Tiketi za SGR 782,000 zanunuliwa lakini hazikutumika ndani ya miezi tisa

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Takribani tiketi 782,000 zilizonunuliwa kwa ajili ya huduma za treni ya Reli ya Kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR) nchini Tanzania hazikutumika kati ya Januari na Septemba 2026, kwa mujibu wa takwimu zilizowasilishwa bungeni.

Shirika la Reli Tanzania (TRC) liliuza tiketi milioni 7.64 katika kipindi hicho, lakini ni abiria milioni 6.85 pekee waliosafiri, huku kukiwa na tofauti ya tiketi 781,966 ambazo hazikutumika.

Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, alisema baadhi ya abiria hununua tiketi lakini hushindwa kusafiri, huku wengine wakiona viti vinavyoonekana kuwa wazi ndani ya treni kumbe vimewekewa nafasi na abiria watakaopanda katika vituo vinavyofuata.

Akitolea mfano, alisema kiti kilichowekewa nafasi na abiria anayesafiri kutoka Morogoro kwenda Dar es Salaam kinaweza kuonekana kuwa wazi kabla treni haijafika Morogoro, ingawa kiti hicho hakiwezi kuwekewa nafasi na abiria mwingine.

Takwimu hizo zilitolewa kufuatia swali la Mbunge wa Tanga Mjini, Kassim Amar Mbaraka, aliyetaka ufafanuzi kuhusu sababu za baadhi ya treni kuonekana kuwa na viti wazi licha ya mifumo ya tiketi mtandaoni kuonyesha kuwa tiketi zote zimeisha.

Katika mwezi Septemba pekee, TRC iliuza tiketi 381,214, lakini abiria 35,343 hawakusafiri, sawa na takribani asilimia 9.3 ya tiketi zote zilizouzwa.

Aidha, Kihenzile alionya kuwa mahitaji ya usafiri wa treni huwa makubwa zaidi nyakati za mwisho wa wiki, huku akiwashauri abiria kukata tiketi mapema ili kuepuka kukosa nafasi za kusafiri.
 
Kinachotakiwa ni kwamba taarifa ya tiketi kuwa wazi kituo kipi hadi kipi iwekwe wazi kwa abiria pia ili kama naenda Dodoma treni imejaa kuna nafasi ya hadi Morogoro naweza kutumia hiyo fursa nikapunguza safari na shirika likapata pesa.

Mfano, abiria amekata tiketi ya Ngerengere-Moro, siti ije wazi toka Dar ili kumchukua? Kwa nini isioneshwe ili kwa mfano mtu mwenye gari yake akate Dar- ngerengere halafu aagize dereva aje kumchukua Ngerengere? Abiria yuko Igandu amaenda Dodoma uaani siti itembee wazi toka Dar/Moro kweli?N.k
 
Takribani tiketi 782,000 zilizonunuliwa kwa ajili ya huduma za treni ya Reli ya Kisasa ya Standard Gauge Railway kuepuka kukosa nafasi za kusafiri.
Mwezi wa 9 nilikata nikaahirisha kwa kutozwa asilimia, siku ambayo nilitarajia kusafiri ikashindikana tena, nikaona nikiahirisha nitalipia zaidi bora niitose tu.
 
Kinachotakiwa ni kwamba taarifa ya tiketi kuwa wazi kituo kipi hadi kipi iwekwe wazi kwa abiria pia ili kama naenda Dodoma treni imejaa kuna nafasi ya hadi Morogoro naweza kutumia hiyo fursa nikapunguza safari na shirika likapata pesa.
Mfano, abiria amekata tiketi ya Ngerengere-Moro, siti ije wazi toka Dar ili kumchukua? Kwa nini isioneshwe ili kwa mfano mtu mwenye gari yake akate Dar- ngerengere halafu aagize dereva aje kumchukua Ngerengere? Abiria yuko Igandu amaenda Dodoma uaani siti itembee wazi toka Dar/Moro kweli?N.k
Watu wengi hawachemshi ubongo. Ukijua hii trick huwezi kukosa tiketi. Mfano unatoka Dar unaenda Dodoma na system inaonesha tiketi hamna. Tafuta tiketi ya Dar-Morogoro ukiipata ,then tafuta ya Morogoro -Dodoms au Ngerengere-Dodoma ukipata zote mbili unanunua,kazi yako itakuwa kuhama behewa tu. Na hii ndio sababu unaweza kwenda hadi Moro kuna kiti kiko empty kumbe kuna mtu alinunua Moro-Dodoma kabla mtu wa Dar-Dodoma au mtu amenunua Dar-Ngerengere wewe wa Dar-Dodoma hupati kwasababu ya hawa wanapshuka njiani.
 
Huu ushairi wako nimeupenda
 
Hahahaha dah smart move.
 
Ndiyo ujanja naotumia. Kama seat zimejaa Dar to Dom, nacheki Dar to Moro au Dar to Mkata au Dar Ngerengere halafu ukibook seat unawahi kuangalia kutoka hizo destination kama kuna nafasi ya kutoka hapo kwenda Dom. Unaweza kupata seat za treni ileile au ukabook inayofuata, kwa maana ya kama ulikata ya saa 12 asubuhi kwenda hivyo vituo vya njiani, ukishuka unasubiri ya saa moja.
 
Watu wengi hawachemshi ubongo. Ukijua hii trick huwezi kukosa tiketi. Mfano unatoka Dar unaenda Dodoma na system inaonesha tiketi hamna. Tafuta tiketi ya Dar-Morogoro ukiipata ,then tafuta ya Morogoro -Dodoms au Ngerengere-Dodoma ukipata zote mbili unanunua,kazi yako itakuwa kuhama behewa tu. Na hii ndio sababu unaweza kwenda hadi Moro kuna kiti kiko empty kumbe kuna mtu alinunua Moro-Dodoma kabla mtu wa Dar-Dodoma au mtu amenunua Dar-Ngerengere wewe wa Dar-Dodoma hupati kwasababu ya hawa wanapshuka njiani.
Shida ya bongo ni kuwekeana ugumu ili wasioweza kuchemsha bongo wahangaike. Kwa nini wao wenyewe TRC wasirahisishe kwa kwa kuweka uwazi wa maeneo yaliyo na nafasi ili wapate faida?
 
Takribani tiketi 782,000 zilizonunuliwa kwa ajili ya huduma za treni ya Reli ya Kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR) nchini Tanzania hazikutumika kati ya Januari na Septemba 2026, kwa mujibu wa

Aidha, Kihenzile alionya kuwa mahitaji ya usafiri wa treni huwa makubwa zaidi nyakati za mwisho wa wiki, huku akiwashauri abiria kukata tiketi mapema ili kuepuka kukosa nafasi za kusafiri.
This is a typical white elephant project.
Mkiwa na katiba dhaifu, halafu wafanyabiashara wakawa ni ⁷viongozi wa kisiasa, tegemeeni miradi ya kiserikali kuhujumiwa Sana.

Abood ni mshindani wa SGR
Shabbiby ni mshindani wa SGR
Ester Luxury ni mshindani wa SGR
Na hawa wote ni wabunge, wana pesa na wana access ya kufanya hujuma kadiri watakavyo.

Hapo TRC lazima achome Sana mahindi
 
Usafiri una pesa nyingi sana, SGR kwa mwaka wanaingiza takribani bilioni mia tano.
 
Shida ya bongo ni kuwekeana ugumu ili wasioweza kuchemsha bongo wahangaike. Kwa nini wao wenyewe TRC wasirahisishe kwa kwa kuweka uwazi wa maeneo yaliyo na nafasi ili wapate faida?
Hakuna ugumu wowote uliowekewa. Wewe unataka direct ticket ya Dar Dom hakuna na system inaona hakuna. Ukiwa pale station unaweza kupewa option hio. Ila online system haiwezi kukupa Dar-Ngerengere wakati wewe unataka Dar-Dom.
 
This is a typical white elephant project.
Mkiwa na katiba dhaifu, halafu wafanyabiashara wakawa ni ⁷viongozi wa kisiasa, tegemeeni miradi ya kiserikali kuhujumiwa Sana.

Abood ni mshindani wa SGR
Shabbiby ni mshindani wa SGR
Ester Luxury ni mshindani wa SGR
Na hawa wote ni wabunge, wana pesa na wana access ya kufanya hujuma kadiri watakavyo.

Hapo TRC lazima achome Sana mahindi
Wakati SGR inaanza mlisema haichukui miezi sita itakufa. Walioipa muda mrefu walisema mwaka tu. Ila huu unaenda mwaka wa tatu onadunda na huduma ni ile ile kiwango cha juu. Mara nyingi wasiotumia SGR au pessimists ndio huwa wanaponda SGR.
 
Hasara ya TRC ni zaidi ya SGR. Ingekuwa wanatoa hesabu ya SGR peke yake usingesikia hasara.
Una uhakika? Kwa nini hawatoi SGR pekee na combination ya vyote kwa pamoja? Huu mradi ni suala la muda tu CCM hawawezi kufanya jambo la maendeleo zaidi ya kuua na kupora. Kna member juu hapo kaweka list ya wanasiasa wenye biashara ya ushindani na SGR, unadhani watataka kupata hasara? Nakuhakikishia hata haya maelezo ya watu kukata tiketi na kutosafiri yameongezwa chumvi ili kulinda wezi. Huu mradi una hujuma nyingi.
 
Sawa.
 
Hakuna ugumu wowote uliowekewa. Wewe unataka direct ticket ya Dar Dom hakuna na system inaona hakuna. Ukiwa pale station unaweza kupewa option hio. Ila online system haiwezi kukupa Dar-Ngerengere wakati wewe unataka Dar-Dom.
Hakuna namna online system ioneshe njia zilizo wazi? Kwa hiyo kama nipo pembeni ya Dodoma ni lazima niende station kuuliza? Nini maana ya maendeleo ya teknolojia!
 
Back
Top Bottom