kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Kampuni ya Mawasiliano ambayo mtu mmoja anaweza kuwa Mwanasheria, akawa afisa tehama, akawa na uwezo wakusoma taarifa za wateja, akaziprint, akazipeleka anapoona panafaa kwa kugonga mhuri wa kampuni, akazisafirisha, akaenda kuzitetea mahakamani. Hii Ni taasisi inayomiliki data za wananchi na wasio wananchi?
Hii kampuni imeruhusu data za watu wanagapi zitumike kinyume Cha sheria? Watu wangapi taarifa za wapenzi wao zimevujishwa na matokeo yake wameumizwa au kuuwawa? Wafanyabiashara wangapi taarifa zao zimeuzwa kwa washindani wao? Viongozi wangapi wamedukuliwa? Raia wa kigeni wangapi taarifa zao za Mawasiliano zimevujishwa?
Kampuni hii wamiliki wake Ni wakina Nani na inajiamini Nini? Kesi ya Nondo Iringa mtu huyuhuyu alikwenda Iringa akatoa ushahidi wa uongo kwa mwamvuli wa Tigo, leo kwa kiburi kabisa anaeleza umma kwamba usiri wa taarifa siyo kipaombele cha kampuni, hiki kiburi anatoa wapi? Hata Kama ni afisa wa Serikali kwanini aruhusiwe atumike adharani kiasi hiki? Huu ni ujima? Serikali imekosa watu hadi inatumia hopeless people kama huyu?
Tigo lazima washtakiwe kuvujisha siri za wateja na kukosa mfumo sahihi wa utoaji taarifa. Wasipofilisiwa ipo siku data za mkuu wa nchi au wasaidizi wake zitapelekwa kwa maasiamu wa nchi jirani au ipo siku mataifa asimu watapandikiza watu wakuhamisha taarifa za wateja