameondolewa na nchi nyingine. Ya Libya ni tofauti na Tunisia na Egypt. Kule wananchi waliamua lakini kwa bahati mbaya Libya ile legitimacy yao imeondoka.
Hebu tulinganishe situation ya Libya na Bahrain. Yale yanayotokea Libya hayana tofauti na yale ya Bahrain. Where are the western powers in controlling the killings of civialian population in Bahrain? Is it because of Iran influences on Shia or because people are not loosing their life. There are alot of double standards. Kuna vita vingi saana hapa duaniani na palikuwa hakuna sababu ya kuanzisha vita nyingine. Mbona Somalia pale hapajatulia na kama wao wana maguvu, kwanini wasipatulize pale?
 
wanaompinga Gadafi ni wahasi kwani nguvu ya umma toka lini wakatumia silaha?
Waafrika haswa wa Tanzania wasomi na wanazuoni kama mmeweza kutambua propaganda za ccm dhidi ya cdm iweje tuwatukuze hawa ngozi nyeupe?
Excellent
 
Eti imagine alikuwa anaenda kukagua gwaride la jeshi akiwa amevaa kandambili. Yaani mtu analewa madaraka mpaka anajisahau. Watu wabishi tuu hapa. Nyerere angekuwa madarakani mpaka leo, na sisi lazima tungekuwa on the streets. Tatizo ni kwamba wabongo hatujawahi kuwa chini ya udikteta. Ndio maana unaona watu hapa wanamfagilia tuu gaddafi. Imagine mume wa mtu alikamatwa miaka 20 iliyopita kwa kupingana na rais. mpaka leo mke hajui kama aliuawa au yuko hai. Akiulizwa hapati majibu. watoto wamekua na hajui kama baba yao yupo hai. They cannot ask b'se they are afraid, nao watafanyiwa kitu mbaya. Imagine ndugu zako wamekamatwa na kuwawa simply because they wrote an article on a newspaper about their politcal view. Just political political opnion nothing more. Imagine you are living in a country, where Jamii Forum is illegal and banned. Watu wanaongea tuu b'se they have never experience living in a dictatorial regime.

Juzi watu wamepigwa risasi na polisi hapo arusha, saw what happened. Imagine ingekuwa nchi nzima tena na wanajeshi. Msingeomba msaada?? Some people here are speaking whatever they want, simply because they have got that freedom to do so. Then, wakati wengine wanajaribu kipigania the same freedom to express themselves, mnawakandia na kumkumbatia dikteta. Watu wanahoji mbona hawavamii Somalia na Ivory Coast. The moment they do so, you will still be saying the same. Lakini siku haya yakitoa bongo, mtakuwa mstari wa mbele kuomba msaada tena kwenye hayo hayo mataifa ya magharibi and sio African Union, b'se you know under gaddafi, AU wont help you.
 
Mimi simmpendi Gaddafi kwa yale yote anayofanya kwa kuwanyima demokrasia na baadae kuuwa watu wake, lakini ningependa kujua maoni yako kuhusu Sudan na Somalia ambako raia wengi sana wameuawa na serikali zao au vikundi vya kigaidi lakini hatujaona effort yoyote ya kijeshi kutoka Western powers, unafikiri ni kwanini?

Hili swali ndilo wengi wanajiuliza bila kupata majibu.
Na nimeshasema kuwa huo uvamizi sio bure, kuna maslahi kwa mataifa ya Magharibi.
Au ni kisasi kama mchangiaji mmoja alivyosema hapo awali.
 
i think this one should be katika jukwaa la jokes na utani
 
Jamani hizi taarifa zimetoka kwa la princessa,msichana ana nifurahisha sana na mawazo yake...leo hii tunasikia Gaddafi kumbe aliandika barua kwa ufaransa Sarkozy, Ban Ki Moon, na Daudi Cameroun wa Uk.. Kweli nimecheka .. Mzee mzima maji shingoni imebidi tu amwambie Mtu Mzima Obama 'Nakupenda' no matter what

UK's prime minister ni David Cameron na si Daudi Cameron

Kumbe David na Daudi kuna tofauti...?

oooh ndio maana Gabriel na Jibrilu pia ni tofauti
 
Hayo mataifa Wameyafanya ya Iraki yamewashinda, wameyafanya ya Afganstan yamewashinda sasa ni Libya!

Sioni sababu ya wao kuingilia na kujifanya wanatetea wananchi, Wana lao jambo wale hamna kitu, Hawawezi kwenda Somalia wala Ivory Coast.
Ndio hawa wanafanya kazi ya kulinda raia katika nchi wanazozishambulia.

US Army apology for photos of soldiers with Afghan body

The US Army has apologised for graphic photographs of US soldiers grinning over the corpses of Afghan civilians they had allegedly killed.

The photos published by Germany's Der Spiegel magazine were said to be among many seized by US Army investigators

BBC News - US Army apology for photos of soldiers with Afghan body
 
Si kweli, Shujaa Ghadafi hata siku moja hawezi jishusha namna hii. Hii letter imepikwa kumdhalilisha Ghadafi.

Najua westerners watamshinda Gadafi, lakini Libya itamkumbuka sana. Wakati walibya wanajenga nchi yao upya...westerers wanachota mafuta ya bure Libya kama vile hayana mwenyewe.

Ni kweli Gadafi aliandika hii barua hata vyombo vya habari vioneshwa ikisomwa na msemaji wake
 
Si kweli, Shujaa Ghadafi hata siku moja hawezi jishusha namna hii. Hii letter imepikwa kumdhalilisha Ghadafi.

Najua westerners watamshinda Gadafi, lakini Libya itamkumbuka sana. Wakati walibya wanajenga nchi yao upya...westerers wanachota mafuta ya bure Libya kama vile hayana mwenyewe.
Ni kweli hiyo barua aliiandika kama maneno hayo yanavosomeka!!
 
Hayo mataifa Wameyafanya ya Iraki yamewashinda, wameyafanya ya Afganstan yamewashinda sasa ni Libya!

Sioni sababu ya wao kuingilia na kujifanya wanatetea wananchi, Wana lao jambo wale hamna kitu, Hawawezi kwenda Somalia wala Ivory Coast.

Waende Somalia kwa no fly zone ya nini wakati hakuna hata ndege?
 
Hayo maamuzi ya 'Useless Nations(UN)' ndiyo yamepelekea virugu zaidi..na ukifuatilia zaidi kwa CNN,BBC na France 24 unaona wanavyokuwa-biased kana na kuonyesha jinsi wanavyojifanya kusaidia.. Check out Aljaazerah na Russia Today utapata upande mwingine wa habari..
I feel sorry for Libyans, naomba hii vita iishe karibuni.
 
Wakati hiyo useless nations (UN) walipokaa kimya kwenye yale mauji ya Rwanda watu mlipiga kelele kama nini. Leo wameact kuzuia another massacre, mnapiga kelele. what you want this useless nations to do?
 
...Ivory coast je?

AU ya kina Kikwete si ilisema iachiwe imalize mgogoro WA ivory coast, wameachiwa ata jibu la kueleweka halipo. Vile vile tayari kuna wanajeshi WA UN uko (wanamlinda Qattara)
 
...Ivory coast je?

Ivory coast mbona ipo simple. AU walisema watautatua huo mgogoro wao wenyewe. Ndio maana wakawatuma akina JK huko. Wamekataa kuomba msaasa toka security council. Umeshasikia wameomba military intervention wakakataliwa? Kama wakiomba watapata. Mbona ECOWAS na OAU waliomba msaada UN with regard to Liberia wakapewa? Ila ya Ivory Coast, AU imetia aibu.
 
For the 100th time, Somalia tayari kuna majeshi ya kulinda amani chini ya AU (yanaongozwa na Uganda)....! Vile vile hakuna nchi inayotaka kujitolea wanajeshi baada ya kile kilichotokea miaka ya 90 kwa wanajeshi wa UN. Muwe mnapitia pitia historia kidogo jamani kha!!
 
Back
Top Bottom