TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Kitu ambacho nakubaliana na wewe ni kweli hairuhusiwi kutaja hadharani nani ni TISS na hakuna aliyetaja hadharani kuwa fulani ni TISS kwa sababu hao TISS wa Nyerere hata mke kujua mume ni TISS ilikuwa shughuli.

Sasa kama TISS wanavaa makirikiri kumsindikiza Bashite kuvamia studio, na TISS mwingine anatoa bastola hadharani kumtishia waziri, nani anakuwa aneiexpose vibaya TISS? .

Alichosema Lisu ndicho nilichosema mimi, hizo data ni za mahakamani hivyo sio classified info zinazolindwa na sheria.

Kweli TISS wana privilege ya confidentiality lakini wasitumie privilege yao kufanya madudu ya kijinga jinga kwa kuitumia kama kichaka cha kufanyia maovu.

Paskali
Si wewe wala Lissu amethibitisha pasipo shaka kwamba wahusika kwenye hayo matukio ni TISS. Kilichopo ni nadharia tu ambazo si sahihi tukazitumia kukichafua chombo nyeti kama TISS. Na hata ingekuwa imethibitika kuwa ni TISS, wao wana procedure zao za kuwajibishana kisheria na si kama Lissu anavyoropoka bungeni. Tuache ujuaji na kuingilia idara zisitokiwa kuingiliwa.
 
Whoever alleges has the burden to prove his allegations. Mayalla ni wakili msomi na anajua. Kwako wewe hujui chochote
Hivi yule askari wa TISS aliyemtolea Nape bastola mchana kweupe sio ushahidi tosha jinsi kikundi hicho kinavyokanyaga haki za raia au wewe unataka ushahidi gani mkuu? Nakushangaa sana.
 
Protocol haziruhusu,wanakufa na tai shingoni.Lakini wao kwa wao na taasisi nyingine zenye mawasiliano mmoja kwa mmoja wanazungumza kwa mipaka ya kazi zao,nafasi zao na majukumu yao.Ni nadra sana kwa taasisi hiyo kujilipua wazi wazi.Yupo mtu mmoja aliwahi kusema mkewe aliishi nae miaka zaidi ya 30 asijue kuwa ni afisa kachero gwiji hadi anastaafu,na alivyogunduliwa alikanusha na kumkana mtu mmoja aliemtambua kuwa ni mwenzao.
kwa hiyo tuwaache waendelee kuua raia huku tumekaa kimya?
 
Kuteka, kutesa na kuua raia wasiokuwa na hatia ni KULINDA AMANI YA NCHI? Hivi uzalendo wa mtu hupimwa kwa unafiki wake wa kukaa kimya huku wananchi wakiuawa kila kukicha na kikundi kimoja cha kigaidi? Ama kweli wewe ni kituko cha mwaka!
Nadhani si vema kuongea kwa mihemuko. Una ushahidi pasipo shaka kwamba TISS ni kikundi cha kigaidi? Una ushahidi pasipo shaka kwamba TISS inahusika na hayo matukio unayoyasema? Ushukuru kwamba Max anahangaika mahakamani kuwatetea watu kama wewe wenye tabia za kuropoka hovyo na kuzichafua idara zetu za ulinzi na usalama kwa maslahi yenu ya kisiasa. Hizi tabia zinanikera mno watu kujitoa ufahamu na kuona siasa ni bora kuliko usalama wa nchi.
 
Maboso,
Hili ni suala la utetezi wa haki za binadamu...hakuna siasa yoyote ndani yake. Wewe ndiye uliyelewa siasa...kwamba mtu yeyote anayetetea raia dhidi ya ukandamizaji wa vyombo vya serikali ni MWANASIASA. Hiyo ni dhana ya kipuuzi sana.
 
Tuache ujuaji na kuingilia idara zisitokiwa kuingiliwa.
Huu ni ushauri mzuri sana tena ungeanzia kwa Mwalimu Nyerere kuwatimua kazi maofisa wa juu wa TISS na kuwaahitaki mahakama za kiraia kwa utekaji, utesaji na mauaji. Tafuta Rejea za Kesi ya Mauaji Mwanza usome madudu ya TISS.

Tafuta kesi ya Uhaini ya 1982 uone madudu ya TISS na mashahidi japo walitumia majina ya Mr. X, Mr.Y na Mr. Z na tunawajua lakini hatujawataja popote.

Then waeleze ma editors wa magazeti likiwemo gazeti la serikali ambalo editor in chief ni rais, wasiripoti madudu ya TISS yaliyoripotiwa mahakamani.

Wakati wa Mkapa lile kampuni la Kagoda lilichota fedha Bilioni 40, kwa mgongo wa TISS ambazo zilitumika kwa kazi maalum iliyotukuka!.

Hivyo naunga mkono kwa asilimia 100% TISS isingiliwe wala kujadiliwa, kama haha wenzetu Marekani wanaijadili CIA, who the hell is TISS? .

Soma kisa hiki cha mtu wa TISS ya US alivyoyauguza madudu ya TISS yao kwenye media hadi rais aliachia bodi!.

What did JPM know and When Actually did he know?

Kama Bunge linauwezo wa kumdajili rais na kumfungisha virago kwa kumfuta kazi kama amefanya madudu, what the hell is TISS isijadiliwe kama imefanya madudu?.

Kitu cha msingi ni isidajidiwe hadharani.
Paskali
 
No huyu anafanana sana sana Nyerere, nilisema hapahttps://www.jamiiforums.com/threads/magufuli-kama-nyerere-ni-mtu-wa-watu-hapapasi-hamungunyi-ni-kazi-tuu-ila-pia-sio-kama-nyerere.991898/page-3

Kama issue ni kuongea kwa ukali huku akikaza maneno, hii ni hulka tuu, nimeizungumza hapahttps://www.jamiiforums.com/threads/kanda-ya-ziwa-na-kuongea-kwa-ukali-ukali-wa-rais-magufuli-ni-asili-tuu-ya-wasukuma-sio-udikteta.1108953/page-7

Lingine ni kutoonyesha kujali majanga nako sio ukatili bali ni ushujaa nimeuzungumza hapa
Kutoonyesha Hisia/Huruma wala pole za sauti si Udikteta bali ni Ushujaa wa Kijeshi!

Hivyo yuko kama Nyerere kwa kiasi kikubwa na kuna maeneo ni zaidi ya Nyerere.

Paskali
Mh!
Nyerere unanafasi bado ya kimfananisha huyu na Mwalimu!
Wana tofauti kubwa kabisa!
Labda kama ilikuuma sana kuona Mzee wako alivyoteseka kwa kuwekwa Ndani!!
 
Ni ujinga kuamini kuwa eti usalama wa Taifa unateka watu na unaua watu, mbona sisi hatujatekwa, watu wamejaa barabarani, wamejaa mashambani mbona hawajatekwa wala kuuwawa? Mbona hata wewe hujauwa wala kutekwa? Leo hii unaibuka na post ya kijinga jinga. Amajweli post za kunukuu ujinga uliotolewa na mjinga flani tena wa upinzani ambaye yeye ameajiriwa kupinga tu. Jitu lililokataliwa kutokana na ufisadi. Lowasa hatakuwa Rais hata mkilala mnaota.
Kwani na wewe ni mtu?! Watu hutumia akili kufikiri na si hisia!!
 
Back
Top Bottom