Tiba/Dawa kwa mtoto au mtu kikojozi

Tiba/Dawa kwa mtoto au mtu kikojozi

pole sana,, usione aibu kwenda kwa doctor maradhi ametuumbia Mungu hujataka uwe hivo. Nenda ukachunguzwe zaidi upatiwe tiba, kama ni mwanaume nenda kwa urologist (wanaodeal na njia za mkojo za kiume) au pengine una upungufu wa hormone ya ADH
 
Asanteni sana kwa ushauri wenu.
duh sina la kusema zaidi ya kukupa pole.
pole sana,, usine aibu kwenda kw doctor maradhi ni ametumbia Mungu hujataka uwe hivo,, nenda ukachunguzwe zaidi upatiwe tiba,, kama ni mwanaume nenda kw urologist(wanaodeal n njia za mkojo za kiume) au pengine una upunguvu wa hormone ya ADH
 
Pole kijana! Kwanza kabla ya kulala usiku usinywe maji mengi au vimiminika kwa kiwango kikubwa, hakikisha unajisaidia kabla ya kulala na jitahidi kuamka usiku ukojoe! Weka alarm ya masaa mawili maana hii itakusaidia pale itakapokuamsha ili ukakojoe! Vile vile kuna njia moja ya kiasili hivi ambayo kama utaiamini inaweza fanya kazi, maana naona hii njia kama ilishawasaidia baadhi ya watu maana ni hivi wewe kojoa kwenye kopo kisha chukua huo mkojo kaumwage barabarani..hapo hiyo kitu inakata!!![emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Kwa msaada wa specialist WA masuala ya urology nipm nikupe namba yake, tena huyu ni kijana mwenzio hivyo hakuna haja ya kuwa mwoga kumweleza tatizo. Pole sana. Mimi pia nina experience na hili jambo but siku niliyokwenda form one shule ya bweni ndio siku nilipokata ghafla hadi leo sijakojoa kitandani
 
Asante mkuu nita fanya hivyo
Pole kijana! Kwanza kabla ya kulala usiku usinywe maji mengi au vimiminika kwa kiwango kikubwa, hakikisha unajisaidia kabla ya kulala na jitahidi kuamka usiku ukojoe! Weka alarm ya masaa mawili maana hii itakusaidia pale itakapokuamsha ili ukakojoe! Vile vile kuna njia moja ya kiasili hivi ambayo kama utaiamini inaweza fanya kazi, maana naona hii njia kama ilishawasaidia baadhi ya watu maana ni hivi wewe kojoa kwenye kopo kisha chukua huo mkojo kaumwage barabarani..hapo hiyo kitu inakata!!![emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
pole sana,, usione aibu kwenda kwa doctor maradhi ametuumbia Mungu hujataka uwe hivo. Nenda ukachunguzwe zaidi upatiwe tiba, kama ni mwanaume nenda kwa urologist (wanaodeal na njia za mkojo za kiume) au pengine una upungufu wa hormone ya ADH
upload_2016-6-7_10-41-47.jpeg
The hypothalamus is a small but important part of the brain. It contains several small nuclei with a variety of functions. It plays an important role in the nervous system as well as in the endocrine system. It is linked to another small and vital gland called the pituitary gland.28 Oct 2012

Kibofu kinapojaa nervous system zinapeleka habari kwenye hypothalumus na inakufanya wewe ugundue haja ya kwenda msalani hata kama upo kwenye usingizi mzito. Mtoto anapozaliwa kunakuwa hakuna full connection katika hizo nervous system na hypothalamus lakini baada ya miezi 24 mtoto anauwezo wa kutambua anahitaji kujisaidia, mtoto wa miaka mitatu kama bado anajikojolea ni vizuri kumuona dr. Jinsi unavyozeeka ni kama viuongo vingine vya mwili uhafamu unapungua, ndiyo maana ni uzeeni unakuwa wajisaidia bila kufahamu. Ajali, maradhi kama dementia yanaharibu mfumo huu wa fahamu. Mganga wa mishipa ya fahamu anaweza kukusaidia zaidi.
 
Tatizo lingine sina.
Mkuu naamini tatizo lako hilo lipo kwenye sehemu za fahamu, yaani kwenye ubongo, hivyo ili kuondokana na tatizo hilo huna budi kujizoesha taratibu kuamka katikati ya usiku, kutokunywa vinjwaji usiku sana, pia epuka kunywa uji, soda, chai, pombe(kama unatumia) nyakati za usiku, kama unalala na ndugu yako mwambie awe anqkuamsha katikati ya usiku kama mara mbili au tatu hivi baada ya muda tatizo lako litaisha jumla.

Chunguza kwanza uone ni muda gani huwa unatokwa na haja ndogo ukiwa umelala na inatokea mara ngapi kwa usiku mmoja, hapo unaweza kumwambia unaye-share naye chumba awe anakushtua nyakati hizo, ukifanya hivyo baada ya miezi kama sita hivi tatizo litakuwa limekoma.
 
Pole sana ndugu! Kama unaishi chumba kmoja na mtu muombe ajitahidi kukwamusha au weka alarm iwe inakwamsha kila baada ya saa. Nimejaribu kwa mwanangu imefanya kazi ndani ya wiki moja.
 
pole sana hata sisi kwetu maid wetu ana tatizo hilo ni msichana mkubwa hata hatujui tufanyaje
 
Asanteni sana ndugu zangu hakika najihisi nimwenye furaha, najihisi kupona kabisa. Hakika hakuna uwamuzi mzuri niliowahi kufanya kwenye maisha yangu kama kuwa elezea wana jf matatizo yangu. Kwani katika michango yenunina amini kuna dawa yaku niponya. Namimi nawa ahidi kufwata kanuni zote mlizo nishauri. Na baada ya miezi miwili Nita leta mrejesho hapa.

Nawashukuru sana walio guswa na tatizo langu na kunipa pole au ushauri, sinchakuwalipa ila naamini mungu atawalipa. Ninajua mmetumia muda wenu kuni tafutia mimitiba nandio maama nasema ASANTENI SANA.
 
Mkuu endelea kupitia Uzi huu dawa za tatizo lako zipo nyingi, ngoja wengine watakuja kukusaidia. Kuna ile ya kunywa maji ya mchele, kula asali nk.
 
Sawa mkuu nitaufwatilia paka mwisho hakika hu Uzi utaniponya Mimi na wengine wanao simbuliwa na tatizo hili. Sita puuza mawazo ya mtu yeyote.
Mkuu endelea kupitia Uzi huu dawa za tatizo lako zipo nyingi, ngoja wengine watakuja kukusaidia. Kuna ile ya kunywa maji ya mchele, kula asali nk.
 
Antidiuretic hormone, also called arginine vasopressin (AVP), is a hormoneproduced by the hypothalamus in the brain and stored in the posterior pituitary gland at the base of the brain. ADH helps regulate water balance in the body.

Nilisahau mkuu
MACHALE, ikiwezekana upime damu waangalie kiwango cha ADH hormone kwenye mwili wako, wanaweza kukupa dawa za kuregulate kama mwili unazalisha nyingi zaidi. Kahawa pia ni antidiuretic, angalia unyaji wako wa kahawa.
 
Back
Top Bottom