Kitu ambacho nakubaliana na wewe ni kweli hairuhusiwi kutaja hadharani nani ni TISS na hakuna aliyetaja hadharani kuwa fulani ni TISS kwa sababu hao TISS wa Nyerere hata mke kujua mume ni TISS ilikuwa shughuli.
Sasa kama TISS wanavaa makirikiri kumsindikiza Bashite kuvamia studio, na TISS mwingine anatoa bastola hadharani kumtishia waziri, nani anakuwa aneiexpose vibaya TISS? .
Alichosema Lisu ndicho nilichosema mimi, hizo data ni za mahakamani hivyo sio classified info zinazolindwa na sheria.
Kweli TISS wana privilege ya confidentiality lakini wasitumie privilege yao kufanya madudu ya kijinga jinga kwa kuitumia kama kichaka cha kufanyia maovu.
Paskali