Sio kukimbia hoja, ukitaka kujadili uovu wa Israel na innocence ya wapalestina anzisha thread yake, hii thread inahusu Libya sasa tusiivuruge.
Mkuu.
Sawa kama unahisi kuwa tuanzishe mada pekee inayozungumzia uovu wa Israel na uvunjaji wao wa haki za wapalestina.
lakini kwangu mimi haikuwa kuzungumzia Israel na wapalestina per se.
Lengo ilikuwa ni kuonesha unafiki wa UK,France na US, pia kuonesha West na US wao wenyewe kwa kulinda maslahi yao hujifanya ni wasambazaji wa demokrasia na kulinda haki za binadamu. Huku wao wenyewe wanakiuka hizo haki za binadamu na hakuna wa kuwadhibiti au kuwaaadabisha. Wameua raia wengapi wasio na hatia katika vita vya Iraq na Afghanistan?
Mifano niliyotoa ni pamoja na ile ya kuivamia Iraq nq Afghanistan....kuunga mapinduzi yaliyomuondoa Chavez kwa siku mbili tatu.. na sasa kuwasaidia rebels kumuondosha Gaddaffi kwa kisingizio kuwa wameombwa na rebels...sio waandamanaji...kwa kawaida wao west na US huwaita wabeba silaha vikundi vya ugaidi na terrorists..unafiki mwengine huu.
Mfano wa kuifumbia macho Israel au kuikinga ni kupinga tu kauli ya wanaosema West na US wameingia Libya kukinga raia. It is a big lie!
Ukipitia wito wa Cameroon na Obama wanasema hawataki kumdhuru Gaddaffi lakini ni sera yao aondoke. Why?
Mimi ni mmoja ninaoona mbali na udikteta wake Gaddaffi ameijenga Libya...sasa west na US wanaibomoa ili wapate contract za reconstruction, kuuza silaha na kuidhibiti serikali itakayokuja Libya. Simply to safe guard their interests.
kama ilikuwa ni kuilinda Bengazi au watu wa bengazi basi wangeeka buffer zone na hii ingekuwa simple solution...wangepeleka ujumbe wa UN libya ili kutatua kidiplomasia mzozo huu.
Je leo raia wa Libya wana maisha bora kuliko pale maandamano yalipoanza na uasi wa kutumia silaha ulipoanza?
Soon ,watafahamu kuwa West na US wanakusudia kuwaekea kiongozi kibaraka tu na ugumu wa maisha ndio wameanza kuuonja. Mzozo ukiendelea kwa miezi miwili ndio watatia akili.
West na Us intervention katika nchi za dunia ya tatu na Mashariki ya kati means maisha magumu kwa raia. Wapi walipoingia pakawa salama? na maisha kuboreka?
Hata kama hatumpendi au hatumtaki Gaddaffi, West na US kwa dhambi waliyoifanyia dunia hii hawana haki wa kufanya wanayofanya.