The story of my life: Ukweli mchungu baada ya kugundua mtoto tulie naye hakuwa mtoto wangu

The story of my life: Ukweli mchungu baada ya kugundua mtoto tulie naye hakuwa mtoto wangu

HISTORIA YA MAISHA YANGU

Naomba nielezee historia ya familia yangu kwa ufupi kidogo ili kuja kupata picha nzur badae.

Mimi ni mtoto wa 3 kwenye familia ya Watoto 5 nina dada ka kaka yangu ambao wakubwa kwangu na wana familia zao na Maisha yao na pia nina wadogo 2,mzee alishafariki tumebaki na bmkubwa.

Bi mkubwa alikuwa amesharetire na anafanya shughuli zake ndogo ndogo za ujasiliamali,kingine ni mtu ambae anapenda sawa Watoto/wajukuu yani yeye hiyo ndio Furaha wajukuu wajae home wale wanywe maziwa (anajishughulisha na ufugaji pia) waondoke wamenenepa basi hiyo ndio Furaha yake.na pia kwenye kila familia alitoa ahadi ya wajukuu zake anawapa asset ye alilkuwa anasema kabla hajafa so kwa brother mkubwa (ana mtoto 1) na sister (2)wale Watoto akawapa Mashamba watagawana wakikuwa na wazazi marufuku kuuza hadi wajukuu wakue basi ikawa hivyo.

Tuendelee

Sasa alivyosikia mchumba wangu mjamzito akaja nyumbani akatoa nasaha zake akaondoka.

Tukaendelea na Maisha pale muda ukafika wa kuanza clinic mchumba wangu akapata gyno mmoja huwa nakuwa na session za clinic kwenye hospital moja ipo maeneo ya mikocheni,basi tukaanza safari za kuattend clinic hapo.Tukashauriana tutafute kausafiri kwa ajili ya sasa ye mjamizto na pia mtoto akija kuzaliwa ili kusiwe tunapata challenge ya usafiri toka sehem moja kwenda nyingine.Nilikuwa na kaakiba changu kama 5m na pia nikachukua mkopo kwenye mfuko wa office kama 2m so nikawa kama na 7m tukaona kwa hii price gari tutakayoweza kuimudu ni kuchukua mkononi kwa mtu.

Bahati nzur on that time pale ofisini kwetu kulikuwa n bro mmoja huyu yeye nilimkuta kazini alikuwa amepata scholarship anaenda nje kusoma na nilikuwa nimezoeana nae sasa katika maongezi yetu siko moja nikamwambia natafuta kigari cha kuzugia nichukue mkononi kwa mtu mana sina budget ya kutosha.Jamaa kama Bahati akaniambia yeye ataondoka kwa hiyo kama vipi aniuzie gari yake yeye alikuwa na ist ilikuwa bado mpya mpya tu kwa makubaliano nimpe 8m nyingine nitammalizia mdogo mdogo,nikapambana nikapata 8m yule mchumba wangu alikuwa na akiba alichangia 500k tukampa jamaa akatuachia gari na Maisha mapya ya kumiliki kausafiri yakaanza kidogo ikawa inatusaidia zile trip za clinic na mizunguko michache.

Baada yah apo nikawa nafikiria means ya kuongeza kipato kwasababu gari inahitaj mafuta/service na huku mshahara wangu ulikuwa umepungua kwasababu ya kukatwa kwa ajili ya ule mkopo,katika kufuria idea ya nncha kufanya nikapata story ya uber ndio ilikuwa imetoka kuanza anza enzi hizo tulikuwa tunatumia hata number plate za njano sharia hazikuwa ngumu sana kama siku hz kwa hiyo nikaanza kula vichwa.

Kwa hiyo ratiba yangu ilikuwa weekdays asubuh naenda job natoka ile saa 11 sharp narud home hapo gari nakuwa nimeiacha nyumbani kusave mafuta then nalala kidogo hadi saa moja the naamka naanza kula vichwa hadi saa 5-6 ndio narud home kulala na weekends nilikuwa naamsha siku nzima na nashkuru nilifanikiwa kuongeza kipato kidogo Maisha yakawa yanaenda.

Siku moja nimempeleka clinic mchumba wangu pale ile hospital amabyo huwa tunaenda nilionana na class mate wangu wa primary school ni madada mmoja alikuwa nurse pale mda huo mchumba wangu alikuwa ndani basi tukasalimiana pale akanitambulisha kwa manurse wenzake na mchumba wangu alivyotoka alikuwa amsharud mezani kwake kwa hiyo nilimuaga kwa mbali tukaondoka.

Huyu dada nilikuwa nimezoeana nae sana kwasababu primary me nilikuwa mtu wa utani mwingi na utundu mwingi kwa hiyo ilikuwa rahisi kuzoeana na watu wengi sana hasa kwenye darasa letu

Miezi ikaenda tukawa tunaenda pale clinic yule classmate nilikuwa simkuti tulikuwa tunapishana yeye alikuwa anaingia shift nyingine so sikuonana kwa muda na me nilikuwa naendelea na ratiba zangu za job na uber na badae nilikuwa nampeleka clinic ila naishia nje akiwa Tayari ananishtua namfata tunarud nyumbani.

Miezi ikaenda ikaenda akakaribia kujifungua nashkuru alijifungua salama wkati anakaribia mama yake alikuja home so tukawa na mama mkwe na dada wa kazi na alipojifungua bmkubwa wangu akafunga safar akaja ila hakukaa sana kwasababu pale nyumbani palikuwa padogo kupokea watu wengi na pia mchumba wangu aliniomba yupo comfortable kuhudumiwa na bmkubwa wake so mama hakukaa sana akarud nyumbani.Sasa kama mnavyojua mtot akizaliwa story za hapa na pale sijui kafanana na nini zinakuwaga Nyingi ila ilionekana hakuwa amefanana na baina yetu wawili yani mimi au huyo mchumba wangu kuanzia rangi na vitu vingine me nilikuwa sijui hayo mambo kwasababu sina uzoef ila wakongwe wale wanaokuja kutembea wanaongea pale, na hiyo wala haikunipa shida nilikuwa najua mambo ya genetics tulisoma shule so nilichukulia kawaida huwa inatokea.

Sasa nakumbuka hapo kabla nyuma nakumbuka tulikuwa tunataniana (kuna muda nilikuwa namuita dogo) kulikuwa na meme flani ya pic sikumbuki vizur ila ilikuwa wazazi wamebeba mtoto halafu mtoto alikuwa amefanana sijui na kiongozi wa dini sijui wa serikali sikumbuku vizur, sasa nikamtania kwa kumtumia ile pic then nilimwambia “mdogo wangu ukileta mtotos copy yangua nakutoa mbio hadi kijijini kwenu nilitaja jina la Kijiji chao”.Lakini ile story tu wala haikuwa hivyo.

Sasa bwana kumbe bmkubwa alivyokuja pale mwanzoni kuna kitu alinotice lakini hakusema akaona ajipe muda mtoto akuwe aone kama kuna kitu aliona utofaut au vp (hii nilikuja kuambiwa badae sanaaa),na pia alibaki nayo moyoni hayo mawazo bila kusema kitu kwa sababu alihisi labda ningeumia au ningeleta shida na kiukweli bimkubwa wangu kwa mujibu wa ndugu na jamaa na majirani wanasema katika makuzi yangu mimi ndio nilikuwa kipenzi chake kwa hiyo akaona areserve comments zake ili kuepusha kuniumiza mimi kwasababu huku mwanae nilishaoza na hivi kuna mtoto mpya basi hauniambii kitu.Kwa hiyo alikaa baada ya miezi kadhaa alirudi tena akatusalimia hii mara ya pili alikaa tena siku kadhaa akaondoka.

Tukawa tuanendelea na maisha baadae tena alirudi baada ya miezi kadhaa alikuja kutusalimia mara hii alikuja na aunt yangu yeye ni dada yake na marehem mzee wangu wanafatana, huyu alikuwa ni nurse huko mkoani ila alikuwa amesharetire kipindi hicho,sasa wakatusalimia wakaondoka, wakazuga kuna mgonjwa walikuja kumuona muhimbili by that time kulikuwa na baba yangu mkubwa mmoja alikuwa anaumwa so wakaniambia yule aunt alikuja kwa sababu hiyo na bmkubwa yeye alimsindikiza na wakaona waje kumsalimia mmjukuu wao.

-Kumbe hicho kipindi chote walikuwa wanaangalia tu me sina hili wala lile,tukawa tunampeleka mtoto clinic na nini.sasa kuna kitu kilijitokeza hapo kika nipa mashaka sana



Itaendelea …………..
Hata sijasoma, lirefu sana
 
Hapo kwenye kuachia vyote ni busara na huruma ya jamaa tu haswa kwa mtoto asiye na hatia...

Jamaa angeweza pia kutumia "ukurya mwingi" kwa kumtimua mama na mtoto na akabaki na mali zake (na wengi ndio hufanya hivi)...
Ni busara na huruma inayoumiza, ila kwavile alifanya kwa moyo mmoja, pongezi kwake.

Katika maisha kuna viporo sio vya kupasha, vitakuumiza tumbo. Huyu Binti kiporo alichopasha na sponsor wake, kimempa majuto ambayo hatoyasahau
 
Mtoa mada, Kuna watu hapa Duniani Kwa sababu ya Ubaya wao Huwa ama hawatakiwi uwape huruma au hawastahili kabisa kuishi... Hi ndio kanuni ya Asili ikiwa Unahitaji Furaha na Mafanikio.

Kwann nimesema haya.....


Kakusaliti, Kabeba mimba, mbaya zaidi kuendelea kudanganya mpaka hatua ya mwisho ya kuomba Msamaha.


Alafu Et bado, Ukamwachia Kila kitu, Ukamwachia na Gari 🤣🤣🤣.

Kwamba ndo Ugud Guy??? ... Wee ni mpuuzi tu.


Kwahiyo ukayaacha hayo yote ukaenda kulala chini ? ???. Wee ni mjinga.



What if , Taasisi uliyopo katika kupunguza wafanyakazi ,nawee ungepunguzwa?.

Hya Bidada , anaolewa na Mwanaume mwingine, au Huyo Mzeee alozaa naye , Gari linakua la Mzee 🤣🤣, Kitandan ulichoanzia Maisha , anatombewa hapohapo.



Vipi Mama yako ana gari?? Vipi thamn za kwenu za ndan Kwa Mama yako? Mama yako anakitanda kizuri??

Hayo maswali yatoshe kukupimisha kama wee ni mpuuzi au Lah !!.



Itoshe tu kusema haya, Inawezekana ni tukio la kweli ila umeongezea chumvi Kwa sehem baadhi au Stori kama zingine !!.



Kwa namna nilivyo mbinafsi , Mwanamke anifanyie ivooo🤣🤣🤣🤣 labda kama Mimi sio wa Kanda ya ziwa !!.
 
-Kwanini ulimwachia vitu vyote hivyo?

-Alitoa asilimia 8 tu kwenye kununua gari. Angeenda kuanza upya na huo mchepuko wake. Alikudanganya sana hakustahili huruma ya kuachiwa vitu.

-Ila karma is a good teacher, yatamrudi ipo siku.

-Kama mwanaume mwenzio nimeumia roho sana. Umepitia mazito na magumu.

-Pole sana kaka.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Kwamba alitoa 8% only apite hivi
 
Halafu watu hapa mmepata somo lakini utashangaa bado wanaenda kubambikiwa. DNA liwe takwa la lazima kisheria Tanzania hii
 
kutaniana kwa sana kukutana mara chache chache mida ya lunch maeneo ya ofisini kwao kwenda kupata lunch kwa hiyo that was our life.
Lunch alikuwa analipa nani😀 swali la kizushi tu
mara Nyingi nilikuwa nawith draw siku za hatar na hii hadi aliniuliza nawezaje kwasababu ex wake alikuwa hawez (hii nilikuja kuconnect dot badae)
This should have been the first clue. Sijafika mbali bado niko ya kwanza but I am wondering whatever went wrong it started here😀
 
Umesema kisa chako ni miaka 9 mpaka 10 iliyopita alafu tena huo mwaka baada ya manzi yako kupata mimba ukanunua gari ukaanza kupiga na mishe za uber na uber imekuwa established bongo 2016??

CHAI
Hivi unajua toka 2016 mpk sasa 2023 ni miaka saba imepita
Na katika MAHUSIANO mpk kuja kuishi pamoja kwa mujibu wa story ukiifatikia kwa umakiniwalidate kwa zaidi ya miaka 2 au 3 mpk mdada aliposhika ujauzito
Soma story kwa umakini utaelewa
 
kumbe dada alikuwa ameshakata shauri la kuachana na mzee ili aje kwangu kwa hiyo alikuwa kama amempa mzee mara ya mwisho kama ndio ya kuagana na mzee alikuwa hawez kuwithdraw since wako pamoja ndio mana kama unakumbuka kule mwanzon aliniuliza ninawezaje kumbe mzee ilikuwa hivyo na anhisi hicho kipindi ndio alipata ujauzito coz alichanganya siku zake na mzee kama alimfanyia kusudi kwasababu alivyomwambia mzee akamwambia atalea.
🤣🤣🤣 I knew it
 
Mkiambiwa muwe ma play boy kama mimi hamtaki mnataka kujitwisha mizigo ya shida,haya niko paaaaaale nawacheki.
 
Mtoa mada, Kuna watu hapa Duniani Kwa sababu ya Ubaya wao Huwa ama hawatakiwi uwape huruma au hawastahili kabisa kuishi... Hi ndio kanuni ya Asili ikiwa Unahitaji Furaha na Mafanikio.

Kwann nimesema haya.....


Kakusaliti, Kabeba mimba, mbaya zaidi kuendelea kudanganya mpaka hatua ya mwisho ya kuomba Msamaha.


Alafu Et bado, Ukamwachia Kila kitu, Ukamwachia na Gari [emoji1787][emoji1787][emoji1787].

Kwamba ndo Ugud Guy??? ... Wee ni mpuuzi tu.


Kwahiyo ukayaacha hayo yote ukaenda kulala chini ? ???. Wee ni mjinga.



What if , Taasisi uliyopo katika kupunguza wafanyakazi ,nawee ungepunguzwa?.

Hya Bidada , anaolewa na Mwanaume mwingine, au Huyo Mzeee alozaa naye , Gari linakua la Mzee [emoji1787][emoji1787], Kitandan ulichoanzia Maisha , anatombewa hapohapo.



Vipi Mama yako ana gari?? Vipi thamn za kwenu za ndan Kwa Mama yako? Mama yako anakitanda kizuri??

Hayo maswali yatoshe kukupimisha kama wee ni mpuuzi au Lah !!.



Itoshe tu kusema haya, Inawezekana ni tukio la kweli ila umeongezea chumvi Kwa sehem baadhi au Stori kama zingine !!.



Kwa namna nilivyo mbinafsi , Mwanamke anifanyie ivooo[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] labda kama Mimi sio wa Kanda ya ziwa !!.
Kila mtu ana maono yake kwenye kichwa chake usitake unavyofikilia ww n mwenzio naye afanye hivyo itoshe kusema kuanza upya sio ujinga jamaa hakutaka kelele za kugawana vitu ndio maana akaamua kusepa na nguo

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom