Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Hii ni miongoni mwa Kauli alizotoa Mwenyekiti wa Kamati ya kuchunguza Dhiki au Matatizo ya uchumi yanavyovikabili vyombo vya habari nchini Tanzania , Tido Muhando.
Mhando ameyasema hayo alipotoa hotuba yake kwenye kongamano la Maendeleo ya sekta ya habari linaloendelea Dar es Salaam
Ni nini hasa maana ya Comedy Journalism?
--
Kutokana na mazingira magumu ya sheria na siasa ambavyo vyombo vya habari nchini vimepitia, vyombo hivi, hivi sasa vimejikuta vikijidhibiti kutoa habari ambazo zinasimamia uwajibikaji wa umma (Public Accountability Strories). Matokeo yake ni kwamba vyomo vya habari kubeba maudhui mengi zaidi ya burudani, mapenzi, mziki, michezo, tamthilia, filamu, na vipindi vya mjadala vyenye tija ndogo kwa jamii.
Aina hii ya uandishi inaleta madhara mawili makubwa;
=====
Kusoma kilichojiri siku ya kwanza ya Kongamano pita hapa:
- Rais Samia akishiriki Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari, Juni 18, 2024
=====
Mwenyekiti wa Kamati ya kufuatilia hali ya uchumi wa vyombo vya Habari, Tido Mhando amesema kutokana na mazingira magumu ya kisheria na kisiasa ambayo vyombo vya habari vimepitia katika Serikali ya awamu ya Tano iliyokuwa chini ya Rais John Magufuli, vyombo vingi vya habari vimejidhibiti kutoa habari za uwajibikaji kwa umma na kuhamia maudhui mepesi ya mzaha ‘comedy journalism.’
Pia amesema vyombo hivyo sasa vimebeba maudhui ya burudani, mapenzi, muziki, michezo, tamthilia na vipindi vyenye tija ndogo kwa jamii.
Mhando ameeleza hayo leo Jumanne wakati akiwasilisha mapendekezo ya kamati yake kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni mgeni rasmi kwenye kongamano la maendeleo ya sekta ya habari.
Mhando amesema aina hiyo ya uandishi inaleta madhara mawili makubwa, kwanza kudhoofisha uandishi unaozongatia uwajibikaji wa umma ambao ni muhimu kwenye jamii lakini pia kutengeneza kizazi kisochoweza kufikiria sawasawa kwa kuwa kinadumazwa na maudhui mepesi.
“Bila shaka sasa hivi tunaelewa kinachoendelea kuna kitu kinaitwa Comedy Journalism kumekuwa na mambo mengi ya mzaha mzaha yote haya yanatokana na wasiwasi waliokuwa nao waandishi, wamekuwa wanaogopa kutokana na mazingira magumu yaliyoletwa hapo mwanzo.
“Tunashukuru kwenye awamu yako hii ya sita yameanza kuondoka kidogo kidogo lakini kama ulivyotoa neno kwa viongozi hawa wa kisiasa wamekuwa wakileta ubabe ubabe katika sekta hii ya habari.
“Ubabe umekuwa mwingi tunaomba utasaidie kukabiliana na suala hili. Nina hakika hakuna chombo cha habari ambacho hakijatikiswa na ubabe huu kutoka kwa baadhi ya viongozi mifano ni mingi lakini nisingependa kuitaja hapa kwa sababu ya muda,” amesema.

- "Inadhohofisha uandishi wenye kuzingatia uwajibikaji wa umma ambao ni muhimu sana kwenye jamii na kutengeneza kizazi kufikiria sawasawa kwa kuwa kinayumbishwa na maudhui mepesi sana.
- "Sasa hivi kumekuwa na comedy journalism, mambo mengi ya mzahamzaha yanaonekana kama vitu vya kawaida. Na yot ehii ni kutokana na wasiwasi ambao waaandishi wa habari wamekuwa wanaogopa kutokana na mazingira magumu ambayo yaliletwa hapo mwanzo.