TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Naamini ku expose madudu kwa nia njema, ni jambo jema kwa nchi yangu, tena hapo ndio nimenyamaza kutoyasema yote ninayoyajua, maana kuna mambo mtu unasikia, halafu unaamua kutoamini na mwishowe kujifanya kama hujasikia, mfano mzuri soma bandiko hili uone nilisikia nini na lini, na nimesema nini!.

Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli
P.
 
Kukemea uovu wa kimfumo yataka mtu wa haki kama Nyerere, ....hawa madalimu wapigania viti walivyokalia leo hawawazi chochote, wanaona Dunia inaishia kwao.
 
MTU mwenye sifa ya Extrovert hafai kufanya kazi ya ISS,pia MTU mwenye IQ ndogo hafai kufanya hiyo kazi, ulimwenguni kote ndivyo ilivyo.Ikumbukwe kuwa ufauru wako shuleni haimaanishi kuwa una IQ kubwa,Madonna ni mwanamuziki aliyeishia elimu ya msingi lakini baada ya kupimwa IQ yake ilionekana imefikia 140 akiwa amewapita maprofesa waliowengi.Hivyo basi uwezo mkubwa wa kifikiri haupatikani darasani,bali MTU huzaliwa nao na baadae huboreshwa na mazingira ya makuzi.
 
Asante kamanda

Ova
 
Pascal Mayalla enzi za Nyerere nafahamu wahindi na waarabu kama watatu hivi wakiwa kwenye pay role ya Usalama.
Leo hawa jamaa hata kuwapa nafasi ya kawaida hawapewi imekuwa taboo ...leo huwezi kuwapata tena kina Alnoor Kassom, Amir Jamal, Leader Sterling, Adolf Walden , Ali Mahfoudh

Kuna hekina zake kuwa na watu wa aina hii ....ila sasa wote kanda ya ziwa
 
Mkuu Crabat, naunga mkono hoja. Ila hili la Kanda ya Ziwa, sii kweli, mnamsingizia tuu, na nimelizungumza hapa
Tuhuma Za Ukabila: Wasukuma Sii Miongoni Mwa Makabila Yenye Ukabila, Tatizo Ndio Walio Wengi!
P
 


Mchambuzi
Mkuu bahati mbaya sana ni ukweli ambao ushausema hapo juu kuwa tuna Weak institutions tayari, so napata tabu sana hawa ndio wapewe jukumu tena la kuisimamia hii idara na reform zake.

Sijuhi kipi kianze katia kuimarisa hizi institutions "Parliamentary, administrative and, judicial."
Japo nilikuwa naona JW ndio pekee imebaki na weledi na hata mkulu kwa kulitambua hilo amekuwa akiteua watu wengi kutoka huko. labda kile kitengo cha jeshi kipewe kuisimamia na kuireform hii kitu.
 
Kwa maana ya Intelligence, hakuna kumumunya maneno.
Intelligence ni outfit ya intelligent people, watu wenye IQ nzuri tu na wenye kuonyesha si ufaulu darasani tu bali hata socially acceptable people, si zombies.

Mimi nimesoma nao, so good at their jobs kiasi kwamba ukiambiwa jamaa yuko TISS huwezi amini.
Mwalimu alikuwa akiwa recruit on merits, toka wakiperform vizuri toka madarasani.

Miaka baada ya Mwalimu sijui upepo ulibadilika.
Wenye TISS wakaanza kuingiza ndugu zao, watoto wao, vigezo vimebadilika!
Sasa hivi si nadra kukuta kijana akiwatishia wenziwe kwa ku fkash kadi yake kuonyesha yuko TISS na anaweza kumfanyizia.

TISS outfit lazima ibaki na majukumu yake kikatiba, yaani data collection, dissemination(intelligent), na ku advise uongozi.

Nakubaliana na Pasko, extortion of data, intimidation na hata torture katika ulimwengu wa sasa, utapata data za kuwafurahisha viongozi lakini zaweza kuwa irrelevant and false.

TSS vilevile ikiingia kuchukua corrective measures itaingilia enforcement.
Matukio ya hivi karibuni ya watu wasiojulukana, by all means haiwezi kuwa kazi ya TISS, bali wanasiasa.

Cha kusikitisha ni kwamba Polisi mara nyingi inaboronga mno katika utendaji, hivyo kuathiri intellijensia wanayopata.
Mfano hatari wa hivi karibuni ni Mkuranga/Ikwiriri/Kibiti.

Sidhanii kwamba vyombo husika havikuwa na intellijensia ya yanayoendelea huko.

Tunashukuru kwa joint task force, na seriousness ya uongozi kukabili tatizo lililo anza kuonekana haliwezekani.

Wengi tuna imani kubwa na TISS, lakini vyombo vya enforcement, Polisi, Mahakama, DPP huko kuna ukakasi.
 

Nimekusoma Pascal pole kwa yote familia yako iliyopitia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…