Timu ya uchunguzi wa Makosa makubwa kutoka ofisi ya DCI yatumwa kuchunguza Mauaji ya Ali Kibao wa CHADEMA

Niliwahi kuandika , tume ya haki jinai nayo ikaona,

Na narudia tena, ipo haja ya kuwa na taasisi inayojitegemea ya upelelezi wa makosa ya jinai.
Yaani ndani ya polisi au nje ya Polisi .
Je waweza kutolea mfano wa Nchi nyingine yenye kitengo kama hicho.
Mimi ninafikiri njia zetu za ukamataji , zibadilike, zisiwe za kimabavu, kama vile polisi wetu ni watakatifu na raia ni waovu.
Hivyo njia ya kwanza ni kumpa MTU wito WA kufika kituoni, asipofika ndio afuatwe, na ki kawaida polisi atapita kwenye serikali zetu WA MTA au watachukua Jirani wakashuhudie ukamataji.
Ni katika matukio machache utaratibu huo unaweza kupindishwa, kwenye matukio makubwa kama ujambazi au fujo za papo Kwa papo .
 
Kwani wao ndio. Walio tenda au walikuwa na uwezo wa kulizuia
 
mkuu hivi upo serious na ulichoandika..? unazijua hatari za kuita wapelelezi toka nchi nyengine..?πŸ˜‚
hii siafiki tumalizane humuhumu mbona tunatoshana watafahamika tu.
Kweli bosi, sijui kabisa maana mi ntu wa Ntwara huku Tandahimba sijui kitu kabisa. Basi tutumie wa kwetu naafiki
 
Najiuliza hayo maeneo ya kibo complex hakuna hata camera za kwenye majengo na za barabarani zilizofanikiwa kunasa hili tukio?
 
Kweli bosi, sijui kabisa maana mi ntu wa Ntwara huku Tandahimba sijui kitu kabisa. Basi tutumie wa kwetu naafiki
umekubali kirahisi sana i atakiwa mpk mti atoke damu hapa!
 
Mimi mbumbumbu ningeambiwa niorodheshe kwanza washukiwa angalao kumi tu.

Ambao ningewaorodhesha hapa, najisikia kutetemeka kuendelea kuandika.

Na katika washukiwa watatu wa juu kwa umuhimu kufanyiwa kazi kuna mmoja ikidhihirika ndiye mhusika, hakuna hata haja ya kuanza huo uchunguzi.

Sababu, akitangazwa anahusika nani atamchukulia hatua. Na ni nani atathubutu kumtaja.

Kwahakika, tukio lile ni kizungumkuti ambacho wahusika au mhusika, wakipewa nafasi nyingine hawawezi lifanya kwa namna ile, ni fedheha kwa macho ya wanadamu. Kwa Mungu hata sijui ni nini, sina hayo mamlaka.
 
Vipi kuhusu Matokeo yatokanayo na Uchunguzi wa timu hii ya wachunguzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…