Thomas: Baba yangu Arcado Ntagazwa, alikuwa akisumbuliwa na tatizo la changamoto ya kupumua na alipata matibabu mbalimbali

Thomas: Baba yangu Arcado Ntagazwa, alikuwa akisumbuliwa na tatizo la changamoto ya kupumua na alipata matibabu mbalimbali

Nadhani Changamoto kubwa niliyoiona hapo kwenye habari na ya kusikitisha ni kule kukosa kitanda hospitali.....

Wizara ya Afya ina hizi taarifa ?, (Yaani hapo hawachomoki) ukizingatia wanazunguka kila mahali wanasema hospitali zipo wazi...

Pia wale wanaowasupport hizi kauli kama wanajua otherwise nao ni wale wale....
 
Covid haina huruma kabisa.

Kwa sasa huenda ndio ugonjwa unaoongoza kuua watanzania wa umri mkubwa.

Kama wewe ni mtanzania mwenye umri zaidi ya miaka 60, na una historia ya ugonjwa wa kisukari, Presha, Moyo au mafuta kuzidi mwilini, Covid inakusaka ulipo!
Kuna kitu unatakiwa kujua ambacho wengi hawajui. Corona inategeme sana namna ilivyokujia. Hata kama huna tatizo la kisukari au high BP, ikikupata, ukaanza kukosa pumzi, inapandisha BP na inakuletea kisukari hata kama hukuwa nacho.

Nimeshuhudia kwa ndugu yetu, kijana mwenye afya njema, umri miaka 35, hakuwa na historia ya high BP wala kisukari, lakini dakika za mwisho vyote vilimjia, akapoteza uhai.

Tunaongea mengi lakini huu ugonjwa ukikujia vibaya, hakuna cha ujana wala afya njema, unakwenda. Wengine wanasema inategemea zaidi idadi ya virus particles vilivyoingia mwilini mwako. Ikiwa ni chini ya 1000 huugui kabisa.
 
Covid haina huruma kabisa.

Kwa sasa huenda ndio ugonjwa unaoongoza kuua watanzania wa umri mkubwa.

Kama wewe ni mtanzania mwenye umri zaidi ya miaka 60, na una historia ya ugonjwa wa kisukari, Presha, Moyo au mafuta kuzidi mwilini, Covid inakusaka ulipo!

Acha kupenda kutisha watu badala ya kuwaelimisha. Nani kakuambia ya kwamba kila mwenye magonjwa hayo uliyoyataja basi yeye lazima uviko-19 imsake aliko. Ina maana sasa akijitenga lazima imfuate alipo. Hiyo si sawa. Toa elimu kwa watu, ukiwajengea hofu unakuwa hujawasaidia, kwa maana hofu pia ni ugonjwa. Inaua pia.
 
Lakin Katibu Mkuu kila siku kwenye taarifa za habari anakwambia hakuna wagonjwa waliojaaa.
Achana naye huyo ana akili za konda wa daladala. Bus hata siku moja halijai. Kinachojaa ni chupa. Regency imejaa. Wanaelekeza Mloganzila na si Aga Khan. Huko nako wangeambiwa hivyo. Changamoto ya upumuaji haitoi bonus kwa aliyeelekeza mgonjwa. Wenye hospitali ulikoelekeza mgonjwa mwenye hiyo changamoto watakununia vibaya sana. Huyo ni wa Vingunguti tu.

i
 
Hawajawa wazi. Hakuna ugonjwa unaoitwa changamoto ya kupumua. Magonjwa yote kwenye hatua zake za mwisho upumuaji huwa wa shida na hatimaye husimama kabisa - ukisimama ndipo tunasema mgonjwa kaaga dunia.

Hivyo hawajawa wazi. Hawajasema aliugua corona kwa mjibu wa vipimo.
Zamani nilidhani kuwa una akili kidogo kichwani, hasa kutokana na elimu unayodai unayo.

Michango ya aina hii haikutofautishi na hawa akina YEHODAYA na wapuuzi wengi wa aina hiyo.
 
Acha kupenda kutisha watu badala ya kuwaelimisha. Nani kakuambia ya kwamba kila mwenye magonjwa hayo uliyoyataja basi yeye lazima uviko-19 imsake aliko. Ina maana sasa akijitenga lazima imfuate alipo. Hiyo si sawa. Toa elimu kwa watu, ukiwajengea hofu unakuwa hujawasaidia, kwa maana hofu pia ni ugonjwa. Inaua pia.
Tanzania hakuna covid msiwe waoga kiivyio. Mh rais ametuhakikishia mara nyingi na Katibu Mkuu afya amekazia sana kuwa hali ni shwari
 
Covid haina huruma kabisa.

Kwa sasa huenda ndio ugonjwa unaoongoza kuua watanzania wa umri mkubwa.

Kama wewe ni mtanzania mwenye umri zaidi ya miaka 60, na una historia ya ugonjwa wa kisukari, Presha, Moyo au mafuta kuzidi mwilini, Covid inakusaka ulipo!
Hata vijana kama unamagojwa hayo jitenge kwa SASA
 
Back
Top Bottom