TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Hata mimi nimemsoma na nimejiuliza mambo mengi sana, tatizo ni Nape!!!, hao TISS wanaoelezwa kuwa wanatesa watu uko Clouds waliteswa? walipigwa? Pasco anayo ajenda, awe wazi katika ajenda yake.
Pasco amezunguka zunguka lakini anayo ajenda.
Mkuu ni kweli nina agenda moja tuu, kutanguliza mbele maslahi ya taifa kwa hoja zenye truthfulness, objectivity na transparency.

Nitasema kweli daima na mada zangu zote ni ukweli daima, nothing but the truth kwa maslahi ya Taifa.

Pascal
 
Pascal pole sana,najua JKN alikuwa anashida lakini hili la kuua na kutesa kwa sababu ya kutukana,kuhojiwa sidhani kama lingekuwepo kwa JKN.

Kiongozi yeyote akishashindwa kuongoza basi matokeo yake ni kutumia idara hii kunyamazisha watu.
nipo huku my
 
Maboso, Mkuu Mabosa, na wewe unakabiliwa na tatizo kubwa linalowakabili Watanzania wengi, kwanza ni wavivu wa kusoma mada ndefu, pili wengi ni too ignorant to comprehend kilichoandikwa.

Kwenye bandiko hili ni mimi ndiye niliyesema waliovamia Clouds ni TISS? .

Hujawahi kusikia TISS wakiongea na media? . Fuatilia mtu anayeitwa Jack Zoka akiwa TISS.

Lissu kaongea hadharani au kaongea Bungeni? . Unajua maana ya tuhuma zozote kushushwa Bungeni na kutokanushwa na yoyote what does that mean? .

Sijasema nazijua kazi za TISS humu na nilichokisema ni kidogo tuu ya ninachokijua. Nimesema Mzee wangu Andrew Mayalla(RIP) ndie alikuwa RSO wa Mwanza na kilichomkuta. Wako watu wengi wazazi wao ni wafanyakazi wa TISS lakini hakuna yoyote ajuaye huko ndani ya TISS wanafanya kazi gani au shughuli gani.

TISS wanaoeleweka shughuli zao ni wale wa Kijitonyama kwa sababu wanaonekana na kazi yao ni kuvaa tuu suti nyeusi na miwani nyeusi na kusimama tuu huku wakiangalia huku na kule.

Nilichoweka hapa ni baadhi tuu ya matokeo mabaya ya kazi za TISS yaliyowasilishwa mahakamani na maofisa wa juu wa TISS kutimuliwa na kushitakiwa na kufungwa jela.

Kuhusu hizi tuhuma za sasa nimetoa a good benefit of doubt kwa kuweka options 3 za different scenarios

1. Tiss huko nyuma iliwahi kufanya makosa ya utekaji, utesaji na hata uuaji, na ikafumuliwa!. Hivyo kwa vile tayari tunayo precedence ya vitendo viovu vya TISS huko nyuma, hivyo kwa kuutumia uthibitisho wa uovu huo, una justify kuwa kuna uwezekano ikawa ni kweli TISS is behind huu uovu na uchafu unaozungumziwa sasa Bungeni.

2. Lakini pia inawezekana sio TISS as TISS bali ni acts za individual members wa TISS wakifanya a "stand alone operations" bila kupokea command yoyote kutoka juu, hivyo vitendo vya wachache, vikaichafua TISS yetu collectively kwenye a collective responsibilities formula.

3. Pia inawezekana kabisa vitendo hivi vinafanywa na wahuni fulani, ambao wana pose as TISS just to make believe kuwa ni TISS kumbe sio TISS bali ni just impostors wanaochafua the good image ya TISS wetu waadilifu.

Whichever the case, TISS ijitokeze iwakane na kurudisha imani na TISS wetu.

Paskali
 
Wewe u.tumbo wako huu ulioandika hapa ndio FACTS eeh? Kama facts unazo si umwage hapa. Usiwe kama serikali yako ya CCM ambao wakiulizwa wamefanya nini kwa miakaz 50 wanasema wamefanya MAMBO MENGI bila kuyataja. Basi wewe kama unazijua facts za utekaji na utesaji huu, funguka ama sio funga bakuli lako.
Whoever alleges has the burden to prove his allegations. Mayalla ni wakili msomi na anajua. Kwako wewe hujui chochote
 
... Uzi huu haukupaswa kuwekwa hapa! TISS ni yetu Watanzania, Yafaa kuienzi, kuilinda, kuwaunga mkono... kuna mambo mengi sana ambayo watanzania hatuyajui ...
 
Whoever alleges has the burden to prove his allegations. Mayalla ni wakili msomi na anajua. Kwako wewe hujui chochote
Mkuu Ibambasi, mimi sio wakili wala sio msomi!. Elimu yangu ni ya hapa na pale kama tuu elimu ya Daudi.

Paskali
 
Pascal Mayalla,
Options hizi, kama ulivyokiri mwenyewe, zinatosha kuweka mashaka kama TISS inahusika kiasi cha kutuhumiwa moja kwa moja (kama Tundu Lissu alivyofanya).

Je, TISS sio kitengo cha serikali? Na Waziri Mkuu anapojibu kwa niaba ya serikali, ina maana kwamba hajibu kwa niaba ya TISS?

Nisaidie (maana nimesoma hapa kwamba wewe ni mwanasheria uliyebobea (kwa wanaokufahamu ila isije ikawa ni kutoka Mlimani - kumbuka mikataba ya Mlimani City)!
 
Wewe u.tumbo wako huu ulioandika hapa ndio FACTS eeh? Kama facts unazo si umwage hapa. Usiwe kama serikali yako ya CCM ambao wakiulizwa wamefanya nini kwa miakaz 50 wanasema wamefanya MAMBO MENGI bila kuyataja. Basi wewe kama unazijua facts za utekaji na utesaji huu, funguka ama sio funga bakuli lako.
Sina nia ya kununua ugomvi wenu, lakini nina uhakika kwamba hata wewe ukiulizwa, kwa umri wako umefanya nini, ama utasema bado unakua au CCM imekukwaza!
 
Mkuu Mabosa, na wewe unakabiliwa na tatizo kubwa linalowakabili Watanzania wengi, kwanza ni wavivu wa kusoma mada ndefu, pili wengi ni too ignorant to comprehend kilichoandikwa.

Kwenye bandiko hili ni mimi ndiye niliyesema waliovamia Clouds ni TISS? .

Hujawahi kusikia TISS wakiongea na media? . Fuatilia mtu anayeitwa Jack Zoka akiwa TISS.

Lissu kaongea hadharani au kaongea Bungeni? . Unajua maana ya tuhuma zozote kushushwa Bungeni na kutokanushwa na yoyote what does that mean? .

Sijasema nazijua kazi za TISS humu na nilichokisema ni kidogo tuu ya ninachokijua. Nimesema Mzee wangu Andrew Mayalla(RIP) ndie alikuwa RSO wa Mwanza na kilichomkuta. Wako watu wengi wazazi wao ni wafanyakazi wa TISS lakini hakuna yoyote ajuaye huko ndani ya TISS wanafanya kazi gani au shughuli gani.

TISS wanaoeleweka shughuli zao ni wale wa Kijitonyama kwa sababu wanaonekana na kazi yao ni kuvaa tuu suti nyeusi na miwani nyeusi na kusimama tuu huku wakiangalia huku na kule.

Nilichoweka hapa ni baadhi tuu ya matokeo mabaya ya kazi za TISS yaliyowasilishwa mahakamani na maofisa wa juu wa TISS kutimuliwa na kushitakiwa na kufungwa jela.

Kuhusu hizi tuhuma za sasa nimetoa a good benefit of doubt kwa kuweka options 3 za different scenarios

1. Tiss huko nyuma iliwahi kufanya makosa ya utekaji, utesaji na hata uuaji, na ikafumuliwa!. Hivyo kwa vile tayari tunayo precedence ya vitendo viovu vya TISS huko nyuma, hivyo kwa kuutumia uthibitisho wa uovu huo, una justify kuwa kuna uwezekano ikawa ni kweli TISS is behind huu uovu na uchafu unaozungumziwa sasa Bungeni.

2. Lakini pia inawezekana sio TISS as TISS bali ni acts za individual members wa TISS wakifanya a "stand alone operations" bila kupokea command yoyote kutoka juu, hivyo vitendo vya wachache, vikaichafua TISS yetu collectively kwenye a collective responsibilities formula.

3. Pia inawezekana kabisa vitendo hivi vinafanywa na wahuni fulani, ambao wana pose as TISS just to make believe kuwa ni TISS kumbe sio TISS bali ni just impostors wanaochafua the good image ya TISS wetu waadilifu.

Whichever the case, TISS ijitokeze iwakane na kurudisha imani na TISS wetu.

Paskali

Pamoja na maelezo yako manzuri, naomba kutoa ufafanuzi kuwa sheria ya TISS haimpi mamlaka mtu yoyote kuzungumzia kazi zinazofanywa na TISS au kutaja mtu yoyote wa TISS hadharani. Kwa maana hiyo hata kutaja Bungeni ni makosa. Bunge halipo exempted kwenye kutoa informations zinazohusu TISS, waajiriwa wa TISS au watu wa karibu na waajiriwa wa TISS. Pengine ndio maana hata bajeti ya TISS huwa haijadiliwi bungeni. Hiii yote ni kwa ajili ya kuimarisha ufanyaji kazi wa chombo hiki muhimu katika kulinda amani na usalama wa nchi yetu. Unapomuona mbunge tena mwanasheria anakaa anaropoka bungeni eti kisa tu yeye ni mbunge hakika inaleta ukakasi kuweza kujua kipimo cha uzalendo wake.
 
Maboso,
Nafikiri hizi ndizo sheria zinatakiwa kufanyiwa marekebisho. Maana kwa staili hii kuna watu nchi hii wako above the law.....ngoja tuwe kimya maana sheria hazituruhusu.
 
Maboso, Kitu ambacho nakubaliana na wewe ni kweli hairuhusiwi kutaja hadharani nani ni TISS na hakuna aliyetaja hadharani kuwa fulani ni TISS kwa sababu hao TISS wa Nyerere hata mke kujua mume ni TISS ilikuwa shughuli.

Sasa kama TISS wanavaa makirikiri kumsindikiza Bashite kuvamia studio, na TISS mwingine anatoa bastola hadharani kumtishia waziri, nani anakuwa aneiexpose vibaya TISS? .

Alichosema Lisu ndicho nilichosema mimi, hizo data ni za mahakamani hivyo sio classified info zinazolindwa na sheria.

Kweli TISS wana privilege ya confidentiality lakini wasitumie privilege yao kufanya madudu ya kijinga jinga kwa kuitumia kama kichaka cha kufanyia maovu.

Paskali
 
Mkuu Ibambasi, mimi sio wakili wala sio msomi!. Elimu yangu ni ya hapa na pale kama tuu elimu ya Daudi.

Paskali

Mkuu,

Achana na Tundu Lissu na Zitto Kabwe wao wanafahamu fika kwamba kujadili suala la TISS bungeni ni kinyume na sheria iloiunda idara hiyo.

Labda ningekuuliza suali moja tu, mnataka TISS ichunguzwe na nani?
 
Back
Top Bottom