Mkuu hueleweki..., kwahio hizo thread 1000 zikitoka zinakuwa hazina moja, yaani ingekuwepo moja ni sawa ila kuanzia mbili mpaka 1000 zinapunguza makali ya hio moja ? Unaongelea facts kwani hizo zote hazina facts...
Ngoja nikupe facts
Makufuli alikuwa Mtendaji mzuri sana tena sana ila hakuwa kiongozi mzuri..., kazi yake nzuri aliifanya akiwa Waziri, au angepaswa kuwa Waziri Mkuu, Kiongozi anahitaji kusikiliza, anahitaji diplomasia na akubali kukosolewa bila hivyo watu wataogopa kumshauri (The Emperor has no cloths)
Pili Makufuli mara nyingi hakufuata sheria na taratibu mihimili yote mitatu ni kama aliivunja na kuwa yeye Jeshi la mtu mmoja...
Tatu Propaganda zilikuwa nyingi ni vigumu kujua wapi alikuwa anasema ukweli na wapi uongo (hio yote italetwa na transparency)
Nne Nepotism na kuonyesha sifa kwamba ninafanya kitu huku au kule sababu nitazikwa huko ni kuleta precedent mbaya sana ambayo itatucost hapo baadae (mfano anashauri watu wachagua viongozi wa kwao au ukichagua huyu au yule sileti maendeleo) alisahahu yeye ni Kiongozi wa Nchi na sio Chama wala Kabila
Mwisho Kabisa nchi hii haiitaji mtu Imara bali Taasisi Imara..., sababu hata akija malaika tutakuwa tunaongea hayahaya, inabidi tuongozwe na kanuni na sio matakwa au utashi wa mtu....