Wakuu kwema,naomba nishare mapito yangu ya utafutaji maisha toka 2019 hadi 2024.Maana nashindwa kuelewa kwanini kila kitu nachokifanya hakifanikiwi.
Naamini kupitia huu uzi nitapata abc za kufanikiwa next time.
Baada tu ya kumaliza chuo niliamua nijiajiri kwenye mifugo(ufugaji wa kuku),nikanunua mashine ya kutotolesha mayai(incubator) yenye uwezo wa kutoa vifaranga 120.
Picha linaanza ile tu naweka mayai kwenye mashine TANESCO nao wakatangaza mgao wa siku14,kichwa kikapata moto nikaanza kuhangaika kutafuta sola ili Isaidie mayai yasiharibike,changamoto ikawa hali ya hewa ya sehemu ninapoishi jua ilikuwa inawaka Mara chache Sana.
Mwisho wa siku kwenye mayai 120 nikapata vifaranga kama25,nikasema so mbaya kwa vile umeme ulisumbua,nikaanza utaratibu wa kuwajengea banda hao vifaranga 25 waliopatikana lakini cha kushangaza siku ya tatu nakuta vifaranga vimeuliwa 20 vimebaki vitano na sikujua nini kiliua kati ya panya na nyoka maana nilivukta vimetobolewa kwenye tumbo.
Sikukata tamaa baada ya muda tena nikasema ngoja nirudie ila awamu hii niliweka mayai60 kama kawaida TANESCO wakatangaza tena mgao mwisho wa siku nikaishia kupata vifaranga15 navyo vikaja kuiliwa tena,hapo sasa wazo la kuondoka nyumbani likanijia nikiamini kwamba kufanikiwa sehemu ulipozaliwa ni ngumu.
Kuna ndugu yangu akaniambia tulime kitunguu maji huko sumbawanga kwamba mambo yakienda vizuri eka1 tunaeza pata hadi 4m,nikasema mambo si ndo haya sasa nikatafuta nauli nikaenda ila makubaliano yetu yalikuwa nitoe milioni moja halaf nisaidie kusimamia kwa vile yeye alikuwa mtumishi wa serikali na mwisho wa siku tungewagana ambacho tungejaliwa, tulilima eka4 tukatumia zaidi ya milioni 4 lakini mambo yalikuwa magumu wadudu walisumbua Sana mwisho hatukupata ata elfu40,nilihisi kuchanganyikiwa ila nilijikaza na kumwachia Mungu.Hii ilikuwa 2020 mwishoni nikarudi nyumbani kinyonge ila baada ya kutiwaa moyo sana nyumbani,2021 huyu ndugu yangu nilielima naye kitunguu tukafeli akaniomba nikamsaidie kusimamia mashamba yake ya mpunga ila mwisho wa msimu angenilipa kutokana na mavuno tutayopata,kweli this time Mungu alijalia nikabahatisha 1m.
Naomba niishie hapa naweka portion ya2 kwenye comments saivi ili nisiwachoshe sana