This man is either a sadist or alimuua kibaka, akanywa bia kusherehekea?

Kwakweli ingawa umeweka angalizo tusihoji mahali alipookotwa, inatuwia vigumu.
Zamani watu walipewa uongozi baada ya kupitia maadili waliyonayo.
RC ni mtu mkubwa, anayekalia kiti hicho ni lazima awe mtu mwenye weledi, anayejua maana ya Katiba na miongozo yake.
Kuwa na mtu wa aina hiyo ni hatari kwa mkoa na nchi
 
Mbona unamuondoa Magufuri kwenye hili yeye si ndio mwanzilishi wa kauli za kibabe? Watendaji wake nao wanatamka kulingana na bosi wao anavyotaka acha uwoga Pascal
 
Sawasawa kabisa! Kinachotisha na kusikitisha ni kitendo cha watu kushangilia, inaleta maana kuwa hawahitaji utawala wa sheria au wanapenda sheria mbovu. Na kama hao ndiyo 'wanaakisi' jamii ya watanzania basi ina maana miaka yote hii tangu uhuru ustaarabu tuliofundishwa, elimu tuliyopewa, na hata taasisi zilizowekwa zimekuwa ni kutwanga maji kwenye kinu.
 
Kwanini umeanza kuweka barrier kwenye mamlaka ya uteuzi kuwa isiguswe! ikiwa hiyo mamlaka haihusiki na ufashist wa RC wake mbona mpaka leo yuko mamlakani
 
Ukisema ni sadist una dilute. Huyu ni babarian kabisa. Yuko uncivilised na ni primitive
 
Ni kweli zile mamlaka za kuwafanyia vetting hazipo tena kabla ya kupewa madaraka/uongozi.
 
K
Katika vitu ambavyo tunatakiwa tumpongeza Jiwe ni kuteuawa baadhi ya wakuu wa Mikoa na wilaya anaofanana nao ki maneno na vitendo, Ali Hapi, Makonda, Mnyeti, Muro, Gambo, Sabaya, Komanya kutaja kwa uchache.
 
Ile kauli inatisha sana kutoka kwa mkuu wa mkoa ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa. Inatisha kuona mtu anasheherekea baada ya kumuua kibaka
 
Mkuu huyu ni mteule wa mkuu wa kaya. Bila shaka ana kibali cha aliyemteua.
 
Hii ni hatari sana,kuna haja ya rais wetu kujitofautisha na wateule kama hawa hapa nategemea atamtafutia kazi nyingine,busara hakuna haelewi kitu kuhusu uongozi sheria au mikataba ya kimataifa,wao wanafikiri hayo mambo yanaishia hapo yanaenda mbali sana,
 
Ngosha ndo anawapenda wateule wa namna iyo, uyo ndo kipenzi chake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…