PostGE2025 THRDC: Maridhiano yafanyike katika njia za ukweli, haki na uwajibikaji

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Bawabu wa pili

Senior Member
Joined
Nov 14, 2025
Posts
147
Reaction score
433
Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa, ametoa wito kwa taifa kuanzisha mapema mchakato wa maridhiano na uponyaji baada ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu yaliyotokea kuanzia Oktoba 29 na siku zilizofuatia.

Kwa mujibu wa Wakili Onesmo, matukio hayo yaliyosababisha vifo vya raia, majeruhi, utekaji, kukamatwa kiholela na baadhi ya watu kutoweka, yameacha taifa likiwa katika hali ya mgawanyiko, hofu na maumivu makubwa ambayo hayawezi kutatuliwa kwa mazungumzo ya kawaida.

Amesema kuwa Asasi za Kiraia zilishauri umuhimu wa kuanza mchakato wa maridhiano mapema kabla ya uchaguzi, lakini kadiri muda ulivyopita bila kuchukua hatua, matukio ya ukiukwaji yalizidi kuongezeka na kufanya suala la maridhiano kuwa gumu zaidi.

“Lakini leo tunazungumzia maridhiano tukiwa tayari tuna majeraha makubwa. Ni lazima kuanza sasa ili kuzuia madhara zaidi,” amesema.

Ametaja misingi muhimu ya maridhiano kuwa ni pamoja na kukiri tatizo, kuondoa hofu kwa wananchi, kujenga upya imani kati ya viongozi na wananchi, kutoa nafasi kwa wahanga kuelezea yaliyowapata, pamoja na kuweka mazingira ya msamaha na fidia.

Ameonya kuwa bila kuzingatia misingi hiyo, jitihada za maridhiano zitakuwa ngumu kuleta matokeo chanya kutokana na ukubwa wa maumivu na hasara iliyosababishwa na matukio hayo. Aidha, Wakili Onesmo amesisitiza kuwa Tanzania bado ina nafasi ya kujenga upya misingi ya haki, utu na amani endapo mchakato wa maridhiano utaendeshwa kwa uwazi, ukweli, uwajibikaji na dhamira ya dhati.
 
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu
 
Kuna watetezi wa haki za Utekaji watashuka hapa Muda si mrefu.
 
Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa, ametoa wito kwa taifa kuanzisha mapema mchakato wa maridhiano na uponyaji baada ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu yaliyotokea kuanzia Oktoba 29 na siku zilizofuatia.

Kwa mujibu wa Wakili Onesmo, matukio hayo yaliyosababisha vifo vya raia, majeruhi, utekaji, kukamatwa kiholela na baadhi ya watu kutoweka, yameacha taifa likiwa katika hali ya mgawanyiko, hofu na maumivu makubwa ambayo hayawezi kutatuliwa kwa mazungumzo ya kawaida.

View attachment 3511673

Amesema kuwa Asasi za Kiraia zilishauri umuhimu wa kuanza mchakato wa maridhiano mapema kabla ya uchaguzi, lakini kadiri muda ulivyopita bila kuchukua hatua, matukio ya ukiukwaji yalizidi kuongezeka na kufanya suala la maridhiano kuwa gumu zaidi.

“Lakini leo tunazungumzia maridhiano tukiwa tayari tuna majeraha makubwa. Ni lazima kuanza sasa ili kuzuia madhara zaidi,” amesema.

Ametaja misingi muhimu ya maridhiano kuwa ni pamoja na kukiri tatizo, kuondoa hofu kwa wananchi, kujenga upya imani kati ya viongozi na wananchi, kutoa nafasi kwa wahanga kuelezea yaliyowapata, pamoja na kuweka mazingira ya msamaha na fidia.

Ameonya kuwa bila kuzingatia misingi hiyo, jitihada za maridhiano zitakuwa ngumu kuleta matokeo chanya kutokana na ukubwa wa maumivu na hasara iliyosababishwa na matukio hayo. Aidha, Wakili Onesmo amesisitiza kuwa Tanzania bado ina nafasi ya kujenga upya misingi ya haki, utu na amani endapo mchakato wa maridhiano utaendeshwa kwa uwazi, ukweli, uwajibikaji na dhamira ya dhati.
uwajibikaji kwanza......watakubali kuwajibika?
 
Back
Top Bottom