Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu demulikuyPaskali TISS ni idara muhimu sana kwa nchi yetu na pia kwa mustakabali wa nchi na kwa kweli si vyema ikajadiliwa Bungeni au po pote pale kwenye kadamnasi. Hata USA kuna Senate Intelligence Committee na House Intelligence Committee iwapo kuna lo lote linapaswa kuongelewa na mara jingi ni "briefs" tu. Tatizo ambalo mimi ninaloliona ni kuwa TISS wajikite Zaidi kwenye "professionalism" ya kazi zao ambayo itokane na Recruitment (with intensive background checks ) na Training. Hii itaondoa kabisa kutajwa tajwa kwa mambo ambayo kwa kiasi kikubwa inawezekana si wahusika (ukumbuke hawawezi kujitetea hadharani. Kwa mfano niliwahi kuhudhuria kesi moja ambapo watuhumiwa kadhaa walidai waliteswa Wakati wa mahojiano wale waliofanya kitendo hicho walipoulizwa kwa nini walifanya "torturing" wakajibu sisi tuliamriwa tuwa"interrogate" watuhumiwa. kwa wahusika there was no difference between "Interrogation and Torturing". Kwa mara ya kwanza wakiwa kwenye mahakama walijua kumbe there is a difference.
===Mkuu demulikuy
thanks kwa objectivity yako kuhusu torture.
Kwa vile TISS iko chini ya Ikulu yetu na Ikulu ni mahali patakatifu, then TISS is expected ni TISS takatifu. Kitendo cha TISS kutajwa kwenye makorokocho sio heshima hata kido go, hiyo torture za TISS nilizozizungumzia humu zilikuwa systematics na zilikubaliwa ila Nyerere aliposikia alikasirika sana.
Kwenye tuhuma za utekaji na utesaji wa TISS, those who live to tell are the lucky and the very fortunate ones, no one knows what happens to unlucky ones who never lived to tell. Dawa ni kwa TISS au kupitia waziri husika kukanusha kuwa hawahusiki na haya makorokocho wanayonyooshewa kidole kwa kuwakana wale makirikiri wa Bashite na yule mpuuzi wa kwa Nape.
Japo silence sometimes means ignoring lakini sometimes silence means yes name
na mahakamani silence means admissibility of guilt. Hapa jf ni mahakama ya umma hivyo the public has the right to think either way.
Paskali
Mkuu===
Wanaoijadili TISS wanafanya jambo la kizalendo.
Nampongeza Paskali kwa hili. Namkubali Mchambuzi.
Siungi mkono kuivunja TISS lakini siyo kwamba haiwezi kuvunjwa na kuundwa upya na bado tukawa salama.
Tishio la kwamba wana TISS watajiunga na vyombo vingine si la muhimu kama kweli wana TISS wa sasa ni wale ninaowajua. Mwana TISS wa kweli hawezi kuuza uzalendo wake.
Kumbukumbu zangu zinaniambia iliwahi kuvunjwa kabla haijaitwa TISS miaka ya 60's .
Kama kuna wasiwasi wa kuhatarisha usalama kutoka ndani ya TISS, then hiyo ni sababu tosha ya kuonyesha haja ya kuivunja. Nchi hii haiongozwi na TISS, bali wanaoiongoza wanasaidiwa na TISS.
Tusiwachafue TISS kwa kuwapa sifa wasiyo nayo.
Naamini ni wazalendo na wameapa kulilinda taifa hata likiwa mikononi mwa mtu asiyeijua TISS.
Mwisho, nisisitize, pamoja na umahiri na uadilifu, usiri na weledi mkubwa, taasisi yetu haikuundwa na malaika. Hata mbinguni malaika waliasi. Imeundwa na watu na inaongozwa na watu.
Tulikofika ile creed yao ya " no person is greater than a nation itumike" ili kusafisha hali ya hewa.
Vijana waaminifu na wazee waadilifu wanachafuliwa na watu wachache wenye ajenda zao kisiasa.
Vinginevyo, kiongozi wao "ajilipue" na anajua namna ya kufanya hivyo.
Pasco kwanini ilikuwa taboo wasidiscusiwe? Huoni huko kutokudiscusiwa ndo kulikuwa kuna wapa bichwa hata LA kufanya maovu kwa vile hamna wakuwahoji. Idara hii inahtaji kuwa huru bila kuingiliwa na yoyote ili iwe huru iache kutumika kwa masilahi ya watu binafsi.Mkuu Mchambuzi
thanks very much for this, its very objective naona kama umemaliza kila kitu!.
It's true kuna lots of details nime avoid kutokana na uzalendo, pia nimemtaja Mzee wangu tuu kwa sababu alihusika direct, lakini sikumtaja mama yangu ambaye she is still alive and retired (hawaritayi kabisa) wala sikusema kuwa hata mimi almanusura!. Anyway haya tuyaache.
Although mhusika mkuu hataisoma kutokana na lingua uliyotumia, wahusika wenyewe wamesoma, na wamesikia labda waendelee tuu kutia pamba masikioni kwa sababu kujadili jambo lolote kuhusu TISS was considered a taboo hivyo bandiko hili kwa TISS ni kama abomination!.
Thanks again.
Paskali
hii taboo ya kutokudiscuss anything to do with TISS ni kutokana na mfumo wa operations, na ulianzia Bungeni budget ya TISS, Wizara ya Ulinzi, Ikulu na PCCB zinawasilishwa tuu Bungeni na kupitishwa bila kujadiliwa, kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inazipitia tuu vote zake bila kuhoji lolote.Pasco kwanini ilikuwa taboo wasidiscusiwe? Huoni huko kutokudiscusiwa ndo kulikuwa kuna wapa bichwa hata LA kufanya maovu kwa vile hamna wakuwahoji. Idara hii inahtaji kuwa huru bila kuingiliwa na yoyote ili iwe huru iache kutumika kwa masilahi ya watu binafsi.
niko salama kwa sababu yote niliyoeleza humu ni mambo ya kweli yaliyotokea na wahusika waliwajibishwa.pascal utasalimika kweli?
Kwa vile huu ni mtambo, sometimes unaweza kutumia self diagnostic equipment ikajisafisha yenyewe kimya kimya huku nje wala tusijue ila tutaona tuu matokeo kwa mabadiliko chanya.Nani wa kuifumua, kama bashite ndiye think tank wao na babake ambaye ndiye mlezi wao kampa awatumie awatakavyo!
Yaani kesi ya nyani aamue ngedere?
Nyinyi ndio wale mnaoishia kusoma heading tuu na kuchangia! . Umemsikia Lisu kasema nini? .ungetuambia kwanza kama torture ni kinyume cha sharia ipi maana utesaji ni moja ya mbinu za kipelelezi
Kwamba jamaa ana ajira ya kuweka akili mfukoniNiunganishe aisee na mimi niwe mtetezi, maisha huku mtaani magumu sana.
Halafu mi ni mtaalamu sana wa kupiga ngeta, mnaweza tu kukiendeleza kipaji changu
No huyu anafanana sana sana Nyerere, nilisema hapa Magufuli kama Nyerere: Ni mtu wa watu, hapapasi, hamung'unyi, ni kazi tuu, ila pia sio kama Nyerere!Pascal Nyerere alikuwa utu, huyu hana kabisa!
Hili swali nadhani ni internal kwa ma TISS wenyewe. Kwa vile mimi sio TISS na sijawahi kuona tangazo la kazi TISS wala kujua job descriptions zao, utanisamehe bure.Naomba kujua kaka Pascal......... kazi/ TOR/Job description za TISS ni zipi??....
Acha kuzunguka mbuyu, anayewatuma anafahamika , mnazunguka nini? TISS ni nini, wako chini ya nani? acha hizo wanatumwa na Ikuru, Ikuru ni nini?, Ikuru ni nani?
Not necessarily. Let's give them the benefits of doubt kwa options 3.Pascal pole sana,najua JKN alikuwa anashida lakini hili la kuua na kutesa kwa sababu ya kutukana,kuhojiwa sidhani kama lingekuwepo kwa JKN.
Kiongozi yeyote akishashindwa kuongoza basi matokeo yake ni kutumia idara hii kunyamazisha watu.
Paskali, nimetokea kukufahamu kupitia vipindi vyako pale Maonyesho ya sabasaba, nikakuona as an influential man and a knowlegeable one, not an informed one! UMENIACHA NA MASHAKA NA WELEDI WAKO... kwanini?Not necessarily. Let's give them the benefits of doubt kwa options 3.
1. Tiss huko nyuma iliwahi kufanya makosa ya utekaji, utesaji na hata uuaji, na ikafumuliwa!. Hivyo kwa vile tayari tunayo precedence ya vitendo viovu vya TISS huko nyuma, hivyo kwa kuutumia uthibitisho wa uovu huo, una justify kuwa kuna uwezekano ikawa ni kweli TISS is behind huu uovu na uchafu unaozungumziwa sasa Bungeni.
2. Lakini pia inawezekana sio TISS as TISS bali ni acts za individual members wa TISS wakifanya a "stand alone operations" bila kupokea command yoyote kutoka juu, hivyo vitendo vya wachache, vikaichafua TISS yetu collectively kwenye a collective responsibilities formula.
3. Pia inawezekana kabisa vitendo hivi vinafanywa na wahuni fulani, ambao wana pose as TISS just to make believe kuwa ni TISS kumbe sio TISS bali ni just impostors wanaochafua the good image ya TISS wetu waadilifu.
Whichever the case, TISS ijitokeze iwakane na kurudisha imani na TISS wetu.
Paskali
Pascal unatuzingua na kung'ata-kupuliza zako.Wanabodi
TISS ni idara nyeti, uadilifu wake unapaswa kuwa wa kiwango cha juu kabisa ambao haupaswi kutiliwa shaka yoyote, unapaswa kuwa ni uadilifu wa kiwango cha mke wa Kaisari, ile kutuhumiwa tuu ni kosa tosha hata bila kuthibitishwa, anahukumiwa!.
Hivyo ndivyo zilivyo tuhuma za TISS wetu, kuwa wale makirikiri wa Bashite ni TISS!, na yule mpuuzi wa Nape ni TISS!. Hivyo kama wale makirikiri wa Bashite waliovamia Clouds TV sio watu wao, TISS wasikae kimya wajitokeze na kukanusha!. Kama yule mpuuzi aliyemtishia Nape kwa bastola sio mtu wao, wajitokeze wakanushe. Huku kukaa kimya kunachukuliwa ni admission of guilt!.
Kama tuhuma dhidi ya TISS zimefika hadi kwenye Bunge letu Tukufu, na TISS iko chini ya Ikulu yetu, na Ikulu ni mahala patakatifu, tuhuma tuu kumhusu mke wa Kaisari zinatosha kumuondoa Ikulu asije akapanajisi patakatifu petu!. Hiyo TISS isikae kimya lazima ijitathimini na kujisafisha na uchafu wa makandokando haya!.
Huu mjadala unaoendelea kuhusu utekaji, utesaji na mauaji ambavyo vinahusishwa na idara yetu nyeti ya Usalama wa Taifa, TISS ni uthibitisho tosha kuwa TISS imechafuka inahitaji au kujisafisha au kusafishwa!.
Pamoja na Tanzania kuridhia mkakati wa Open Government Initiatives lakini kuna vitu huwezi kuvijadili openly lakini bado unaweza kuvichunguza na kuvifanyia kazi kimya kimya ila public ikaona matokeo na kurudisha imani.
Kuna watu wanadhani Usalama wa Taifa TISS wao ni malaika na hawawezi kabisa kufanya makosa kama madudu haya wanayotuhumiwa nayo sasa. No!, TISS sio malaika kwa sababu nayo inaongozwa na binadamu!.
Tiss huko nyuma iliwahi kufanya makosa ya utekaji, utesaji na hata uuaji, na ikafumuliwa!. Hivyo kwa vile tayari tunayo precedence ya vitendo viovu vya TISS huko nyuma, hivyo kwa kuutumia uthibitisho wa uovu huo, una justify kuwa kuna uwezekano ikawa ni kweli TISS is behind huu uovu na uchafu unaozungumziwa sasa Bungeni.
Lakini pia inawezekana sio TISS as TISS bali ni acts za individual members wa TISS wakifanya a "stand alone operations" bila kupokea command yoyote kutoka juu, hivyo vitendo vya wachache, vikaichafua TISS yetu collectively kwenye a collective responsibilities formula.
Pia inawezekana kabisa vitendo hivi vinafanywa na wahuni fulani, ambao wana pose as TISS just to make believe kuwa ni TISS kumbe sio TISS bali ni just impostors wanaochafua the good image ya TISS wetu waadilifu.
Whichever the case, TISS ijitokeze iwakane na kurudisha imani na TISS wetu
Hebu kwanza msikilizeni Tundu Lissu anasema nini kuhusu utekaji na utesaji wa TISS, hao anaowatetea ndio wenye bahati who could live to tell, hivyo ndio waliosalimika, only God knows kwa wale wasio na bahati hatima yao ilikuwaje because they couldn't live to tell!.
Kama tuhuma hii ni kweli, then serikali yetu ni serikali dhalimu! .
Hii sio mara ya kwanza kusikia serikali inafanya torture!. Hapa chini ni kisa cha kweli kabisa cha udhalimu wa TISS wa enzi hizo ambacho kilimhusu member wa familia yangu kujaribu kuwanusuru watuhumiwa wa torture na katika kufanya wema, wema wake ulimponza, RIP Mzee wangu Andrew Mayalla.
Kitendo kilichofanywa Clouds Media ni uthibitisho wa uhuni kama huu wa gross abuse of power na Nape alipotaka kufanya wema kuikingia kifua serikali yake isijinasibishe na uchafu huu, wema wake ulimponza.
Mwaka 1976 kule Mwanza kwenye eneo la Kigoto, watuhumiwa wa mauaji ya vikongwe walikuwa tortured na maofisa wa polisi.
Mzee wangu, Andrew Mayalla akiwa RSO wa Mwanza, akawanusuru watuhumiwa wawili, Masanja Makula Mazengenuka na Isaak Mwanamkoboko kutoka eneo la Kigoto baada ya mateso makubwa, wakiwa njiani wakamweza hawajala chochote kwa muda wa siku 3 za mateso ya usiku na mchana!.
Akaamua kuwapeleka Bugando, on their way akasimama mahali kuwanunulia soda na kitafunio, soda waliweza kunywa, kutafuna walishindwa.
Bugando akawakabidhi kwa Dr. Nkulila. The next day they were both dead.
Hizo ni enzi za Nyerere, tulikuwa tukiishi Isamilo ya chini, next door ni RPC alikuwa akiitwa Mkwawa, nyumba ya tatu ni DSO. Just imagine majirani watatu wanaishi nyumba zinazofuatana wanapokutwa na kisanga.
Baada ya Taarifa kumfikia Nyerere, kuanzia Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hassan Mwinyi alipoteza uwaziri, IGP wa wakati huo Pundugu alipoteza kazi, Mkurugenzi wa Tiss, Mzena, alipoteza kazi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Peter Kisumo, alipoteza kazi,
Mzee wangu, Mzee Mayalla, RSO, RPC, DSO na OCD wa Mwanza wote walistaafishwa kwa manufaa ya umma, tulihamishwa usiku usiku na kurudishwa kijijini (detention fulani za Nyerere).
Wakati yote haya yakifanyika, mimi nilikuwa mdogo sana, ili kilichofuatia na ilipoanza kuunguruma, ndipo nilibaini ni nini kilitokea. Kesi ya Mauaji Mwanza iliuguruma na thanks God, mtu pekee aliyenasuka ni Andrew Mayalla (RIP) kufuatia kazi kubwa iliyofanywa na wakili Murtaza Lakha.
Kwa wale tuliofuatilia ile kesi ya Uhaini ya mwaka 1982 tulisoma jinsi TISS wanavyoteka, wanavyo tesa na wanavyo ua yakiwemo mauaji ya Martin Tamimu. Utekaji wa Hatty Magee, kule jijini Nairobi, etc.
Mahakama ndio Mhimili pekee wa haki ndani ya katiba yetu, kwenye kesi hiyo ya uhaini, tumeshuhudia watuhumiwa wakitoa ushuhuda jinsi walivyoteswa na TISS kwenye torture chambers zao na kulazimishwa kukiri, hivyo kupelekwa kwa Walinzi wa Amani kukiri kuhusika kwao halafu walipofika mahakamani wakavikana viapo vyao kwa Walinzi wa Amani na kusema waliteswa ndio maana wakakiri.
Japo torture ni kinyume cha sharia, TISS zote duniani wanatumia mbinu hizo kuhoji ambazo nyingine ni halali na nyingine ni haramu.
Marekani ndio inayoongoza kwa kutumia torture na kuihalalisha ila kwa vile ni kinyume cha sheria za nchi hiyo, wanalitumia gereza la Guantanamo Bay lililoko kwenye kisiwa cha Cuba ambako sio ardhi ya Marekani kufanya ushenzi huo.
Hivyo kama tuhuma hizi za Lisu ni kweli, hii sio mara ya kwanza kwa TISS kuhusishwa na makando kando ya ajabu!. Ya Ulimboka tuliyasoma Mwanahalisi, hadi yakamuibua msemaji wa Tiss ya wakati huo Jack Zoka.
Ya Kibanda nilishikwa sikio na mtu tete a tete ila hii nilielezwa ni wale vijana wa Kijitonyama ila it was a personal social issue!.
Yaliyotokea Clouds TV wote tumeyashuhudia kupitia CCTV, na yale makirikiri tumeyaona, na ya Nape Mnauye tumeyashuhudia live mubashara kwenye TV huku huyo mpuuzi akionekana wazi hadi sura watu wanamjua.
Naunga mkono TISS isijadiliwe na Kamati ya Bunge kama ambavyo bajeti yao na ile ya defence hazijadiliwi, lakini bado wanaweza kuchunguzwa.
Serikali yetu lazima ifanye damage control kwa msemaji wa TISS kuibuka na kumkana yule mpuuzi aliyemtisha Nape Bastola na kuwakana wale makirikiri wa Bashite!.
Huu ukimya wa Mwigulu, na serikali ni uthibitisho kuwa serikali has a hand kwenye hayo!. Ili kuonyesha kuwa serikali haihusiki na uhuni,upuuzi na ushenzi huu, rais Magufuli lazima akasirike kama Nyerere alivyo kasirika idara ya TISS inapochafuliwa, aliifumua mwanzo mwisho bila huruma.
Ukiondoa hizo torture za TISS zilizoibuliwa mahakamani, torture za jeshi la polisi ndio isiseme kabisa, innocent (until proven guilt) people have been tortured to death, hakuna kesi and nobody cares as if polisi are doing the right thing!.
Tukio la mwisho ni gunning down waendesha bodaboda wawili na abiria wao wawili kisa wamesimamishwa pale daraja la Mkapa wakapitiliza!. Polisi wakawaripoti hivyo walipofika next check point walimiminiwa tuu na kumaliza kazi hapo hapo, hawakukutwa na silaha yoyote!.
Haya ya polisi tumeisha yapigia sana kelele humu jukwaani.
IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality!. Utampeleka JK The Hague-Part II!
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa!, Polisi Wako Ni Wauaji!. P'se Stop This
Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know!
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?
Na kwa wale wenye interest na TISS kuijua zaidi, tembelea
Namna ya kujiunga na usalama wa Taifa | JamiiForums | The Home of
Kujiunga na Chuo cha Usalama wa Taifa kilichopo Mbweni, Bunju
Afisa usalama wa taifa "shushushu" ni nani? Anafanya shughuli gani
Shushushu (Afisa Usalama wa Taifa) ni mtu wa aina gani .
Natafuta Kazi Usalama Wa taifa | JamiiForums | The Home of Great .
Nadharia ya Usalama wa Taifa (TISS) ibadilike kuanzia sasa ...
Dr. Hassy Kitine, aliyekuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa .
Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE ...
Paskali
Update
Mkuu Mchambuzi
thanks very much for this, its very objective naona kama umemaliza kila kitu!.
It's true kuna lots of details nime avoid kutokana na uzalendo, pia nimemtaja Mzee wangu tuu kwa sababu alihusika direct, lakini sikumtaja mama yangu ambaye she is still alive and retired (hawaritayi kabisa) wala sikusema kuwa hata mimi almanusura!. Anyway haya tuyaache.
Although mhusika mkuu hataisoma kutokana na lingua uliyotumia, wahusika wenyewe wamesoma, na wamesikia labda waendelee tuu kutia pamba masikioni kwa sababu kujadili jambo lolote kuhusu TISS was considered a taboo hivyo bandiko hili kwa TISS ni kama abomination!.
Thanks again.
Paskali