Thread ya Show ya "I am Zuchu": Kutoa Tsh. million 5 kumuona Zuchu kwenye VVIP inaitaji uwe na utajiri wa Bakhresa

Thread ya Show ya "I am Zuchu": Kutoa Tsh. million 5 kumuona Zuchu kwenye VVIP inaitaji uwe na utajiri wa Bakhresa

Huyu zuchu mbona amekua overrated sana? Amekuja kasi kama kikombe cha babu
 
Kuna ule msemo wa "usiseme watu hawana hela semea nafsi yako kuwa huna hela."

Wewe waache wenye hela zao wataenda,wewe kama huna hela na kama unataka kuangalia lipia king'amuzi chako angalia na vile kama hutaki UNAWEZA UKALALA UKA-ASSUME KAMA HAMNA KINACHOENDELEA HAMNA UTAKACHO PUNGUKIWA.

Ila waache wenye hela zao wakazitumie ndio maisha hayo,kuna wengine uwezo wao V8,wengine PRADO,PAJERO,wengine VITZ,IST ,wengine BAJAJ,wengine PIKIPIKI,wengine TZ 11 cha msingi pambana na hali yako.
Hakika. Usiseme TWAFA, sema NAFA. Wewe huna hata buku ya nauli, mwenzako anaunguza 5m kwa usiku mmoja kumuona Zuhura Kopa
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Mungu wangu weeeeeeeeh, nmecheka hadi Tumbo linauma mweeeeeh, ila shishi jamaniiiiih khaaaaah, amenifanya niisave kabisaaa hii clip lol
 
Chuchu hamna kitu. Ni lebel tu ndo inambeba. Now nimeelewa why alikaa miaka minne bila kusaigniwa. Hana kipaji,sauti mbaya,kutawala jukwaa hajui.
Diamond hivi kweli si bora ungemsign Ruby. Ruby ni moto kabarikiwa yule binti. Ni vile hana promo tu .Angekuwa Mwislam im sure angesainiwa pale wasafi.
Baada ya kuona hii comment ikabidi nizame mwenyewe U-Tube kushuhudia hayo uliyoyasema. Nilichokugundua wewe ni mtu mwenye chuki na roho mbaya, ukizeeka hakika utakuwa mchawi

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Shilole ni comedian zaidi ya Steve Nyerere na Mpoki.
 
Bro nimeshangaa sana kuonekana ni mwenye chuki ilhali nimeshasema namsapoti dogo.
Kuna watu bado wapo kwenye ule upuuzi wa uteam sijui nini ambao kwangu hivi sasa ni ushamba tu, mambo kama haya ndiyo yanayosababisha wengine tuwe watazamaji tu wa JF siku hizi.
You missed
Wewe si unajulikana sikuzote ni mtu mwenye roho mbaya. Wewe ni wa kukataa uteam leo hii wakati ndo ulikuwaga unashupalia uteam 'Team Kiba' au sio wewe?[emoji1][emoji1]

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo mleta unataka kusema show nzima haikuwa na kasoro au mapungufu? Yaani mada yako nzima ni kusifia na kupongeza tu, wakati watu wengi wanasema wameona mapungufu kibao.

Japokuwa mimi sio mpenzi wa mziki wa bongo flavour kabisa lakini by default nimejikuta nawajua wasanii wengi wa Bongo flavour. Na kiukweli kabisa Zuchi mpaka sasa simjua kabisa. Hivyo nahisi huyo binti huenda atakuwa overrated au underground fulani.
Sasa huoni mpaka hapo kama wewe ni mpumbavu?
 
Kwa hiyo mleta unataka kusema show nzima haikuwa na kasoro au mapungufu? Yaani mada yako nzima ni kusifia na kupongeza tu, wakati watu wengi wanasema wameona mapungufu kibao.

Japokuwa mimi sio mpenzi wa mziki wa bongo flavour kabisa lakini by default nimejikuta nawajua wasanii wengi wa Bongo flavour. Na kiukweli kabisa Zuchi mpaka sasa simjua kabisa. Hivyo nahisi huyo binti huenda atakuwa overrated au underground fulani.
Kwani wewe nani katika nchi hii? Kama Magufuli anamjua inatosha

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Last Saturday Zuchu alitambulishwa rasmi katika ulimwengu wa Muziki. Huu ni ulimwengu uliojaa vitimbwi na vioja vya kila aina ya ushetani. Huwezi kupata unachokitaka bila kukubali kuishi maisha ya kumtumikia shetani.

Ni lazima ukubali yafuatayo:- Kudhalilisha mwili wako kwa kuvaa nusu uchi, kujirekodi picha za utupu, kutukanana na wenzako mitandaoni, kuishi na mabeef,kufeki maisha ya uongo na kurogana.

Kuimba mziki mzuri pekee havijawahi kumsaidia msanii kudumu kwenye hicho mnachokiita "Game". Ukiingia kwenye fani ya mziki ni kuchagua moja kwa moja kumtumikia shetani. Najua wengi hawapendi kusikia haya lakini huo ndo ukweli. Sawa utamiliki magari,majumba,n.k ila kwa gharama ya kuuza nafsi na utu wako.

Jiulize kwanini V- Money kakimbia huko, huku akikiri wazi Secular music imejaa ushetani! The likes of Ray C, na Mzee Yusufu. Umaarufu wa kimuziki kamwe hautompa mtu furaha zaidi ya msongo wa mawazo na majuto.Shetani ni mjanja sana. Anajua mwanadamu anatamani vitu vya thamani km majumba na pesa. Naye amevitanguliza vitu hivyo machoni kama beit or Trap . Ni kama anakuambia," Take these and serve me". Ila hakuonyesha maumivu yaliyo nyuma ya hivo vitu anavyokupa.

Wengi wanazani wasanii wakubwa wana furaha na kuinjoy maisha si kweli!! Mfano Diamondi mi naona mziki umempa majanga mengi zaidi kuliko kabla ya kuwa mwanamziki.Ni heri angeendelea kuuza mitumba angeishi kwa amani kuliko ilivyo sasa. Mnazani anapenda kuishi na uadui na baba yake? No! That is a Satanic attack which he doesn't know!. Very sad to say that.

Sipo hapa kueleza majanga ya Diamondi ila kwa ufupi thamani ya chozi la furaha ulilolitoa Zuchu wakati ukikabidhiwa gari ya kutembelea, ni mwanzo wa maumivu makubwa ya kiroho na kifikra utakayoyapitia japo kimwili utaonekana umenona. Kama huamini muulize Rachel aliyezaniwa kuwa Ray C mpya bongo atakuambia.Mikel Jackson pamoja na mapesa yake alikufa akiwa hana furaha, Whitney Huston vile vile. Muziki uliharibu kabisa maisha yao.

Muziki ni nyenzo muhimu kwa Shetani kuharibu maisha ya vijana. Kwa watoto wa kike mziki umepelekea wengi kuzalishwa na kushindwa kuolewa. Wengi wameingizwa kwenye utumwa wa ngono na madawa ya kulevya bila kupenda na pindi umaarufu unapoisha ndio hugundua kuwa wamepotea. Wachache sana wanaobahatika kutoka salama.

Ni mbinu hiyo hiyo ndio iliyowasambaratisha Bongo movie na sasa wamechoka hata hawajulikani walipo.Wengi mnawajua si vema kuwataja.

Karibu sana mdogo wangu Zuchu kwenye ulimwengu wa wasanii uliojaa ushetani.
 
Back
Top Bottom