Thomas Sowell: Jinsi Ujamaa wa Nyerere ulivyoiharibu Tanzania

Ifio
 
Nafikiri ujinga wa kwanza ni wewe mwenyewe kutokujua nilichoandika,tena sio ujinga inawezekana ukawa mpumbavu, nimesema Mao ndie kajenga misingi ya China,huyo mwingine kafungua nchi kipindi watu wana mindset ya nchi kwanza kutoka kwa Mao,kama nimeandika ujinga kwanini Mao bado anaendelea kuheshimika nchini China?
 
wewe umezidisha sifa tena. Sisi wengine tumekulia katika kipindi chake na kuyaona mengi sana ambayo nyinyi generations za sasa munadhania ni uongo.
 
👇
 

Attachments

  • Screenshot_20241012-181144 (1).jpg
    52.3 KB · Views: 1
Kuendelea kumlaumu Nyerere kwa katiba mbovu ni kuonyesha jinsi gani sisi tuliopo sasa tusivyo na uwezo wowote.

Kama tunajua ni mbovu kwa nini hatutengenezi nyingine iliyo bora zaidi?

Hapo Nyerere hastahili lawama yoyote ile.
Utabadilishaje katiba kwa aina hii ya bunge tulilo nalo lililojaa wabunge wa Ccm wanaopatikana kwa favour ya katiba iliyopo?.
Sio rahisi kukata mkono unaokulisha
 
Kitabu Cha 'Kaptula la Marx" Cha Prof Kenzirahabi
 
NENO!

Mwalimu Nyerere alijitahidi kuyafanya yake, na sisi tuyafanye Yetu...

Ikiwa kweli tunajifahamu, sisi tunasimama juu ya mabega yake kiutaasisi.

HAPANA, Nyerere alikuwa mtu mwenye akili, fasaha ya kimafikara na ukomavu wa mawaidha na dhamiri kupita vituko vya hoja na viroja -- hoja na viroja vya mengi yanayozungumzwa humu mpaka hapa...

Kiufundi, ukweli wa mambo haupo kwenye 'Hoja ama Malumbano ya Hoja'--Upo kwenye 'Uono na Ufikirifu Mifumo'...

Kwenye Uono na Ufikirifu MIfumo, kila Shauri linamuktadha wake wa kufaa 'vina vya tafsiri' kwa wakati...

Shughuli ya Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano, Mwalimu Kambarage Nyerere, ilikuwa na mabidishi/imperatives yenye kuzingatia Mazingira Tofauti ya (1) Ndani na hata (2) Nje ya 'Jamii Mabadilikoni : Taifa Changa la Watanzania/Waafrika'...

Hata Thomas Sowell, kama ilivyo kwa wasomi/msomi yeyote ambaye hajajiongeza kwa uono na ufikirifu mfumo, mashauri yake ya kihoja ni namna ile ya 'utambuzi wenye kuona mambo kwa sehemu'... Daima mashauri hayo yanaweza kubabaisha zile kambi za watu tofauti tofauti--kambi za udadavuaji wa mambo kwa hata ile misingi ya 'kukusanya data ama/na kujizima data' kidhamira ya utafiti na uchambuzi; na tena mahitimisho yake mahsusi ya visomo empirikali...

Ni kituko, mbele ya jicho la wenye ku-JUA ilivyobora, kuchanganya mashauri pasipo muktadha maridhawa wa ujuaji wa mambo... Ni ontolojia ya Ujinga/Unaivu! Mambo ya kuendekeza porojo na kuhorojoka...

Jamii na Ujamaa wake; ni fanusi tata ya sura-jamii, hadhi na utukufu wake... Ujamaa ni jambo la 'kufikirika' ama kusemwa 'uadilifu ulioni nadra/adimu' kupata kutimilika...

Ujamaa unahitaji jamii iwe na kiasi cha juu cha u-homojinesi ya kuyaishi mashauri ya Uhuru, Udugu, Haki na Amani...

Mambo ya Uhuru, Udugu, Haki na Amani ni mbegu ya utu-bora ambao wakati mmoja hata mwingine 'hupanda ama kuvuna' matokeo tofauti ya 'Mema/Maovu ya Ustawi wa Jamii'...

Uadilifu wa kiuongozi ni kuchunga idili la jambo/taifa -- maadili na miiko ya Sura, Hadhi na Utukufu wa Utaifa--iwe katika Nchi-taifa changa ama Nchi-Taifa iliyokomaa...

Ikiwa (m)wanajamii hajiongezi ili kulifikia hata lile daraja la kung'amua kuwa 'kuishi na maisha' ni mambo ya kuchagua na kujichagulia; basi wataacha kuwajibika na 'Wito wa Kiraia' na kujibwaga kwenye ulimwengu wa kunyoosheana vidole na kupakaziana lawama kwa mambo yao wenyewe kwenda kombo wakati mmoja hata mwingine.

Umoja na Uhuru--si kibwagizo cha 'Ngonjera Fulani' ya kitaifa... Ni shauri la uadilifu, linalotuwajibisha sisi sote tunaojitambulisha kuwa ni raia wa taifa la Tanzania...

Tusidanganyike nakupotezana kwenye 'Nguvu ya Hoja' ama 'Hoja ya Nguvu' , kwenye mashauri nusu nusu; kwa kuwa humo, kwenye michezo/mikato hiyo, kunaweza kuwa ni mambo ya 'Nyani haoni Kundule'...

Tuutafute mwangaza wa kujua ilivyobora juu ya mambo yote na yote... Hii ni nidhamu ya kuiishi 'Hekima'--hekima ya Utu bora.

Hekima inaleta Umoja...

Hekima inaleta Amani...

Hekima ni Uhuru !

Hmmm
 
tafadhali tupatie mfano wa hizo faida zilizopatikana kwenye umiliki wa ardhi, ambao kwa sasa ni utapeli na dhuluma kwa asilimia kubwa
Watu wachache hawajahodhi ardhi kubwa na kuwaacha raia wengi bila ardhi kama ilivyo Kenya. Kuhodhi ardhi na dhuluma za ardhi zilianza kuja baadaye sana baada ya Nyerere kuachia madaraka.
 
Mzee Mohamed Said tupe mwanga zaidi kuhusu huyu "mzee wako" Abdullah Babu aliyeshiriki kutuingiza kwenye zimwi la Ujamaa.
 
Mfumo wa Nyerere japo uliitwa ujamaa ila kiutendaji ulikaa zaidi kama Ukomunisti kwa kuangalia sera za vijiji vya ujamaa (villagization), serikali kuendesha biashara hadi za maduka ya mtaani yaliyoitwa ya ushirika na mfumo wa chama kimoja. Ujamaa wa nchi za Ulaya kama Denmark, Norway na Sweden ni ''Welfare states" ambapo sehemu kubwa ya uchumi bado ni soko huria lakini serikali inahakikisha raia wote wanapata huduma bora za afya na elimu bila kujali kipato chao, pia demokrasia imeshamiri.
 
Umedanganya waziwazi uko shuleni sijui mnasomaga nini
Karl marx ndo muanzilishi wa huu ujamaa yeye ndo aliyepropose comunism manifesto acha uongo

Ussr chini ya vladimir lenini na stalin mwaka 1917 ndo watu wakwaza kuweka idea ya ujamaa kwenye matendo
 
Hata Nyerere bado ana endelea kuheshimika Tanzania hapa hatuzungumzii habari za kuheshimika ulichoandika sasa na muda uliopita ni muendelezo wa ujinga
 
Social democracy.
 
Mao mwenyewe alikuwa kashaingia chaka , mamilioni waliokufa kutokana na sera zake tushukuru hatukupitia hayo
Nyerere dini ilimuingia iliyotengeneza hofu ndogo.

Huyu alivutiwa na ukomunisti wa huko Uchina alipoenda lakini kuiacha dini ilikuwa ngumu kwake alikuwa mkomunisti uchwara
 
Tanzania ilikuwa na ukomunisti uchwara wa China na North Korea na iliongozwa na mkomunisti uchwara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…