This is too much now, hivi ni mapepo au ni hali ya kawaida kwenye utafutaji?

Fede15

Member
Joined
Jan 18, 2023
Posts
45
Reaction score
67
Wakuu kwema, naomba nishare mapito yangu ya utafutaji maisha toka 2019 hadi 2024. Maana nashindwa kuelewa kwanini kila kitu nachokifanya hakifanikiwi.

Naamini kupitia huu uzi nitapata abc za kufanikiwa next time.

Baada tu ya kumaliza chuo niliamua nijiajiri kwenye mifugo(ufugaji wa kuku), nikanunua mashine ya kutotolesha mayai(incubator) yenye uwezo wa kutoa vifaranga 120.

Picha linaanza ile tu naweka mayai kwenye mashine TANESCO nao wakatangaza mgao wa siku14, kichwa kikapata moto nikaanza kuhangaika kutafuta sola ili isaidie mayai yasiharibike, changamoto ikawa hali ya hewa ya sehemu ninapoishi jua ilikuwa inawaka Mara chache Sana.

Mwisho wa siku kwenye mayai 120 nikapata vifaranga kama 25, nikasema so mbaya kwa vile umeme ulisumbua, nikaanza utaratibu wa kuwajengea banda hao vifaranga 25 waliopatikana lakini cha kushangaza siku ya tatu nakuta vifaranga vimeuliwa 20 vimebaki vitano na sikujua nini kiliua kati ya panya na nyoka maana nilikuta vimetobolewa kwenye tumbo.

Sikukata tamaa baada ya muda tena nikasema ngoja nirudie ila awamu hii niliweka mayai 60 kama kawaida TANESCO wakatangaza tena mgao mwisho wa siku nikaishia kupata vifaranga 15 navyo vikaja kuiliwa tena, hapo sasa wazo la kuondoka nyumbani likanijia nikiamini kwamba kufanikiwa sehemu ulipozaliwa ni ngumu.

Kuna ndugu yangu akaniambia tulime kitunguu maji huko Sumbawanga kwamba mambo yakienda vizuri eka 1 tunaeza pata hadi 4 milioni, nikasema mambo si ndo haya sasa, nikatafuta nauli nikaenda ila makubaliano yetu yalikuwa nitoe milioni moja halafu nisaidie kusimamia kwa vile yeye alikuwa mtumishi wa Serikali na mwisho wa siku tungewagana ambacho tungejaliwa.

Tulilima ekari 4 tukatumia zaidi ya milioni 4 lakini mambo yalikuwa magumu, wadudu walisumbua sana mwisho hatukupata hata elfu 40, nilihisi kuchanganyikiwa ila nilijikaza na kumwachia Mungu. Hii ilikuwa 2020 mwishoni nikarudi nyumbani kinyonge ila baada ya kutiwaa moyo sana nyumbani.

2021 huyu ndugu yangu nilielima naye kitunguu tukafeli akaniomba nikamsaidie kusimamia mashamba yake ya mpunga ila mwisho wa msimu angenilipa kutokana na mavuno tutayopata, kweli this time Mungu alijalia nikabahatisha 1 milion.

Naomba niishie hapa naweka portion ya 2 kwenye comments sasahivi ili nisiwachoshe sana.
 
Mkuu sijamalizia vzr stori yako ila nataka kujua kama mashine ya kutotolesha bado unayo na je unaiuza? Pole sana maisha ndivyo yalivyo endelea kukomaa iko siku yako pwaaaaaaa unatoboa.. njoo Lindi ujaribu ufuta.. banda la kukaa nitakupa na shamba.
 
Tuliza kichwa maisha hayana mstari uliyonyooka. Unayopitia yanakujenga ili uweze kufanya maamuzi sahihi kabla ya kuliendea jambo. Ninavhokusoma hapa nadiriki kusema wewe ni mmojawapo wa watu wanaofanya jambo na kufikiria risk ni 0%. Halafu achana na mambo ya mapepo kwenye vitu vinavyohitaji elimu ya kawaida ya binadamu.
 
Kila siku tunasema mafanikio huanzia ulimwengu wa kiroho baadae ndo ulimwengu wetu huu....... Usipoijua hii formula hutoboi

Ulimwengu wa kiroho umegawanyika sehemu mbili tu
A.Mungu
B.Shetani

Sasa ili ufanikiwe kirahisi lazima ujiweke kikamilifu upande wowote kati ya hizo side mbili, elewa neno kikamilifu 🤝

Ukitaka kubaki katikati lazima uwe msindikizaji.... Fanya maamuzi chagua upande mmoja hapo utaona effect yake
 
Pole sana kwa changamoto hizo. Ila nikupe moyo usikate tamaa. Ila jitahidi kustick kwenye kitu ambacho unapenda kufanya ata kama matokeo hayakuwa chanya mwanzoni. Chukua changamoto zifanyie kazi then fanya tena utafanikiwa.
 
Asante sana kwa ushauri mkuu
 
Hapa najua nilifeli Sana mkuu
 
Huwezi kufanikiwa kama rohoni umegandamizwa na mauchawi na giza la mapepo.

Maisha huwa ni mepesi sana kama mwili wako na nafsi yako haijagandamizwa na matakataka "yasiyoonekana".

Ukishaanza kujazwa mauchafu utapata uzito wa ajabu, kila kitu kinakwama au kinaharibika. MASHETANI.

Asikwambie mtu, kufanikiwa ni rahisi sana wala huhitaji nguvu nyingi iwapo vipawa vyako havijaharibiwa. NI RAHISI MNO unateleza tu huhitaji hata digrii.
 
Mtafute sana Bwana kwa Yesu kunalipa asikwambie mtu hizo hasara Bwana angekutaarifu mapema ata kabla haujaingia site
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…