Nafuatilia game ya Mbeya city na Yanga , kiukweli kiwango kibovu kinachoonyeshwa na Yanga inashangaza ! haijulikani wanacheza fomesheni gani , yaani haijulikani wamewezaje kuongoza ligi mpaka sasa , Mbeya city inayoburuza mkia haionekani kama ina tofauti yoyote na Yanga yenye wachezaji wa Kimataifa .
Tatizo la timu hii haijulikani kama ni wachezaji au ni kocha , ni timu mbovu kuliko maelezo .
Sisi kama nchi tukithubutu kukubali kuwakilishwa na timu hii kwenye michuano ya kimataifa itakuwa aibu ya karne .