Tigo rekebisheni mtandao wenu, tangu jana mpaka sasa ni shida sana kuupata

Tigo rekebisheni mtandao wenu, tangu jana mpaka sasa ni shida sana kuupata

Kuna pesa za mgonjwa kwemye tigopesa,na tigopesa haifanyikazi.Mgonjwa anatakiwa apelekwe hospital,na hospital kunatakiwa pesa.
 
TIGO
mawasiliano yao yalikata toka saa 21:15HRS
Hasara walonipatia kwa jana sina ham nao kabisa na kama ningekuwa natumia kampuni moja tuu jana ningelipata bonge la lose.
 
fiber cut ndiyo nini

Fiber cut maana yake kukatika kwa mkongo wa mawasiliano wa fiber...

Ili kusafirisha mawasiliano baina ya point na point na kuweza kufikia mnara wa simu, mitandao ya simu hutumia ama fiber cable au mawimbi kwa njia ya anga (microwave)...

Sasa nyakati za mvua mara nyingi cable hizi za fiber ambazo huwa zimetandazwa ardhini, kuzolewa na maji na kupeleka kukatika na hivyo kufanya kuwe na katizo la mawasiliano...

Kwa upande mwingine, njia mbadala ya mawimbi kwa anga (microwave) huweza kuathiriwa na mvua kubwa kwa effects kama fading au minara kuchezeshwa na upepo n.k...

Mwisho wa siku unakuta njia kuu na mbadala zote zimepata hitilafu, hivyo kupelekea mawasiliano kuwa hafifu au chini kabisa...
 
Back
Top Bottom