TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Pascal nimekuelewa , tatizo lako nowadays ata uhaminiki, yaani umekuwa vuguvugu Kwa Mungu haupo na Kwa shetani haupo.
 
Pascali, unakumbuka siku ile pale Ikulu ulipomuuliza swali mkuu wa ikulu alivyokuzalilisha kisha akajibu nje kabisa ya swali, hii hoja yako hawezi kuifanyia kazi sembuse yeye mwenyewe ndiye anayetoa instruction haweze kujali ushauri wako, ujumbe umefika. Nakuaminia komando,
 
Kumbe polisi na tiss ni watu hatar kuliko jwtz
 
Duuh mkuu Pascal hatari kweli...
 

Paskali paskali paskali, uuuuuwiiiiiii, paskali umejizira au? Mungu akulinde maana mhhhh paskali.

Ila paskali serikali yetu imejitoa kwe open goverment initiative,haiko tena labda ni ili kuficha madudu uliodadavua hapo juu. Ikibidi jibadili sura maana najua hao jamaa wanakuwinda kwa sasa.
 
Duh!!, umenikumbusha mbali sana kwa habari ya sekeseke la Kigoto, ilikuwa ni zaidi ya gereza la Guantanamo na kibaya zaidi mateso yaliyokuwa yanaendelea hapo enzi hizo yalijulikana hata na watoto wadogo binafsi nimekulia Mwanza (Mabatini) na huyo mzee mhanga mmojawapo marehemu Mazegenuka alikuwa jirani yangu in fact ktk suala la tuhuma za mateso na mauaji ya Kigoto yaliyosimamiwa na maafisa waandamizi wa polisi na Idara ya usalama Mzee Nyerere (RIP) kama head of state alionyesha concern ya kipekee sana ktk kuwatetea raia wake wanyonge dhidi ya udhalimu huo ktk sakata hilo lililokuwa na mvuto wa kipekee karibu nchi nzima enzi hizo, maamazi aliyochukua Mwl. Nyerere dhidi ya watuhumiwa yalimjengea heshima kubwa sana mbele za raia wake na hata taasisi za haki za binadamu kimataifa.
 
Ni kweli ndg. Zipo nyakati mwl. Nyerere (Hayati) alisimama mpaka mtu unaona kweli sura halisi ya urais, uzalendo na utu.

Ni masikitiko leo watu wanalia na serikali yao wanaomba wasibomolewe nyumba, bado wanabomolewa, wapo walioenda mahakamani kufungua kesi, mahakama ikaweka stop order, lakini bado serikali ikaendelea kubomoa.. Ni hatari.
Ajabu benki ya dunia Ndio imeweza kuwasikiliza wanyonge hawa na kusisitiza haitatoa hela za ujenzi wa barabara hiyo (kimara) kama bomoa bomoa inayowatia watu ufukara itaendelea.
Mtetezi wa waTz amekuwa ni bepari world bank huku serikali ya weusi ndio mtesaji mkuu.
Kweli nyakati zinaenda kasi.
 
Mkuu Agustino Fannuel Massongo, kiukweli kabisa hii kesi iliyomkumba mzee wangu, imeniathiri sana, kila nikisikia mtu amekufa mikononi mwa polisi, naumia sana na kutamani Nyerere afufuke.

Angalia kelele zangu humu kuhusu vifo mikononi mwa polisi.

Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa!, Polisi Wako Ni Wauaji!. P'se Stop This

IGP Kamanda Sirro, Usiruhusu Vifo Vya Uzembe Kama Huu Kuchafua Jeshi Letu Safi la Polisi!.

Waziri Nchimbi na IGP Mwema, Mnasubiri Nini Kujiuzulu?

IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality!. Utampeleka JK The Hague-Part II!

ACJ na Mhimili wa Mahakama, Kemeeni Tabia Ya Jeshi la Polisi Kujigeuza Mahakama na Kuhukumu Watuhumiwa Kutumia Media
 
Paschal ume cross the red line!
 
Paschal ume cross red line!
How?.
Kila mtu anafahamu TISS wanadukua simu za watu illegal, kiongozi anatoa taarifa simu ya fulani imedukuliwa na hajacross the red line!.

Mimi ni Mtanzania mzalendo wa kweli ambaye natambua umuhimu wa TISS, the biggest red line crossing ni ku expose ma agents wetu!, kiongozi anafanya exposure ya agents with names, hamsemi ame cross the red line, sisi tunaoibua madudu ya TISS ya more than 40 years ago, ndio crossing the red line?.

Kwa taarifa tuu, gestation period ya government secrets ni 30 years, na 50 years kwa top secrets. Tungekuwa na waandishi makini, by now kuna makala nyingi za what happened in the dark 30 years ago. Ukienda pale idara ya nyaraka, unawakuta wazungu ndio wanatafuta documents, sisi wenyewe ambao ndio tuhusu, hata habari hatuna!.
P.
 
Mayalla najua yote uliyoongea.Hata hivyo kumbuka kwamba Tanzania bado ni nchi ya kiafrika where transparency is not the norm.Paschal what do you loose by keeping quiet. Hawa watu huwa hapendi criticism na hawapendi kabisa mambo yao yafahamike.Please take care.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…