Zile ni fedha ambazo zililipa mishahara, nauli, chakula Na posho (utilities) Na kwisaha kabisa. Hii ni tofauti Na kujenga uwanja utakaodumu miaka 100 ukiingiza pesa. Haiwezekani ni change Mimi lakini pesa ule we we? Je, kama timu ikifa uwanja unabaki kwa nani? Je kama uwanja utafanya faida pesa zitamnufaisha nani Na nani?
Naamini ushawah sikia kitu kinaitwa board of trustee... kazi yao ni kulinda mali za taasisi.. sheria haitambui club ya mpira kupitia wachezaji na viongoz ila inatambua club ya mpira kama
taasisi kupitia katiba na miongozo iliosajiliwa so kiuhalisia club haitakufa bali inaweza ikasitisha kufanya shughuli zake za kimichezo
lakini mali za club bado zitakuwa mali za club hakuna cha kusema mali zinakwenda kwa nani
kwa msaada zaidi rejea Pan Africa na Nyota nyekundu.. Pan Africa hawana team ila wana jengo kariakoo na kila mwaka wanakutana na kila miaka minne wanafanya uchaguzi wa viongoz.. ingawa hawazidi hata watu 30..
ni kweli watu wanaweza kutumia jengo kupangisha na kula pesa ila watakula hizo pesa kupitia jina la club kwa maana ya kuwa lazima huyo mtu awe ametambulika kisheria kuwa ni kiongoz wa club husika na ana mamlaka ya kuingia mikataba kwa niaba ya club..
so kwa namna hiyo tunaweza kusema kuwa majengo ya Pan Africa pale
kariakoo kuna watu wanakula pesa badala ya kuwekeza kufufua club.. ila kwa mfano huo huo hata sasa hivu kuna viongoz wa hizi club za ligi kuu wanakula pesa za club kupitia mgongo wa club so hawana tofauti na viongoz wa team iliojifia ya Pan Africa
ila wote hawawezi kuuza mali za club sababu zinalindwa kisheria
NB: Jiulize mchakato wa Simba kwa nn ulichukua mda mrefu wakiwa wanapigizana kelele na Mzee Hamisi.. sababu ni kuwa Ilibidi Simba wawe na docz zote za kuonyesha mali zao so Mzee Hamisi akiwa kama mjumbe wa bodi ya wadhamin akawa anagoma kutoa docs..
kitu ambacho kitawakuta yanga pia wakifika kwenye uhakiki wa mali za club sababu docz zimetapakaa kila mzee wa zaman ana yake huyu ana ya kiwanja huyu ana sijui ya jengo