The Supreme Conqueror
JF-Expert Member
- Feb 13, 2017
- 609
- 1,584
Wana jamvi habari zenu? Awali ya yote poleni kwa Msiba mzito kwa Taifa kwa ndugu yetu Kipenzi Spika wa Bunge la JMT Mstaafu Ndugu yetu Mhe. Job Augustino Ndugai bila kujali itikadi zetu za kisiasa na hisia.
Niende kwenye mada moja kwa moja.Hivi karibuni JMT ilizindua Dira ya Maendeleo 2025/2050 lakini kuna jambo moja walishindwa kuling'amua au kulikubali na kuliweka wazi kuwa Watumishi wa Umma walikaa miaka 9 bila nyongeza ya Mshahara kiasi kwamba kuna mambo yalisimama mtaani kwani gharama za maisha yalipanda ila Watumishi na Wafanyabiashara waliotegewa kujenga mfumo wa uchumi wa kati hawakuzingaitiwa kabisa.
Marehemu hawezi kujitetea tena ila kuna vipengele vingi tulikosea kama Taifa na lazma tujisahihishe na hata leo Samia lazma akubali maamuzi ya muongozo na ajisahihishe ili Taifa lisonge mbele kwani Tanzania ya miaka ijayo siyo Tanzania ya leo,Vizazi vyake vitarithi Mema na Mabaya ya Matendo yake.
Taasisi zinazosimamia mfumo wa fedha nchini zinapaswa kuangalia mstakabali mpana wa mzunguko wa Fedha pamoja na mikopo zitolewayo kwa Watumishi,Wafanyabiashara na Wajasiriamali ili kuendana na mabadiliko ya Maisha na mfumuko wa kwasasa kuelekea uchaguzi Mkuu,Serikali Mpya na Bajeti Mpya ya Kiserikali 25/26 Lazma Riba zipunguzwe kusadifu uhalisia wa Maisha ya Sasa,kinyume na hapo naona Serikali Mpya kushindwa kutawala Taifa na kuna anguko kubwa la Dola tulitarajie siku za usoni.