Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata yeye tido amejadili watu na issues kwaiyo na yeye ajadiliweWatanzania ndio tulivyo, hatujadili issue, tunajadili mtu. Ukipitia thread nzima, Sijaona mtu ambaye amempinga kwa fact Ila kwa hisia.
Na ni ukweli usiopingika kuwa uchawa wa kisiasa na vyombo vya habari kugeuka praise team inayopigia promo mediocrity ili kufidia ukosefu wa content za maana za kisiasa. Vilishamiri kipindi cha awamu iliyopita
Hata kinachoendelea bungeni kimetokana na awamu iliyopita
So, tukubali kuwa Anko alikuwa na mazuri yake mengi sana Ila kwa upande mwingine, alifeli pia. Sio kumsimanga, Ila ni kuongea uhalisia
Ilikua kipindi cha zahama kwa kifupiAu pia "Mheshimiwa Mungu..."
Hongera jasiri 😂Coward mwingine huyu hapa
Kama ni kujikomba watu walijikomba sawasawa, yaani sijui ni mzimu gani uliingia.kifupi
Sasa mnamiliki vyeti feki mlitegemea awachekee tuIlikua kipindi cha zahama kwa kifupi
Hongera jasiri 😂
Sijataka yatokee mengine bali mtueleze mengine tusiyoyajua, haya tushayasikia sana mpaka tumechoka.Bado hayajatokea mengine
Ingekuwa aibu sana kwa Tido Mhando kuwa Waziri wa ccmTidi alipaswa kuwa waziri wa habari sema yule wabao la mkono anamizizi Toka enzi za babayake. Tunashida ya maudhui yeye anatuletea maroboti as if ndo big deal kwenye habari 😞 so sad
Watu wengine hawajui hata tunayozungumzia hapaAlitimuliwa...?? Uongo unawasaidia nini!?
Kabisa... Na hili ndiyo limekuwa tatizo la watanzania.Watu wengine hawajui hata tunayozungumzia hapa
Ndo pakujifichia mkiwa mnamtetea dhalimu 😂Sasa mnamiliki vyeti feki mlitegemea awachekee tu
Na nyie tafuteni pa kujifichia mkiwa mnatetea mapopoma yenuNdo pakujifichia mkiwa mnamtetea dhalimu 😂
Huko ni kujipendekeza tu kwa mama Kizimkazi maana JPM alimnyoosha huyo Tido. Waandishi wa Habari wengi ni vilaza na hicho wanachokiandika ndo uwezo wao ulipofikia, huwezi kuwalinganisha waandishi wa habari wa sasa na akina Jonson Mbwambo, Stan Katabalo na wengineo waliokuwa wanaandika na msomaji unavutika kuzisoma habari zao zilizokuwa zimejaa ueledi wa kiuandishi. Tatizo lingine la Waandishi wa sasa wamekuwa na uandishi wa upande mmoja hawana uwezo wa ku-balance story, kwa ufupi hawajui kitu na ukiwapeleka kwenye habari za uchunguzi ndo kabisaaa debe mshindo.Hii ni miongoni mwa Kauli alizotoa Mwenyekiti wa Kamati ya kuchunguza Dhiki au Matatizo ya uchumi yanavyovikabili vyombo vya habari nchini Tanzania , Tido Muhando.
Mhando ameyasema hayo alipotoa hotuba yake kwenye kongamano la Maendeleo ya sekta ya habari linaloendelea Dar es Salaam
Ni nini hasa maana ya Comedy Journalism?
--
Kutokana na mazingira magumu ya sheria na siasa ambavyo vyombo vya habari nchini vimepitia, vyombo hivi, hivi sasa vimejikuta vikijidhibiti kutoa habari ambazo zinasimamia uwajibikaji wa umma (Public Accountability Strories). Matokeo yake ni kwamba vyomo vya habari kubeba maudhui mengi zaidi ya burudani, mapenzi, mziki, michezo, tamthilia, filamu, na vipindi vya mjadala vyenye tija ndogo kwa jamii.
Aina hii ya uandishi inaleta madhara mawili makubwa;
Sasa tunashukuru kwenye serikali yako mambo haya yameanza kuondoka kidogo kidogo. Lakini kama ulivyokuwa umetoa neno la viongozi hasa wa ngazi za juu za kiasiasa hasa ambao wamekuwa wakiingiza ubabe ubabe katika sekta hii ya uandishi wa habari. Ubababe huo umekuwa mwingi, na tunaomba vile vile ungeweza kutusaidia kukabiliana na suala hili. - Amesema Tido
- "Inadhohofisha uandishi wenye kuzingatia uwajibikaji wa umma ambao ni muhimu sana kwenye jamii na kutengeneza kizazi kufikiria sawasawa kwa kuwa kinayumbishwa na maudhui mepesi sana.
- "Sasa hivi kumekuwa na comedy journalism, mambo mengi ya mzahamzaha yanaonekana kama vitu vya kawaida. Na yot ehii ni kutokana na wasiwasi ambao waaandishi wa habari wamekuwa wanaogopa kutokana na mazingira magumu ambayo yaliletwa hapo mwanzo.
=====
Kusoma kilichojiri siku ya kwanza ya Kongamano pita hapa:
- Rais Samia akishiriki Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari, Juni 18, 2024
=====
Mwenyekiti wa Kamati ya kufuatilia hali ya uchumi wa vyombo vya Habari, Tido Mhando amesema kutokana na mazingira magumu ya kisheria na kisiasa ambayo vyombo vya habari vimepitia katika Serikali ya awamu ya Tano iliyokuwa chini ya Rais John Magufuli, vyombo vingi vya habari vimejidhibiti kutoa habari za uwajibikaji kwa umma na kuhamia maudhui mepesi ya mzaha ‘comedy journalism.’
Pia amesema vyombo hivyo sasa vimebeba maudhui ya burudani, mapenzi, muziki, michezo, tamthilia na vipindi vyenye tija ndogo kwa jamii.
Mhando ameeleza hayo leo Jumanne wakati akiwasilisha mapendekezo ya kamati yake kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni mgeni rasmi kwenye kongamano la maendeleo ya sekta ya habari.
Mhando amesema aina hiyo ya uandishi inaleta madhara mawili makubwa, kwanza kudhoofisha uandishi unaozongatia uwajibikaji wa umma ambao ni muhimu kwenye jamii lakini pia kutengeneza kizazi kisochoweza kufikiria sawasawa kwa kuwa kinadumazwa na maudhui mepesi.
“Bila shaka sasa hivi tunaelewa kinachoendelea kuna kitu kinaitwa Comedy Journalism kumekuwa na mambo mengi ya mzaha mzaha yote haya yanatokana na wasiwasi waliokuwa nao waandishi, wamekuwa wanaogopa kutokana na mazingira magumu yaliyoletwa hapo mwanzo.
“Tunashukuru kwenye awamu yako hii ya sita yameanza kuondoka kidogo kidogo lakini kama ulivyotoa neno kwa viongozi hawa wa kisiasa wamekuwa wakileta ubabe ubabe katika sekta hii ya habari.
“Ubabe umekuwa mwingi tunaomba utasaidie kukabiliana na suala hili. Nina hakika hakuna chombo cha habari ambacho hakijatikiswa na ubabe huu kutoka kwa baadhi ya viongozi mifano ni mingi lakini nisingependa kuitaja hapa kwa sababu ya muda,” amesema.