Timu ya uchunguzi wa Makosa makubwa kutoka ofisi ya DCI yatumwa kuchunguza Mauaji ya Ali Kibao wa CHADEMA

Timu ya uchunguzi wa Makosa makubwa kutoka ofisi ya DCI yatumwa kuchunguza Mauaji ya Ali Kibao wa CHADEMA

Huu ni utani mwingine kwa watanzania. Polisi wana tuhumiwa halafu ati wana tuma kikosi kuchunguza.. We are not serious. Halafu alie tuma ni Kingai ambae historia yake ina julikana.
Rais Samia asimuue Mbowe ambaye ni mmoja wa wapinzani wake wakubwa wa siasa za Tanzania aje kumuua mjumbe wa CHADEMA?.

Tupunguze lawama, hiyo Kibao aliishi kama binadamu wengine na hatuujui ubinadamu wake ulikuwa vipi haswa.
 
Jeshi la Polisi limesema Ofisi ya DCI imetuma Timu ya uchunguzi wa Makosa makubwa kwenda kuongeza nguvu upelelezi wa mauwaji ya Ally Mohamed Kibao
Eti "timu ya uchunguzi makosa makubwa" Hawa ni wale tangu 2017 wanachunguza tulio la Lissu au ni wachunguz wengne? Wakija na jpya ambalo Haina maigizo ndan yake nachoma vyeti vyangu vya darasa la saba, Cha ubarikio,na ubatizo.
 
Unamjuwa ❌ Unamjua ✅

Ukatowe ❌ Ukatoe ✅
Unaandika kwa kufundishwa shuleni. Kiswahili siyo lugha mama kwako. Naandika Kiswahili kinavyotamkwa na kama kilivyokuwa kinaandikwa kwa asili yake, maandishi ya Kiarabu.

Kiswahili ni lugha mama kwangu.
 
Kama kila mtu akiandika Kiswahili kwa namna anavyotamka yeye na jamii yake, hicho kitakuwa ni Kiswahili tena mkuu?

Maana yake ni kwamba Mchagga ataandika Kiswahili anachokijua yeye na Msukuma ataandika cha kwake and before we know it, hatuna lugha.

Ni vyema kufuata taratibu za kisarufi wakati wa uandishi.
 
Wewe andika ujuwavyo, tatizo nini?

Mradi usichanganye R na L na usiongeze ma ga ga ga.
 
Jeshi la Polisi limesema Ofisi ya DCI imetuma Timu ya uchunguzi wa Makosa makubwa kwenda kuongeza nguvu upelelezi wa mauwaji ya Ally Mohamed Kibao
Meku DCI ni yule Kingai wa kesi ya Mbowe ya " kuchoma vituo vya police na kukata miti? 😳
 
1. Ziwe za kweli

2. Ziwe za uhakika

3. Zifuate taratibu

============

Haya, kwa yule anaemjua Muuaji kwa majina matatu, alikuwepo porini akashuhudia kipigo, kifo, kutupwa - LAKINI YEYE WAKAMWACHA SALAMA - na anajua taratibu za kipolisi na kisheria za kutoa taarifa atoke mbele atusaidie.

Vinginevyo tips zako kaa nazo !!!!!
 
Timu ya uchunguzi wa matukio makubwa toka Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai toka Makao Makuu imetumwa kuongeza nguvu ili kuhakikisha waliofanya mauaji ya Ali Kibao Kada wa CHADEMA wanakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Jana Septemba 7, 2024 Jeshi la Polisi lilitoa taarifa juu ya Ally Mohamed Kibao kuhusishwa kutoka kwenye basi la Tashrif na kuchukuliwa na watu ambao hawakuweza kutambuliwa na kwamba uchunguzi ulianza baada ya kupokelewa taarifa hiyo.

Baada ya kutolewa taarifa za kuonekana mwili wa mtu mwanaume ambaye hakuweza kutambuliwa kwa wakati huo ni mwili wa nani huko Ununio Jijini Dar es Salaam, utambulisho umefanyika kwa mujibu wa taratibu na kubainika ni mwili wa Ally Mohamed Kibao.

Soma Pia:
Aidha, uchunguzi wa mwili wa marehemu (postmortem) umefanywa leo tarehe 08/09/2024 na Madaktari bingwa kwa kushirikisha familia.

Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hili la kusikitisha na timu ya uchunguzi wa matukio makubwa toka Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai toka Makao Makuu imetumwa kuongeza nguvu kwenye timu ya awali ili kuhakikisha waliofanya mauaji haya wanakamatwa na kufikishwa mahakamani.
Misime asilete siasa kwenye damu anafanya Kama tangazo yaani baada ya President kulaani wakati awali idara ya Polisi ilikuwa kimya kutoa taarifa ya Nini kinaendelea.....
Shame on them
Nyambaf!!!
 
1. Ziwe za kweli

2. Ziwe za uhakika

3. Zifuate taratibu

============

Haya, kwa yule anaemjua Muuaji kwa majina matatu, alikuwepo porini akashuhudia kipigo, kifo, kutupwa - LAKINI YEYE WAKAMWACHA SALAMA - na anajua taratibu za kipolisi na kisheria za kutoa taarifa atoke mbele atusaidie.

Vinginevyo tips zako kaa nazo !!!!!
Kwenye tashrif bus hakuna hata aliyepiga picha wakimchuka mzee wetu?
 
Unaandika kwa kufundishwa shuleni. Kiswahili siyo lugha mama kwako. Naandika Kiswahili kinavyotamkwa na kama kilivyokuwa kinaandikwa kwa asili yake, maandishi ya Kiarabu.

Kiswahili ni lugha mama kwangu.
Dear usiku mwema!
 
Yaani Dkt Samia aite wa USA au UK waje wachunguze kama anataka haki itendeke, hao polisi sidhani
mkuu hivi upo serious na ulichoandika..? unazijua hatari za kuita wapelelezi toka nchi nyengine..?😂
hii siafiki tumalizane humuhumu mbona tunatoshana watafahamika tu.
 
Mara paaaaa cctv camera inatoa picha
Nchi za wenzetu waloendelea waziamini sana CCTV kwamba ndo suluhisho pekee katika kufanya uchunguzi wowote kuhusiana na uhalifu wa aina yoyote.

Kwasababu katika uchunguzi hatua ya kwanza kabisa ni kukusanya ushahidi kazi ambayo ni ngumu.

Tena siku hizi polisi (detectives) hutumia masaa mengi kupitia footage za matukio yoyote kupitia CCTV, DashCam kutoka kwa raia wema ambao wana vifaa hivyo katika magari na smartphones ambazo raia wamechukua picha na video.

Kwa hapa tulipofikia nchi yetu kwa sasa wananchi wapaswa kuzinduka na kuwa alerted kwa kila jambo khasa hili la utekaji.
 
Najiuliza hivi mtu gani anaweza kushika silaha nzito ya kivita na kuingia nayo ndani ya basi mchana kweupe na kumfunga pingu raia na kisha kuindoka naye kwa kutumia Toyota Landcruiser HardTop.
Jibu nalopata huyo mtu lazima awe wa Serikali na Serikali lazima inamjua.
Ingekuwa vyema Serikali ikajitoa kwenye hili iwaite scotland yard waje wafanye uchunguzi ili ukweli ujulikane
Waasi Adf Nalu, M23 , wale waasi wa msumbiji
 
Back
Top Bottom