Thomas Sowell: Jinsi Ujamaa wa Nyerere ulivyoiharibu Tanzania

Sio Kweli kuwa matokeo hayo hayakuathiri uchumi wa Tanzania? Pamoja na matukio hayo viongozi wengi wa wakati huo hawakuwa pamoja na Nyerere kama waumini wa siasa ya ujamaa hivyo implementation yake ilikuwa half hearted ; kwa lugha ya leo Tungesema wengi wao walikuwa CHAWA. Wamekuja kujulikana unafiki wao baada ya Nyerere kustaafu.
 
China sio wakomunisti pure na sio wabepari sifa za ubepari zinawakataa kabisa
Hoja yako ina msingi mzuri: China si wakomunisti wa asili kama ilivyokuwa chini ya Mao, lakini pia si wabepari kamili kama nchi za Magharibi. Hata hivyo, kusema kwamba "sifa za ubepari zinawakataa kabisa" kunaweza kuwa tafsiri yenye utata, hasa tukizingatia jinsi uchumi wa China unavyofanya kazi leo.

Je, China bado ni nchi ya kikomunisti?
Ndiyo, kwa maana ya kuwa Chama cha Kikomunisti bado kinashikilia mamlaka yote ya kisiasa, na mfumo wa siasa ni wa chama kimoja bila ushindani wa vyama vingi. Serikali inahakikisha kuwa sekta nyeti kama benki, nishati, na miundombinu zinabaki chini ya udhibiti wake. Kwa mtazamo huo, China bado inafuata misingi ya ujamaa wa kisiasa.

Lakini je, mfumo wa uchumi unafuata ukomunisti?
Hapana kabisa. Tangu mageuzi ya kiuchumi ya miaka ya 1980, China imefungua milango kwa soko huria, sekta binafsi, na uwekezaji wa nje. Makampuni makubwa ya Kichina kama Alibaba, Huawei, na Tencent yanaendeshwa kwa misingi ya kibiashara inayofanana na ile ya nchi za kibepari. Wafanyabiashara binafsi wanakuwa mabilionea, na ushindani wa soko upo kama ilivyo katika nchi za Magharibi.

Kwa hiyo, ni nini hasa?
China imetengeneza mfumo wa kipekee – sio ujamaa wa kimarxist safi, lakini pia si ubepari wa kawaida. Inaweza kuelezwa kama uchumi wa soko unaodhibitiwa na serikali ya kikomunisti. Mfumo huu umewapa nafasi ya kukuza uchumi kwa haraka huku wakidhibiti siasa kwa mkono wa chuma.

Kwa hivyo, kusema kwamba "sifa za ubepari zinawakataa kabisa" si sahihi. Badala yake, ni sahihi kusema kwamba China imechukua vipengele vya ubepari lakini kwa namna ambayo vinadhibitiwa na dola, badala ya soko kuwa huru kabisa kama ilivyo katika mataifa ya Magharibi. Swali kubwa ni je, mfumo huu utaendelea kudumu, au kuna mabadiliko makubwa yanayokuja siku za usoni?
 
Siku hizi mfumo wa China wameupa jina la Party-State Capitalism.
 
wewe umezidisha sifa tena.
Ase. Nimezidisha sifa zipi hizo tena? Ieleweke kuwa najitambua.
Sisi wengine tumekulia katika kipindi chake na kuyaona mengi sana ambayo nyinyi generations za sasa munadhania ni uongo.
tunadhania ama tunajua?

Ww huwa unasubiri uambiwe jinsi ulivyo na mzungu ndio 'Ujitambue?'

Hata hivyo, ni haki yako kama ilivyokuwa haki yangu kutokudanganyika kirahisi hivo na hizo propaganda za wazungu.

"Emancipate yourself from mental slavery"
 

Ndio maana nashangaa wanaosema Nyerere alikuwa mjamaa kuliko Babu. Babu, CIA na wenzake walimuogopa sana na walihakikisha anakaa mbali na kuitawala Zanzibar, sababu ya misimamo ya itikadi zake
 
Malengo ilikuwa ni kuwafukarisha watu weusi ili wao watawale Kwa uhuru
 
Nyerere dini ilimuingia iliyotengeneza hofu ndogo.

Huyu alivutiwa na ukomunisti wa huko Uchina alipoenda lakini kuiacha dini ilikuwa ngumu kwake alikuwa mkomunisti uchwara

Inawezekana. Unajua waraka wa kwanza wa TEC aliandikiwa Nyerere baada ya kutaifisha mali za kanisa na ardhi na mali ya baadhi ya wafanyabiashara
 
Tanzania ni kubwa karibia mara mbili ya Kenya, ina rasilimali nyingi zaidi ya Kenya na ardhi kubwa ya kilimo kuliko Kenya.
Lakini Kenya Kuna masikini na mafukara wengi kuliko Tanzania
 
Tanzania ndio ina masikini wengi kuliko Kenya
Sio kweli mkuu Kuna makala iyohusu poverty index tena ya world bank ilieleleza Hilo.

Cha pili gap ya wenye nacho na wasionacho kenya ni kubwa sana tofauti na Tanzania
 
Kwanza sahihisha jina lake: Abdurrahman Babu, na sidhani kama alikuwa na influence kubwa kwa Nyerere kama ulivyoshadidia wewe. Zilikuwa ni fikra za Nyerere mwenyewe na ujamaa wake wa kiafrika.

Vyama vya ushirika vilivunjwa na Nyerere kwa kudhania kuwa vilikuwa vinaleta unyonyaji lakini baadae alikuja kujutia kosa la kuviua vyama vya ushirika.

Nadhani wewe umesikia stories tu kutoka kwa babu zako halafu ukaunga unga na kuja kuandika hapa kama facts - hilo shamba darasa lilitokea wapi kwenye miaka ya sitini wakati hizo fikra ni za kwenye miaka ya elfu mbili na kuendelea?
 
Ieleweke.Kwa wale wasiojua, Muasisi wa Ujamaa alikuwa Otto Van Bismark wa Ujerumani. Na baadae kuigwa na Nchi zingine.
van Bismark ndiyo muanzilishi wa ujamaa? Halafu unabishia ati unajua, kha!
 
Born 1954,darasa la kwannza 1962,
 
Punguwani wewe...
 
Nimeusoma ujamaa in deep huko uzunguni nikaelewa vizuri na kubaki nikicheka kuwa how comes that a genius person like Nyerere adopted this utopian ideology? Yaani iliwezekanaje asishike capitalism ambayo msingi wake ni uwekezaji na mapinduzi ya viwanda , yani mwenye nguvu na mtaji apambane serikali imboreshee tu miundombinu kama maji, umeme, barabara, elimu na afya. Kisha anachopata alipe kodi imjengee tena miundombinu bora zaidi. Kwa vile mtu anapigania maendeleo yake binafsi kupitia uwekezaji wake kamwe hawezi kukubali kuanguka na hawezi kujiibia mwenyewe tofauti na ujamaa ambapo kuiba mali ya umma au shamba la ushirika ni sawa kutoka na human nature of selfishness!! How come Mwl Nyerere did not understand clear weakness of Karl Marx's theory of capitalism and proletariat revolution which is a clear utopian? Mi mjukuu wake mbona nimeelewa?

Kifupi ujamaa ni ideology ambayo haitekelezeki, ni mawazo ya kufikirika tu, yaani serikali ndio eti imiliki njia kuu za uchumi na tukaona mashirika yote ya umma yakafa kwa ubadhirifu, maana mali haina mwenyewe eti kwanza nchi iwe na matajiri au iache matajiri wajitengeneze kwa bidii zao kisha eti kwa kisingizio kuwa wamepata mali kutokana na unyonyaji basi kupitia mapinduzi ya wanaonyonywa ambao asilimia kubwa elimu hawana eti hao matajiri wanyang'anywe viwanda vyao, bizness zao na pesa zao eti zigawiwe kwa majitu mavivu yasiyo na elimu yaliyojaa nchini!

Mara eti Babu akaamua watu waungane akiita vijiji vya ujamaa na mashamba ya ushirika eti watu wazalishe kwa pamoja how stupid was that? Watu wakaliwa na simba maporini na kuwa mafukara kwa kupelekwa maendeo yasiyo na rutuba wala maji, kilimo kikagoma, hivi hiyo mambo ya ushirika inawezekanaje na sote tunajua binadamu ni tofauti katika kila kitu? Mwanaume na mwanamke hawako sawa, mtu wa bush na wa mjini hawako sawa, kuna wajinga kibao kila mahali, kuna wavivu lukuki, maprofessa na darasa la saba hawa wote hawako sawa. A human being is very selfish being hiyo pia Nyerere hakujua? kwenye kulima shamba la ujamaa lazima wengine wategee, na wengine waumwe halafu eti tuje kugawana sawa sawa? How stupid was that idea from a genius Nyerere?

Another pillar ya ujamaa ni serikali kuendesha miradi ya umma na bizness na kwa kukosekana mwenye mali yaani kuita mali ya umma ni shamba la bibi tunaona hakuna uwajibikaji mfano halisi ni mradi wa mwendokasi unavyokufa mabasi yanakufa kwa kujaa maji ya mvua jangwani and no body cares!!

Nyerere was genius but kwenye elimu ya ujamaa binafsi naamini hakuelewa chochote what we call the basic tenets of socialism and how they manifest in the real life hivyo kuitumbukiza nchi kwenye umaskini hadi alipokuja Magufuli na sasa Mama Samia , hawa ni jibu la Nyerere failures kupitia kujenga mazingira bora ya uwekezaji na miundombinu kama reli, barabara, energy etc na kisha kukusanya kodi kutoka kwa wawekezaji kama Azam etc.

I wish ningepata chance kufundisha socialism and capitalism kwa kiswahili huko vyuoni gen z wanakaririshwa tu hawaelewi chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…