Yaani ndani ya polisi au nje ya Polisi .Niliwahi kuandika , tume ya haki jinai nayo ikaona,
Na narudia tena, ipo haja ya kuwa na taasisi inayojitegemea ya upelelezi wa makosa ya jinai.
Je waweza kutolea mfano wa Nchi nyingine yenye kitengo kama hicho.
Mimi ninafikiri njia zetu za ukamataji , zibadilike, zisiwe za kimabavu, kama vile polisi wetu ni watakatifu na raia ni waovu.
Hivyo njia ya kwanza ni kumpa MTU wito WA kufika kituoni, asipofika ndio afuatwe, na ki kawaida polisi atapita kwenye serikali zetu WA MTA au watachukua Jirani wakashuhudie ukamataji.
Ni katika matukio machache utaratibu huo unaweza kupindishwa, kwenye matukio makubwa kama ujambazi au fujo za papo Kwa papo .