MTU mwenye sifa ya Extrovert hafai kufanya kazi ya ISS,pia MTU mwenye IQ ndogo hafai kufanya hiyo kazi, ulimwenguni kote ndivyo ilivyo.Ikumbukwe kuwa ufauru wako shuleni haimaanishi kuwa una IQ kubwa,Madonna ni mwanamuziki aliyeishia elimu ya msingi lakini baada ya kupimwa IQ yake ilionekana imefikia 140 akiwa amewapita maprofesa waliowengi.Hivyo basi uwezo mkubwa wa kifikiri haupatikani darasani,bali MTU huzaliwa nao na baadae huboreshwa na mazingira ya makuzi.
Kwa maana ya Intelligence, hakuna kumumunya maneno.
Intelligence ni outfit ya intelligent people, watu wenye IQ nzuri tu na wenye kuonyesha si ufaulu darasani tu bali hata socially acceptable people, si zombies.
Mimi nimesoma nao, so good at their jobs kiasi kwamba ukiambiwa jamaa yuko TISS huwezi amini.
Mwalimu alikuwa akiwa recruit on merits, toka wakiperform vizuri toka madarasani.
Miaka baada ya Mwalimu sijui upepo ulibadilika.
Wenye TISS wakaanza kuingiza ndugu zao, watoto wao, vigezo vimebadilika!
Sasa hivi si nadra kukuta kijana akiwatishia wenziwe kwa ku fkash kadi yake kuonyesha yuko TISS na anaweza kumfanyizia.
TISS outfit lazima ibaki na majukumu yake kikatiba, yaani data collection, dissemination(intelligent), na ku advise uongozi.
Nakubaliana na Pasko, extortion of data, intimidation na hata torture katika ulimwengu wa sasa, utapata data za kuwafurahisha viongozi lakini zaweza kuwa irrelevant and false.
TSS vilevile ikiingia kuchukua corrective measures itaingilia enforcement.
Matukio ya hivi karibuni ya watu wasiojulukana, by all means haiwezi kuwa kazi ya TISS, bali wanasiasa.
Cha kusikitisha ni kwamba Polisi mara nyingi inaboronga mno katika utendaji, hivyo kuathiri intellijensia wanayopata.
Mfano hatari wa hivi karibuni ni Mkuranga/Ikwiriri/Kibiti.
Sidhanii kwamba vyombo husika havikuwa na intellijensia ya yanayoendelea huko.
Tunashukuru kwa joint task force, na seriousness ya uongozi kukabili tatizo lililo anza kuonekana haliwezekani.
Wengi tuna imani kubwa na TISS, lakini vyombo vya enforcement, Polisi, Mahakama, DPP huko kuna ukakasi.