Tido Mhando: Awamu ya Hayati Magufuli imechangia 'Comedy Journalism'
Uhuru na demokrasia isiyo na mipaka ni vurugu. Halafu hiyo ina apply kote kuanzia ngazi ya familia labda kama we huna familia..hata mbinguni malaika walipozidisha uhuru na demokrasia kwa maana lucipher alitaka ajiweke position ya Mungu, Mungu aliwakata.

Hata Mbowe akiona demokrasia imezidi kwenye chama chake huwa anafanya maamuzi magumu..wapi Chacha Wangwe, muulize Zitto na sasa Tundu Lissu.
Haya wamepewa uhuru na Magu hayupo, kiko wapi??
Kwa kiwango cha uwezo wako wa kufikiri,mipaka ya demokrasia huanzia wapi na kuishia wapi hasa?
 
Vumilia ukweli, dhalimu magu alishiriki sana kuua Uhuru wa vyombo vya habari katika ile kampeni yake ya kujifanya anakubalika.
Kwani sasa hivi vyombo vya habari havimsifu Samia!!!
 
Watanzania ndio tulivyo, hatujadili issue, tunajadili mtu. Ukipitia thread nzima, Sijaona mtu ambaye amempinga kwa fact Ila kwa hisia.

Na ni ukweli usiopingika kuwa uchawa wa kisiasa na vyombo vya habari kugeuka praise team inayopigia promo mediocrity ili kufidia ukosefu wa content za maana za kisiasa. Vilishamiri kipindi cha awamu iliyopita

Hata kinachoendelea bungeni kimetokana na awamu iliyopita

So, tukubali kuwa Anko alikuwa na mazuri yake mengi sana Ila kwa upande mwingine, alifeli pia. Sio kumsimanga, Ila ni kuongea uhalisia

Marehemu kwenye masuala ya kuheshimu uhuru wa maoni, uhuru wa vyombo vya habari, kulinda haki, kuheshimu utawala wa sheria, kuheshimu haki za watu, kuhesimu demokrasia, ALIPATA 0%.
 
Huyo kastaafu azam anatafuta ukurugenzi ikulu..ni awamu ya Magufuli ndipo lilitoka tamko waandishi lazima wawe na diploma. Lakini awamu ya Magufuli hatukusikia magazeti ya ijumaa, uwazi wala msanii.
Anstafuta ukurugenzi wa nini kama alishakuwa mkurugenzi na kiongozi wa BBC. Unachopinga ni nini? Hao akina Zembwela, Masanja, Mwijaku, Mpoki, Bi Kazumari and Cos wameatokea katika kipindi kipi?

Sasa kuna watangazaji machawa tupu na hata ukisikiloza redio au vyombo vya habari, hakuna waandishi wenye "critical thinking" na hawana cha maana zaidi ya udaku tu wa akina Mange.
 
Comedy journalism unafanya na kina
Kitenge
Mwijaku
Babalevo
Gerald hando
Zembwela
Musa kipanya
Mpoki
Etc
Utakuta ishu ni serious kama ya do world au uhamishaji wamasai ngorongoro wao uwasilishaji wao hauna mtirirko wa kimantiki
 
Viongozi dhaifu, siku zote hutafuta pa kutupia lawama. Unafiki huwa hauendelei mbali sana.
 
Hawa ndo wale wanaitwa cowards wanapaza sauti kwa mtu asiye hai ila kipindi kile waliufyata mkia nyuma km mijibwa koko
 
Nimeimiss comedy journalism yaani mtu anajirekodi na kuanza kutisha watu ama kusifu hata kucheza makilikili
Nilidhani ni mimi tu ninaona 'comedy journalism's kumbe tuko wengi. Majeruhi wa awamu ya tano kumbe wengi.
 
Kutokana na mazingira magumu ya sheria na siasa ambavyo vyombo vya habari nchini vimepitia, vyombo hivi, hivi sasa vimejikuta vikijidhibiti kutoa habari ambazo zinasimamia uwajibikaji wa umma (Public Accountability Strories). Matokeo yake ni kwamba vyomo vya habari kubeba maudhui mengi zaidi ya burudani, mapenzi, mziki, michezo, tamthilia, filamu, na vipindi vya mjadala vyenye tija ndogo kwa jamii.

Aina hii ya uandishi inaleta madhara mawili makubwa;

  • "Inadhohofisha uandishi wenye kuzingatia uwajibikaji wa umma ambao ni muhimu sana kwenye jamii na kutengeneza kizazi kufikiria sawasawa kwa kuwa kinayumbishwa na maudhui mepesi sana.
  • "Sasa hivi kumekuwa na comedy journalism, mambo mengi ya mzahamzaha yanaonekana kama vitu vya kawaida. Na yot ehii ni kutokana na wasiwasi ambao waaandishi wa habari wamekuwa wanaogopa kutokana na mazingira magumu ambayo yaliletwa hapo mwanzo.
Sasa tunashukuru kwenye serikali yako mambo haya yameanza kuondoka kidogo kidogo. Lakini kama ulivyokuwa umetoa neno la viongozi hasa wa ngazi za juu za kiasiasa hasa ambao wamekuwa wakiingiza ubabe ubabe katika sekta hii ya uandishi wa habari. Ubababe huo umekuwa mwingi, na tunaomba vile vile ungeweza kutusaidia kukabiliana na suala hili. - Amesema Tido

"
Kila sekta iliharibika,utetezi wao ni Sgr,bwawa na ndege tuu hakuna Kingine Cha maana.
 
Nauliza tu ndugu Waandishi wa habari, Comedy Journalism ndio nini?

Mungu wa Mbinguni awabariki!
 
Yule jamaa alikuwa na big ball's, hakuna mwingine katika yenu blah blah mwenye uwezo wa kufikia hata robo ya uthubutu na ushababi wa yule jamaa.

Mtamsimanga lakini sisi tunajua mpaka sasa yeye ndiye mshindi kwenye kile tulichokuwa tunakihitaji kutoka kwa head of state.

JPM alikuwa ndio nembo ya Ikulu na kiongozi mkubwa mwenye maamuzi.
Alikua sadist,uthubutu alikua nao ila neno lake lilikua sheria,zama zake zimepita, tufocus mbele
 
Kila sekta iliharibika,utetezi wao ni Sgr,bwawa na ndege tuu hakuna Kingine Cha maana.
Alikua anaiharibu nchi kimsingi kwa kuongeza chuki na matabaka, kwamfano baina ya watumishi wa umma na raia.Mwanzo mwisho alikua attention seeker,kila anapoenda lazima awe live 😂,Mungu atuepushe na janga km lile
 
Hawa ndo wale wanaitwa cowards wanapaza sauti kwa mtu asiye hai ila kipindi kile waliufyata mkia nyuma km mijibwa koko
Yule alikua killer,kamuulize Lissu 😂,alafu sio kila mtu ni jasiri jombaa,hata resistance zilikua za aina tofauti
 
Ulikuwa na umri gani wakati Makonda anatumwa na Magufuli kuvamia vyombo vya habari na makombora?
Makonda alivamia clouds kwa matakwa yake ila si kwa kutumwa na Magufuli Mungu amrehemu.
Labda utaje chombo kingine cha habari kilichovamiwa tofauti na clouds shilawadu.
 
Marehemu kwenye masuala ya kuheshimu uhuru wa maoni, uhuru wa vyombo vya habari, kulinda haki, kuheshimu utawala wa sheria, kuheshimu haki za watu, kuhesimu demokrasia, ALIPATA 0%.
Hakikata mkuu 🙏🏽🙏🏽
 
Back
Top Bottom